CHADEMA, mbona mnauma maneno suala la kuanguka uchumi wa Tanzania?

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,780
3,227
Hivi karibuni CC ya CDM kupitia katibu mwenezi wake JJ MNYIKA ilitoa angalizo kwa serikali ya JK kuhusu kuanguka kwa uchumi wa nchi.

Angalizo hilo lina mapungufu kwani halina msisitizo wa kuonyesha hata viashiria vya kuanguka kwa uchumi wa nchi.

Sisi tunaamini chama kikuu cha upinzani ndicho mkosoaji mkuu wa serikali iliyo madarakani, lakini kwa hili la kuanguka kwa uchumi CDM hawajauonyesha umma madhara ambayo tayari yamejitokezza kwa kuathiri shughuli za uchumi wa wananchi.

Mwaka jana Zitto Kabwe alijiripua bungeni kwa kusema ukweli kuwa serikali ya JK imefirisika hiyo iliamsha watu toka usingizini kuwa kumbe nchi inaelekea shimoni.

CDM inahitaji kutuonyesha ni kwa kiwango gani anguko la uchumi wa nchi limeathiri shughuli za kiuchumi za watanzania mmoja mmoja. Mnyika tafadhali jilipue kama Zitto kabwe usingoje madhara yawe makubwa watanzania wanahitaji kuelimishwa na uenezi wako.

Nawasilisha
 
Kwa mtanzania mmoja mmoja nadhani ni ngumu kupata kiwango cha athari.
 
Mkuu,

Hujaona kama uchumi umeanguka na athari zake hujui hadi uambiwe na Mnyika?

Get serious kamanda wangu!
 
hujaona anguko la uchumi ww? Mfumuko wa bei huuoni? Serikali kushindwa kulipa watumishi wake ni dalili za nini unadhani? Je hujawahi kusikia serikali ikikili kwamba haina pesa? Vipi ugumu wa maisha kwa wananchi wake au hadi siku bot ikifungwa ndiyo utaelewa ndugu yangu? Mie niliwaelewa hivo nadhani kuna kila dalili za serikali kama haitachukua hatua mathubuti ikashindwa hata kuendesha shughuli zake.

 
sasa nimepata ufahamu kwamba CDM ndiyo inayotegemewa kutoa uelekeo wa nchi, kila kitu CDM inatajwa humu
 
Wapeni mamlaka ya kuunda serikali muone kama hawatafanya mambo ya maana!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom