Chadema: Madai ya katiba yapo palepale

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
CHADEMA imesema licha ya Rais Jakaya Kikwete kutia saini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011, itafanya kila linalowezekana kuhakikisha Tanzania inapata Katiba bora.

Matamko haya yametolewa jana na viongozi wa Chadema walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina ya siku moja ya viongozi wa chama hicho kutoka katika mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Slaa:

"Sisi tuliomba tuonane na rais ili tumshauri aache kusaini katiba ile lakini hatuna uwezo wa kumzuia kwa kuwa katiba yenyewe inamruhusu, hivyo kama ameisaini shauri yake, sisi bado tunaendelea na msimamo wetu wa kuipinga sheria hiyo," alisema.

Alisema kuwa kitendo hicho kimeonesha kuwa Kikwete hakujali hoja za Watanzania na wadau wengine kwa ujumla. Alisema pamoja na yote yaliyotokea, CHADEMA wataendelea kupeleka maoni yao kwa ajili ya marekebisho hayo kama ambavyo walikubaliana kwa pamoja.

Zitto:

"Ni vema juhudi hizi ziendelee, tusikubali kushindwa kupata mwafaka wa kitaifa," alisema Zitto na kusisitiza; "Kwa namna yoyote ile Chadema itaendelea kuchukua hatua zote muafaka kuhakikisha Watanzania wanapata Katiba nzuri na yenye manufaa kwa taifa.

"Watanzania waelewe kwamba hakuna ushindani katika jambo hili. Tunaandaa mazingira mazuri ya kuliandaa Taifa letu liwe na demokrasia zaidi na liweze kutumia rasilimali za nchi kwa maendeleo ya Watanzania," aliongeza.

"Nimewahi kusema na ninarudia kusema tena, Katiba ya nchi inaweza kutafutwa barabarani, lakini kamwe haiandikwi barabarani. Katiba huandikwa mezani kutokana na mazungumzo yanayozaa mwafaka wa Kitaifa," alionya Zitto

Lissu:

"Ninachosema ni kuwa Rais alitukatalia mapendekezo yetu kwa sababu katika kikao kile hatukukubaliana kuwa hataisani muswada huo," alisema Lissu na kuongeza:

"Sisi tunaendelea kufanya efforts (juhudi), kuendelea kusimamia hoja zetu na tunajiandaa kupeleka hoja bungeni kubadilishwa kwa sheria hii," alisema.

"Tutawaambia wabunge waangalie maslahi ya wananchi, wapige kura kwa maslahi ya wananchi na si kwa maslahi ya chama fulani," alifafanua.
 
Hapa kuna tatizo sijui niliite la kiufundi au vipi.
Baada ya kikao cha Ikulu ilitolewa taarifa ya pamoja 'joint statement' ikieleza jinsi gani wamekubaliana. Hakukuwa na mahali Chadema walieleza kumshawishi rais asitie saini. kilichoonekana ni makubaliano kuwa katiba ya sasa itumike kusimamia uandikaji wa katiba mpya. Taarifa ikaongeza kama yapo marekebisho basi yatafanyiwa kazi kadri tunavyosonga mbele.

Hata pale waipojua kuwa sheria ya bunge hutenguliwa na bunge bado waliridhia kuwa mabadiliko yanaweza kufanyika nje ya bunge.
Aliyetia saini kwa Chadema ni J.Mnyika na Nchimbi kama sikukosea.

Kwa mtazamo huo kwanza kabla ya kumlaumu mtu wanawajibu wa kuwaambia watu kuhusu 'joint statement' kama walishiriki kuandika na sasa hawakubaliani nayo au hawakushiriki kabisa.

Hoja ya Dr Slaa kuwa hawawezi kumzuia Rais ina walakini kwasababu lengo lao lilikuwa kwenda kumuelezea madhara yatokanyo na kutiwa saini mswada huo. Kwahiyo kusema tu kuwa hawawezi kumzuia haitoshi.
 
Katiba inamruhusu rais ulitaka Chadema wamshike mkono asisaini, fafanua una maana gani.
 
Chadema kila mtu anaongea kivyake kuhusu ili suala, ukimsikia Freeman Mbowe, au Dk. Slaa, juzi John Mnyika, kasema Chadema wamejitoa kwenye suala la Katiba, leo tena mnasema madai ya Katiba yapo pale pale,

Kuna ubabaishaji mkubwa katika uiongozi wa Chadema!
 
Wewe ndiye imechanganyikiwa wamesema kama sheria hazitarekebishwa hawatashiriki kwenye mchakato.
 
Katiba inamruhusu rais ulitaka Chadema wamshike mkono asisaini, fafanua una maana gani.
Nina maana kuwa walipokubali kuandika kauli ya pamoja hapo tu walishakubali atie saini( rejea makubaliano niliyoyaorodhesha)

Pili hawakukanusha kauli iliyotolewa na Ikulu juu ya makubaliano.
Tatu lengo lao lilikuwa kumueleza Rais madhara na kutoridhiswa kwao na utiaji wa saini. Kama hilo ndilo ilikuwa lengo je limefikiwa? na kama halikufikiwa kwanini waliikubali kauli ya Ikulu huku wakijua kuwa haikuwa na maudhui ya walichokusudia.
 
Kutia saini si kila kitu ulichotaka ukipate siku hiyo hiyo kuna mikataba ya miaka 20 lakini sahihi inatiwa siku ya kuanza mkataba.
 
Wewe ndiye imechanganyikiwa wamesema kama sheria hazitarekebishwa hawatashiriki kwenye mchakato.

Sheria zipi zirekebishwe? wakati Rais Kikwete, kaishasaini sheria? viongozi wenu wamejichanganya huo ndio ukweli, wewe una mapenzi na Chadema huwezi kuona, jipangeni upya mje kutoa maoni yenu kwenye tume ya Katiba
 
Kwelli ujinga mzigo unachekelea tobo la mtumbwi eti haliko upande wako wakati wote mmepanda mtumbwi mmoja.
 
Miruzi (/kelele/mbinja) mingi humchanganya/humpoteza mbwa.
 
mkuu hi nimeipenda!
Kuna watu wanakenua meno kuchekelea eti madai ya Chadema yameshindwa hawajui kuwa sheria ni msumeno wamuulize Banda wa Zambia atawaeleza alikataa katiba isibadilishwe sasa anajuta na wadosi wake.
 
Suala katiba mpya ni la wananchi wa Tanzania. Wananchi walilalamikia kuwa katiba iliyopo imepitwa na wakati, inakandamiza demokrasi. Sasa tunataka katiba mpya, lakini cha kushangaza muundo wake unafanana na katiba hii mbovu tuliyonayo. Kama mswada huu uliosainiwa na Mkwe.re utafanikiwa tutakuwa hatujafanya lolote, zaidi demokrasia kuendelea kukandamizwa, kutokana na rais kuwa na madaraka makubwa ya mamlaka ya uteuzi.
 
Back
Top Bottom