Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Kama mnaamini wengi kuwa Mama Prof. ni mzuri na Taifa kwanza ndiyo Slogan ya CHADEMA, sasa mnalia nini?
Au na nyie mnaojifanya mna uchungu sana na Chadema mmeanza kuuguwa ugonjwa wa CCM wa kila kitu sisi?
Kwa kuijua CCM, hata mie ningelikuwa na uwezo kiasi gani, nisingeligombea kwa kupitia CDM.
Ila ukiangalia matokeo, yameleta mwanga kuwa CCM nao wameanza kubadilika na wanaweza kuwapa kura wagombea wa Chadema. Itabidi chaguzi zozote zijazo, lazima awepo mgombea wa kuaminika.
Kama Chadema wameweza kulazimisha na kuwa nafasi mbili za wapinzani, nafikiri ni hatua moja nzuri sana kwenye demokrasia ya kweli kwa taifa letu. Hatua inayofuata ni kulazimisha sasa, bunge lijalo, lazima Naibu Spika watoke kwenye vyama vya Upinzania kulingana na idadi ya wabunge wake.
Kuna nchi ambazo hii system inatumika na kwangu mie ni njia nzuri sana kuwalazimisha chama tawala kugawana madaraka na wapinzani. Kwa hali ilivyo sasa hivi hapa Tanzania, Naibu spika alitakiwa kuwa wa CHADEMA na CUF.
Acha mama atuwakilishe Watanzania na siyo NCCR au Chadema pekee kama wengine wanaojifanya wamekunywa maji ya bendera ya CDM wanavyotaka tuamini ingawa wengi tunawafahamu kuwa ni waongo wa kutupwa.
Ni bunge la EALA na wengi tunaamini mama Prof. atakuwa muwakilishi mzuri. Tuache vyama pembeni sasa na tugange yajayo. Nina imani kuwa baada ya mwaka 2015, CHADEMA watakuwa kwenye position ya kupeleka nusu ya wabunge wa EALA ingawa pia utaratibu utabadilika kwani watakuwa wanapigiwa kura.