CHADEMA lazima kijipange Arumeru Mashariki

The Hunter

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
1,049
305
Kimsingi tumeshuhudia pilika pilika na mbwembwe nyingi pindi inapotokea uchaguzi mdogo, mambo haya yamekuwa yakienda pamoja na gharama kubwa za maandalizi miongoni mwa vyama vinavyogombea.
Naamini Uchaguzi ujao wa Meru Mashariki, CDM lazima kifanye maamuzi magumu na maandalizi makubwa hii nikutokana na sababu zifuatazo;-

. Meru Mashariki ipo Arusha mkoa ambao CDM ina amini ndio ngome yake, huku CCM kikijaribu kurudisha heshima
. Ni jimbo ambalo 70% ya vijana wake hawana ajira rasmi na hii nikutokana na wengi wao kulazimishwa kuondoka machimboni kule Mbuguni
.Wakina mama wa jimbo lile ndo wafanyakazi wakubwa katika sekta nzima ya kiuchumi, kwani wanaume wengi si wafanyaji kazi
.Ni jimbo ambalo vijana wengi ni wajanja na waliotayari kufanya lolote ili kupata pesa
.Ni jimbo la mtego kwa Mh.Lowasa kwani bila shaka atakuwa kwenye kamati maalumu ya kuhakikisha jimbo linarudi CCM
.Wengi ya wakazi wa jimbo hili ni Wameru,Waarusha, Wamasai,Wachaga na makabila mengine madogo.
. Jimbo la Meru Mashariki lipo karibu na mjini anapotoka Kamanda Lema hivyo CCM wanajua ugumu watakao kumbana nao

Nionavyo

CDM lazima kimpitishe mtu anaekubalika na mwenye kuaminika,
siamini kama kijana wetu alieshindwa 2010 bwana Nasari ni chaguo muhafaka kwa kinyanganyiro hichi
hii ni kutokana na ukweli Sumari hakufanya kampeni lakini alimshinda hii ina leta picha kwamba huyu kijana hakubaliki sana
Ikumbukwe CCM watakuwa radhi kuingia gharama mara mbili ya Igunga ili kushinda jimbo hili
Na ni ukweli usiposhiba jikoni huwezi shibia sebuleni kama 2010 ulishindwa je 2012 ambapo Wapinzani wote wanaangalia jimbo hilo hilo utashinda vipi?

. Mtu alie karibu na anaefamika na kufikika wakati wote
Kuwa mbali na wananchi wako ni jambo jingine ambalo kijana Nasari litamfanya asichagulike,
mfano, Bashe, Shigongo na wengine wengi japo hawakupata nafasi za kupitishwa na vyama vyao still wapo kwenye majimbo yao mara kwa mara wakishiriki na wananchi wenzao shughuli za kila siku.
 
Kwani yule mgombea wetu wa 2010 yuko wapi? kama kuna dalili nzuri kwanini asirudishwe yule yule? labda kama hauziki.
 
Post zingine zimejaa uongo huna hata aibu unasema Kingwangala hakupitishwa wakati tayari ni mbunge duh
 
nijuavyo mimi Nasari anauzika na hata baada ya uchaguzi alikuwa bado anaendelea kupiga ndogo ndogo jimboni, ni kijana na yuko smart, apewe nafasi. by the way HAKUSHINDWA!!!
 
Post zingine zimejaa uongo huna hata aibu unasema Kingwangala hakupitishwa wakati tayari ni mbunge duh

Wakati mwingine kosa la kiuandishi halikupi busara ya kuona post ni ya uongo, after all hukulazimishwa kuisoma
 
Kama kuna wenyeji wanaotokea Meru watafahamu nayoyaongelea zaidi tunapoangalia wakazi wake, kama umefika Akeri, Shangarai, Tengeru, na maeneo mengi zaidi kuelekea miinuko ya mlima Meru ambapo barabara ni shida wakazi wao wengi bado wanatumia maji ya mifereji kama maji ya kunywa, biashara kubwa ya vijana ni kuchana mbao,kubeba mizogo ya watalii, kubeba na kuuza maziwa kwa kutumia baiskeli huku wimbi kubwa la vijana likiwa halina ajira
 
nijuavyo mimi Nasari anauzika na hata baada ya uchaguzi alikuwa bado anaendelea kupiga ndogo ndogo jimboni, ni kijana na yuko smart, apewe nafasi. by the way HAKUSHINDWA!!!

Kama hakushiba kwenye sinia atashiba kwenye bakuli,tuache kudanganyana huyu kijana chadema ikimsimamisha hawezi kushinda hata kwa dawa,muarubaini wa arumeru ni dr.slaa full stop.
 
ARUSHA
WILAYA YA MERU
ARUMERU MASHARIKI
Candidate
Political Party
Number of Votes
Percentage Votes
SUMARI JEREMIAH SOLOMON
CCM
34,66162.23
JOSHUA SAMWEL NASARI
CHADEMA
19,12334.33

kulingana na matokeo hayo hapo juu nakubaliana nawe kuwa chadema inabidi ifanye kazi wafanye home work kwanza kabla ya kukurupuka na kumsimamisha Nasari. lazima kufanya uchunguzi wa kina wa zaidi ya kura ziliibiwa ingawa inaweza ikawa ni moja ya sababu. CDM inaweza ikaibadili kabisa hali hiyo hapo juu kama walivyofanya igunga kutoka kura sifuri za ubunge mpaka 24000
na kuipunguzia kura CCM kutoka 34000 mpka 26000 kwahiyo inawezekana kabisa ku flip hizi kura lakini kuna haja ya kufanya research ya kujua ni nini hasa kilitokea hasa ukizingatia mgombea wa ccm hakufanya kampeni ?? la pili ni kuruhusu demokrasia ichukue mkondo kwa kumpa kila mtu fursa ya kugombea kama Nasari. atakayeshinda ndiyo huyo huyo asimamishwe.

tatu chadema izingatie zaidi matokeo ya uchaguzi kufanya kampeni zake maeneo ambayo walipata kura nyingi wakaakikishe kujiandikisha ni kwa nguvu na waliojiandikisha wanapiga kura na nguvu nyingi ziamishiwe maeneo ambayo Nasari hakufanya vizuri kabisa kwa kuchunguza kwanini hawakumpigia kura Nasari na nini cha kufanya ili kubadili hali hiyo. majeshi yote ya front line yaamie maeneo hayo ili mziki wa chadema upigwe mpaka waliolala waamke. ili ni jimbo zuri sana kuliko igunga kwani chadema ina picha nzuri ni maeneo gani yenye udhaifu kulingana na uchaguzi uliopita na kuanza kuyafanyia kazi kwa kuanzia kampeni ya nguvu maeneo hayo.
 
ARUSHA
WILAYA YA MERU
ARUMERU MASHARIKI
Candidate
Political Party
Number of Votes
Percentage Votes
SUMARI JEREMIAH SOLOMON
CCM
34,66162.23
JOSHUA SAMWEL NASARI
CHADEMA
19,12334.33

kulingana na matokeo hayo hapo juu nakubaliana nawe kuwa chadema inabidi ifanye kazi wafanye home work kwanza kabla ya kukurupuka na kumsimamisha Nasari. lazima kufanya uchunguzi wa kina wa zaidi ya kura ziliibiwa ingawa inaweza ikawa ni moja ya sababu. CDM inaweza ikaibadili kabisa hali hiyo hapo juu kama walivyofanya igunga kutoka kura sifuri za ubunge mpaka 24000
na kuipunguzia kura CCM kutoka 34000 mpka 26000 kwahiyo inawezekana kabisa ku flip hizi kura lakini kuna haja ya kufanya research ya kujua ni nini hasa kilitokea hasa ukizingatia mgombea wa ccm hakufanya kampeni ?? la pili ni kuruhusu demokrasia ichukue mkondo kwa kumpa kila mtu fursa ya kugombea kama Nasari. atakayeshinda ndiyo huyo huyo asimamishwe.

tatu chadema izingatie zaidi matokeo ya uchaguzi kufanya kampeni zake maeneo ambayo walipata kura nyingi wakaakikishe kujiandikisha ni kwa nguvu na waliojiandikisha wanapiga kura na nguvu nyingi ziamishiwe maeneo ambayo Nasari hakufanya vizuri kabisa kwa kuchunguza kwanini hawakumpigia kura Nasari na nini cha kufanya ili kubadili hali hiyo. majeshi yote ya front line yaamie maeneo hayo ili mziki wa chadema upigwe mpaka waliolala waamke. ili ni jimbo zuri sana kuliko igunga kwani chadema ina picha
nzuri ni maeneo gani yenye udhaifu kulingana na uchaguzi uliopita na kuanza kuyafanyia kazi kwa kuanzia kampeni ya nguvu maeneo hayo.

Niukweli dhahiri jimbo hili inapaswa CDM chini ya kamanda Lema waanze kulipitia na kuweka sawa hapa na pale, maana niwazi magamba watamwaga pesa nyingi na kujaribu hila mbalimbali
 
Nawambieni awamu hii hata chadema wangesimamisha jiwe ligombee na jk arumeru mashariki, jiwe litashinda!
wameru wanajua jk ameuza nchi
 
nilikuwa huko December hii wanawake wengi na wazee wa kule wana taswira mbaya kuhusu CDM na maandamano yenu. Jipangeni mkiwa mnaelewa ni jimbo ambalo halina vijana wengi kwani wako mijini na vyuoni. Nashauri busara zaidi ya jaziba. Tena Lema ndo hawampendi kabisa kwani wanaukabila zaidi tumieni wazee wa kule na wengine wenye busara kama Dokta wa Ukweli
 
can however talks about kusimama slaa stop it kwa sababu kullishajadiliwa nyuma na tulishaelimishwa kwa nini sio sawa? ama hamsomi, ama hamsikii, ama ni ku sabotage mazungumzo haya mazuri. Tafadhali acheni watu progressive watusomeshe sipendi watu wenye kujibu mambo makini na magumu kiurahisi tu ili mradi nao wasikike wamesema. Sisi wengine tunaangalia big picture ya ukombozi wa nchi hii unapoleta huu ubutu katikati ya mambo muhimu unatu disturb sana. Please Please let us allow this forum to do its job! kama unaona thread kwa mara ya kwanza jipe muda uone flow ya comments ama search kuona thread kama hiyo iliishia wapi mara ya mwisho, ukijua kwamba wasomaji ni sisi sisi wa thread zote kwa hiyo usiturudishe nyuma jamani heeeee. Kuna wenzetu wameshatuelimisha humu ndani kwamba tunaangalia the big picture, kuchukua nchi sio kuwa wabunge kwa hiyo lazima tujipange slaa ana nafasi yake sasa sasa nini tena kurudi huko nyuma
 
Back
Top Bottom