CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.
Hiki ndicho alichokitaka Zitto Bungeni, swali je ndicho alichokipata?

Siasa haiendi hivyo Mwanakijiji. You dont always get exactly what you want(ed). Jambo moja ambalo hatulioni ni kuwa katika nchi yetu practically, Rais ana nguvu kuliko chombo kingine chochote. In fact, Rais akiamua jambo linafanyika, lakini inawezekana mahakama, bunge, nk wakaamua jambo likabaki katika maamuzi na lisifanyike.

Bado wote wewe na Mwafrika wa kike hamjajibu swali langu juu athari za ushiriki wa Zitto katika hii kamati kwa nchi, CHADEMA na Zitto mwenyewe!
 
Athari za zito kushiriki ni hizi ingawa kuna faida pia

1. Hizi kamati hazina historia ya kuleta tija yoyote katika nchi yetu ipokuwa kutafuna pesa za walipa kodi. Zito kete yetu ya turufu inaingizwa kwenye hako kamtindo
2. Wakiamua kumuua itakuwavigumu kwa watu kuamini kuwa ameuwawa kwani watu watajiuliza "kama walitaka kumuua kwa nini walimchagua kwenye kamati" hii ni alibi kali sana.
3. Atatengeneza urafiki na watu anaowakosoa next time itakuwa rahisi sana kwa mtu kama Mwakyembe au mark bomani kuambiwa hebu mnyamazisheni huyo kijana na kwa sababu wanaelewana inakuwa rahisi kumuingia na kuongea naye
4. anatumika kusafisha nyota ya mkuu wakati mkuu anauwezo wa kuchukua hatua nyingi tu za kuiendeleza hii nchi na ameamua kukaa kimya. watu wameanza kumbomoa hana jinsi ila kufanya mambo madogo madogo yanayoweza kuwachanganya watanzania wengi wao wakiwa na upeo mdogo kuwa yuko serious.
5. Wengi wa watu wanzdhani kuwa jamaa kakurupuka tu kumchagua wanashindwa kuelewa kuwa uteuzi huu watu wamekesha kupanga kitu ambacho kitapolarise country kwa manufaa yao, zito angekataa au kutoa masharti ya kuwepo kwenye hii tume
6. Tume haitafanya kitu ila watapewa fedha nyingi sana. maisha ya kabwe yatabadilika hata raia wa kawaida wataona.halafu watapewa kazi wakina kada mpinzani, ES, mtu wa pwani n.k kuanza kuzusha kuwa kabwe kaongwa fedha kukaa kimya na watu wakilinganisha na fedha alizonazo wataamini na ndiyo itakuwa mwisho wake
7. Sijaona duniani mwanasiasa yoyote anayemchagua mpinzani wake kuwepo kwenye kitu chochote ambacho sio pilitically calculated - msiwadharau hawa!
8. Walikaa vikao kukufungia hao hao, wanakaa vikao vingine kukuchagua hao hao. wanakuchanganyia na watuhumiwa humo humo halafu unategemea utatoka politically live... no way
 
Shalom, pamoja na kwamba sikubaliani na majibu yako, nimeridhika nayo. Umweza kuonyesha kwa mbali athari kwa Zitto, japokuwa hujasema taifa litaathirikaje! Ahsante sana.
 
Shalom, pamoja na kwamba sikubaliani na majibu yako, nimeridhika nayo. Umweza kuonyesha kwa mbali athari kwa Zitto, japokuwa hujasema taifa litaathirikaje! Ahsante sana.

Taifa litaathirika:

Tutakubali kuendelea na utamaduni wa kuundiwa kamati zingine wakati zile za mwanzo hajijatoa matokeo yake, Rais aweke matokeo ya kamati ya Masha aliyoiunda yeye mwenyewe hadharani.

Taifa litakuwa limekubali kuwaacha mafisadi na watu wenye mgongano wa kimaslahi kusimamia suala la kitaifa. Ni precedence mbaya huko mbeleni hata tutawateua wauza unga na wabakaji katika kamati nyeti za kitaifa.

Umaarufu wa Kikwete na CCM waliokwisha jichokea utaanza kurudi tena bila hatua zozote za maana za kuleta mageuzi kufanyika, hii itarudisha nyuma safari ya taifa ya kuondoa viongozi mafisadi na walioshindwa kutoa mwelekeo kwa taifa

Kodi zetu mamilioni yatatumika katika kamati isiyokuwa na mamlaka itayatoa toa mapendekezo kwa Rais tena inawezekana kwa siri

Tayari itakuwa kamati imeshafanya kazi hivyo huwezi tena kudai kamati juu ya kamati ama tume ya Rais. Tayari Kikwete atakuwa amemaliza kazi yake. Itachukua miaka mingi kupata chombo kingine cha kufanya kazi hiyo kwa ufanisi

Zitto atatumika kuhalalisha ghiliba ya kina Kikwete na wenzake.

Mchezo huu wa kisiasa umesababisha sasa orodha ya mafisadi haijadiliwi tena- kila mtu anampongeza Rais utadhani all is well katika taifa letu.

Hadidu rejea za kamati zimeacha mambo ya msingi kama masuala ya mazingira na haki za binadamu katika maeneo ya migodi; kwa kamati hii kufanya kazi yoyote atakayedai haya ataambiwa tayari kuna kamati nyingine ilishaundwa. Hivyo haya yatasahaulika.

Kuna makundi yameachwa tofauti na ahadi ya Rais mathalani mashirika ya kijamii(asasi za kiraia); kamati ikiendelea itakamilisha kazi yake bila ushiriki wake hivyo Kikwete ataonekana alitoa ahadi ya uwongo na uzandiki na maslahi ya kitaifa ya makundi haya hayatazingatiwa.

Zitto akitoka au akiweka masharti kamati ya Rais itapoteza uhalali wake(si kisheria) bali kimtazamo wa umma na hivyo kufanya marekebisho mbalimbali kufanyika kabla ya kamati kuendelea na kazi yake. Rais alipaswa kuunda tume.
 
Nafutari kwamba kwenye nchi hii kuna watu makini kama akina Kitila Mkumbo, ni kwa bahati mbaya sana watu makini kama hawa huwa hawapati popularity kulinganisha na watu wa kawaida...

Kaka yangu Kitila mimi nakuaminia kwenye kusimama katika kulitetea Taifa...

Ingawa natamani sana watu kama ninyi msingekuwa kwenye vyama!!!

Tuendelee,,, nasubiri ujibiwe maswali yako.
 
Siasa haiendi hivyo Mwanakijiji. You dont always get exactly what you want(ed). Jambo moja ambalo hatulioni ni kuwa katika nchi yetu practically, Rais ana nguvu kuliko chombo kingine chochote. In fact, Rais akiamua jambo linafanyika, lakini inawezekana mahakama, bunge, nk wakaamua jambo likabaki katika maamuzi na lisifanyike.

Bado wote wewe na Mwafrika wa kike hamjajibu swali langu juu athari za ushiriki wa Zitto katika hii kamati kwa nchi, CHADEMA na Zitto mwenyewe!

Mkuu Kitila,

Maneno yako kwenye bold ndiyo yanajibu swali ambalo bado unaona kuwa halijajibiwa. Hili suala la kuwa kila anachoamua Rais ndio kinafanyika ndilo linafanya the whole thing hapa isiwe na faida yoyote kwa taifa ikiwemo CHADEMA.

Kikwete ameonyesha arrogance ya juu sana kwa kumuweka Machunde na Mama Kejo kwenye kamati/tume/usanii ambayo ndio the solution hapa katika swala la madini. Kutokana na uteuzi wa wajumbe, utaona kuwa Kikwete hana nia kabisa ya kusolve hili suala bali kuendeleza ubovu ambao Machunde na Kejo wameiletea Tz - IPTL na Buzwagi.

Nimeshasema mengi sana kuhusu Mwakyembe na Mark Bomani. Uteuzi tu wa wajumbe, unaonyesha kuwa Kikwete hana nia yoyote ya kuleta mabadiliko katika sekta ya madini - au kusahihisha makosa yote yaliyofanyika. Zitto anapojiunga na .... hii, atafungwa na hii.. na wala hatakuwa huru kusema yote ambayo ameshasema na kutueleza kuhusu kinachoendelea huko serikalini. Hii ni njia ya kumfunga mdomo Zitto na CHADEMA ili wasiendelee kuuanika wazi uozo wa serikali hii.

Kuna watu wanadai kuwa, mambo mengi sana yanafanyika kutokea ndani ya system, historia ya civil and women rights in America na duniani kote inaonyesha kabisa kuwa maamuzi makubwa ya nchini yaliletwa zaidi na confrotation na sio apeasements.

Kumbuka kuwa mimi silazimishi kuwa zitto asiingie katika hii ... hata sijui jina lake. Zitto ni independent guy na anaweza kufanya chochote atakachopenda kwa manufaa yake, ya CHADEMA, na ya Tanzania nzime. Nilichotoa mimi ni tahadhari kwa zitto kuwa akikapichuleti na kusalimu amri akasahau kulinda maslahi ya nchi kama ambavyo amekuwa anafanya all the time, basi ategemee kuwa atapata moto kutoka kwangu maana hapa hapendwi mtu wala chama bali ni maslahi ya Taifa.
 
Sababu za zitto kujitoani,
1,kamati imeundwa na baadhi ya wajumbe wasio waadilifu(ccm hawalioni ili kwa sababu wote hiyo ndiyo sera yao,pia ndio mfumo wa maisha ya watanzania waliowengi)
2,tumekuwa na kamati tano zilizopita kwa kufanya kazi hiyi hiyo na hakuna mabadiliko zaidi ya buzwagi.
3,kamati haina nguvu za kisheria zaidi ya kufuraisha mkuu wa kaya.
4,Rais amekuwa haaminiki katika maamuzi yake zaidi ya kuwalida rafiki zake na maslahi yao binafsi.
5,tatizo ni sheria ya madini, ndio kikwazo cha mabadiliko na hilo lipo wazi sasa hii kamati ni kutumbua tu pesa za walipa kodi(hasara juu ya hasara)
6,Kwa upande wa taifa ni kuwanyamazisha wanaharakati ktk kudai mabadiliko ya kweli,kwa kuwaahadaa na kamati.
 
Mkuu Kitila,

Maneno yako kwenye bold ndiyo yanajibu swali ambalo bado unaona kuwa halijajibiwa. Hili suala la kuwa kila anachoamua Rais ndio kinafanyika ndilo linafanya the whole thing hapa isiwe na faida yoyote kwa taifa ikiwemo CHADEMA.

Kikwete ameonyesha arrogance ya juu sana kwa kumuweka Machunde na Mama Kejo kwenye kamati/tume/usanii ambayo ndio the solution hapa katika swala la madini. Kutokana na uteuzi wa wajumbe, utaona kuwa Kikwete hana nia kabisa ya kusolve hili suala bali kuendeleza ubovu ambao Machunde na Kejo wameiletea Tz - IPTL na Buzwagi.

Nimeshasema mengi sana kuhusu Mwakyembe na Mark Bomani. Uteuzi tu wa wajumbe, unaonyesha kuwa Kikwete hana nia yoyote ya kuleta mabadiliko katika sekta ya madini - au kusahihisha makosa yote yaliyofanyika. Zitto anapojiunga na .... hii, atafungwa na hii.. na wala hatakuwa huru kusema yote ambayo ameshasema na kutueleza kuhusu kinachoendelea huko serikalini. Hii ni njia ya kumfunga mdomo Zitto na CHADEMA ili wasiendelee kuuanika wazi uozo wa serikali hii.

Kuna watu wanadai kuwa, mambo mengi sana yanafanyika kutokea ndani ya system, historia ya civil and women rights in America na duniani kote inaonyesha kabisa kuwa maamuzi makubwa ya nchini yaliletwa zaidi na confrotation na sio apeasements.

Kumbuka kuwa mimi silazimishi kuwa zitto asiingie katika hii ... hata sijui jina lake. Zitto ni independent guy na anaweza kufanya chochote atakachopenda kwa manufaa yake, ya CHADEMA, na ya Tanzania nzime. Nilichotoa mimi ni tahadhari kwa zitto kuwa akikapichuleti na kusalimu amri akasahau kulinda maslahi ya nchi kama ambavyo amekuwa anafanya all the time, basi ategemee kuwa atapata moto kutoka kwangu maana hapa hapendwi mtu wala chama bali ni maslahi ya Taifa.

Mambo matatu dadangu kwa post yako hii ambayo nimeifurahia sana:

i) Nakubaliana nawe kabisa kwamba tahadhari kwa Zitto ni muhimu na naamini Zitto anafahamu hili na atakuwa amejiandaa. Ninachokataa mimi ni hii dhana kwamba ukikaa nao karibu basi umekwisha kwa hiyo solution ni kujitenga. Mimi falsafa yangu ni kuwa kama wewe ni jasiri, ujasiri wake usiharibiwe eti kwa sababu umekutana na Kikwete. Kwa sababu tupende tusipende, ukishakuwa kiongozi lazima utakutana na hawa jamaa wa juu. Kwa hivyo swala hapa sio kwamba hutajaribiwa, kujaribiwa lazima kuwepo, issue ni wewe kushinda hayo majaribu. Hatuwezi kupima ujasiri wa mtu kwa kukimbia majaribu bali kwa kuyashinda hayo majaribu. Kama mnampenda Zitto acheni aingie kwenye kamati, apambana na majaribu kisha ayashinde, then ndipo ujasiri wake uweze kujipambanua.

ii) Halafu kuhusu hoja yako ya kwamba maamuzi makubwa huko America "yaliletwa na confrotation rather than apeasement", well inawezekana ni kweli. Lakini ulisoma hili jambo from a historical perspective. Obviously, all gurus in social scientists watakwambia kabisa kwamba confrostation should be the last resort na pengine is the most primitive way of dealing with a problem. Mimi naamini katika falsafa ya many fronts, one struggle. Kama kuna haja ya confrotation twende, kama kuna haja ya kui-engage katika serious debate tufanye hivyo. Mimi nadhani kwamba hili swala tulilonalo sasa linahitajo debate kwanza madamu JK bado anaonyesha haja ya kulizungumza. Ikifika wakati wa confrotation, haya twende.

iii) Credibility ya akina members wa kamati: yes, kuna serious reservations kuhusu wajumbe kibao wa kamati. Lakini waingereza wanasema "you work with the people you have". Hawa akina Mwakyembe ndio aina ya wasomi tulionao TZ. Watu wana akili sana tu lakini wanaamua kutumia akili zao kuhalalisha yasiyohalalishika! Hata hivyo, mimi naamini wazee kama akina Mark Bomani na Idd Simba ni watu credible sana tu katika jamii yetu. Unajua dunia hii inabidi uwe na some level of trust unapofanya kazi na watu. Sasa ikifika mahala tukaona watu wote kwenye system hawafai tunashida, maana ndio tulio nao lazima tufanye nao kazi.

Well, tuendelee na debate; it is getting better and better!
 
Bado wote wewe na Mwafrika wa kike hamjajibu swali langu juu athari za ushiriki wa Zitto katika hii kamati kwa nchi, CHADEMA na Zitto mwenyewe!

mzee sikuliona swali lako hapo awali;

Je kuna athari gani kwa Zitto kushiriki katika Kamati hii?

a. Zitto anaingia kwenye kamati hii akiwa na bias. Bias hii inatokana na ukweli kuwa yeye alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa mikataba ya awali na ni yeye aliyeibua suala la Buzwagi. Ni yeye ambaye alithubutu kumnyoshea kidole waziri wa Madini na Nishati na alikuwa tayari kuadhibiwa kwa "kosa" hilo. Hivyo anapoingia kwenye kamati hii, haji akiwa mtu neutral au mwenye mawazo huru (hata kama tutahakikishiwa mara mia moja). Anaingia akiwa na bias ya mikataba mizima na hivyo hataitendea haki Kamati hiyo.

b. Ni yeye ambaye alimtuhumu Waziri wa Nishati na Madini kufanya vitendo ambavyo vinashuku ya improperity katika utendaji kazi. Ni yeye aliyetoa hoja kuwa Karamagi alifanya utiaji sahihi wa mkataba wa Buzwagi kwa siri na ulifanyika sirini na alishangaa kwanini Taifa halikuambiwa. Sasa leo hii anapoingia katika Kamati ya kuchunguza mikataba hiyo ukiwemo ule alioupigia yeye kelele atakuwa huru gani kupata majibu ya kweli? Kama kutoa tuhuma kunamfanya mtu aqualify kwa position fulani kwanini basi na mtuhumiwa asiwe humo humo ili kuhakikisha anatendewa haki? Binafsi siamini anayemtuhumu mwizi basi na yeye apewe cheo polisi kwenda kuchunguza wizi ulifanyikaje! When we seek justice, justice should be done, and should be SEEN done! katika hili siamini kuwa Zitto atamtendea haki Karamagi na Buzwagi.

c. Ni kwa sababu hiyo ya (b) ndiyo maana nikajenga hoja pia kuwa Bw. Machunde (rafiki wa karibu na mwajiriwa at one point wa Karamagi) hastahili kuwemo kwenye Kamati hiyo. Mtu ambaye anajua rafiki yame ametuhumiwa mambo mengi na mazito, na mtu ambaye wakati fulani "kula" yake ilimtegemea rafiki huyo anapoingizwa katika Kamati ambayo inaweza "kumnyonga" rafiki yake basi ni lazima tufikiri kuna zaidi ya hilo kwa yeye kuwekwa humo. Lengo ni kuhakikisha rafiki yake anatendewa haki. Kwa hilo utaona mgongano mkubwa. Hivyo kama mtuhumiwa (Karamagi) hakuwekwa kwenye Kamati hiyo, basi rafiki yake asiwekwe na Mtuhumu wake asiwekwe!

d. Kama nilivyoonesha hapo juu kuwa kilichotokea kwa Zitto kukubali kuingia kwenye Kamati hii ni major compromise albeit unnecessary one. Zitto alipozungumza Bungeni hakumuomba Rais aunde Kamati ya kupitia Mikataba; na katika ziara zao mikoani hoja haikuwa Rais kakataa kuchunguza mikataba. Sasa Rais anapounda Kamati kana kwamba yeye ni Bunge kufanya kile ambacho kilitakiwa kufanywa Bungeni basi naamini ni mazingaombwe ya hali ya juu. Sasa kitendo cha Rais huyo huyo kumteua Mbunge aliyepigia kelele suala hilo Bungeni kuwa mjumbe wa Kamati sidhani kama ni cha bahati mbaya. Natofautiana kabisa na wale wanaoamini kuwa ni kitendo cha "imani ya Rais" kwa Zitto. Binafsi naliangalia suala hili from a political angle (being a political analyst)

Zitto kapigia kelele mikataba => Zitto ataka Bunge liunde Kamati Teule kuchunguza mikataba=>Bunge lakataa kuunda Kamati=> Zitto aadhibiwa kwa kusema 'uongo'=> Zitto and co. wanaenda kwa wananchi=>CCM wanatetea uamuzi wa Bunge =>Zitto na wapinzani wanapata umaarufu mkubwa kwa wananchi=> Rais anatambua kuwa CCM wametegwa anawaahidi wana CCM ataingilia kata => Wakati Bunge linaunda Kamati Teule (nyingine), Rais anaunda Kamati Isiyoteuliwa siku hiyo hiyo => Tunaambiwa Zitto na Mpinzani mwingine wako ndani => Zitto anakubali kwa furaha kuteuliwa na Rais

Sasa, kwa kuangalia mtiririko huo utaona kuwa CCM wamewapiku wapinzani. Kwa sababu kama Rais angeunda hiyo Tume bila kuwashirikisha wapinzani na hasa bila Zitto kuwemo ndani, Zitto alikuwa na haki yote ya kusema "hicho sicho nilichokijengea hoja Bungeni, na Rais amewazuga Watanzania" angekuwa amesema kweli. Sasa hivi hawezi kusema hivyo kwa sababu yumo ndani na lolote litakalotokea mbele ya safari hana budi kwenda nalo kwani.

a. Akigundua kuwa mambo hayaendi kama alivyotarajia, docs haziletwi, watu hawatoi ushirikiano au wanapoteza muda tu ili miezi mitatu ipite na akaamua baada ya mwezi mmoja hivi kusema "haridhishwi na mwelekeo wa Tume" (Kama alivyofanya Ndesamburo), hivi nani atakubali? Wananchi wanaweza kusema "ndiyo shujaa wetu" lakini Rais akija na kusema "nilimuamini Zitto na tukampa nafasi nzuri ya kufuatilia lakini naona mwenzetu hawezi kuridhishwa na ninasikitika kuwa ameamua kuweka maslahi ya chama mbele kuliko Taifa" kuna mtu atalalamika?

b. Huko mbeleni akitokea na kusema mchakato ulikuwa ni mzuri na Mkataba wa Buzwagi ulisainiwa katika hali halisi na licha ya matatizo mbalimbali ulikuwa hauna utata (hivyo akijipinga na hoja yake mwenyewe) hivi ataonekana vipi mbele ya umma?

So, binafsi hoja yangu za msingi ni hizo na athari zake ni hizo. Next question please!!
 
kilitime,kitila,shalom,asha abdala,

1.Tume ya Dr.Kipokola ilitoa mapendekezo gani? Je, serikali imetekeleza mapendekezo hayo?

2.Tume ya Bomani ina jukumu gani tofauti na Tume ya Dr.Kipokola? Kamati ya Laurian Masha ilikuwa na wajumbe gani, na majukumu yake yalikuwa ni yapi?

3.Wawekezaji wameishakataa kubadili masharti ya mikataba yao. Kwa mtizamo wangu Raisi anatafuta njia ya kusalimu amri kwa wawekezaji.

4.Kama Raisi angekuwa anataka mabadiliko ya kweli basi angemteua Tundu Lissu kwenye hiyo kamati. Zitto hana ujuzi na uzoefu ktk masuala ya madini na mikataba kulinganisha na Lissu.

5.Hili suala ni muhimu sana kwa maslahi ya taifa letu. Nilitegemea Raisi atakusanya the best brains ktk masuala ya madini na mikataba, badala yake ameteua watu ambao ujuzi na uadilifu wao unatia mashaka.

6.Nakumbuka wakati wa Tume ya Prof.Wangwe Zitto alianza kubabaika na kusema mambo ya ajabu ajabu, nategemea this time atatulia na kuwa makini zaidi.
 
Mambo matatu dadangu kwa post yako hii ambayo nimeifurahia sana:

i) Nakubaliana nawe kabisa kwamba tahadhari kwa Zitto ni muhimu na naamini Zitto anafahamu hili na atakuwa amejiandaa. Ninachokataa mimi ni hii dhana kwamba ukikaa nao karibu basi umekwisha kwa hiyo solution ni kujitenga. Mimi falsafa yangu ni kuwa kama wewe ni jasiri, ujasiri wake usiharibiwe eti kwa sababu umekutana na Kikwete. Kwa sababu tupende tusipende, ukishakuwa kiongozi lazima utakutana na hawa jamaa wa juu. Kwa hivyo swala hapa sio kwamba hutajaribiwa, kujaribiwa lazima kuwepo, issue ni wewe kushinda hayo majaribu. Hatuwezi kupima ujasiri wa mtu kwa kukimbia majaribu bali kwa kuyashinda hayo majaribu. Kama mnampenda Zitto acheni aingie kwenye kamati, apambana na majaribu kisha ayashinde, then ndipo ujasiri wake uweze kujipambanua.

ii) Halafu kuhusu hoja yako ya kwamba maamuzi makubwa huko America "yaliletwa na confrotation rather than apeasement", well inawezekana ni kweli. Lakini ulisoma hili jambo from a historical perspective. Obviously, all gurus in social scientists watakwambia kabisa kwamba confrostation should be the last resort na pengine is the most primitive way of dealing with a problem. Mimi naamini katika falsafa ya many fronts, one struggle. Kama kuna haja ya confrotation twende, kama kuna haja ya kui-engage katika serious debate tufanye hivyo. Mimi nadhani kwamba hili swala tulilonalo sasa linahitajo debate kwanza madamu JK bado anaonyesha haja ya kulizungumza. Ikifika wakati wa confrotation, haya twende.

iii) Credibility ya akina members wa kamati: yes, kuna serious reservations kuhusu wajumbe kibao wa kamati. Lakini waingereza wanasema "you work with the people you have". Hawa akina Mwakyembe ndio aina ya wasomi tulionao TZ. Watu wana akili sana tu lakini wanaamua kutumia akili zao kuhalalisha yasiyohalalishika! Hata hivyo, mimi naamini wazee kama akina Mark Bomani na Idd Simba ni watu credible sana tu katika jamii yetu. Unajua dunia hii inabidi uwe na some level of trust unapofanya kazi na watu. Sasa ikifika mahala tukaona watu wote kwenye system hawafai tunashida, maana ndio tulio nao lazima tufanye nao kazi.

Well, tuendelee na debate; it is getting better and better!

Asante sana Kitila,

Inafurahisha sana kuwa hii debate kati yetu (tuliotakiwa kuwa wapinzani wa ccm) inaendelea na kuonyesha haja ya kuwa na mawazo ya kupingana ili kujenga taifa bora.

Uliyosema ni kweli kabisa, inahitaji many fronts na ukweli kuwa confrotations inabidi iwe last resorts. Kitila, nimesoma hapa kuwa wewe umekuwa rais wa DARUSO. Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa katika miaka yenu, pesa ya boom ilikuwa inaweza kucheleweshwa kwa wiki hata mbili kwa madai kuwa hakuna pesa lakini wanafunzi wakigoma au kutishia kugoma - jioni hiyo hiyo wanapata pesa (sijui huwa zinachapishwa mpya au vipi).

Kuna mtu aliwahi kuwa anakuongelea kwenye bash moja hapa akasema kuhusu speech yako ya Maandamano sio Gwaride - ambapo wanafunzi walitishia kugoma kuwa pesa zimechelewa na jioni yake wakapata pesa toka wizarani (zilitoka wapi - sijui).

Serikali kwa miaka mingi sana imebembelezwa kuhusu suala la madini. Yaliyotokea Bulyanhulu wote tunayajua. Yaliyotokea kwa wachimba madini wa buhemba na tarime wote tunayajua. Kina Lissu wamepiga kelele for years wameshindwa na jamaa wanazidi kuleta richmonduli, and the company.

Nakubaliana na wewe kuwa ni vyema zitto akaingia ndani ya hii tume au kamati au ?, nitakusubiri hapa JF (MUNGU akipenda) kwa miezi mitatu kisha kwa maneno yako uniambie kuwa Taifa limefaidika na nini au litegemee nini kutoka kwa .... hiyo!
 
b.
So, binafsi hoja yangu za msingi ni hizo na athari zake ni hizo. Next question please!!

No more question for now. You have brilliantly answered part of my question. But then, I dont see how Zitto is biased because in the parliament he was trying to find out the truth about the Buzwagi contract. Part of this committee's ToRs is to seek the truth about the Buzwagi and other contracts. Sasa mimi hapo sioni kabisa Zitto anakuwa biased kabisa. Anyway, hoja zako nimezielewa sana hata kama sikubaliani nazo!
 
JokaKuu:

Hili ndilo nalikataa mimi la kufikiri kwamba Tundu pekee ndio mwenye kujua matatizo na solutions za madini Tanzania. With due respect to him, he is not a panacea to our mining problems jamani. In any case, Mark Bomani is senior to him professionally by far. Ndugu, yangu wanaovuma majini zaidi ni papa, lakini haina maana kwamba hakuna viumbe wengine humo! Lets trust people wanaopewa kazi, wakishindwa tuwahoji. BTW yeye angeteuliwaje kwenye kamati wakati hataki kamati iwepo in the first place?
 
Asante sana Kitila,

Uliyosema ni kweli kabisa, inahitaji many fronts na ukweli kuwa confrotations inabidi iwe last resorts. Kitila, nimesoma hapa kuwa wewe umekuwa rais wa DARUSO. Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa katika miaka yenu, pesa ya boom ilikuwa inaweza kucheleweshwa kwa wiki hata mbili kwa madai kuwa hakuna pesa lakini wanafunzi wakigoma au kutishia kugoma - jioni hiyo hiyo wanapata pesa (sijui huwa zinachapishwa mpya au vipi).

Kuna mtu aliwahi kuwa anakuongelea kwenye bash moja hapa akasema kuhusu speech yako ya Maandamano sio Gwaride - ambapo wanafunzi walitishia kugoma kuwa pesa zimechelewa na jioni yake wakapata pesa toka wizarani (zilitoka wapi - sijui).

Wewe dadangu unataka nivunje moja ya miiko yangu muhimu: huwa sipendi kujijadili. Hata hivyo ili nikujibu inabidi. Ni kweli nikiwa kiongozi wa Daruso mimi niliongoza migomo na hata maandamano pale ilipobidi. Lakini siku zote nilithamini zaidi nguvu ya hoja, pale iliposhindikana ndipo nikatumia hayo maandamano. Na ndio nasema hakuna haja ya kuwakwepa hawa jamaa. Mimi siku zote nilikaa na hawa waheshimiwa wote wazito akiwemo mkuu wa nchi wakati huo, tukacheka, tukala, tukanywa; lakini ilipokuja kwenye swala la maslahi ya wanafunzi, ambayo ndiyo ilikuwa constituency yangu, nilikuwa mkali na very serious, na walinijua hivyo. Mwanzoni nilipewa majina yote, kuna kipindi wanafunzi wakafikiri nimenunuliwa, na kuna kipindi wakubwa wakafikiri mimi ninakitu fulani kinachonifanya nisiogope. Lakini nashukuru Mungu at the end of the day, wote walinielewa (students na watawala)kwamba I was just princpled. Kama wanafunzi tulikuwa tumekosea nawaambia hapa tupo wrong, na watawala hivyohivyo. Kwa hiyo kuna kipindi nilianzisha na nikaongoza migomo na kuna kipindi niliwakatalia wanafunzi katakata kufanya mgomo pale nilipoona hapakuwa na haja ya huo mgomo.

The bottom line: As a leader, you must always heed to your convictions and the core business that put in the position you are. Not always what the majority say is correct. In fact in leadership the only time the majority are absolutely correct is during elections. Otherwise, most of the time, people's opinion is flawed simply because they do not have the necessary information to inform their opinion. That is why even in this Zitto's saga we are fumbling around for the simple reason that we do not have much information about the issue as JK, including as you correctly pointed out: ToRs, etc.
 
No more question for now. You have brilliantly answered part of my question. But then, I dont see how Zitto is biased because in the parliament he was trying to find out the truth about the Buzwagi contract. Part of this committee's ToRs is to seek the truth about the Buzwagi and other contracts. Sasa mimi hapo sioni kabisa Zitto anakuwa biased kabisa. Anyway, hoja zako nimezielewa sana hata kama sikubaliani nazo!

Kitila ukweli haupatikani kwa ridhaa kama ambavyo Kamati ya Rais inataka tuamini kuwa kwa vile ni Kamati ya Rais basi ukweli utajulikana. Ukweli na haki hutafutwa kwa kulazimisha ukweli. Unafanya hivyo ukiwa na nguvu ya kisheria, uwezo wa kucross examine, tishio la adhabu n.k Sasa hivi Kamati hii haina uwezo wa kupata ukweli ila ina hamu ya kuambiwa ukweli. Hakuna mtu anayelazimika kwenda kwenye kamati hii ya Rais hata akiitwa!

Bias ya Zitto ni kuwa mikataba ni mibovu na Waziri hakusema ukweli Bungeni kuhusu Buzwagi na kwa hilo alikuwa tayari kuadhibiwa. He is not a neutral party in this.
 
Wewe dadangu unataka nivunje moja ya miiko yangu muhimu: huwa sipendi kujijadili. Hata hivyo ili nikujibu inabidi. Ni kweli nikiwa kiongozi wa Daruso mimi niliongoza migomo na hata maandamano pale ilipobidi. Lakini siku zote nilithamini zaidi nguvu ya hoja, pale iliposhindikana ndipo nikatumia hayo maandamano. Na ndio nasema hakuna haja ya kuwakwepa hawa jamaa. Mimi siku zote nilikaa na hawa waheshimiwa wote wazito akiwemo mkuu wa nchi wakati huo, tukacheka, tukala, tukanywa; lakini ilipokuja kwenye swala la maslahi ya wanafunzi, ambayo ndiyo ilikuwa constituency yangu, nilikuwa mkali na very serious, na walinijua hivyo. Mwanzoni nilipewa majina yote, kuna kipindi wanafunzi wakafikiri nimenunuliwa, na kuna kipindi wakubwa wakafikiri mimi ninakitu fulani kinachonifanya nisiogope. Lakini nashukuru Mungu at the end of the day, wote walinielewa (students na watawala)kwamba I was just princpled. Kama wanafunzi tulikuwa tumekosea nawaambia hapa tupo wrong, na watawala hivyohivyo. Kwa hiyo kuna kipindi nilianzisha na nikaongoza migomo na kuna kipindi niliwakatalia wanafunzi katakata kufanya mgomo pale nilipoona hapakuwa na haja ya huo mgomo.

The bottom line: As a leader, you must always heed to your convictions and the core business that put in the position you are. Not always what the majority say is correct. In fact in leadership the only time the majority are correct is during elections. Otherwise, most of the time, people's opinion is flawed simply because they do not have the necessary information to inform their opinion. That is why even in this Zitto's saga we are fumbling around for the simple reason that we do not have much information about the issue as JK, including as you correctly pointed out: ToRs, etc.

point nzuri sana hiyo Kitila, ndio maana mimi sipingi Zitto kuwemo humo kwa sababu "anachanganyika na mafisadi". Hiyo siyo hoja ya msingi kwani hata yule mwana wa Mariamu alikula na kunywa na wenye dhambi bila yeye mwenyewe kuwa mwenye dhambi; na ni yeye aliyesema "mwenye afya haitaji tabibu, bali aliye mgonjwa"... Watawala ni watawala wetu na hatuna budi kuzungumza nao, hatuwezi kuwakimbia na hatutawaziria nchi.
 
Yeah, tena hiyo mifano safi sana. Kuna watu wameng'ang'ania kwamba Zitto atalewa, nafikiri hiyo sio hoja maana mpaka hapo alipo kwa yeye kuwa mbunge anakutana na watu wa kila aina na kila mara.
 
Wewe dadangu unataka nivunje moja ya miiko yangu muhimu: huwa sipendi kujijadili. Hata hivyo ili nikujibu inabidi. Ni kweli nikiwa kiongozi wa Daruso mimi niliongoza migomo na hata maandamano pale ilipobidi. Lakini siku zote nilithamini zaidi nguvu ya hoja, pale iliposhindikana ndipo nikatumia hayo maandamano. Na ndio nasema hakuna haja ya kuwakwepa hawa jamaa. Mimi siku zote nilikaa na hawa waheshimiwa wote wazito akiwemo mkuu wa nchi wakati huo, tukacheka, tukala, tukanywa; lakini ilipokuja kwenye swala la maslahi ya wanafunzi, ambayo ndiyo ilikuwa constituency yangu, nilikuwa mkali na very serious, na walinijua hivyo. Mwanzoni nilipewa majina yote, kuna kipindi wanafunzi wakafikiri nimenunuliwa, na kuna kipindi wakubwa wakafikiri mimi ninakitu fulani kinachonifanya nisiogope. Lakini nashukuru Mungu at the end of the day, wote walinielewa (students na watawala)kwamba I was just princpled. Kama wanafunzi tulikuwa tumekosea nawaambia hapa tupo wrong, na watawala hivyohivyo. Kwa hiyo kuna kipindi nilianzisha na nikaongoza migomo na kuna kipindi niliwakatalia wanafunzi katakata kufanya mgomo pale nilipoona hapakuwa na haja ya huo mgomo.

The bottom line: As a leader, you must always heed to your convictions and the core business that put in the position you are. Not always what the majority say is correct. In fact in leadership the only time the majority are absolutely correct is during elections. Otherwise, most of the time, people's opinion is flawed simply because they do not have the necessary information to inform their opinion. That is why even in this Zitto's saga we are fumbling around for the simple reason that we do not have much information about the issue as JK, including as you correctly pointed out: ToRs, etc.

Kitila asante sana kwa majibu mazuri.

Naomba pia ieleweke kuwa sikuwa na nia ya kutaka ujijadili maana hili ulishaliweka hapa. Nili-quote speech ya maandamano si gwaride hapa maana hii ni one of your best moments ambapo ulifanikiwa kuzuia mgomo na maandamano lakini pia wanafunzi nao wakapata walichotaka.

Kuna wakati principle ya maandamano sio gwaride inafanya kazi esp pale ambapo side nyingine inagundua kuwa haina nguvu zaidi ya kushindana. Katika hili nakubaliana nawe na namtakia Zitto kila la heri. Natumai kuwa yote yatakuwa kwa manufaa ya nchi na kuwa baada ya miezi 3 tutakuwa na stori tofauti hapa JF.

Kitila, always heshima kwako na naomba nieleweke kuwa hii debate ya ndani ya CHADEMA ni kitu kizuri na nafurahi kuona kuwa Mnyika alikubali kuwa atafanyia kazi maoni yangu na wengine ambao wako upande mwingine wa hii issue.

Kwa sasa, kama nilivyosema kule kwenye thread nyingine. Mimi sina uwezo wa kumuamulia Zitto cha kufanya, na as longer as CHADEMA sio CCM na watu wana uwezo wa kutoa maoni yao na kufanya wapendavyo, nakubaliana nawe kuwa ni vyema zitto kuingia huko na nategemea kuwa kutakuwa na mwisho mema katika hili.
 
Zitto sasa kama 'upupu' CHADEMA

Habari Zinazoshabihiana
• Hiza, Akwilombe watumika kummaliza Zitto 27.09.2007 [Soma]
• Polisi yachunguza kauli za Mbowe, Kabwe 07.09.2007 [Soma]
• CHADEMA wafadhaishwa na sakata la Kabwe, Amina 11.05.2007 [Soma]

*Kamati Kuu yatabiriwa 'kutofua nazi' Jumamosi
*Akigawa chama katika makundi na aitwa 'fisadi'

Na Mwandishi Wetu

KAMATI Kuu ya CHADEMA ambayo inatarajiwa kukutana Jumamosi ijayo kujadili pamoja na mambo mengine ushiriki wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, katika Kamati ya Kuangalia Upya Mikataba ya Madini nchini, inaweza isibadili msimamo wa Mbunge huyo, imebainika.

Hatua hiyo inatokana na mbunge huyo kusimamia upande wa kutetea maslahi ya Taifa na si yake binafsi, hali ambayo imesababisha mtafaruku ndani ya chama chake na kuzaa kambi mbili, moja ikitetea msimamo wake na nyingine ikiupinga.

Habari zilizopatikana ndani ya chama hicho jana, zilisema wakati muasisi wa chama hicho, Bw. Edwin Mtei, akimtetea Bw. Zitto kuendelea kushiriki ndani ya Kamati hiyo, Mbunge wa Tarime, Bw. Chacha Wangwe, anaonekana kukereka.

"Kibaya zaidi hata kama mlivyoona jana kwenye magazeti sasa Wangwe anahisi kuwa Bw. Zitto amepewa 'kitu kidogo' na CCM ili akubali kuwa ndani ya Kamati hiyo...kosa ni nini kama ndicho tulikuwa tukikipigia kelele hata bungeni?," alihoji Bw. Mathayo Lazaro aliyejitambulisha kuwa mwanachama wa CHADEMA.

Alisema yatakuwa ni maajabu kwa Bw. Zitto kujitoa katika Kamati hiyo wakati ndiye aliyewasilisha hoja binafsi kuhusiana na mikataba ya madini na kuibua suala la Buzwagi.

Ndani ya CHADEMA tayari kuna hisia kuwa CCM ina mpango wa kukisambaratisha chama hicho na ndiyo sababu Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, akamwingiza Bw. Zitto katika Kamati hiyo na yeye kukubali na kumpongeza Rais.

Hatua hiyo ilisababisha hasira miongoni mwa viongozi na wanachama wa CHADEMA ambao walieleza kushangazwa kwao na Bw. Zitto kumsifia na kumpongeza kiongozi wa chama tawala.

Akisisitiza msimamo wake wa kutaka kuona Bw. Zitto akiendelea kubaki ndani ya Kamati hiyo, Bw. Mtei alikaririwa akisema hiyo ni fursa nzuri kwa chama chake kufikisha maoni na msimamo wake serikalini.

Watu wa karibu na Bw. Zitto wanaofahamu msimamo wake, walisema Kamati Kuu ya CHADEMA katika kikao chake cha Jumamosi isipokuwa makini itakuwa imemegua jiwe moja muhimu katika msingi wake.

"Inaonekana Zitto hawamwelewi vizuri ni mtu mwenye msimamo na mbishi constructively (enye manufaa), hawezi kusimamia katika ubishi wa kijinufaisha binafsi, ingawa anaweza kutumiwa na wengine kujinufaisha,wasipomwelewa kama anavyoamini yeye watamkosa," alisema mwana CHADEMA mwandamizi ambaye hakutaka atajwe gazetini.

"Tayari tunaona hivi sasa anahusishwa na ufisadi, huyu ni yule ambaye baada ya kusimamishwa kazi bungeni, alipitishwa mikoani kama Mwenge wa Uhuru...leo anapewa nafasi nzuri ya kulitetea Taifa, anaanza kusakamwa eti kanunuliwa, mbona hatutaeleweka wana CHADEMA?," alihoji mwanachama huyo.

Baadhi ya wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanasema ingekuwa bora kama CHADEMA ingelichukulia suala hili kwa umakini mzuri kwani kumbadilisha Bw. Zitto kunaweza kusababisha mgawanyiko mkubwa na hata chama hicho kumeguka.

"Mambo ya siasa huanza hivi hivi, huwezi kujua, mbunge huyu machachari wa CHADEMA anaangalia wapi na ana hisia zipi ndani ya chama chake, alikuwapo Dkt. Walid Kabourou, akiwa na wafuasi wengi tena Kigoma, yuko wapi sasa? Na huyu ni wa huko huko!

"Tumesikia, wazee wa Kigoma wao wanataka aendelee kubaki ndani ya Kamati, sasa hicho kikao cha Jumamosi kitasaidia nini? Kama si cha kubadili msimamo wa Bw. Zitto, sawa kifanyike, lakini kama ni kinyume chake, hatudhani kama Zitto atakubali kuwa kinyonga kwa hili," alisema Bw. Elibariki Ulotu, aliyejitambulisha kuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Wakati huo huo, Reuben Kagaruki, anaripoti kwamba
Mwenyekiti wa TLP, Bw. Augustino Mrema, amesema hatua ya Rais Kikwete kumteua Bw. Zitto kwenye Kamati huyo kunalenga kuwagombanisha katika umoja wao.

"Kamati aliyounda Rais Kikwete ni ya 'magrini' itatufanya tugombane na kutugawa bure."

Bw. Mrema alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na gazeti hili kwa simu alipoombwa atoe maoni yake kuhusiana na hatua ya Rais Kikwete kumteua mbunge huyo kuwa katika Kamati hiyo.

Bw. Mrema alisema hawezi kumzungumzia, lakini anajua wazi kuwa Kamati hiyo haiwezi kufanya chochote.

Alisema yeye aliwahi kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani hivyo anafahamu mambo mengi.

"Tulipopata misukosuko tulikuwa tunatafuta mbinu za kuzima moto kwa lengo la kuwapoza wananchi, ili jambo lisogezwe mbele," alidai Bw. Mrema.

Alisema mbinu hiyo ndiyo anayotumia Rais Kikwete kumteua Bw.Zitto katika katika Kamati hiyo. Alitolea mfano Tume nyingi zilizoundwa baada ya Serikali kupata misukosuso lakini baada ya mambo kupoa, hakuna hatua zilizochukuliwa.

Alitaja baadhi ya tume hizo kuwa ni pamoja na ya Jaji Nyalali,ya Jaji Warioba na ya Jaji Kisanga. Alisema mbali na tume hizo, zipo tano zilizoundwa kwa ajili ya kushughulia mambo ya madini, lakini hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.

Alisema kamati hiyo haiwezi kubadili chochote kwenye mikataba ya madini kwani mingi iliyosainiwa ni ya muda mrefu. "Mikataba ambayo Serikali imesaini ni ya miaka mingi hatuwezi kuibadili kwa sasa, labda Yesu arudi," alisema Bw. Mrema.

Alisema endapo Rais Kikwete atachukua hatua ya kuvunja mikataba iliyosainiwa, wahusika wanaweza kushitaki kwenye Mahakama ya Kimataifa na kuifanya Tanzania ikumbwe na yale yanayotokea Zimbabwe.

Bw. Mrema alisema kama Rais Kikwete anataka kutunga sheria ya mikataba ya madini hilo ni jambo rahisi. "Ni kiasi cha kuweka sheria kuwa mwekezaji akija atapata asilimia 49 na sisi (Watanzania) tutapata 51 ya mapato hakuna haja ya kuunda kamati," alisema Bw. Mrema na kuongeza kuwa kuunda kamati za aina hiyo, ni sawa na kuwachezea Watanzania.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom