elimukwanza
Senior Member
- Dec 27, 2010
- 168
- 23
- Thread starter
- #21
hizo ni hadithi tu,watanzania wanahitaji huduma za jamii siyo CDMMkuu, unachanganya mambo. Wanafunzi wa vyuo vikuu wenyewe ndiyo waliwaalika viongozi wa Chadema kwenye kongamano lao wawahutubie. Chadema inaungwa mkono sana na wanafunzi wa vyuo, wasomi, wafanyakazi na watu wengine walioelimika. Hii ni kutokana na kuwa elimu yao imewafanya waweze kuchambua hoja za Chadema na kuzielewa na kuzikubali. Elimu yao pia imebaini kuwa CCM wametawala nchi hii kwa nusu karne (miaka 50) na kushindwa kuleta maendeleo hivyo ni muda sasa wa kuleta mabadiliko.
CCM bado inaendelea kuungwa mkono na baadhi ya wananchi wa vijijini kutokana na elimu yao duni. CCM wanatumia ujinga wa wananchi wake kuendelea kuwatawala kwa kuwatisha wasilinde kura vituoni, waogope wapinzani kuwa wataipeleka nchi iwe kama Rwanda au Somalia na wajigambe kuwa CCM ndiyo chama pekee cha kuleta amani na utilivu.
Kadri elimu inavyozidi kusambaa ndiyo jinsi CCM inavyozidi kuporomoka madarakani, watoto wa sasa wa primary na sekondari wakifikia umri wa kupiga kura 2015 wakaungana na wenzao wa vyuo ni kiama zaidi kwa CCM.