CHADEMA kuzindua kampeni Arumeru Jumamosi kwa maandamano makubwa.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Meneja kampeni wa Mgombea ubunge Jimbo la Arumeru kwa tiketi ya Chadema Vicent Nyerere amesema CHADEMA wanatarajia kuzindua kampeni zao rasmi Jumamosi asubuhi ambazo zitazinduliwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Alisema kuwa uzinduzi huo utakwenda sambamba na maandamano makubwa yatakayotokea Arusha mengine yatatoka KIA na yote yatakutana eneo la Usa River katika viwanja vya eneo la mkutano.

“Mkutano huo utazinduliwa kwa kishindo kwa helkopta, magari, baiskeli na pikipiki, vyote vikiwa vinapeperusha bendera za Chadema, hivyo nawaomba wapenzi wa Chadema wafike eneo husika mapema kushuhudia uzinduzi huo,” alisema Nyerere.Alisema kutokana na maandalizi waliyofanya na jinsi chama chake kinavyoungwa mkono jimbo hilo wanatarajiwa yatakuwa ni maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa katika mkoa wa Arusha.

Nyerere alisema kuwa Chama chao kitafuata taratibu zote za sheria ya maandamano kwa kuelekeza wafuasi wao kutii amri ya barabarani kwa kutembea upande mmoja wa barabara na kuyaachia magari kupita na kumaliza mikutano yao kwa wakati uliopangwa wa kumalizika kwa kampeni za uchaguzi.

Source:Nipashe
 
Hivi Feasibility study mataokeo yake yakoje? Tunaomba mrejesho!
 
Safi makamanda tupo pamoja katika mapambano ya kumng'oa mkoloni mweusi CCM katika jimbo la Arumeru Mashariki.
 
Na ccm wanazindua lini ?

Wanazindua siku hiyo hiyo ya Jumamosi. Baada ya kuona watu wengi sana watahudhuria uzinduzi wa CHADEMA, wakaona bora wakazindulie Tengeru pale sokoni, siku ambayo ni siku ya Gulio. Wamecheza alama za nyakati
 
Baada ya hapo ni kata ya Kirumba (Mwanza).Magamba Walituwekea vipingamizi,wanadhimu tukavunja.
Peeeeeeeeeooooooooooooopppppppppleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee......................................power.
 
Mkuu Helkopta itakuwa inapita angani kutoa saluti kwa makamanda chini
 
Baada ya hapo ni kata ya Kirumba (Mwanza).Magamba Walituwekea vipingamizi,wanadhimu tukavunja.
Peeeeeeeeeooooooooooooopppppppppleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee......................................power.

Mkuu mmepangua mapingamizi yote
 
Meneja kampeni wa Mgombea ubunge Jimbo la Arumeru kwa tiketi ya Chadema Vicent Nyerere amesema CHADEMA wanatarajia kuzindua kampeni zao rasmi Jumamosi asubuhi ambazo zitazinduliwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.Alisema kuwa uzinduzi huo utakwenda sambamba na maandamano makubwa yatakayotokea Arusha mengine yatatoka KIA na yote yatakutana eneo la Usa River katika viwanja vya eneo la mkutano.

"Mkutano huo utazinduliwa kwa kishindo kwa helkopta, magari, baiskeli na pikipiki, vyote vikiwa vinapeperusha bendera za Chadema, hivyo nawaomba wapenzi wa Chadema wafike eneo husika mapema kushuhudia uzinduzi huo," alisema Nyerere.Alisema kutokana na maandalizi waliyofanya na jinsi chama chake kinavyoungwa mkono jimbo hilo wanatarajiwa yatakuwa ni maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa katika mkoa wa Arusha.

Nyerere alisema kuwa Chama chao kitafuata taratibu zote za sheria ya maandamano kwa kuelekeza wafuasi wao kutii amri ya barabarani kwa kutembea upande mmoja wa barabara na kuyaachia magari kupita na kumaliza mikutano yao kwa wakati uliopangwa wa kumalizika kwa kampeni za uchaguzi.

Source:Nipashe

Kamanda naomba weka wazi kama kweli wewe ni John Mrema
 
Mwenye taarifa kamili atujuze kwani nimechizika kinoma chalii angu,japo nipo arusha ila sijajua uzinduzi wa kampeni arumeru mashariki ni lini.
 
wakati huo huo Magamba wao watafanyia kwenye soko la tengeru ili kujaribu kuonyesha umma kuwa wao wana kubalika kulliko CDM ikumbukwe Jmosi ni siku ya soko hapo Tengeru lakini ninaamini tutawafunka na hatutakuwa na magari ya kusomba watu.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom