CHADEMA kuweni makini sana, kilicho nyuma ya pazia hiki hapa!

nenda tena hapo kwenye ka kijiwe kisha uwaulize hao wanywaji wenzao juu ya mahali walipo wale vijana waliomkamata maige mwaka jana pale kibo palace akipokea pesa toka kwa wale jamaa wa vitalu akabanwa na kuulizwa na nani amemtuma kisha akutoboa na kueleza siri nzito juu ya biashara za mkuu wa nchi....wakikujibu waulize tena juu ya watu sita waliopelekwa bulgaria..wamekwenda kufanya nini na kwa nini kinaitwa kikosi maalumu kwa ajili ya kuidhibiti chadema kabla ya 2015??

wakiwa na majibu hayo basi nami ntakuja nijiunge

Unajifaragua tu, kama unajua chochote weka hapa. Tena nahisi we ndio Hutaki Unaacha unaetaka kuilewesha CDM kwa sifa za kijinga ili wajisahau!

Hakuna mkakati hapo. Bilal abadilishe mambo?, upuuzi mtupu.
 
Utaki unaacha karibu sana. Kupitia threads zako watu wameweza kujua nani ni nani na ananguvu kiasi gani katika siasa za nchi hii na hata system ilivyo na inavyofanya kazi. Karibu sana, but remember we are heartily longing to read your part 3.
 
Watanzania wa leo hawataki kusikia ya State Department, sijui private candidate atakayehongwa na kufanyiwa kampeni na fisadiz. Watanzania wanalilia ukombozi wa pili na wanajua huo ukombozi utaletwa na watanzania wenyewe. Hakuna mtu wa kusaliti demokrasia kama watanzania wakitaka huo ukombozi, na ninaamini wamechoka kulaghaiwa. Maisha yanakuwa magumu kila kukicha, sidhani 2015 watanzania watakubali kuchezewa maisha na uhuru wao.

Mambo aliyoongea Hutaki Unaacha yaweza kuwa strategies za hao wanaoamini kuwa Tanzania ni yao, but wenye mali wenyewe (WATANZANIA) hawatakubali hilo kutokea hata kama ni kwa mishale na mapanga. Wanahitaji UKOMBOZI WA KWELI.
 


ntantoka nje ya mada kidogo ili kukusaidia..hili ulikuwa unalijua?


Mkapa hakuwa mtu wa JK tokea mwanzo. Lakini pia Mkapa hakuwa na chaguo lolote la wazi. Je ni Kwanini? Ni kwasababu, Nyerere miaka yote amekuwa anamtaka Salim kuwa Rais. Nyerere aliposhindwa kuamsha tena jina hilo chini kwa chini mwaka 1995, Mkapa ndiye akawa "his fallback position" (yani kwa Nyerere). Kwahiyo Mkapa kumbeba mtu mwingine nje ya yule ambae Nyerere alimpenda, ingekuwa kama usaliti kwa mtandao wa Nyerere. Lakini chini kwa chini, Mkapa alimtaka Hassy Kitine kumpokea mwaka 2005. Alianza kwa kuunda nafasi mpya kabisa tangia uhuru ya Uwaziri wa nchi utawala bora (Usalaam wa taifa), na kumfanya kitine kuwa waziri wa kwanza, ili ajijengee mazingira ya 2005. Lakini kina ENL, RO,
waliligundua hili mapema sana na hivyo kummaliza Kitine bungeni kwa kashfa ya kutumia dola elf 60 kwa ajili ya matibabu ya mkewe Canada. Baada ya hayo, Mkapa alibakia anaelea, asijue la kufanya. Isitoshe, hata mabalozi wa
Marekani, Uingereza, na nchi nyingine kubwa walikuwa wanamuonya sana Mkapa kwamba Kikwete hafai, ataingiza nchi katika matatizo.


Mwaka 2005, mkakati wa mkapa inasemekana ulikuwa ni kuwatosa wagombea wote ambao walikuwa na nguvu kubwa kwenye jamii, ili kuepuka mfarakano iwapo kundi moja litaonekana limeonewa. Kwa mfano, Sumaye
alikuwa na kundi kubwa la wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, na viongozi wengi wa halmashauri za wilaya. Malecela alikuwa na kundi kubwa sana viongozi wa CCM kitaifa, lakini pia wenyeviti na makatibu wa CCM mikoa
na wilaya. Kikwete alikuwa na kundi kubwa sana la viongozi wa kitaifa wa UVCCM, UWT kutokea mwaka 1995 hadi 2005, huku akidokoa dokoa wengine wengi kutoka katika makundi hayo hapo juu. Mikakati ya Mkapa
ikaingia dosari pale ENL, JK, RA, walipotoa msimamo kwamba iwapo Kikwete atatoswa, watahamia Chadema. Ndipo Mkapa akaunda timu ya kutembea nchi nzima kutafiti hilo, chini ya Absom, ambae whether ni kutonana na utafiti wa kweli au uliokwisha andaliwa mapema na kina EL, RA, akamletea taarifa Mkapa kwamba Kikwete akiachwa, CCM itapasuka, na nchi
itaingia katika machafuko. Huu ndio ukawa mwanzo wa Mkapa kulibeba jina la Kikwete kwa mtindo wa kura moja badala ya tatu Dodoma.

hivi unaijua tanzania unayodai ni nchi yako?!! ulikuwa unajua kuwa mkapa alimtka hans kitine amrith?

Mkuu mwisho wa yote Mkapa aliunda kamati ya kumshauri ikiwa na mkuu wa usalama wa taifa, mkuu wa majeshi na mkuu wa polisi. Kamati ilikubaliana kuwa kikwete hafai na wakati wanajiandaa kumpelekea mkapa taarifa JK na Lowasa walizinyaka taarifa hivyo wakamuweka sawa mkuu wa usalama wa taifa ambaye alikuwa mwenyekiti basi akapeleka mawazo siyo yaani kikwete anafaa kulingana na situation mkapa akuwa na jinsi. Hii ndi tanzania. Habari ya leo hii mimi naona kuna harufu ya ukweli kwanza Mbowe kukutana na JK, pili-ritz alikoment thread moja kuwa CCM wanatumia kigezo cha dini kuwachanganya chadema, tatu JK kusisitiza suala la mgombe binafsi mwanzoni nilihisi anamlenga Lowasa na kuna uwezekano Membe amelifahamu hili ndio maana anabook mapema CDM. Hofu yangu kama mataifa kama marekani wanaingilia inamaana hata Mossad wamo kwahiyo chadema wawe makini. nitafanya jitihada kuconfirm hizi habari kwa watu wangu wa karibu. Chadema hii habari ipeni nafasi.
 
Thread hii naiona ni mpango mkakati wa TISS kuipasua Chadema. Kumbukeni kauli ya Wasira kuwa Chadema itaparaganyika kabla ya 2015. Uzi umekaa kimtego saaana,someni kati kati ya mistari. Mimi sijainunua lakini siachi kwani naiona sumu iliyomwagwa itaingia mpaka kwenye uboho na itakuwa ngumu kuiondoa. Du TISS ni janga la nchi hii badala ya kuwa usalama wake.
 
Mkuu mwisho wa yote Mkapa aliunda kamati ya kumshauri ikiwa na mkuu wa usalama wa taifa, mkuu wa majeshi na mkuu wa polisi. Kamati ilikubaliana kuwa kikwete hafai na wakati wanajiandaa kumpelekea mkapa taarifa JK na Lowasa walizinyaka taarifa hivyo wakamuweka sawa mkuu wa usalama wa taifa ambaye alikuwa mwenyekiti basi akapeleka mawazo siyo yaani kikwete anafaa kulingana na situation mkapa akuwa na jinsi. Hii ndi tanzania. Habari ya leo hii mimi naona kuna harufu ya ukweli kwanza Mbowe kukutana na JK, pili-ritz alikoment thread moja kuwa CCM wanatumia kigezo cha dini kuwachanganya chadema, tatu JK kusisitiza suala la mgombe binafsi mwanzoni nilihisi anamlenga Lowasa na kuna uwezekano Membe amelifahamu hili ndio maana anabook mapema CDM. Hofu yangu kama mataifa kama marekani wanaingilia inamaana hata Mossad wamo kwahiyo chadema wawe makini. nitafanya jitihada kuconfirm hizi habari kwa watu wangu wa karibu. Chadema hii habari ipeni nafasi.
Kilichomponza Mkapa ni ufisadi. Mkapa angekuwa msafi asingeweza kuwa compromised kiurahisi na akina Rostam. Lakini kwa sababu naye alikuwa na mkono mchafu na mafaili yake yalikuwa mikononi mwa Rostum baada ya Ikulu kuungua. Kuna mtu hapa kasema TISS inatumikia watu 7. Na kati ya hao Rostam yumo. Iweje mafaili ya siri ya Mkapa yaishie mikononi mwa Rostam? Hapo ndipo Mkapa alijikuta hana jinsi bali kuachia jina la fisadi mwenzake Kikwete lipite. Na Rostam alitumia mafaili hayo kuhakikisha Mkapa hatakwepa mtego wao. Lakini kwa kuangalia mbele, itakuwa vizuri kama Lowassa atagombea kama mgombea binafsi kwa sababu at the end of the day atachukua kura za CCM masalia, kwa sababu wale wasiokubaliana na Lowassa ndani ya CCM wataipigia kura Chadema. Tunakusubiri Nteko Vano uje na data zaidi.
 
Wakuu kila mmoja anaweza kuchanganya na zake kwa kutumia busara hii.'Ili kupata mstari timilifu, tunaunganisha nukta kwenda nyuma na sio kwenda mbbele' nukuu ya Steve Jobs,'we cannot connect the dots by looking foward but by looking backwards' kuna watu wameshaidia kuunganisha mambo na mengine yametajwa ironically. Kazi kwetu
 
Cha muhimi ni kua katika hali kama hii kila taariifa ni muhimu. Ole wake atakayesaliti harakati za kujiletea Tanzania mpya. Ni heri angefungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutumbkizwa baharini.
 
Asante kwa kutuhabarisha.
ni kweli kabisa cdm wanatakiwa kuwa makini hasa hiki kipindi cha kuelkea 2015. Jambo nilionalo ni kuhakikisha kwamba Imani ambayo imeanza kujengeka miongoni mwa wapenda mabadiliko haipotei bure. Mikakati Kama ya m4c inatakiwa ifanyike mara kwa mara ili kueneza elimu ya uraia kwa wananchi.
Kuna Jambo linalonikera Mimi binafsi la wabunge wengi kutumia muda wao mwingi kuwa Dar badala ya kuwa majimboni mwao. Hii si tu kwa wale wa cdm Bali ni kwa wabunge karibia wote. Hii inapunguza ukaribu wa mbunge kwa wapigakura wake na hivyo kutofahamu kwa ukaribu matatizo yanayowakabiri wapigakura wake. Kwa sasa niko kwenye jimbo la hai takribani wiki tatu sasa na sijamwona mbowe huku. Nafahamu kwamba ata kuwa ana majukumu mengi Hasa kipindi hiki cha bajeti. Baadhi ya wananchi hasa katika kata za masama kusini na masama rundugai wameanza kulalamika na kudai kuwa hawaoni umuhimu aw kuwa na mbunge japokuwa ni "jembe" lakini muda mwingi yuko Dar ES salaam.
Ni wakati muafaka sasa kwa wabunge wengine wa cdm kuliangalia hili kwa jicho la umakini.
 
Hutaki Unaacha na Wana JF,

Kamanda kwanza Pole na majukumu,

Pili tunakushukuru sana kwa mchango, maono, habari zako iwapo wengi mwanzo huwa hatuziamini ila mwisho wa siku tunakuja kukuta tumepigwa Bao la Kisigino,

Tatu tukirudi kwenye mada yako kwa kweli nikiunganisha Dot hizi za Siasa na Mambo ya Siasa yanavyoenda, ukweli kuna mengi zaidi ya haya.

My Take: Kuna mambo mengi sana ambayo sisi Watanzania wengi hatujui.
Nawakilish
 
Duh, I'm terribly shocked to learn that there are secret meetings between JK and F Mbowe. Any credible source to open our eyes on this pls??
 
Id ya mtoa mada ni bonge la disclaimer...'Hutaki unaacha'. You can't demand for the source kwa sababu kama hutaki then unaacha...very tricky.

Kitwange, huyu jamaa namkubali. cheki ame join JF Sept 2010, posts 9 tu. Ina maana hakurupuki na wala si mchangiaji wa mara mara ila tu pale inapobidi na ana hit kweli!
Inaelekea yuko jikoni kweli na anaipenda nchi yake.
 
Hii hadithi mtu yeyote anaweza kusema,hivi unadhani kutaja jina apson tu ndo tukuone wewe ni shushushu mkubwa heh?.
Utawaokota wajinga kama wale waliomuamini ambilikile wa loliondo.
Eti nundu alikua kaandaliwa yaani yule mzee alivochoka ndo awe consindered kuwa rais BE SERIOUS MAN .
Katunge hadithi yako upya,hii haiuzi hata globo publisher.
 
Hivi kama kweli Dr. Slaa alifika hadi kura 47.3% uchaguzi uliopita tena bila ya M4C, itakuwaje hatma ya sisiem 2015?
Mbona naona kama akina Nepi wanachelewa kujiunga CDM?.
Hata hivyo sijui kama makamanda watamkubali tena. Na sijui kama Nepi atakubali kuwa 'Oil chafu' (tatizo la kutukana mamba kabla ya kuvuka mto)
 
It's an early doors. It's also the first page of the book. Further there's more ahead.

Mheshimiwa Hutaki Unaacha; nasuburi sana kwa hamu urudipo "safari" ili tupate taarifa zaidi zitakzokuwa zimeratibiwa vema na kuwasilishwa vizuri. Ila asante sana kwa dokezo hili muhimu.

Timiza ahadi yako usikawie kurudi hapa
 
I absolutely admire this greatl man i.e. HUTAKI UNAACHA. Kajiunga Septemba 2010, amepost mara 9 tu!

Vijana wa Nape within a day circle wana over hundreds of *****.

I SALUTE YOU MR. SIR!
 
Back
Top Bottom