CHADEMA kuweni makini sana, kilicho nyuma ya pazia hiki hapa!

Sep 19, 2010
9
478
Wapendwa wanaJF,

Kwanza niwaombe radhi kwa kukaa kimya kwa muda mrefu baada ya kutoa part II na kuahidi kuendelea kutoa part III ambayo ingekuwa ya mwisho. Ninajisikia vibaya kwa kukaa kimya bila kuwajulisha chochote. Mnisamehe kwa hilo. Ninafahamu wengi mtanielewa nikisema kwamba nimeacha kwa sasa kuendelea na ile series mpaka pale muda mwafaka utakapowadia tena. Kuna mipango mingi ambayo nilitaka kuielezea ya ndani zaidi (hasa kama ningefikia kwa Apson na Edward) ambayo kwa namna moja nyingine ingekuwa na matokeo ya aina mbili tu yaani kutengeneza mwanzo wa njia ya kuelekea kwenye ukombozi wa taifa letu au uvunjifu wa amani kubwa ambayo haikuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu (nime-consider taifa kwanza ingawa ya kwangu ni tofauti na intelijensia ya mwema). Muda ukifika nitaleta habari yote ikiwa kamili na kwa hili sitakaa muda mrefu kama ambavyo huwa nafanya. Naomba tena mnielewe kwa hilo na kusema ukweli nawaomba radhi sana tena sana kwa hili.

Lakini kuna hili ambalo imebidi nisiliache na kwa haraka haraka na mpangilio mbovu naomba nilitoe hasa kwa CHADEMA na rafiki zake. Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa. JK anakiri na ameendelea kukiri kwamba EL ameharibu mipango yake mingi sana. Analalamika sana jinsi ambavyo EL ameharibu strategies zake za kumweka mtu wake Ikulu. Kwa bahati mbaya sana JK amekuwa akishinikizwa na baadhi ya "washika dini" kumweka muislam kwenye urais wa 2015 kwa muda mrefu sasa. Niseme wazi kuwa sina shida na Islam na hata wakiongoza consecutively kwa miaka 400. Tatizo naliona pale ambapo dini inakuwa sifa. Na wapo waislamu wengi ambao hawaipendi tabia hii maana baadhi wanasema inawadhalilisha. Najaribu kutoa habari tu. Sitaki tuingie kwenye malumbano ya dini. I love my country. Mtu wa mwisho ambaye EL amemharibu ni Nundu..JK ameumia sana. Sikuwahi kumwona JK akiumia kiasi hiki baada ya mpendwa wake wa 2015 (Nundu) kuharibiwa. Nafahamu wengi watashangaa kumwona JK akihangaika kumweka Nundu 2015 akiwakilisha CCM. Nataka niseme wazi kuwa, yeye ndiye alikuwa anaandaliwa. Ninao ushahidi wa wazi kabisa. Nahodha, Hussein, Asharose (ambaye ame-underperform na "kufukuzwa" na Ban) etc wameonekana hawawezi kushindana na EL ndani ya CCM. Hata Emmanuel, Membe etc ambao labda wangeweza kutumika kushawishi kanisa hawawezi kushindana na EL ndani ya CCM.

Kwa ufupi sana, ripoti iliyomfikia JK kutoka state department ilimnyong'onyeza JK pale ilipobainika wazi kuwa hakuna mwanaCCM ambaye atamshinda EL 2015. Baada ya kuona hakuna namna nyingine, mwezi uliopita JK na EL wamekutana karibu mara 4 na "kusameheana" ili kujenga mtandao wa kuendelea kuwa na mtu wao 2015 as a president..Katika mkutano ule ambao Rostam hakuhudhuria labda kwa sababu ya ugonjwa wa baba yake mzazi (anamuuguza baba yake kwa sasa), lengo lilikuwa ni kupanga mipango ya nini kifanyike ili CHADEMA wasishinde urais 2015. Katika mikutano yao, imeonekana kwamba, ni vigumu kumshinda Dr Slaa kwa kura (kumbuka huyu katika uchaguzi wa 2010 alipata 47.3% kama matokeo halisi kabla ya uchakachuaji wa kishamba kufanyika). Kwa maana hiyo mambo/alternatives yafuatayo yaliazimiwa (hili ni muhimu sana na ushabiki uwekwe pembeni ili muweze kunusuru chama chenu na mikakati yenu);

1. Ule mpango wa kuipasua CHADEMA (unaohusisha viongozi wa dini walio karibu na CHADEMA au Slaa na kuratibiwa na idara kwa usiri wa hali ya juu) usitishwe kwa muda ili kuona kama mipango mingine itafaulu.

2. JK ajiuzulu urais mnamo mwaka 2013 hivi ili chini ya Bilal na kwa muda mfupi mabadiliko makubwa yafanyike na CHADEMA waweze kujumuishwa katika serikali hasa Dr Slaa ili kujipanga kukimaliza CHADEMA kwa urais zaidi. Ingawa JK alihofia hii technique kwa maana ya Bilal but hii naona ina mkono wa "wafanyabiashara" wakubwa wa mataifa Fulani ambao wanataka biashara zao ziende vizuri kama JK ataondoka madarakani kwani akiendelea hataweza kumweka mtu wao ili aendelee kulinda 'maslahi Fulani'

3. Katiba ijayo iruhusu serikali tatu na by any means ilazimike kuwa EL awe rais wa Tanganyika, Dr Slaa/CHADEMA wa Muungano (asiye na nguvu yoyote) na Shein aendelee Zanzibar.

4. Moja ya watu wenye nguvu ndani ya CHADEMA ashawishike kugombea kama independent candidate (sio Zitto) na malipo yake yawe competitive na campaign yake 2015 iwe sponsored kwa gharama yeyote ile.

CHADEMA kuweni makini sana na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ambao wanaweza kuwaharibia your way to 2015. Muda umeniishia kwa leo maana nasafiri muda si mrefu otherwise nikipata muda tena nitawapa updates. Thank you.
 
...CHADEMA kuweni makini sana na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ambao wanaweza kuwaharibia your way to 2015. Muda umeniishia kwa leo maana nasafiri muda si mrefu otherwise nikipata muda tena nitawapa updates. Thank you.
Mkuu Hutaki Unaacha, karibu tena.

Msamaha wako nimeuelewa na nimefarijika kukuona bado upo maana nilihisi watu wako wameisha kupotezea!.

Tukija kwenye haya usemayo kuhusu Chadema na 2015, this is too good to be true!.

Hata hivyo nasubiria!.
 
Hutaki unaacha, asante kwa nondo, sisi tunatafakari na kuangalia upepo uvumavyo.

Kitu ninachokubali moja kwa moja ni Chadema kuweni makini, kila clue inayopatikana, kwa watu makini ni jambo la kufanyia kazi.
Nani asiyejua kuwa kura za Dk Slaa zilichakachuliwa? CCM wanajua wazi kuchakachua kura za urais 2015 itakuwa kazi ngumu sana, na yawezekana matokeo ya uchakachuaji kura za urais 2015 yanaweza kuingiza nchi yetu kwenye historia na ukizingatia ICC imeshatinga Kenya, wanatutolea macho Tanzania.
 
...2. JK ajiuzulu urais mnamo mwaka 2013 hivi ili chini ya Bilal na kwa muda mfupi mabadiliko makubwa yafanyike na CHADEMA waweze kujumuishwa katika serikali hasa Dr Slaa ili kujipanga kukimaliza CHADEMA kwa urais zaidi. Ingawa JK alihofia hii technique kwa maana ya Bilal but hii naona ina mkono wa "wafanyabiashara" wakubwa wa mataifa Fulani ambao wanataka biashara zao ziende vizuri kama JK ataondoka madarakani kwani akiendelea hataweza kumweka mtu wao ili aendelee kulinda maslahi Fulani
Haya twende kazi.
 
Back
Top Bottom