CHADEMA kuweka Mawakili Kaliua

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Hili swali nilimuuliza Dr.Slaa jana japo hakunijibu nimefurahi kupata habari hii.Nawashukuru sana CHADEMA kwa kulitambua hili na kuwasaidia wana Kaliua wanaonyanyasika mikononi mwa watoto wa Mafisadi


CHADEMA kuwatetea wakazi Urambo
na Joseph Senga, Tabora

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeapa kusimamia kesi zote zinazowakabili wakazi wa jimbo la Urambo Magharibi zikiwamo za manyanyaso, kupigwa na wengine kuuawa na baadhi ya viongozi wa jimbo hilo.


Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa akizungumza katika mkutano wa hadhara jana mkoani hapa alieleza kusikitishwa na manyanyaso yanayofanywa na viongozi wa jimbo hilo hususan kwa wananchi wa mji wa Kaliua.


Dk. Slaa alipewa taarifa ya manyanyaso hayo na baadhi ya wananchi wa mji huo kabla ya kuanza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa tarafa ya Kaliua.


Katika majibu yake, Dk. Slaa alisema chama chake kitasimamia kesi zote zinazohusu manyanyaso hayo kwa kuwaweka mawakili, ili wahusika wafikishwe mahakamani.


"Nimesikitishwa sana kwamba dunia ya leo kuna watu bado wananyanyasa wenzao kwa sababu ni vigogo au watoto wa vigogo.

"Sasa CHADEMA tumeapa kuwa tutasimamia kesi zote ambazo zimetupwa na polisi na kuwaweka mawakili ili haki itendeke," alisema Dk. Slaa.

Awali, baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo walidai mtoto wa mbunge wa jimbo hilo amekuwa akiwanyanyasa wananchi husasan wale wanaojiunga na vyama vya upinzani.


Walidai mtoto huyo ambaye alikuwapo eneo la mkutano huo, hutumia wadhifa wa baba yake kuwatisha na kuwapiga vijana ambao hukataa kutii matakwa yake na kwamba askari hukwepa kumtia mikononi mwa sheria.


Source:Freemedia.co.tz
 
Kwa kweli Dr. W. Slaa amedhamiria kukomboa watz dhidi ya viongozi wa ccm! Niliisoma thread iliyotujuza kuhusu wenzetu wanavyonyanyaswa na watoto wa viongozi na wazazi wao specifically kapuya, huko Tabora yalinisikitisha sana. Nimeirudia hadi page ya tano nikijaribu kuangalia mwanasheria yeyote ambaye angejitokeza kuwasaidia lakini sikuona. Naamini tuna wanasheria wengi humu na nilijua wataguswa kwa hili lakini hakuna aliyejitokeza! Kama kuna sababu sijui ila nashukuru hatimae chama kimeibeba hii dhamana. Big up chadema. Tupo pamoja daima. People's power!
 
Anaona jimbo kama ni ufalme wake!!!

huko vjjn kuna viongozi wengi sana ni miungu watu. Yaani mjumbe wa nyumba 10 utadhani chifu. Wanawanyanyasa wananchi wanavyotaka na kuwapa vitisho kiasi kwamba w/chi hawawezi kufanya kitu. Wale wenye ujasiri kidogo wakienda polisi wanaishia kupigwa wao, kufungwa na wengine wanauawa. Hakuna wa kuwatetea maana wote wameshajengewa hofu! Nchi haina maadili ya viongozi kabisa hii!
 
Kwa kweli Dr. W. Slaa amedhamiria kukomboa watz dhidi ya viongozi wa ccm! Niliisoma thread iliyotujuza kuhusu wenzetu wanavyonyanyaswa na watoto wa viongozi na wazazi wao specifically kapuya, huko Tabora yalinisikitisha sana. Nimeirudia hadi page ya tano nikijaribu kuangalia mwanasheria yeyote ambaye angejitokeza kuwasaidia lakini sikuona. Naamini tuna wanasheria wengi humu na nilijua wataguswa kwa hili lakini hakuna aliyejitokeza! Kama kuna sababu sijui ila nashukuru hatimae chama kimeibeba hii dhamana. Big up chadema. Tupo pamoja daima. People's power!

Nachukizwa sana na hii "Spectator Approach" tuliyonayo wengi wetu ya kungoja kupongeza utendaji wa Dr Slaa n.k. Kwani Mitaani tunapoishi unafikiri hakuna mapungufu yanaypfanana na hayo? Nani ambye haishi katika Mitaa ambayo wenyeviti na watendaji hawatozi wananchi fedha ndipo kuwapatia huduma mbali mbali? Ni Vijiji na Mitaa mingapi tunayoishi ambayo Mapato na Matumizi husomwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni? Kama hili halifanyikia sisi wengine tuanatumia vipi elimu, uwezo na vipaji tulivyo navyo0 kubadili hali hiyo au mpaka Dr Slaa aje katika vijiji na mItaa yetu? Haya mambo ya kungoja Dr Slaa pekee afanya yanaboa sana; tunamgeuza Dr Slaa kuwa sitting duck kwa Propaganda machinery ya CCM. Kila mmoja wetu anatakiwa kuw Dr Slaa, Mbowe, Lissu, Mnyika, Zitto n.k Tunafanya nini katika mazingi9ra yetu (in our environs) kuisaidia CHADEMA kuonekana different na inayoweza kuaminiwa na kupewa madaraka ya kuongoza taioafa hili wananchi walio neutral?
 
Huyo mtoto anayenyanyasa wenzake ni mtoto wa Six au wa yule professa bogus anayemiliki bendi ya Akudo?
 
Ni mtoto wa mmiliki wa akudo sio kunyanyasa pekee anapiga risasi pia
 
Back
Top Bottom