Elections 2010 Chadema kuwatumia wanazuoni kuwa mawakala wake vituo vyote tanzania

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,780
3,227
Nakuja tena kwenye jamvi kama ifuatavyo.

Kuna haja ya kujadili sote uwezekano wa kuwatumia wanazuoni ambao haki yao ya kuchagua imechakachuliwa na wachakachuaji. Lakini vijana hawa wanaweza kushiriki katika uchaguzi huu na kufanya mambo makubwa kuliko hata kudumbukiza kura katika ballot.

  • Vijana hawa wakitumika kama mawakala watafanya kazi nzuri sana, kwa kuwa kurubunika kwa vijisenti vya mafisadi haitakuwa rahisi, na kama itatokea kwa baadhi ya kiwango chake chaweza kuwa chini ya 5% kwa kuwa hawa ni waelewa na wanajua madhara ya kuuza haki
  • CHADEMA watakuwa na uhakika wa usalama wa kura zao kwa kiwango cha 95%
  • Tuangalie je? Wanazuoni hawa kwa ushiriki wao kama wakala watumika kiukanda kufuatana na wanakotoka au kwa vyuo wanvyosoma? Mfano wanazuo wanaotoka kanda ya ziwa wapewe uwakala Lake zone posts, au wanaosoma vyuo vya Lake zone ndiyo wapewe?
  • Tunangalie uwezekano wa chama kuwapa motisha kwa kiwango gani?
Naamini kuwapata wanazuoni usalama wa kura utakuwa kwa kiwango cha juu na pia hata zoezi la kuchakachua halitawezekana kwani hawa ni wasomi wanajua kuwa THE FUTURE OF OUR COUNTRY WILL BE BRIGHT SOON.

Tujadili tafadhali
 
Back
Top Bottom