CHADEMA kuwakataa viongozi wa CCM

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,198
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kusitisha kuwapokea viongozi wa ngazi zote watakaohama kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vingine, baada ya kutemwa katika kura za maoni kwa lengo la kutaka kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama hicho.

Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitoa msimamo huo jana alipokutana na wanafunzi wa vyuo vikuu vitatu vya Udom, CBE na St John, katika hafla ya kuwaaga wenzao wanaomaliza masomo yao.

Mbowe alisema kuwa, CHADEMA kinataka sasa kupata viongozi na wanachama wanaosukumwa na uzalendo wa kweli, na wanaoamini itikadi na sera zake, na si wanaotaka kukitumia kama ngazi ya kufanikisha malengo yao.

Alisema wamejifunza kwa kiasi kikubwa hasara ya kuwapokea wanachama, na hasa waliokuwa viongozi wa vyama vingine dakika za mwisho, hususan wakati wa uchaguzi, hivyo kuanzia sasa hawapo tayari kufanya hivyo.

Mbowe alisema wapo tayari na wanawakaribisha wanachama ama viongozi wa CCM ambao wanaona kuwa CHADEMA ni chama makini, kikomavu na wanaoamini kina malengo halisi ya kuikomboa nchi na kuwaletea maendeleo wananchi wote bila kujali itikadi ya vyama, dini, kabila ama eneo la nchi.

"Wale wapambanaji waliochoshwa na matendo ya wenzao ndani ya CCM, na wanaoamini kwa dhati kabisa na kusukumwa na dhamiri ya kweli ya kupigania maslahi ya wanyonge, waje sasa.

"Hakuna haja ya wao kusubiri hadi dakika za mwisho, na hasa pale wanapopigwa chini katika kura za maoni ndio waje. Wajue kuwa wakisubiri muda huo, hawataweza kupokelewa hata kama watakuwa ni wazuri namna gani," alisema Mbowe

Source: Tanzania Daima

SAM_2793.JPG

My take: Hii itasaidia sana kukwepa kadhia kama ya Shibuda. Na ingekuwa vizuri kwa kila chama. Haiwezakani leo uko chama hiki lakini kesho uko upande wa pili. Unasimamia nini? Tumeona Kenya jinsi siasa zimegubikwa na wakubwa kuhama hama kila mara. Mwishoni mnajikuta vyama vyote viko contaminated maana viongozi wanakuwepo si kwa sababu ya principle bali kuendeleza 'ulaji'. Thanks Shibuda - learned the hard way!
 
Ni uamzi mzuri ingawa si mzuri sana, Issue nikuwa makini na watu wote wanaomba uongozi coz wengi wa viongozi na wanachama wanatokea vyama vingine, muhimu wanapojiunga nilazima ziwepo kanuni na taratibu za mtu kujiunga na CDM ambazo hazitakua zinabagua watu wengine kuruhusiwa na wengine kukataliwa kuomba kugombea.

Mwaka 2010 CDM haikusimamisha wagombea majimbo yote, tatizo kulikua hakuna watu wa kugombea na inaweza tokea tena 2015 ni vipi watu wakaomba wakakataliwa wakati majimbo hayana wagombea?

Nashauri namna nzuri itafutwe kukabiliana na wahamiaji toka vyama vingine coz wapo watu makini pia ktk vyama vingine waruhusiwe
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ni uamzi mzuri ingawa si mzuri sana, Issue nikuwa makini na watu wote wanaomba uongozi coz wengi wa viongozi na wanachama wanatokea vyama vingine, muhimu wanapojiunga nilazima ziwepo kanuni na taratibu za mtu kujiunga na CDM ambazo hazitakua zinabagua watu wengine kuruhusiwa na wengine kukataliwa kuomba kugombea. mwaka 2010 CDM haikusimamisha wagombea majimbo yote, tatizo kulikua hakuna watu wa kugombea na inaweza tokea tena 2015 ni vipi watu wakaomba wakakataliwa wakati majimbo hayana wagombea? Nashauri namna nzuri itafutwe kukabiliana na wahamiaji toka vyama vingine coz wapo watu makini pia ktk vyama vingine waruhusiwe

Bob, kupokea 'reject' ni hatari sana. Viongozi wanaoomba kujiunga kwa sababu wameshindwa upande mwingine ni wazi kabisa wajiunga ili kupata uongozi na hatari ni kuwa na mtu kama Shibuda. Bado Shibuda ni CCM damu damu na kama sio busara ya CHADEMA wangejikuta wanatumia muda mwingi kumjadili kwenye vikao badala ya kufanya mambo mengine.

Watu wapime na waamue sasa you are either with party X or party Y. Lakini mchezo wa kamari uishe!

Kuhusu kusimamisha wagombea 2015. Nadhani this time around CCM wanaweza kujikuta wanakosa mtu wa kumsimamisha kwenye baadhi ya majimbo. Chama hakiuziki kabisa na tayari mwaka huu wamekosa watu wa kugombea nafasi za ubalozi. Wamepuuza kero za wananchi mno hivyo inakuwa shida hata kwa mgombea kusema analeta mambo mapya.
 
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kusitisha kuwapokea viongozi wa ngazi zote watakaohama kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vingine, baada ya kutemwa katika kura za maoni kwa lengo la kutaka kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama hicho.

Mbowe kavunja katiba ya CHAMA.
 
mi kwa maoni yangu ni kwamba wawapokee lakin wawe members tuu. mpaka watakapowaona wamekomaa ndo wawape fursa ya kugombea.
tukisema tuwakatae tu si nzuri coz kuna wengine wamesha kombolewa ki fikra na wapo tayari kikomboa nchi yao. je hao wakimbilie wapi??
 
Nadhani tukisoma vizuri utakuta Mbowe anazungumzia wanaokuja ili kugombea uongozi; na imefafanuliwa wote wanakaribishwa ila si kuja tu kutaka uongozi. Nawapa big up kwa hilo! Hii itasaidia sana kupata wajenga chamabadala ya wajengea tumbo
 
kama ni hili hapo sawa
 
alway chadema ni chama makini and viogonzi wake wanamaamuzi ya busara.

long live mwenyekiti makini.!!!!
 
Lengo la mbowe si kwamba hawawapokea,la hasha watapokelewa isipokuwa hawatapewa kipaumbele katika nafasi za kugombea uongozi katika nafasi za juu kama ubunge,katibu wa mkoa/wilaya n.k

wao watakuwa ni wanachama wa kawaida maana kama umekaa magamba miaka 20 na hakuna cha maana ulichokifanya katika jimbo lako wala huna uzalendo kwa wananchi utakuwa huna faida. Kauli ya mbowe inawahusu wale wapenda matumbo yao na wabinafsi kama shibuda
 
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kusitisha kuwapokea viongozi wa ngazi zote watakaohama kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vingine, baada ya kutemwa katika kura za maoni kwa lengo la kutaka kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama hicho.

Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitoa msimamo huo jana alipokutana na wanafunzi wa vyuo vikuu vitatu vya UDOM, CBE na St John, katika hafla ya kuwaaga wenzao wanaomaliza masomo yao.

Mbowe alisema kuwa, CHADEMA kinataka sasa kupata viongozi na wanachama wanaosukumwa na uzalendo wa kweli, na wanaoamini itikadi na sera zake, na si wanaotaka kukitumia kama ngazi ya kufanikisha malengo yao.

Alisema wamejifunza kwa kiasi kikubwa hasara ya kuwapokea wanachama, na hasa waliokuwa viongozi wa vyama vingine dakika za mwisho, hususan wakati wa uchaguzi, hivyo kuanzia sasa hawapo tayari kufanya hivyo.

Mbowe alisema wapo tayari na wanawakaribisha wanachama ama viongozi wa CCM ambao wanaona kuwa CHADEMA ni chama makini, kikomavu na wanaoamini kina malengo halisi ya kuikomboa nchi na kuwaletea maendeleo wananchi wote bila kujali itikadi ya
vyama, dini, kabila ama eneo la nchi.

"Wale wapambanaji waliochoshwa na matendo ya wenzao ndani ya CCM, na wanaoamini kwa dhati kabisa na kusukumwa na dhamiri ya kweli ya kupigania maslahi ya wanyonge, waje sasa.

"Hakuna haja ya wao kusubiri hadi dakika za mwisho, na hasa pale wanapopigwa chini katika kura za maoni ndio waje. Wajue kuwa
wakisubiri muda huo, hawataweza kupokelewa hata kama watakuwa ni wazuri namna gani," alisema Mbowe.
 
i think it is a good strategy... kama wanataka mabadiliko ya kweli wajiunge sasa, na sio kusubiri kura za maoni za ccm.... maana watakua wanataka uongozi na si mapinduzi ya kweli ya mtanzania wa kawaida
 
1) Anamla vijembe Slaa.

2) Anarukia hoja ya uzalendo.

Kuna kila sababu ya kuona kuwa, ingawa Slaa ana hamu sana ya kugombea tena, hatopewa fursa hiyo na Mwenyekiti Mbowe.
 
mi kwa maoni yangu ni kwamba wawapokee lakin wawe members tuu. mpaka watakapowaona wamekomaa ndo wawape fursa ya kugombea.
tukisema tuwakatae tu si nzuri coz kuna wengine wamesha kombolewa ki fikra na wapo tayari kikomboa nchi yao. je hao wakimbilie wapi??

Hawatapokelewa kama wameshindwa kura za maoni ccm halafu wakaona wakihamia CDM watashinda. Kama wanadhani ccm hakiwafai, wasingoje wakati wa uchaguzi bali wajiunge sasa.

Huo ni uamuzi wa busara sana. Naamini CDM imejipanga kusimamisha wagombea katika kila jimbo. Wako wasomi wengi na wapenda mabadiliko wanaoamini katika nguvu ya umma.
 
Si kweli ,lazima itakuwa zaidi ya hicho kiwango chama kinaweza kujiendesha chenyewe bila kutegemea ruzuku maana yake kina wanachama wengi wanaoweza kutoa fedha za ada tuu zaidi ya 7bilion kwa mwezi basi kina wanachama zaidi ya 10milioni 500x7,000,000=3,500,000,000/= wametoka

Tayari tuna wanachama miliöni 7 sasa wanaweza kwenda CUF/NCCR chadema kumejaa!
 
idea nzuri, hii kitu ya kuwaza kwamba wakija CDM watapea nafasi ife kabisa, waende CHAUSTA,
 
1) Anamla vijembe Slaa.

2) Anarukia hoja ya uzalendo.

Kuna kila sababu ya kuona kuwa, ingawa Slaa ana hamu sana ya kugombea tena, hatopewa fursa hiyo na Mwenyekiti Mbowe.
Hivi wewe uliwahi kusikia lini Slaa na Mbowe wakatofautiana?Mfumo wa cdm uko makini sna,wanajadili kwa pamoja na kutoa uamuzi kwa pamoja.Wanachokiamua wanakisimamia kwa pamoja tofauti na nyinyiem kila kundi lina mamlaka
na uwezo wa kukisemea chama.
 
Back
Top Bottom