CHADEMA kutumia Helkopta nne katika M4C kushambulia mikoa yote Tanzania

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
*Ni awamu nyingine ya M4C
*Zitashambulia mikoa minne


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinakusudia kuendelea na Operesheni Sangara kwa nguvu kubwa ikiwemo kutumia helkopta nne na kuongeza idadi ya magari katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuyafikia maeneo mengi ambayo miundombinu yake ni mibovu.

Chama hicho kitatumia helikopta hizo wiki mbili zijazo kitakapoendelea na operesheni hiyo yenye kauli mbiu ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) katika Mkoa wa Iringa.

Operesheni hiyo ilitarajiwa kuanza mkoani Iringa Agosti 28, mwaka huu, lakini ilisitishwa baada ya chama hicho kukubaliana na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, kwamba iendelee baada ya kumalizika kwa sensa ya watu na makazi.

Baada ya sensa kumalizika, Chadema kilitangaza kuisitisha operesheni hiyo kufuatia tukio la mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi kwa bomu wakati polisi wakikabiliana na wa wafuasi wa chama hicho kwenye ufunguzi wa tawi katika kijiji cha Nyololo katika wilaya ya mufindi, mkoani Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro jana baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Mwenyekiti wake, John Heche, alisema kuwa operesheni hiyo inatarajia kuanza tena ndani ya wiki mbili zijazo na itanzia mkoani Iringa na kuendelea katika mikoa mingine.

“Kwa taarifa yenu, sasa tutaruka angani na chopa nne kuongeza nguvu Operesheni Sangara, tutaendelea na Mkoa wa Iringa ambako tuliisimamisha kutokana na mauaji ya Mwangosi,” alisema Heche na kuongeza: “Tukitoka hapo tunapiga mikoa mingine.”

Heche alisema lengo la kutumia helikopta hizo nne ni kuwafikia wananchi wengi kuanzia ngazi ya kitongoji ili kuwaeleza mambo mbalimbali, yakiwemo maovu yanayofanyika nchini.

Mwenyekiti huyo wa Bavicha alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya sehemu katika wilaya mbalimbali na mikoa nchini kutofikika kwa njia ya gari kutokana na ubovu wa mindombinu ya barabara ambayo katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru Serikali ya CCM imeshindwa kuiboresha.

Akizungumzia maazimio ya kikao cha kamati ya Utendaji cha Bavicha, alisema kuwa mstakabali wa vijana wa taifa hili hivi sasa unakabiliwa na na changamoto nyingi kutokana na serikali ya CCM kushindwa kusimamia mambo mbalimbali.

Alisema kutokana na hali hiyo, Kamati Tendaji ya Bavicha imeiagiza sekretarieti yake kuunda kikosi kazi au kamati ya kufanya utafiti zaidi ili kujua kwa kina matatizo ya vijana hususani kuanzia masuala ya kuporomoka kwa elimu, ukosefu wa ajira na kutoa ushauri juu ya mstakabali wa taifa baada ya mwaka 2015.

Heche alisema kuwa Bavicha itaendelea kuwaunga mkono walalahoi nchini, wakiwamo wamachinga na matatizo yanayowakabili wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu katika kupata mikopo yao pamoja na kuvifuatilia viwanda ambavyo vilikuwa vikitoa ajira mbalimbali na hivi sasa vimegeuka kuwa mabanda ya mifugo.

Mbali na maazimio hayo, pia baraza hilo limetoa tahadhari kwa vyombo vya dola na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kuepusha kauli za vitisho zinazohatarisha amani ya nchi.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bavicha Zanzibar, Sharifa Suleiman, alisema vurugu zote zinazotokea kwenye majukwaa ya kisiasa kwa sehemu kubwa zinatokana na propaganda zinazofanywa na CCM kwa lengo la kuichafua Chadema na kupendekeza kuwa ni muhimu CCM kikaondolewa kwenye orodha ya vyama vya siasa nchini.

“Tumeshuhudia wananchi wakiendelea kunyanyaswa na vyombo vyao vya dola wanavyovilipa kwa kodi zao,” alisema Sharifa.

Akifafanua zaidi alisema vyombo vya dola viondokane na mfumo wa kinyanyasaji wa kujichunguza vyenyewe na kulitaka Jeshi la Polisi kujisafisha kabla wanachi hawajaamka na kukataa kukandamizaji unaofanywa na baadhi ya askari wake bila kuchukuliwa hatua zozote.

Chadema ilianzia Operesheni Sangara katika Mkoa wa Morogoro na ilitarajia kuendelea nayo katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Njombe.
CHANZO: NIPASHE
 
Kile chama cha kukopi na kupest hapo si dhan kama kitaweza. Ngoja waje wazee wa balagashia wajibu hili
 
mmmmmmh hapa twendwa lazima ashinikizwe kukifuta loh......

@nnauyejr unasikia haya? Jipange
 
Chadema mnawachangisha wananchi pesa sasa mnaanza kuzitafuna kwa njia tofauti ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi.
 
Pesa zao zinakwenda kuwaelimisha na kuwaamsha waliolala ready for ukombozi.matumizi mazuri ya pesa
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mi nawashauri watumie michango ya wananchi pia kuibua miradi ya maendeleo na kutatua kero ambazo CCM imeshindwa kuzitatua.

Kwa mfano, asilimia 50 ya michango ya wananchi iwarudie wananchi wenyewe kwa kuboresha miundo mbinu hospitalini, kusambaza huduma za maji, kujenga nyumba za watumishi kwa mfano walimu na madaktari.

Naamini kwa kufanya hivyo, kwanza wataonesha nidhamu ya pesa za walipakodi, na miradi mingi itasimama kwa pesa kidogo huku ubora wa miradi ukishinda mbali ile iliyosimamiwa na serikali ya CCM
.
 
Hatua hiyo itakuwa ni aliyoita marehemu the great Kanamba, "twanga kotekote" Vipi changamoto ya vibali kutolewa na police na mpango wa kuzuia viwanja ambavyo ni mali ya serikali, wananchi na hata vya watu binafsi wasiwakodishie??:cool:
 
Hakuna hazina kubwa kama kuwaelemisha wananchi elimu ya kujijua, kujua haki zao kuliko wanavyoporwa haki, mali zao mchana kweupe.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
kodi wakusanye CCM, maendeleo wafanye CDM? Mkuu, fikiria vzuri! CDM wamewaomba wananchi wachangie fedha kwa ajili ya kufanikisha m4c, halafu unataka wao wakazifanyie mambo mengine! Na hapo unadhani itakuwa ndio nidhamu ya matumizi? Jipange upya.
 
Nina kila sababu ya kukipenda CDM,chama kinaendeshwa kisasa bwana.Mkuu Ritz umesahau tulipoanza kutumia huo mwewe mlituponda sana lkn muda si mrefu mkala matapishi yenu.

Fedha hizo hazikuchangwa kwa ajili ya hospital,barabara nk bali kujenga chama.Hivyo waliotoa wanatarajia kuona impact yake,hoja kwamba zitumike kwa shughuli za kijamii ni mufilisi,CCM wanapaswa kufanya hivyo kwasababu wanakusanya kodi
.
 
Back
Top Bottom