CHADEMA kutinga na kutikisa Mtwara; shughuli kuanzia Mjini Mtwara leo

All the Best makamanda, Mungu ni mwema, mtafika salama na mtafanya kazi ya kuvua watu magamba na kuwavalisha magwanda...
 
Best wishes CDM, Mungu na malaika wote wawatangulie katika operesheni hii ili mpate ufanisi mkubwa na hatimaye Brigade nzima ipate kurejea nyumbani kwa familia zenu salama salimini AMEN
 
mbona viti maalum mnagawana kaskazini, yaani ubunge mgawane nyie sisi tule vumbi. Haiwezekani njooni tuwashangae tu.

ufinyu wako wa mawazo unafanana na inzi mla kinyesi, hivyoviti maalum vinakusaidia nini wewe/ hata kama utapewa uwaziri na hakuna msaada wowote wa ukombozi wa kifikra na kiuchumi cheo kina maana gani kwako? Kuna wabunge wangapi wa kuchaguliwaambao hawajasaidia chochote kwao nao wanafaida gani? Subiri uone jinsi watu walivyokusudia kuleta mabadiliko ya kweli ya maisha kwa kuwapa elimu ya kujitambua utaifa wako, na hii sio ni faida ya chadema tu hata kwa chama chochote kwa siku zijazo.
 
Hakuna kulala mpaka kieleweke VUA GAMBA VAA GWANDA

PEEEEEE OOOOOOOOOOOO PLLLLESSSSS POOOOOOOOOOOOOOOWEEEEEEEEERRRRRRRRRRR
 
mbona viti maalum mnagawana kaskazini, yaani ubunge mgawane nyie sisi tule vumbi. Haiwezekani njooni tuwashangae tu.

Huyu ana elimu ndogo sana ingawaje anaweza kuaccess JF.Viti maalumu hawapewi kama njugu.Lazima uwe mwanachama wa chama husika na ugombee nafas hiyo.Hawataweza kumpa mtu ambaye yeye mwenyewe hataki kujiunga.Nilishaandika hapa kuonya juu ya suala la viti maalum.Mimi nipo Songea ambako hakuna mbunge wa viti maalum wa cdm.Lakini hilo kwangu si tatizo kwani wanaopaswa kugombania viti hivyo sharti wawe wanachama.Acha ujinga na uelimike.Huko ccm ambao mmepata viti maalum waliwaletea nyumbani au kuna wanachama walijitokeza ndipo wakapata tena kwa kuhonga hela nyingi.Acha ukurutu wa ubongo,bandua huo.
 
Ni gwanda tu mpaka kieleweke
kunja ngumi watu wote
peoplesssssssssssssssssssssssssssssssssssssss ,
powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
m4c mnanikosha kweeeeeeeli kweli!!!!kama mmeamua kuchakaza mpaka vijijini basi shughuli ipo 2015.kila la heri wakubwa!!!!
 
Msikose kufanya kazi pale Masasi watu wameelimika toka uhuru hivyo basi wanahitaji mwamko mdogo tu wafanye mabadiliko ya kweli. Hongereni.
 

Wakuu;

Leo tunatinga Mjini Mtwara. Tumelala Mjini Lindi. Advance team katika operesheni hii ya Kusini inasema mipango yote inakwenda vyema kabisa. Hamasa ni kubwa. Wenyeji wanatusubiri wageni. Mgeni njoo, mwneyeji apone. Katika hili wenyeji watapona kwa kupata elimu ya siasa, hasa juu ya mchakato wa katiba mpya.

Wenyeji watapona kwa oganaizesheni ya chama kujengwa kuanzia ngazi ya vijijini mpaka mijini. Wenyeji watapona kwa kuendelea kupata hoja na namna ya kudai uwajibikaji wa serikali kwa ajili ya maendeleo ya watu. Watapata hoja za namna ambavyo serikali inapaswa kuwajibika kwa kushughulikia vyanzo/viini vya matatizo yanayoikabili jamii kwa sasa, kisiasa, kijamii na kiuchumi. Badala ya kushughulikia matokeo ya matatizo kama ambavyo serikali ya CCM inafanya sasa.

Baada ya Mjini Mtwara leo, kesho timu itagawanyika katika makundi kadhaa kwa ajili ya 'kuvamia' kata zote za Mtwara Vijijini. Keshokutwa itakuwa zamu ya Tandahimba. Kazi ni moja tu. Kusambaza chama kwa kasi mithili ya moto wa petroli. Amesema Kamanda Mbowe juzi pale Chadema Square. Nitawapatia ratiba ya maeneo mengine kadri muda unavyokwenda.

Unaweza kuona kuna watu wameanza kuweweseka hapa. Tumesikia wengine tangu shughuli pevu ya juzi pale Chadema Square hawajapata usingizi sawasawa. Mambo kichwani hayawaendei sawasawa. Wengine wameanza kuelewa kuwa inaweza isifike na si lazima mwaka 2015. Wengi wao wameanza kuiona 2015 inakaribia kwa kasi sana. The exit is very obvious!

Kiwewe cha M4C, Vua Gamba na Vaa Gwanda, Watanzania wanyonge kuchangia vuguvugu bila uoga (kama ilivyokuwa wakati wa kupigania uhuru), safari yetu ya Kusini na mengine mengi yanawafanya waanze kuandika uongo hapa. Wanahangaika kweli! Jogoo, awike asiwike, kucha kutakucha. Wanajua hilo! Wajiandae.

Kama ilivyo ada, Operesheni hii ya Kusini pia itafanywa na timu ya watu makini. Imekuwa hivyo katika operesheni zote za Chadema. Kamanda wa Anga, Freeman Mbowe anaongoza jahazi, Kamanda wa Ardhi, Dkt. Willibrod Slaa yuko tayari. Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed yuko kamili.

Wabunge kadhaa wametangulia field, John John Mnyika, Tundu Lissu, Ezekiah Wenje. Wengine wako njiani muda si mrefu kuuungana na makamanda waliotangulia. Timu ina mchanganyiko wa vijana na wazee, wazoefu na wapya. Wenyeji watapewa nafasi ya kufanya kazi zaidi ili wapate uwezo wa kusonga mbele wageni wakiondoka.

Operation Commander kwa shughuli hii ya Kusini ni John Heche, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA). Kiuhalisia, kama ilivyo jeshini timu nzima iko chini ya Heche. Viongozi wakuu watalazimika kuingilia pale panapohitajika sana na katika masuala mengine machache ambayo ni wazi yanahitaji uongozi wa juu kusimamia, kuelekeza, kuagiza na kuamuru. Kuongoza!

Walioko Mtwara Mjini karibuni sana. Wengine walioko mbali tutawajuza kila kinachotokea. Punde tunaondoka Lindi, kwenda Mtwara. Baada ya Mkoa wa Mtwara, shughuli itahamia Mkoa wa Lindi. Ratiba mtaipata hapa hapa. Asanteni.

Penye nia pana njia, twawataki ukombozi mwema.
 
Makene kwakuwa wewe unapipita JF naomba unifikishie ujumbe wangu huu kwa viongozi wa juu wa CDM. CDM kama chama kinachojiandaa kushika dola 2015, na kweli upepo unavuma in favour of CDM, unless CDM mkosea kucheza karata zenu. CDM imejiandaa vipi kuhusu suala la mgombea mwenza?. No disrespect to the guy who was a running mate 2010, lakini ukweli lazima usemwe Elimu yake ilitia doa kampeini za CDM 2010. Pia hakushiriki aggrresive kwenye kampeini 2010 kama ilivyokuwa kwa running mate wa CCM Dr. Bilal.

Kwa mambo yanvyokwenda mgombea wa CDM 2015 atatoka Tanganyika, sijui, Mbowe(?), Dr. Slaa(?), Zitto(?) Shibuda simuhesabu. Je CDM imejipanga vipi kupata mtu credible kutoka ZNZ ambaye atakuwa running mate? CDM lazima muanze ku focus mbali kama chama makini, Tusiwape hata punje ya advantage CCM. Ninajua ni vigumu sana kumpata mtu wa aina hiyo ZNZ kwasababu imetawaliwa na Siasa za CCM na CUF.

Lakini kama requirement mojawapo kutokana na katiba yetu inabidi kuwa engage wazanzibari kwa ukaribu. Naomba Tumaini Makene unifikishie hili jambo kwa viongozi wa juu wa CDM.

Msiniambie kwamba 2015 tutakuwa na katiba mpya. Nigependelea iwe hivyo but believe me 2015 tutakuwa hautuna katiba mpya mark my words.

Ninawakia M4C yenye mafanikio. Freedom is Coming Tomorrow
 
all the best makamanda.Mungu atawapigania and naamini matumaini ya ukombozi yatabaki kwa wananchi wa huko.

together we can!!!!!!
 
Safi makamanda...Lindi tunawasubiri..naamin Lindi Cuf imeshakufa vs Ccm pia..tunazizika..Najiandaa kuchukua jimbo la MTAMA
"Vox Populi,Vox dei"
 
Back
Top Bottom