CHADEMA kutikisa Tanga kuanzia kesho, Zitto kuongoza mashambulizi

wakiritimba machozi yanawatoka ccm kwaheri karibu CHADEMA!!!!!!!!! PEOPLEEEEEEEEEEEEEEZ
 
Mungu awatie Nguvu katika ziara hii ya ukombozi, wasitange tange kama wana wa Israeli walivyotangatanga jangwani bali awafikishe nchi ya ahadi haraka.
Mh. Zitto na timu yote tunawatakieni afya njema na watu wa Tanga wafanyiwe wepesi wa kuwaelewa tamaa na nia ya ukombozi idumu ndani yao
.
 
katika kuwahamasisha wananchi kujitokeza kupokea ujio huo, ningependa kushauri wanachama na wananchi wenye maduka ya yale mavazi ya kuhamashisha ukombozi kuchukua nafasi ya kuagiza mzigo na kuuza kwani zimekuwa zikipatikana kwa taabu sana! cdm for the people!
 
Mnalijua suala la Mkonge vizuri Tanga au nijushabikia tu,

Unafikiri wale wabunge wa Tanga walivyokataa ni wajinga?

Sasa iko hivi...

Yale mashamba ni ya serikali ila tatizo amepewa mtu mmoja ayamiliki na kuyaendesha baada ya kipindi Kile Mkonge kuyumba...

Kwahiyo sasa hivi huyo aliepewa ndio anamamlaka ya kuwakodisha watu tu na sio kuwamilikisha hoja ya wananchi sisi wa Tanga tunataka watu wapewe na iwe hiari kuuza Mkonge popote na kwa utaratibu ambao wananchi wakua na miliki isiyokua chini ya mtu mmoja..

Na inasemekana hayo mashamba yameombewa mkopo mkubwa tu kinyume na utaratibu sasa hii hoja sio yakukurupuka ataaibika vibaya sana.

Ndio maaana serikali waliunda tume ndogo kufuatilia hiyo issue baada ya Mhe Maji marefu kuuliza swali sijui namba Mia Tatu na ngapi I can't recall , I bet u all bn following up closely during Bunge....

Na pia kuna Taarifa kulikua na kundi la waandishi wa habari na Mhe Zito alikuwepo kwenye hiyo Ziara mkoani Tanga na amepewa Mkwanja Mrefu kati ya hizo Pesa zilizoomba kupitia mashamba hayo ya Tanga.


Nadhani Tuwe tunafuatilia mambo kwa kina.

Kalagbaho babu weeeeeee Zitto ameshawashika pabaya nyie wabunge wa tanga kasoro JM ni mjanja kuliko nyie wazee ndo maana hatafika bumbuli,nyie wote mtapitiwa na kirus cha CDM SOON AND VERY SOON,MWITENI SUGU AWAPE DOZ YA ANTIVIRUS.
 

TAARIFA KWA UMMA

Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), inapenda kuutarifu umma kuwa viongozi kadhaa wa kitaifa, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mheshimiwa Kabwe Zitto watafanya ziara ya kichama mkoani Tanga.

Ziara hiyo itakayoanza Jumamosi, Februari 18, 2012, itaanzia Wilaya ya Handeni, Korogwe, Mheza, Pangani, kisha Tanga Mjini. Katika maeneo yote hayo Naibu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Zitto atakagua uhai wa chama mkoani humo, ambapo atafanya mikutano na wanachama wa CHADEMA.

Viongozi hao wa CHADEMA pia watazungumza na wananchi mkoani Tanga katika mikutano ya hadhara, kwenye maeneo yote hayo. Watatumia fursa hiyo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na yale ya maeneo husika.

Mbali ya kukagua uhai wa chama mkoani Tanga, katika ziara hiyo, Mheshimiwa Zitto , pia atatumia fursa hiyo kuipeleka kwa wananchi na kuifafanua hoja yake aliyoiwasilisha bungeni katika mkutano ulioisha hivi karibuni juu ya zao za mkonge, ambapo baadhi ya wabunge wa Tanga, walisimama kuipinga hoja hiyo.

Kurugenzi ya Habari na Uenezi, inatoa wito katika maeneo yote ambayo msafara huo wa CHADEMA utafanya mikutano, wananchi wahudhurie kwa wingi ili wanufaike na ziara hiyo.

Imetolewa leo Februari 16, 2012, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene

Afisa Habari wa CHADEMA
Zitto yeye anasema hivi:
Zitto Kabwe


Kwa siku 5 nitakuwa na ziara ya kukagua uhai wa chama mkoa wa Tanga. Nitakutana na viongozi wa chama ngazi za Kata na Majimbo na mikutano ya hadhara katika Wilaya za Handeni, Korogwe, Muheza, Pangani na Jiji la Tanga. Tutawakumbusha wananchi wa Tanga umuhimu wa kufanya mabadiliko katika siasa za nchi yetu na nafasi ya mkoa wa Tanga katika historia ya Tanzania.
unaona hizo NI, NI, ....Zina maana yake!
 
"
Ziara hiyo itakayoanza Jumamosi, Februari 18, 2012, itaanzia Wilaya ya Handeni, Korogwe, Mheza, Pangani, kisha Tanga Mjini. Katika maeneo yote hayo Naibu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Zitto atakagua uhai wa chama mkoani humo, ambapo atafanya mikutano na wanachama wa CHADEMA".

MBONA LUSHOTO HAMUENDI??? AU MAFISADI WASHAMUWEKA SAWA HUYU KIJANA WA KIGOMA ILI ASIENDE KUSEMA UKWELI KWENYE JIMBO LA KIJANA WA MAFISADI???? ZITO MUOGOPE MUNGU.. ANGALIA JINSI WATU WALIVYO NA MAENDELEO DUNI HUKU USIKOENDA??? NILITEGEMEA UTAANZIA HUKO... DUUHH IMANI JUU YA HUYU BWANA INATOWEKA KABISAAA..............
 
Back
Top Bottom