CHADEMA kutikisa Tanga kuanzia kesho, Zitto kuongoza mashambulizi

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071

TAARIFA KWA UMMA

Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), inapenda kuutarifu umma kuwa viongozi kadhaa wa kitaifa, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mheshimiwa Kabwe Zitto watafanya ziara ya kichama mkoani Tanga.

Ziara hiyo itakayoanza Jumamosi, Februari 18, 2012, itaanzia Wilaya ya Handeni, Korogwe, Mheza, Pangani, kisha Tanga Mjini. Katika maeneo yote hayo Naibu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Zitto atakagua uhai wa chama mkoani humo, ambapo atafanya mikutano na wanachama wa CHADEMA.

Viongozi hao wa CHADEMA pia watazungumza na wananchi mkoani Tanga katika mikutano ya hadhara, kwenye maeneo yote hayo. Watatumia fursa hiyo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na yale ya maeneo husika.

Mbali ya kukagua uhai wa chama mkoani Tanga, katika ziara hiyo, Mheshimiwa Zitto , pia atatumia fursa hiyo kuipeleka kwa wananchi na kuifafanua hoja yake aliyoiwasilisha bungeni katika mkutano ulioisha hivi karibuni juu ya zao za mkonge, ambapo baadhi ya wabunge wa Tanga, walisimama kuipinga hoja hiyo.

Kurugenzi ya Habari na Uenezi, inatoa wito katika maeneo yote ambayo msafara huo wa CHADEMA utafanya mikutano, wananchi wahudhurie kwa wingi ili wanufaike na ziara hiyo.

Imetolewa leo Februari 16, 2012, Dar es Salaam na;

Tumaini Makene

Afisa Habari wa CHADEMA
 
Kazi nzuri,mgawanyo huu wa kazi utaleta ukombozi kwa haraka sana,na kwa hakika utawala huu uliochoka utachanganyikiwa na hii spidi yetu...hakuna kulala mpaka kieleweke.Na nikushukuru wewe pia kwa kutupatia hizi taarifa nzuri na endelea kutujuza mambo yanayoendelea kwenye chama chetu.
 
Kuna wimbo fulani tuliuimba miaka ya 1983 Darasa la kwanza :flypig: jogoo awikaaaa, kuwaamsha watuuuu, Wale waliolalaaaa,, Waamke sasaaaaa..Kokorikoooooooooooooooooo....ooohhh:lalala:
 
Imetulia kupita maelezo, maana huko ni moja ya maeneo ambayo baadhi waliamini hayaingiliki na chadema.

Ila hapo mmeisahau wilaya ya Kilindi wakuu.
 
well done chadema....tupo nyuma yenu kwenye hizi harakati.....ukombozi unakaribia
 
Hii ndo yenyewe,this way 2015 itakuwa kama kumsukuma mlevi,litokee kundi jingine liongozwe na naibu katibu mkuu visiwani mh Hamad kuelekea mikoa ya Lindi na Ntwara!
 
Kuna taarifa ya kuwa Mheshimiwa Zitto atafanya ziara katika mkoa wa Tanga amabapo anatarajia kutembelea wilaya zote za mkoa huo. Napenda kutanguliza shukrani zangu kwako na uongozi kwa kuamua kufanya ziara hiyo huko na kuwaelezea wananchi lengo lako la hoja yako binafsi kuhusu zao la mkonge.Ukweli nataraji ziara yako iwe darasa la kuwaasha watu wa Tanga kwamba wakati umefika wa kuchagua uongozi unaojali wanachi.Kila la kheri mkuu !
 
Imetulia kupita maelezo, maana huko ni moja ya maeneo ambayo baadhi waliamini hayaingiliki na chadema.

Ila hapo mmeisahau wilaya ya Kilindi wakuu.

Mkuu usisahau kuwa CHADEMA iliwahi kupiga Operesheni Sangara kali sana mkoa mzima wa Tanga, mwaka 2009. Iliongozwa na Kamanda wa Anga, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, kisha ikamalizikia Same. Ilikuwa kali sana kiasi kwamba, iliwachanganya CCM na serikali yao pale mkoani. Nakumbuka, Mkuu wa Mkoa, Said Kalembo aliagiza watu wa usalama wafuatilie CHADEMA kw akaribu kujua wanafanya nini hasa, mikakati yao, wamejipangaje, pia wakaanza kuleta mikwara mikwara kwenye helkopta, wakitaka kuizuia, mara kuhoji kibali cha rubani na mambo kama hayo.

Chama kipo sana mkoani Tanga, lakini kukagua uhai ni muhimu sana pia. Ndiyo maana Naibu Katibu Mkuu Zitto na makamanda wengine, wanakwenda sasa kufanya kazi hiyo!
 
TAARIFA KWA UMMA

Mbali ya kukagua uhai wa chama mkoani Tanga, katika ziara hiyo, Mheshimiwa Zitto , pia atatumia fursa hiyo kuipeleka kwa wananchi na kuifafanua hoja yake aliyoiwasilisha bungeni katika mkutano ulioisha hivi karibuni juu ya zao za mkonge, ambapo baadhi ya wabunge wa Tanga, walisimama kuipinga hoja hiyo.

Hawa jamaa kweli ni nooouma. Kumbe ile hoja ya Zitto juu ya zao la mkonge Bungeni hivi majuzi ilikuwa ni one of the strategies za kupenya miongoni mwa ngome kongwe za *****. Nao (wabunge wa **** Tanga) kwa ujinga wao wakaingia kichwa kichwa bila kujua wenzao wanaangalia miles ahead. Sasa imekula kwao; wana kazi ya ziada kuondoa "sumu" itakayomwagwa. Bravo Zitto.
 
Mbali ya kukagua uhai wa chama mkoani Tanga, katika ziara hiyo, Mheshimiwa Zitto , pia atatumia fursa hiyo kuipeleka kwa wananchi na kuifafanua hoja yake aliyoiwasilisha bungeni katika mkutano ulioisha hivi karibuni juu ya zao za mkonge, ambapo baadhi ya wabunge wa Tanga, walisimama kuipinga hoja hiyo.
yaani akiipeleka hii hoja kwa wananchi wa Tanga , Magamba yatazidi kubabuka piga up CDM..
 
Hawa jamaa kweli ni nooouma. Kumbe ile hoja ya Zitto juu ya zao la mkonge Bungeni hivi majuzi ilikuwa ni one of the strategies za kupenya miongoni mwa ngome kongwe za *****. Nao (wabunge wa **** Tanga) kwa ujinga wao wakaingia kichwa kichwa bila kujua wenzao wanaangalia miles ahead. Sasa imekula kwao; wana kazi ya ziada kuondoa "sumu"
itakayomwagwa. Bravo Zitto.

nimelisema hilo hapo chini mkuu, yaani CCM wana hali mbaya kwa kweli
 
Hii ndo yenyewe,this way 2015 itakuwa kama kumsukuma mlevi,litokee kundi jingine liongozwe na naibu katibu mkuu visiwani mh Hamad kuelekea mikoa ya Lindi na Ntwara!

Ushauri mzuri. Mikoa ya Kusini itafanyiwa kazi kama ilivyo kawaida makamanda. Hakuna kulala.Naibu Katibu Mkuu Visiwani, Hamad Musa Yusuf ni mpambanaji sana, kama ilivyo kwa makamanda wengi wa CHADEMA. Anaweza kupangiwa kazi mahali popote bara na visiwani na akapiga mzigo. Asante.
 
Naomba muwaeleze wananchi wa Tanga umuhimu wa zao la mkonge na makosa yaliofanywa na serekali kuua zao hili. Inatia uchungu kuona kuwa pamoja na serekali kuwekeza kwa hali ya juu kwenye viwanda vya mkonge mkoani kwetu zao hili limieachwa kufa kifo cha kawaida. Kiwanda cha kamba Ngomeni na Mgombezi ni moja ya viwanda bora kwa kutengeneza mazao ya mkonge nakumbuka hata vilipowekewea hizo mashine kuna vijana walikwenda nje kusoma lakini sasa ni kama uwekezaji huu tumeutupa.
 
Mkuu usisahau kuwa CHADEMA iliwahi kupiga Operesheni Sangara kali sana mkoa mzima wa Tanga, mwaka 2009. Iliongozwa na Kamanda wa Anga, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, kisha ikamalizikia Same. Ilikuwa kali sana kiasi kwamba, iliwachanganya CCM na serikali yao pale mkoani. Nakumbuka, Mkuu wa Mkoa, Said Kalembo aliagiza watu wa usalama wafuatilie CHADEMA kw akaribu kujua wanafanya nini hasa, mikakati yao, wamejipangaje, pia wakaanza kuleta mikwara mikwara kwenye helkopta, wakitaka kuizuia, mara kuhoji kibali cha rubani na mambo kama hayo. Chama kipo sana mkoani Tanga, lakini kukagua uhai ni muhimu sana pia. Ndiyo maana Naibu Katibu Mkuu Zitto na makamanda wengine, wanakwenda sasa kufanya kazi hiyo!
Nashukuru kwa kunikumbusha mkuu. Nimekumbuka pia fitna za kuzuia chopa ya makanda isitue huko.Mwendo mdundo mpaka kieleweke. NitakuPM muda muafaka.
I hope Lindi, Mtwara and some parts of Coast region will come next.......
 
Hizi habari nimezipokea kwa furaha kubwa sana kupita maelezo kwani Tanga ni miongoni mwa mikoa michache inayoleta upinzani mkali kwa CHADEMA!
 
Mkakati mzuri! elimu ya uraia inahitajika zaidi katika eneo hilo! Hongereni makamanda kwa kuliona hilo, tuko pamoja.
 
Kuna taarifa ya kuwa Mheshimiwa Zitto atafanya ziara katika mkoa wa Tanga amabapo anatarajia kutembelea wilaya zote za mkoa huo. Napenda kutanguliza shukrani zangu kwako na uongozi kwa kuamua kufanya ziara hiyo huko na kuwaelezea wananchi lengo lako la hoja yako binafsi kuhusu zao la mkonge.Ukweli nataraji ziara yako iwe darasa la kuwaasha watu wa Tanga kwamba wakati umefika wa kuchagua uongozi unaojali wanachi.Kila la kheri mkuu !

tunamkaribisha kamanda hata mikoa ya jirani tutakuja
 
Back
Top Bottom