CHADEMA Kususa Mwenge na sherehe za miaka 50 ya UHURU ni KUKOSA UZALENDO

Mafilili kwa nini unatuhamasisha tuungane katika sherehe za uhuru miaka 50 uhuru ambao wengine hatujauona bado??????????
 
Hatukatai maendeleo yapo, ila ni kipimo kisichoendana na ilivyotakiwa kuwa. Hii ni sawa na mtu amepewa vitumbua ambavyo vinatosha kuwagawia watu kumi wapate vitatu kila mmoja, lakini huyo mtu akachukua kitumbua kimoja tu na kuwafinyia kwa ukucha kila mmoja halafu akaja kujisifu kuwa nimewalisha vema. Sasa hao watu waliopunjwa na wanajua siri ya dhuluma unadhani watakuwa na la kupongeza!, la hasha!
 
Hawa chadema ndio leo unagundua kuwa si wazalendo. Kama walidiriki kutoka nje ktk mchakato wa katba, uzalendo uko wapi hapo?. Hawa jamaa tunapaswa kuwapinga kwa nguvu zote.
 
Mafila nenda peke yako kwenye hili li mwenge na uhuru wa nchi iliyokwisha fukiwa na wasiotutakia mema.Tena namuunga mkono Dr. Slaa alivyosema akipata madaraka hilo limwenge anaenda kuliweka juu ya mlima kilimanjaro moja kwa moja.
 
Mafilili kwa nini unatuhamasisha tuungane katika sherehe za uhuru miaka 50 uhuru ambao wengine hatujauona bado??????????

Iwapo haujaona maendeleo, basi wewe ni kipofu ama hauna shukrani.

1. DSM - Mtwara ilikuwa unachukua zaidi siku 4 kwa basi; siku hizi masaa 8

2. DSM - Songea ilikuwa unachukua siku 3, siku hizi masaa 11

3. DSM - Bukoba ilibidi ipitie Kenya na Uganda; siku hizi moja kwa moja masaa 17 umefika.

Achana na itikadi za vyama, mnyonge MNYONGENI, haki yake MPENI!!!

Tatizo la watu wengine ni kuwa na wivu wa maisha na roho ya korosho. Mlizoea barabara nzuri ya kwenda Moshi. Ondoa roho mbaya maendeleo yametawanywa TZ, mashahidi ni wananchi walio wengi mikoani
 
Katika hili hata mimi ntawaunga mkono kwani hakuna lolote lililofanyika ktk miaka hii 50 inayotugarim hela nyingi zakufanya maandalizi huku kukiwa na watanyania ambao hawajui hata watakula nini
 
Yaani wanaoikomalia hiyo miaka 50 nawashangaa sana. Haina haja ya kuwalazimisha wananchi kusheherekea kitu ambacho hakipo mioyoni mwao. Mi naona hizo ni sherehe za serikali na viongozi wake. Hivi kweli ukimuuliza mwananchi wa kawaida amefaidika nn na hiyo miaka 50 ataweza kutoa takwimu ya mafanikio aliyoyapata kweli? Halafu ndio viongozi wamekomaa na takwimu za mafanikio zilizopo vitabuni (Intangible and invaluable achievements).
Kwanza wakoloni wenyewe walisharudi tena kututawala tangu zamani. Ona wanavyokamua madini yetu, ardhi yetu na kuthubutu kutuambia inabidi tutambue ndoa za jinsia moja! To hell with their puppets!
Mbio za mwenge hazina manufaa. Ni matumizi mabaya ya fedha zetu za kodi, huchangia maambukizi mapya ya VVU kila unapolala. Tena ina wezekana kuna vi-element vya ushirikina ndani yake.
Sio suala la CHADEMA tu, ni la kila mtu aliyeacha uvivu wa kufikiri ndiye anayeweza kugundua kwamba mwenge na sherehe za uhuru sio priorities kabisa katika nchi inayoongoza kwa kupewa misaada Afrika na ya tatu duniani!
 
Miaka hamsini tujipime kwa haya hapa, na si unafiki eti tumethubutu tumeweza na tunasonga mbele!

Year 2005/6 2006/7 2007/8 2008/9
Government Recurrent Revenue (Shs. billion) 2066.8 2739 3502.6 4293.1

Government Recurrent Expenditure (Shs. billion) 2649.9 3137.5 3796.9 4681.5

Government Development Expenditure(Shs. billion) 1385.2 1337.2 2201.1 2130.4
 
Maneno yako unaonyesha aidha ni mrundi ama una hasira za kukosa kuingia jumba la magogoni mwaka jana. Wewe kama ni mtz, utatembea kifua mbele kutokana na mafanikio ya miaka 50, sikulaumu sana kwa vile umri wako ni mdogo yaliyotokea baada uhuru huoni ni ya kujivunia.

Jaribu kukaa kitako na mama yako muulize kabla ya uhuru wao walizalishwa maeneo gani. Wewe hauna shukrani, UMEZALIWA zahanati, umeshoma shule ya msingi na sekondari bora.

Tujipongeze watz, TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!!!

HILI NALO JINGA, nani kakataa kuwa kuna maendeleo? wote tunakubali kuwa ccm imeleta maendeleo, lakini kwa kiwango cha maendeleo hayo ni aibu na ujinga kujisifu, maendeleo haya tuliyo nayo kama ingekuwa ni mwaka 1985, ingekuwa ni halali.
 
Maneno yako unaonyesha aidha ni mrundi ama una hasira za kukosa kuingia jumba la magogoni mwaka jana. Wewe kama ni mtz, utatembea kifua mbele kutokana na mafanikio ya miaka 50, sikulaumu sana kwa vile umri wako ni mdogo yaliyotokea baada uhuru huoni ni ya kujivunia.

Jaribu kukaa kitako na mama yako muulize kabla ya uhuru wao walizalishwa maeneo gani. Wewe hauna shukrani, UMEZALIWA zahanati, umeshoma shule ya msingi na sekondari bora.

Tujipongeze watz, TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!!!

Nimesikitishwa na kauli zako hizi. Hamsini ni namba, kama zilivyo zingine. Kwanza wenzako kwenye ccm hawataki tukubali kuwa ni miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, unafiki wao unataka kupoteza historia ya nchi ya Tanganyika, sijui wewe unatoa wapi ujasiri wa kuitaja Tanganyika.

Baada ya miaka hamsini tumepiga hatua Kidogo tena kwa mwendo wa kinyonga. Linganisha maendeleo yetu wakati wa uhuru na nchi za asia, angalia rasilimali tulizonazo kisha linganisha na maendeleo yaliyopo sasa. Lazima uwe mpumbavu kutaka tukubaliane nawe kuwa tumepiga hatua za kuridhisha za maendeleo. Sioni huko 'kuthubutu' wamethubutu nini, 'Kuweza' wameweza nini na 'Kusonga mbele' kuelekea wapi? Ukiniambia 'Mmethubutu kuifilisi nchi' sawa, 'Mmeweza Kuifilisi nchi' sawa na 'Mnaendelea kuifilisi nchi' sawa. Hata hivyo mwisho wa ccm na serikali yake uko karibu. Bora muanze kufungasha.

Miaka hamsini ya Tanganyika sawa, lakini hatuna cha ajabu tulichofanya kinachostahili sifa mnazotaka mpewe.
 
Katika hili swala la Mwenge na Maadhimisho ya miaka 50 ya UHuru wa Tanganyika kusema kweli mimi sintakubaliana na Chadema na kwa sababu zangu maana mimi ni Mhafidhina na Utaifa wangu unatangulia kwanza hata kama kesho Afrika itaungana na kuwa nchi moja.

Tafisri ya neno UHURU itabakl palepale kama siku wananchi wa nchi fulani wamepoata UHURU wao, ikiwa na maana hoja ni WATU waliokuwa huru ktk mipaka ya NCHI hiyo. Na UHURU huu unaweza weka mipaka ama kupunguza mipaka lakini kitu muhimu ni raia wananchi wake kuondokana na kutawaliwa..Na kama nilivyosema, kila nchi ina WATU na MZINGIRA tofauti hivyo hatuwezi kuiga nchi kama Mareakani ambayo inasherehekkea Uhuru wake July 4, kwa sababu ndiyo siku nchi hiyo ime declare Uhuru kutoka kwa koloni la Muingereza na zikiwemo nchi 13 tu, leo hii zimefikia 50 na zaidi na bado wanaweza kuongeza nchi nyingine wakiendelea kutumia jina la USA..

Tofauti na wao, sisi tumebadilisha jina baada ya kuunganisha nchi zetu mbili bila kufikiria mbele maana ni asili yetu kufikiria kwa marefu ya mkono. Kesho tukiungana na Kenya au Uganda lazima tutabadilsiha jina na vivyo hivyo maana Muungano wetu bado una tabaka za kijamii ambazo tumeshindwa kuzivunja. Zanzibar wana/taendelea kusherehekea siku ya Mapinduzi na halali kwao lakini haramu kwa Bara kusherehekea Uhuru wao. Kwa nini tunajaribu sana kujidanganya? ukweli unabakia kwamba Bara ipo ni nchi ambayo kisiasa tu tunaindoa ktk ramani lakini hatuwezi kufuta historia kwa siasa vile vile, Mungu apitishie mbali kesho Muungano ukifa tutarudi kwa nani?

Na kwa nini watu waseme tusherehekee miaka 50 ya Tanzania ifikapo April 2014 ikiwa hizo zitakuwa sherehe za Muungano wa nchi ambazo tayari zilikwisha kuwa HURU.. Je kweli tunakubali kupoteza historia ya UHURU wetu kwa siasa na majivuno ambayo ndiyo yalipelekea tukasahau hata kuweka kumbukumbu za vita ya Maji Maji, ukweli kamili wa biashara za Utumwa, tukawasahau wazee walioshiriki kuupata Uhuru wetu ambao kesho ktk sherehe hizi tunatakiwa kuwatunukia tunu za Ushujaa..

Jamani Watanzania wenzangu, kwa mara ya kwanza tuwe na roho ya kitajiri maana umaskini huja na mengi. Leo hii hata Mwenge umepoteza maana yake kabisa kwa sababu wananchi wameshindwa kuikubali hali halisi na hivyo mwenge unawakumbusha machungu tu. Wanafikiria gharama ya kuutembeza Mwenge lakini hawataki kupunguza posho zao wala kuacha mashangingi yao. Wanafikiria gharama za Mwenge lakini watazame ktk maharusi wakinunua pete za mamillioni zenye vito vinavyopatikana ndani ya ardhi yao. Wasifikirie haya na jinsi leo tunavyotawaliwa ktk mazingira ya ajabu ajabu lakini haramu kujikumbusha tulikotoka na tunataka kwenda wapi.

Mimi kusema kweli siku hiyo nitasimama na kufanya kitu kama Yoga, yaani nita meditate na kukumbuka nili/tulikotota, kumshukuru Mungu tumefika hapa tulipo japokuwa maskini na tuna matatizo yetu ya ndani... kumbukumbu hii ya Uhuru itanipa ari zaidi kuendelea kudai Haki na UHURU walopigania wazee wangu hata kama umeporwa na jamaa zetu.
 
mwenge ni wizi mtupu kazi kukata mishahara ya watumishi bila ridhaa yao next kuhamasisha ngono na kueneza ukimwi mahali mwenge unapolala
 
mafillliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii we need men hu can dream of things that never were, bt pamoja na utandawaz wote huu wa karne hii ya 21 still honering the wastless effort made in 50yrs na ccm wakat unaona kabisa picha nzima yz uchumi wetu, 50yrs score nchi haina ndege zake stable zaid zaid ni mitumba ambayo haielewek, 50yrs score serikali inapokea amri kutoka uingereza za kuwakamata na sue mafisadi wa manunuz ya rada, 50yrs score serikali haijui hata inachokisherehea kinaitwaje bcoz uhuru wa tanganyika ulikufa mwaka 64 na sijui hii nchi iitwayo tanzania bara imetokea wap na bendera yake ikoje na ipo kwenye geographia gan? angalia kijana naona ur mind is to small to cope with de 21st-century's demands of its men being
 
Waungana katika pitapita zangu nimegundua wana CDM hawafurahi TZ kusheherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Dalili zimejoinyesha;-

1. Viongozi wao katika ngazi zote kutoshiriki vikao vya maandalizi ya Mwenge wa Uhuru
2. Viongozi wao kushindwa kushiriki kuukimbiza mwenge ulipofika katika maeneo yao; mfano Ubungo (mhe.Mnyika) na Kawe (mhe. Mdee ).
3. Wabunge wao wameshindwa kushiriki katika vikao vya maandalizi ya miak 50 ya uhuru pasipo kutoa udhuru.

Watanzania inabidi tutumia akili ya mbaimbawi tuwahukumu CDM katika masanduku ya kura kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2012 na tuwape kichapo kikubwa uchaguzi mkuu 2015. Hawa wamekosa uzalendo, wamebaki kushabikia sera za Mfadhili wao David Cameroon.

Nini cha kusherehekea? Washerehee mfumuko mkubwa wa bei unaosababishwa na serikali dhaifu? washerehekee Tanzania bara ambayo kikatiba haipo? Mwambie aliyekutuma atamke wazi kuwa tunasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ambayo haina serikali... Shame on you CCM.

Je, viongozi wa CDM, wafuasi wao na watanzania washerehekee uwepo wa shule nyingi za kata zisizo na walimu, madawati, vitabu na maabara? Je, watoto wa aliyekutuma wanasoma katika shule hizo?

Tusherehekee kukosa dawa katika hospitali za serikali; viongozi wa serikali legelege wanatibiwa India
 
Tunafanya sherehe kushangilia hali hii?
View attachment 42840View attachment 42841 kasi mpya 4.jpg
 
Mwenge ni KOROBOI au KIBATARI cha wadanganyika kwa sababu ya kutokuwa na umeme wa uhakiki kila siku migao haiishi.

Mwenge ni KOROBOI linalotukumbushia migao ya umeme ya kila mwaka.
 
Katika hili swala la Mwenge na Maadhimisho ya miaka 50 ya UHuru wa Tanganyika kusema kweli mimi sintakubaliana na Chadema na kwa sababu zangu maana mimi ni Mhafidhina na Utaifa wangu unatangulia kwanza hata kama kesho Afrika itaungana na kuwa nchi moja.

Tafisri ya neno UHURU itabakl palepale kama siku wananchi wa nchi fulani wamepoata UHURU wao, ikiwa na maana hoja ni WATU waliokuwa huru ktk mipaka ya NCHI hiyo. Na UHURU huu unaweza weka mipaka ama kupunguza mipaka lakini kitu muhimu ni raia wananchi wake kuondokana na kutawaliwa..Na kama nilivyosema, kila nchi ina WATU na MZINGIRA tofauti hivyo hatuwezi kuiga nchi kama Mareakani ambayo inasherehekkea Uhuru wake July 4, kwa sababu ndiyo siku nchi hiyo ime declare Uhuru kutoka kwa koloni la Muingereza na zikiwemo nchi 13 tu, leo hii zimefikia 50 na zaidi na bado wanaweza kuongeza nchi nyingine wakiendelea kutumia jina la USA..

Tofauti na wao, sisi tumebadilisha jina baada ya kuunganisha nchi zetu mbili bila kufikiria mbele maana ni asili yetu kufikiria kwa marefu ya mkono. Kesho tukiungana na Kenya au Uganda lazima tutabadilsiha jina na vivyo hivyo maana Muungano wetu bado una tabaka za kijamii ambazo tumeshindwa kuzivunja. Zanzibar wana/taendelea kusherehekea siku ya Mapinduzi na halali kwao lakini haramu kwa Bara kusherehekea Uhuru wao. Kwa nini tunajaribu sana kujidanganya? ukweli unabakia kwamba Bara ipo ni nchi ambayo kisiasa tu tunaindoa ktk ramani lakini hatuwezi kufuta historia kwa siasa vile vile, Mungu apitishie mbali kesho Muungano ukifa tutarudi kwa nani?

Na kwa nini watu waseme tusherehekee miaka 50 ya Tanzania ifikapo April 2014 ikiwa hizo zitakuwa sherehe za Muungano wa nchi ambazo tayari zilikwisha kuwa HURU.. Je kweli tunakubali kupoteza historia ya UHURU wetu kwa siasa na majivuno ambayo ndiyo yalipelekea tukasahau hata kuweka kumbukumbu za vita ya Maji Maji, ukweli kamili wa biashara za Utumwa, tukawasahau wazee walioshiriki kuupata Uhuru wetu ambao kesho ktk sherehe hizi tunatakiwa kuwatunukia tunu za Ushujaa..

Jamani Watanzania wenzangu, kwa mara ya kwanza tuwe na roho ya kitajiri maana umaskini huja na mengi. Leo hii hata Mwenge umepoteza maana yake kabisa kwa sababu wananchi wameshindwa kuikubali hali halisi na hivyo mwenge unawakumbusha machungu tu. Wanafikiria gharama ya kuutembeza Mwenge lakini hawataki kupunguza posho zao wala kuacha mashangingi yao. Wanafikiria gharama za Mwenge lakini watazame ktk maharusi wakinunua pete za mamillioni zenye vito vinavyopatikana ndani ya ardhi yao. Wasifikirie haya na jinsi leo tunavyotawaliwa ktk mazingira ya ajabu ajabu lakini haramu kujikumbusha tulikotoka na tunataka kwenda wapi.

Mimi kusema kweli siku hiyo nitasimama na kufanya kitu kama Yoga, yaani nita meditate na kukumbuka nili/tulikotota, kumshukuru Mungu tumefika hapa tulipo japokuwa maskini na tuna matatizo yetu ya ndani... kumbukumbu hii ya Uhuru itanipa ari zaidi kuendelea kudai Haki na UHURU walopigania wazee wangu hata kama umeporwa na jamaa zetu.

Tulipata uhuru... lakini umeporwa na wakoloni weusi...Magamba
 
Nini cha kusherehekea? Washerehee mfumuko mkubwa wa bei unaosababishwa na serikali dhaifu? washerehekee Tanzania bara ambayo kikatiba haipo? Mwambie aliyekutuma atamke wazi kuwa tunasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ambayo haina serikali... Shame on you CCM.

Je, viongozi wa CDM, wafuasi wao na watanzania washerehekee uwepo wa shule nyingi za kata zisizo na walimu, madawati, vitabu na maabara? Je, watoto wa aliyekutuma wanasoma katika shule hizo?

Tusherehekee kukosa dawa katika hospitali za serikali; viongozi wa serikali legelege wanatibiwa India
Labda nikuulize wewe WHO are YOU! leo hii.. wewe unajiita Mtanzania wakati umetawaliwa na CCM hiyo hiyo na utasherehekea Muungano lakini sii Uhuru ambao vyote vimetokana na CCM.. Jamani ebu nambie kweli nyie ni akina nani leo hapo mlipo!
 
Tatizo tulichagua vipofu watuongoze. Matokeo yake tumeingia shimoni. Angalia vipaumbele vyao, ngoma, safari zisizoisha, tafrija kila kukicha namaanisha (Juzi kaja bush tafrija), kujichotea posho nne nne, kujiongeza posho za kusinzia bungeni, kujilipa transit allowance kwa safari ya masaa manne, kujilipa travelling allowance ndani ya transit allowance, posho ya mabosi, posho ya kuwajibika, posho ya kukirimu wageni, nadhani sasa kutokana na kuvimbiwa posho wataanzisha posho ya kupunguza uvimbe wa posho. Na ndio sababu kuu za maendeleo ya sherehe. Kwa hili la kusherehekea kusherehekea, tumepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo. Hivi ni mwaka gani hazikufanyika sherehe kubwa za uhuru wa Tanganyika tangu JK ashike madaraka? Nini faida ya mwenge wa uhuru wa leo?
Tumeacha kushughulikia mambo ya msingi tumekalia upuuzi tu. Kilimo kwanza tumeimbiwa weeeeeee mpaka leo wajinga fulani hawajafikisha pembejeo mashambani wakati msimu wa kilimo umeanza. Matrekta toka mwaka jana yapo DSM, juzi kagasheki (naibu waziri wa Mr. Misifa) kapigwa picha ati anakabidhi trekta DSM????!!!!!!
Simamieni sera zenu si kuruka ruka na visherehe visivyo na tija stupid.
 
Mafilili mwanangu, mafilili,
Ebu kuwa mzalendo japo kidogo,
Baba kumnunulia shati mtoto wake sio maendeleo ni wajibu, serikali kujenga barabara ni wajibu wake kwani wananchi wanalipa kodi na hiyo serikali ndio inasimamia mali asili zote,
Miaka 50 ya UHURU sijui wa wapi, bado tunategemea hela zilizorudishwa na wezi kuinua elimu, mwana mafili fili we,
Miaka 50 ya Uhuru, kikundi kidogo cha waTanzania ndio wenye uhakika wa milo mitatu kwa siku, asilimia kubwa ni afadhali ya jana,
Mwanetu Mafili fili, miaka ya awali iliwezekana kusomesha watoto bure, leo hii miaka 50 ya uhuru ni balaaaaaaaa, jiulize
Mtoto wewe unaetazama lakini hauoni, mafili fili, miaka 50 ya uhuru wakina mama wanaletewa Bajaj za kuwapeleka hospital wakati hakuna barabara za kuaminika
We mtoto, miaka hamsini ya uhuru, mshahara kwa mwezi ni 250,000/= kwa mtumishi wa serikali wakati posho ya waheshimiwa ni 300,000/= kwa siku
Najua unasikia lakini hauelewi, makampuni makubwa ya madini yanavyochota madini yetu na kutuachia mashimo, na sehemu nyingine kuwanywesha sumu wana wa nchi hii, toa kamasi kwanza ktk ubongo wako, mwanagu mpenzi
Lini utakuwa WE mtoto, uache ukojozi wako, ili uone wanaoitwa wawekezaji wakikwepa kodi kila baada ya miaka 5 kwa kubadili majina ya makampuni yao, huku wakilipa fadhila za suti na kulipiwa chumba kwenye mahoteli viongozi wetu
Ni muda wako wa kuoga, nenda, usije ukayasikia haya ya mwizi wa mamilioni akibembelezwa arudishe, na mwizi wa kuku akifungwa jela miaka 20.
Nenda kalale, labda ukiamka utaelewa.
 
Back
Top Bottom