CHADEMA kusambaratika ndani ya mwaka mmoja ujao - Wassira

Huenda alishatega timing bomb huko CDM na anaona linakaribia kulipuka! Haya mambo ya siasa magumu kweli. Watu hatukuamini kama NCCR ingesamabaratika na kubaki historia. Nikikumbuka NCCR ya 1993 ikaja ile ya Mrema ya 1995 na kisha ukaja ule msambaratiko wa Tanga naogopa. Nikikumbuka akina Marando, Selasini na Komu kuwa walikuwepo Tanga siwezi kusema kitu hadi tufike 2015 na kuipita CDM ikiwa salama.

Mkuu bomu lipo tayari, ni Shibuda. CDM wasiposhituka na kulitegua mapema. Anachosema Wasira kitatokea , nadhani mitambo wameshaiseti tayari na pandikizi lao limeanza kutema cheche.
 
Huenda alishatega timing bomb huko CDM na anaona linakaribia kulipuka! Haya mambo ya siasa magumu kweli. Watu hatukuamini kama NCCR ingesamabaratika na kubaki historia. Nikikumbuka NCCR ya 1993 ikaja ile ya Mrema ya 1995 na kisha ukaja ule msambaratiko wa Tanga naogopa. Nikikumbuka akina Marando, Selasini na Komu kuwa walikuwepo Tanga siwezi kusema kitu hadi tufike 2015 na kuipita CDM ikiwa salama.
Kimbunga,
Mimi mpaka leo naamini kuwa kilichoiua NCCR ni tamaa ya kuipiku CDM kipindi kile 1995 kwa kumpa Mrema uenyekiti kinyemela bila kuangalia long-term effects za uamuzi ule. CDM haijaanza kuwa tishio miaka hii. Wakuu walipoangalia kile kikosi cha wale wazee waanzilishi, walijua siku moja hiki chama kitakuja kuwa tishio kwao. Marando anaweza kuwa CDM leo, lakini alichangia sana ku-slow down ukuaji wa CDM. Wengine hata tunapokuta hawa kina Komu ndio wakurugenzi wa idara nyeti tunahoji kulikoni? Hata hivyo CDM imekua kitaasisi tofauti na NCCR iliyokuwa mgongoni kwa Mrema, hivyo hata tishio la kusambaratishwa na mtu silioni.
 
Isaya 54:17,Kwilasa silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na Kwilasa bulimic utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa ni makosa........!

"Listen Ccm, chadema its not only a party! Its a point of change an revolution to our country! I'm trying to imagine bila chadema kutumiwa na Mungu kwa ajili mambo yote Haya toka. 205 hadi leo tingekuwa wapi? So tanzanians we are praying for t! Na Mungu atasimama kutitetea!

Mkuu hapo umegusa penyewe na Mungu wa israel akubariki kwa ujumbe mzuri kwa huyu fedhuri wassira.
 
Kimbunga,
Mimi mpaka leo naamini kuwa kilichoiua NCCR ni tamaa ya kuipiku CDM kipindi kile 1995 kwa kumpa Mrema uenyekiti kinyemela bila kuangalia long-term effects za uamuzi ule. CDM haijaanza kuwa tishio miaka hii. Wakuu walipoangalia kile kikosi cha wale wazee waanzilishi, walijua siku moja hiki chama kitakuja kuwa tishio kwao. Marando anaweza kuwa CDM leo, lakini alichangia sana ku-slow down ukuaji wa CDM. Wengine hata tunapokuta hawa kina Komu ndio wakurugenzi wa idara nyeti tunahoji kulikoni? Hata hivyo CDM imekua kitaasisi tofauti na NCCR iliyokuwa mgongoni kwa Mrema, hivyo hata tishio la kusambaratishwa na mtu silioni.

Well said mkuu wangu
 
Asante sana mzee Sitta kwa kusema kuwa kuna viongozi wanaofikiri kwa kutumia matumbo. Nashukuru huyu mzee wa tabia pono amejirahisha tumemjua.
 
Asante sana mzee Sitta kwa kusema kuwa kuna viongozi wanaofikiri kwa kutumia matumbo. Nashukuru huyu mzee wa tabia pono amejirahisha tumemjua.

Usintanie mkuu.Sitta alitamka kweli haya maneno kumlenga Wasira?
 
Kauli kama hizi ni kero kwetu wanachama hai wa NCCR, sisi hatujabaki historia tupo na tunaendelea kuwepo. Maneno yenu mengine yanatukosea adabu

Duuuh! Kumbe bado NCCR ipo na inawanachama.. Sijawahi kusoma kabla mwanajf akijitanabaisha NCCR..

Pole mjumbe!
 
kazi ya uwaziri imemshinda na sasa kaigeukia ya utabiri jamani kimbunga ni nouma namkumbuka mh Sugu pale bungeni akichangia hoja ya CAG,
 
Kama nguvu wanazotumia kushughulikia kujua nini kinatokea na kitakachotokea CDM katika kutatua matatizo ya nchi kama uchumi na ajira kwa vijana Tanzania ingekuwa mbali sana.

Badala ya kutabiri neema kwa watanzania kwa serikali ya CCM kuwaletea yale yaliyoshindikana kwa miaka 50 yeye anatabiri kusambaratika kwa chama cha siasa?. Kweli mti utundao ndio upopolewao na mawe.
 
Hivi yule waziri wa maliasili na utalii hajaanza kazi rasmi!!? Mbona harudishi wanyama waliotoroshwa mbugani na kupelekwa ikulu eti wazungu wasipate tabu ya kwenda maporini!!?

Hii hee kumbe hiyo nyara ya taifa! chausingizi nae analopoka tu,apelekewe jimboni kwake M4C hima,yaeleke anaongea kinyume huyu. Huwa ni kawaida kuchekana hao eti anamwambia mwenzake nyuma umeungua kumbe naye yupo vivyo hivyo.
 
Nadhani wamekosea sana kumtumia Shibuda kwa wakati huu.Wangekuwa wajanja wangemwambia Shibuda azushe vurugu kipindi cha kukaribia uchaguzi mkuu.

Tatizo hakuna asiyejua kuwa Shibuda yuko kazini! hana jipya.
 
Ata viongozi wa cdm 50% wakiamua kusaliti. cdm imeingia mpaka kwenye ukucha wa wa-tz 94%. Hata wanafunzi wa form2 sikuhizi ni wana-cdm wasio na kadi. Atachora chini na goti.
 
Mkuu wangu Slaa hajawahi kusema chochote kibaya kwa hiyo atakayemsema vibaya nitamshambulia.Lakini Wasira anasema wazi amepandikiza mamluki CDM ili waiue huoni ni uhuni huo? Ningekuwa na baba wa aina hii ningemkana siyo baba yangu.Wasira akitaka aheshimiwe ajiheshimu kwanza mwenyewe!

mkuu hawa magamba ni hovyo tu na dawa yao na ss ni kuwapiga na siasa za majitaka maana ustarabu walishashindwa.
 
viongozi aina ya wasira ni janga la taifa maana wanafikiria matumbo yao.!
 
Back
Top Bottom