CHADEMA kupoteza mashabiki na wanachama ikiwa watamruhusu Sumaye kujiunga

mpigauzi

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
275
71
Wakuu habari za weekend. Wiki hii magazeti mengi yameandika habari za Sumaye kuteta na CDM kuhusu mipango yake ya kuangalia kujiunga na CDM. Ikumbukwe Sumaye ndiye waziri mkuu ambaye wakati wa utawala wa awamu ya tatu alisimamia ubinafsishaji wa mali za umma. Na katika hilo mali nyingi alijiuzia ikiwemo MT MERU HOTEL ya Arusha.

Inashangaza sana leo hii huyu ambaye ni fisadi anawesema wenzake kuwa ni mafisadi. Hivi yeye na Lowasa nani ni msafi. Asitake kuwadanganya watanzania kuwa anapigania haki zao wakati alishindwa akiwa waziri mkuu.

Tahadhari tu, iwapo CDM watampokea huyu jamaa, basi wajue ndoto yao ya kuongoza nchi ndiyo mwisho, kwani watu wengi watakimbia na kuona nacho ni chama cha mafisadi.

CDM inatakiwa ijifunze kwa Shibuda, watu wanaojiunga nacho ili wapate uongozi kamwe hawatasaidia Chama zaidi ya kukivuruga kwa uchu wa madaraka.
 
Mr.Sumaye siyo kama Mr.shibuda, pia CDM ni chama kikubwa na chenye utashi mkubwa, CDM imeweka mbele kanuni na taratibu na siyo maslahi binafsi ya mtu.
 
TAFAKURI: Siyo kweli kuwa watapoteza ila watapata sana kama atajiunga kama mwanachama wao. ILA kama watamchukua kama mgombea U-rais watapoteza sana. Hata kwa Shibuda hawakupoteza ila walipata kwa kuongeza namba ya viti mbungeni, ruzuku na idadi iliyowatosha kuwa kambi rasmi ya upinzani Mbungeni. Nafasi yake ndani ya chama hana madhara
 
kujiunga na chama tuu sio tatizo, ila kwenye uongozi hana jipya atavuruga atmosphere.... Ikumbukwe enzi zake ilifikia kuitwa zero kwa sababu za kupwaya kwake kwenye uongozi!! leo hii ana lipi jipya la kumfanya aonekane wa maana????
 
CDM wako makini katika kila jambo wanalolitaka na kuamua kulifanya. So wala usiwe na wasiwasi!!!!!
 
sidhani kama imekaa vizuri Sumaye kujiunga Chadema,ni sawa na kumchukua Chenge au Mafisadi wengine ndani ya ccm wajiunge Chadema,Sumaye na shemeji yake Mkapa walifanya ufisadi mkubwa sana na ccm wanalijua hilo,uongozi wa Chadema ufikirie mara mbili kabla hawajamchukua huyu jamaa,anaweza kusaidia kuimarisha chama au kukivunjilia mbali
 
ye sumaye yamemshinda ya ccm ya chadema atayaweza? zitto urais wako 2015
 
kujiunga na chama tuu sio tatizo, ila kwenye uongozi hana jipya atavuruga atmosphere.... Ikumbukwe enzi zake ilifikia kuitwa zero kwa sababu za kupwaya kwake kwenye uongozi!! leo hii ana lipi jipya la kumfanya aonekane wa maana????

Hakika mkuu umenena. Huyu jamaa anang'ang'ania uongozi wakati hawezi. Hivi kama waziri mkuu mstaafu anataka nini tena. Maana analipwa kila kitu
 
sidhani kama imekaa vizuri Sumaye kujiunga Chadema,ni sawa na kumchukua Chenge au Mafisadi wengine ndani ya ccm wajiunge Chadema,Sumaye na shemeji yake Mkapa walifanya ufisadi mkubwa sana na ccm wanalijua hilo,uongozi wa Chadema ufikirie mara mbili kabla hawajamchukua huyu jamaa,anaweza kusaidia kuimarisha chama au kukivunjilia mbali

Yaani mkuu sioni buton ya like, ngoja niitafute nikugongee
 
Subirini muone kitakachojiri kuliko kuanza kusema vitu ambavyo bado havipo,Sumaye ni mtu mdogo sana katika safu ya CDM na hata kama ataingia CDM atakuwa kama Mabere Marando.pro Safari,Arcado Ntagazwa na wengine walioamua kuingia CDM.
 
TAFAKURI: Siyo kweli kuwa watapoteza ila watapata sana kama atajiunga kama mwanachama wao. ILA kama watamchukua kama mgombea U-rais watapoteza sana. Hata kwa Shibuda hawakupoteza ila walipata kwa kuongeza namba ya viti mbungeni, ruzuku na idadi iliyowatosha kuwa kambi rasmi ya upinzani Mbungeni. Nafasi yake ndani ya chama hana madhara

Mkuu ni bora kukosa hiyo ruzuku kuliko mparaganyiko aliouleta. Hapa tusiangalie vitu vidogo kama hivi. Ni watu kama hawa unapowafukuza athari zake kwa chama zinakuwa kubwa. Angalia ya madiwani wa Ars na Mza
 
Subirini muone kitakachojiri kuliko kuanza kusema vitu ambavyo bado havipo,Sumaye ni mtu mdogo sana katika safu ya CDM na hata kama ataingia CDM atakuwa kama Mabere Marando.pro Safari,Arcado Ntagazwa na wengine walioamua kuingia CDM.

Hao wote walikuwa ni wasafi kwa kiasi fulani tofauti na huyu fisadi. Yaani unataka kuniambia hata Lowasa na Chenge wakishindwa CCM wapolkelewe CDM. Mkuu hapa bado hujanikuna
 
Sio suala la kukukuna bali kama wataingia CDM hakuna atakayepata cheo na watakuwa ni wanachama wa kawaida tu kama walivyo hao niliowataja.
Kuna wakati inabidi ukae na shetani ili uweze kujua anafanyaje ushetani wake hivyo kuwaogopa Lowassa na mafisadi wengine si hoja wanaweza kuja CDM na unawafungulia mashitaka wakiwa ndani maana watakuwa wamekwishasema ukweli na tutakuwa na ushahidi juu yao.
Ni heri kuishi na shetani unayemjua kuliko kuishi na malaika usiyemjua(kumbuka shetani alitokana na malaika)
 
Tutamtumia Sumaye kisiasa kuidhoofisha CCM, anajua siri nyingi kwanini tusimtumie, hatapata uongozi wowote ila tutampa jukwaa la kuichafua CCM! Hizo ndo siasa! Wanachadema tuache hofu!
 
Kwanza akijiunga na CDM hata kugombea ubunge mbona kazi maana nadhani jimboni kwake kuna Rose Kamili ambaye alikuwa mgombea ubunge,labda agombee udiwani
 
kwanini viongozi wa ccm washindwe uchaguzi kwanza, ndio wakimbilie CDM? Je wangeshinda wangeijua CDM? Kama atapokelewa kama mwanachama , that is good! akae akomazwe na sera za kimapinduzi kwanza.Kimtazama haijulikani kama baadae cdm ikikamata dola ,nae atakuja kuwalinda wapora mali wenzie kina mkapa na genge lake.BE CAREFUL
 
Wakuu habari za weekend. Wiki hii magazeti mengi yameandika habari za Sumaye kuteta na CDM kuhusu mipango yake ya kuangalia kujiunga na CDM. Ikumbukwe Sumaye ndiye waziri mkuu ambaye wakati wa utawala wa awamu ya tatu alisimamia ubinafsishaji wa mali za umma. Na katika hilo mali nyingi alijiuzia ikiwemo MT MERU HOTEL ya Arusha.

Inashangaza sana leo hii huyu ambaye ni fisadi anawesema wenzake kuwa ni mafisadi. Hivi yeye na Lowasa nani ni msafi. Asitake kuwadanganya watanzania kuwa anapigania haki zao wakati alishindwa akiwa waziri mkuu.

Tahadhari tu, iwapo CDM watampokea huyu jamaa, basi wajue ndoto yao ya kuongoza nchi ndiyo mwisho, kwani watu wengi watakimbia na kuona nacho ni chama cha mafisadi.

CDM inatakiwa ijifunze kwa Shibuda, watu wanaojiunga nacho ili wapate uongozi kamwe hawatasaidia Chama zaidi ya kukivuruga kwa uchu wa madaraka.

Mkuu, yawezekana hoja yako ina mantiki, lakini ninaamini hata ndani ya CDM mafisadi wamo pia japo yawezekana siyo viongozi.
Iwapo huyo Mhe. atataka kujiunga kama mwanachama mwingine yeyote wa kawaida na si kwa sharti la kupewa uongozi au kuruhusiwa kugombea urais, mimi binafsi sioni tatizo. Aruhusiwe kujiunga.

Binafsi ninalichukulia hilo kama kuongoka baada ya kubaini madhambi yake. Ninaimani hata hao wanaoitwa kwa sasa mafisadi wapo baadhi watajirudi na kuomba kujiunga na CDM baada na hata kabla ya 2015. Subiri utaona.
 
Kama Ccm haikupoteZa wanachama alipojiunga Tabwe hizza ,sasa iweje kupokea mtu Mwenye akiili timamu ?
 
Back
Top Bottom