Chadema kupiga mbizi maandamano ya Kigamboni kesho?

Ground Zero

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
342
95
Kuna tetesi kwamba cdm inapanga maandamano kesho kupinga ongezeko kubwa ya nauli ya kivuko. Je kwa kuwa wanapinga nauli mpya, itawabidi wapige mbizi au watatii amri ya magufuli ya kulipa nauli mpya?na wakilipa si watakuwa wameunga mkono?tujadili

GZ
 
bandugu, tuache ushabiki, katika vitu vyoooote kila kukicha vinapanda nyie mlichokiona tu ni ongezeko la sh. mia, ile miposho mbona kimya, mafuta pia kimya, gharama za umeme pia kimya wakati hizi ndo zinawagusa watanzania wengi,
 
Utakubali kiaina utakubali kiaina.magufuri anawapenda sana wakazi wa kigambonino.ameshauri kupiga mbizi imekua nongwa mbona juzi bonde la jangwani watu wamepigambizi.alafu kupiga mbizi bigdill anaweza kupatikana bingwa wa kuogelea akatuwakilisha olimpiki..mr pombe bwana good idea.
 
bandugu, tuache ushabiki, katika vitu vyoooote kila kukicha vinapanda nyie mlichokiona tu ni ongezeko la sh. mia, ile miposho mbona kimya, mafuta pia kimya, gharama za umeme pia kimya wakati hizi ndo zinawagusa watanzania wengi,

kuna ukweli uliojificha wananchi wa kigamboni hawapingi kulipa sh 200 ila wanachopinga ni ongezeko la nauli kwa wenye maguta kutoka sh200 hadi sh 1800 hii itasababisha gharama za maisha kupanda sababu wafanyabiashara wengi utumia usafiri huo kubeba bidhaa kutoka mjini na kama unavyojua hizo gharama atabeba mtumiaji wa bidhaa
 
Inawezekana pia ni kufikisha ujumbe kuwa kigamboni ni mji mpya kwa hiyo wasiweza kumudu gharama za maisha wahame wenyewe kuipunguzia serikali gharama za kuhamisha watu mradi utakapo anza.
 
Kesho kwenye maandamano hayo kutakuwa na Masomo bure ya kupiga mbizi??
 
Jambo la kwanza CDM hawana mpango wa kuandamana. Inaonesha kuwa mtu akitaka thread yake ishike kasi basi lzm ajumuishe CDM au Dr.Slaa (Daktari wa ukweli, sio a.k.a za kupewa na mashemeji).

La pili ni kuwa hiyo sh mia mbili ni moja tu ya kichefuchefu cha mamlaka zinazotuongoza. Guta na pikipiki ndio mzozo wa kigamboni kwani ndio vifaa vinavyoendesha uchumi mdogo wa huko. Kulitoza guta 1800 ni kupandisha bei ya nyanya, viazi, kitunguu, bamia n.k ambavyo wote twajua vinafika huko kwa maguta.

Na baya zaidi ni kuwa, si kweli kuwa 100 haikutosha kuendesha kivuko bali tatizo ni kuwa fedha zinaishia mifukoni kwa watumishi.

STENDI YA MKOA:
Kuingia pale tu kumsindikiza ndugu yako unatoa 200. Kiukweli sijui ni ya nini kwani huko ndani hata choo ni cha kulipia. Napo kama feri, mapato ni mengi lkn yanaishia mifukoni mwa watu na hata hayo yanayokusanyika sijui yanafanya shughuli gani za uboreshaji manake kila sehemu kumebanduka.

Badala ya kuandamana kupinga mambo ya maana, kwa nini tusiandamanage kupinga haya ya wizi?! Au tunadhania ni fedha chache kwa kuwa ni 200' 200?
 
Back
Top Bottom