CHADEMA kupata ofisi mpya ya Makao Makuu-Mwenge

Nadhani pale sio Mwenge ni Mikocheni...angalizo Chadema kuweni makini kuna baadhi ya vitu chama kinatakiwa kufanya kwa nguvu zake, siku Sabado hakiwa hayupo familia yake wakalitaka jengo lao itakuwaje?

maandishi ndo yana matter. Shughulisha ubongo wako we kilahaza.
 
Nadhani pale sio Mwenge ni Mikocheni...angalizo Chadema kuweni makini kuna baadhi ya vitu chama kinatakiwa kufanya kwa nguvu zake, siku Sabado hakiwa hayupo familia yake wakalitaka jengo lao itakuwaje?
Pale ni mwenge
 
Ila one thing sijapenda, Dr Slaa anasema 'watatumia sehemu ya 100m kwa matengenezo ya hiyo ofisi'! Kwani walijua watapewa mshiko na ofisi? Nini mipango ya CDM kuwa ofisi kabla ya mchango wa Sabodo?

Nway ni muhimu sana kupata copy kamili ya stori husika katika gazeti lenyewe, lakini nukuu hiyo inaweza kuwa haijakamilika au haikuchukua maneno yote ambayo Dokta Slaa aliyasema pale mbele ya wanahabari. Alisema kuwa msaada huo wa Mzee Sabodo umekuja wakati mwafaka, maana tayari CHADEMA walikuwa na mpango ya kuanza ujenzi wa ofisi za makao makuu.
 
Nway ni muhimu sana kupata copy kamili ya stori husika katika gazeti lenyewe, lakini nukuu hiyo inaweza kuwa haijakamilika au haikuchukua maneno yote ambayo Dokta Slaa aliyasema pale mbele ya wanahabari. Alisema kuwa msaada huo wa Mzee Sabodo umekuja wakati mwafaka, maana tayari CHADEMA walikuwa na mpango ya kuanza ujenzi wa ofisi za makao makuu.
Nimeinukuu hapa

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mustafa Sabodo, amemshambulia Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kwa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, huku akisema hajawahi kuona nchi yoyote duniani kiongozi mstaafu kufanya hivyo.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi fedha kiasi cha sh milioni 100 kwa uongozi wa CHADEMA, Sabodo alisema alichukizwa na kitendo cha Mkapa kupanda jukwaani katika kampeni za uchaguzi huo na hasa alipotoa maneno ya hovyo.
Sabodo ambaye ni kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alisema alitamani chama chake hicho kishinde, lakini alifedheheshwa na hatua ya Mkapa kujitumbukiza katika kampeni hizo, jambo alilosema anaamini limewaudhi Watanzania wengi.
Kutokana na tukio hilo, Sabodo aligeuza matamanio yake na kuelekeza sala zake kwa mgombea wa CHADEMA.
"Najisikia fahari CHADEMA kushinda Arumeru…Naapa, najisikia fahari na CHADEMA na najisikia fahari na Dk Slaa," alisema Sabodo na kuongeza kuwa wananchi na taifa kwa ujumla limechoshwa na CCM.
Sabodo ambaye Mei 14 mwaka huu atatimiza miaka 71, alisema pamoja na kutoa fedha hizo, pia atachimba visima 10 katika jimbo la Arumeru Mashariki na kuikabidhi CHADEMA baiskeli 100 kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Aidha mfanyabiashara huyo alisema pia anafanya mazungumzo na wataalamu wake kuangalia uwezekano wa kuipatia CHADEMA jengo lake la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, liliko eneo la Mwenge, Dar es Salaam ili wafanye ofisi ya kisasa.
Akimshukuru mfanyabiashara huyo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa, alisema Sabodo ni mtu mwenye upendo kwa Watanzania wote bila ubaguzi na daima amekuwa akikisaidia chama hicho kwa uwazi na bila kumuogopa mtu yeyote.
"Dhamira yako safi na uadilifu wako ndio unaokufanya ufanye hivyo. Kuhusu baskeli 100 za walemavu tutaandaa utaratibu wa kuwafikishia. Hatuna maneno mengine ya kukwambia zaidi ya kusema asante," alisema.
Alisema sh milioni 100 wanatarajia kuzitumia kujenga ofisi ya chama, wataziingiza katika mfuko wa ‘CHADEMA Movement for Change' uliozinduliwa hivi karibuni.
Kuhusu Rais Mkapa kujihusisha katika kampeni huku akitumia fedha za walipakodi, Slaa alisema hastahili kuendelea kulipwa fedha hizo na kuongeza kuwa wataanzisha mchakato ili kiongozi mstaafu anayekiuka maadili asiendelee kulipwa fedha za wananchi.
"Ingawa haki inaweza kucheleweshwa, lakini tutahakikisha tutalisimamia hili ili itungwe sheria kiongozi mstaafu anayekiuka maadili asiendelee kulipwa fedha za walipa kodi," alisema.
 
Kuna uhusiano gani kati ya sabodo na mbowe? (au ndio ile biashara ya yetu haram)

Naona anatumia sana jina la mwalimu nyerere kuna nini?
 
"Chadema kinatumia alama ya vidole viwili kama manati, manati kamwe haiwezi kuua tembo" Livingstone Lusinde (2012[/COLOR]] k

Lusinde sio mfuatiliaji wa mambo!! aulize walioongoza mageuzi ya Misri, Tunisia na libya walikua wanatumia alama ya kidole kimoja au viwili? akipata jibu awaambie ccm wenzake wajipange coz we mean "V" VICTORY.
 
Mkuu Rejao,
Emu tabiri kabisa. Arusha mtashinda kwa asilimia ngapi??
Arusha tutashinda kwa garama yoyote. Kumbukeni Arumeru tuliwaachia kwasababu tunazozifahamu sisi. Am hapy mmeanza kujitambua
 
Huyu Mzee ni Msafi na hakuna wa kumgusa, na anachukizwa na Ufisadi uliojaa serikalini. Sabodo ni Mzalendo kuliko Fisadi wa Magogoni anayeongoza Kundi la Majambazi lenye sare ya Yanga

Biashara zake anafanya Wallstreet (New York Stock Exchange),Mzee ni mtaalam wa securities trading.Tanzania hawana uwezo wa kuingilia biashara zake given kwamba ni safi
 
Nimekupata sana, manake wanaCDM wengi wanaliogopa vazi la Jangwani, kumbe wao walilivamia na walikuta chama la jangwani wanalivaa, jaribu futatila sekeseke la 1957 eti jamaa walitaka jangwani wabadilishe sare, mchonga akagoma akasema tuliwakuta wanalivaa
 
Nadhani pale sio Mwenge ni Mikocheni...angalizo Chadema kuweni makini kuna baadhi ya vitu chama kinatakiwa kufanya kwa nguvu zake, siku Sabado hakiwa hayupo familia yake wakalitaka jengo lao itakuwaje?

Famili ya Sabodo siyo vilaza wala hawana wivu wa kike kama Magambaz!
 
Back
Top Bottom