Chadema kunyimwa usingizi na chaguzi za ccm na kuwa na hoja za vipindi inatia shaka

Almasi Omary ni dhahiri kwamba wewe bado mdogo sana kisiasa na kijamii. Hapa JF tunaleta na kujadili hoja za vyama vyovyote vya siasa, serikali, NGO, dini na mengine mengi.
Hapa JF sisi ni familia moja pamoja na kuwa kila mmoja ana itikadi yake ya kisiasa ama kidini.
Inaonekana wazi kwamba wapenzi wa Chadema ndio wenye nguvu na moyo wa kuleta habari zinazotokea hapa nchini toka kona mbalimbali za nchi hii kwa lengo la kuwajulisha wanaJF kinachojiri huko waliko.
Sasa usipojua wajibu wako kama mwanaJF utaishia kushangaa hata vitu visivyoshangaza kama hili uliloleta hapa.
Habari iwe ya Chadema, ccm, cuf, nccr, tlp ama udp tutaileta hapa na tutaichambua vilevile bila kuangalia makunyanzi!

Lakini imethibitika kuwa hoja ambazo ni anti CDM huishiai kutupiwa matusi. Hii inadhihirisha kuwa most of pro CDM aidha ni vilaza au hawana uwezo wa ku counter issues against them
 
Lakini imethibitika kuwa hoja ambazo ni anti CDM huishiai kutupiwa matusi. Hii inadhihirisha kuwa most of pro CDM aidha ni vilaza au hawana uwezo wa ku counter issues against them

Anti Chadema wengi sana hawaleti hoja zenye mashiko hapa JF juu ya Chadema zaidi ya udaku, majungu, fitna na husda, sasa hao ndio hukiona cha mtemakuni.
Matusi na kejeli ni mambo ya kawaida sana kwenye mambo ya siasa zetu za Tanzania ambazo ccm na serikali yake pamoja na vyombo vya dola wanafanya ghilba kubwa sana dhidi ya wapinzani na wananchi kwa ujumla, si JF, fb ama huko kwenye majukwaa mitaani.
Ukileta hoja isiyo na mashiko utaishia kudhihakiwa lakini ukileta hoja yenye mashiko utapata positive response.
Sasa kama ulitegemea ulete hoja za majungu na fitna dhidi ya chama fulani ukitegemea watu wakupotezee ama kukuunga mkono basi hapo ndipo ulipokosea sana na kupoteza mwelekeo.
 
Kulikoni wana M4C, kila kikicha sasa hivi hoja za chaguzi ndani ya CCM na vigogo kuchezeana rafu ndo topical issues ndany ya CDM. Kuna watu wanasema hii ni dalili ya kuingiwa kiwewe na mageuzi ndany ya CCM ambayo yanatapanga safu ya kuinyamazisha CHADEMA. Sasa ni hili la CDM kupoteza muda saana kumuandama Zitto linaleta shaka nyingine. Kunahaja ya CHADEMA kuonesha ukomavu kidogo na kuwa focused na si kudandia kila issue inayotokea nchini. Maana tulianza na Ole Milia, tukaja, Migomo ya wanavyuo tukaja Madaktari na Ulimboka, tukaja Mwangosi, tukaja Kinana kungatuka, mara Sumaye, Mara Kilango sasa ZITTO. Vipi wana mikakati CDM hamuoni kama chama kinakosa umakini kwa kutokuwa na focus kwenye issues????. Mie ni haya tu kwa leo


Hili jamaa sijiui hata kama STD VII lillimaliza. Maana sijaelewa hapa akili yake ilitaka kuweka nini. Kwenye kanuni za JF pale Mods ongezeni kinterview kidogo cha maswali kujua mtu kama kidogo yupo ahueni kuliko hii style.
 
Mara nyingi CDM haikubali ukweli natarajia kwa hili mtakubali tu yaishe. CDM inaanza kuelekea kwa TLP na NCCR mageuzi. Kwa nini ZITTO kabwe anaandamwa kupindukia, kwa nini chaguzi za CCM ziwe issues?. Ninahakika kuna watu makini CDM hata maprofesa watakuwa na muona kama wakwangu. Mbona huwa hautwasikii maprofesa Baregu na Safari, au Ndesamburo na Halima mdee wakikazania hoja hizi zote nilizoziulizia?Ni watu fulani wachache sasa angaliei bwana tunataka siasa madhubuti Tanzania siyo usaniii

Naamini ulichotaka kufanya si kuleta mjadala, bali ni kupandikiza maoni yako kuhusu ZITTO. ZITTO ni kiongozi mzuri kwa wengi na wengi pia hawamkubali. Mimi simkubali kabisa. ZITTO sikukubali kwa sababu nyingi sana ikiwa ni pamoja na (1) wewe kuwa mbinafsi, badala ya kujenga chama wewe unataka kujijenga wewe kama wewe kisiasa; (2) kupandikiza chuki na vitisho, kwamba ukigombea lazima ushinde, iwapo ukigombea nafasi yoyote na usipoipata basi utakuwa umedhulumiwa au umebaguliwa kwa sababu za udini na ukabila. Yaani unataka watu wakiogope, wasikuguse, unalotaka lazima liwe; (3) misimamo isiyoeleweka, leo unapinga mafisadi, kesho ni mtetezi wao nk - uko opportunistic - na uwadilifu wako HAUNIRIDHISHI nk.

USHAURI wangu ZITTO zingatia taratibu za chama, usijenge chama chako ndani ya chama rasmi CDM kama mtandao ULIVYOJIJENGA NDANI YA CCM; acha kelele na wakati ukifika gombea na unaweza kuchaguliwa au usichaguliwe kwa kuzingatia taratibu za chama, au unaweza kugombea kama mgombea binafsi IKIWA KATIBA ITARUHUSU (naamini katiba mpya haitakuwapo 2015, soma kif 36 cha sheria ya mabadiliko ya katiba, itakwamishwa na ZANZIBAR).
 
Back
Top Bottom