Chadema kumekucha - vijana kazi kwenu

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,796
12,239
[h=2]Chadema yaalika wagombea[/h]Katika jitihada za kujiandaa na uchaguzi mkuu wa 2015 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka wanachama wake wenye nia ya kugombea ubunge na udiwani kuwasilisha barua za maombi, picha, vyeti, wasifu na jimbo wanalotaka kugombea kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu, tayari kwa maandalizi.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema jana na kuwaagiza wanafunzi ambao ni wanachama wa Chadema wanaohitimu mwaka huu katika vyuo vikuu vya Mkoa wa Dodoma kufanya hivyo mara moja.

Akihutubia katika mahafali ya kuwaaga wanachama hao wanaosoma vyuo vikuu vya Dodoma, St. John’s na Chuo cha Biashara (CBE), Mbowe, alisema kila anayetaka kugombea awasilishe maombi na kwamba mwaka 2015 wagombea watakuwa wengi kwa kila jimbo ili kuleta ushindani.

Alisema taarifa za wagombea hao zitafanywa kuwa siri na watakaojitokeza kugombea 2015 watapata mafunzo maalumu ya uongozi, kampeni na pia watapewa ajenda za kuzungumzia majukwaani wakati wa kampeni.

“Kama CCM ilidhani kuwa mwaka 2015 kutakuwa na jimbo au kata ambalo mgombea atapita bila mgombea, safari hii wameula wa chuya. Tumefanya operesheni Mtwara na Lindi, tutaendelea na operesheni Dar na Pwani kisha tutaendelea Dodoma, Morogoro na Singida………
MIKAKATI YA CHADEMA

Mbowe ametangaza kuwa katika uchaguzi mkuu wa 2015 Chadema haitapokea 'maskrepa' yaliyokosa nafasi katika vyama vingine, biashara ya kupokea watu waliokosa nafasi katika vyama vingine ilikuwa 2010……..

Source: NIPASHE 18/06/2012
 
Haya vijana wasomi wito ndo huo mjiandae kuwa viongozi bora,hili kupokea walokosa nafasi ya kugombea toka vyama vingine nalo ni vyema alivyolizungumzia mkiti. Pana funzo hasa Jimbo la Segerea mgombea wetu kila mbinu alopewa yeye alikuwa anakubali utekelezaji sifuri, kama angelikuwa imara jimbo hilo tungeshinda uchaguzi.Lakini ndo hivyo tena kwa makosa tunajifunza.

VIVA CHADEMA, VIVA M4C NA PIA VIVA VUA GAMBA VAA GWANDA
 
Muda huo unatosha kuwaanda katika kila eneo ili wakiingia katika kampeni wawe tayari wameshajua matatizo ya maeneo watakayogombea ili pamoja na mambo mengine ziwe hoja za kushughulikia wakati wa kampeni.
 
wadau jf,
hii strategy ni the best. maandalizi mapema hakuna kusubiri hadi 2015ndo mambo yaanze. yanaanza leo.
viva cdm,
merci cdm.
 
Magamba nayo yatadesa... ni good strategy, itawasaidia sana wagombea wapya wa 2015
 
Back
Top Bottom