Elections 2010 CHADEMA kuitisha Maandamano Makubwa wiki ijayo

Kaka kama suala la spinning ya maneno ya watu, u know I am exceptional qualified.......

Duu, nilikuwa nasikia tu kuwa wee ni Mzee wa Spinning, kumbe ni kweli? Hongera.

Kumbe yooote unayoongea humu ndani ni kuwa unatumia UJUZI wako uliofaulu na kuwa na uzoefu?

Hope they pay you well.........
 
Maandamano haya, kama yako kweli, yakipangwa vizuri yanaweza kuwa na faida kubwa zifuatazo:

(1) Yataonyesha dunia nzima kwamba CHADEMA inaungwa mkono na Watanzania wengi.

(2) Waangalizi wa Uchaguzi kutoka nchi za Ulaya ambao wako Dar tayari, wataona
wenyewe jinsi wananchi wanavyomsikiliza Dr Saa kwa utulivu. Wanamtambua kuwa kiongozi wao.

(3) Kama IGP Mwema atatoa amri kwamba kusiwe na maandamano (ambayo itakuwa kinyume cha HAKI), na CHADEMA ikaweza kuikataa hiyo amri na kufanya maandamano makubwa, basi itaonyesha SHIFT OF POWER from CCM to CHADEMA.

(4) Kama Polisi wataamriwa kuwapiga wananchi virungu kuna uwezekano mkubwa kwamba wengi hawatafanya hivyo. Wengi wao wanapenda mabadiliko vile vile, na waandamaji ni ndugu zao. Polisi hawawezi kupambana na wananchi laki 2 au 3 ambao wanaandamana kwa amani. Scenario hii, kama ikitokea, itakionyesha CCM kwamba wakihujumu uchaguzi wananchi wataweza kukusanyika na kudai haki itendeke.

(5) Media coverage itakuwa kubwa sana. Hilo litaipa CHADEMA nafasi nzuri ya kueleza ULIMWENGU msimamo wake. Itakuwa ni pamoja na kugusia siasa ya Dr Slaa ya mambo ya nchi za nje.
 
Mwenye taarifa atujuze lini CCM walinyimwa kibali cha kuandamana???
 
Kuwe na Mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Kwa mfano:

Maisha Bora yako wapi? Tulidanganywa 2005, mwaka huu HATUDANGANYIKI....

Chadema ni chama cha amani,Haki, Mshikamano na maendeleo....

Chadema itapigana na maadui 3 kumuenzi Mwl Nyerere, Ndio maana tunasema Elimu bora, Afya Bora BUREEEE. Pamoja tutaondoa umasikini..

CHADEMA TUTAPUNGUZA MFUMUKO WA BEI KWENYE BIDHAA MUHIMU KAMA SUKARI,MAFUTA YA KUPIKIA, SODA NA ZANA ZA ELIMU. KUONDOA VAT KWENYE BIDHAA MUHIMU.

Rushwa na Ufisadi ni Adui wa Haki, Chadema itaondoa Ufisadi na kujenga uchumi imara...

TUKINYIMWA KIBALI, TUANDAE KONGAMANO KWENYE UKUMBI UNAOWEZA KUINGIA WATU WENGI.

AU MAANDAMANO NA KONGAMANO VYOTE KWA PAMOJA.
 
Maandamano haya, kama yako kweli, yakipangwa vizuri yanaweza kuwa na faida kubwa zifuatazo:

(1) Yataonyesha dunia nzima kwamba CHADEMA inaungwa mkono na Watanzania wengi.

(2) Waangalizi wa Uchaguzi kutoka nchi za Ulaya ambao wako Dar tayari, wataona
wenyewe jinsi wananchi wanavyomsikiliza Dr Saa kwa utulivu. Wanamtambua kuwa kiongozi wao.

(3) Kama IGP Mwema atatoa amri kwamba kusiwe na maandamano (ambayo itakuwa kinyume cha HAKI), na CHADEMA ikaweza kuikataa hiyo amri na kufanya maandamano makubwa, basi itaonyesha SHIFT OF POWER from CCM to CHADEMA.

(4) Kama Polisi wataamriwa kuwapiga wananchi virungu kuna uwezekano mkubwa kwamba wengi hawatafanya hivyo. Wengi wao wanapenda mabadiliko vile vile, na waandamaji ni ndugu zao. Polisi hawawezi kupambana na wananchi laki 2 au 3 ambao wanaandamana kwa amani. Scenario hii, kama ikitokea, itakionyesha CCM kwamba wakihujumu uchaguzi wananchi wataweza kukusanyika na kudai haki itendeke.

(5) Media coverage itakuwa kubwa sana. Hilo litaipa CHADEMA nafasi nzuri ya kueleza ULIMWENGU msimamo wake. Itakuwa ni pamoja na kugusia siasa ya Dr Slaa ya mambo ya nchi za nje.

What I see here ni maadalizi ya kitachofuatia baada ya kushindwa uchaguzi. Maandamano haya yanalenga kulazimisha hisia kuwa Slaa ameshashinda uchaguzi na isipokuwa hivyo itakuwa kwa sababu amedhulumiwa. Hii ni strategy ambayo imetumiwa sana na makundi mengine kisiasa ambayo yanajua wazi kuwa bado hawana nguvu ya kutosha kufanya mabadiliko kidemokrasia.

Kama nilivyosema mwanzo, kama mko tayari kujiexpose zaidi na propaganda za udini na uwakuja bila ya kusahau ya wapenda vurugu/umwagaji damu, then go on.

Hamjiulizi kwanini CUF wana constant political base ambayo always ina-swing kutegemea Mgombea wa CCM tu na si vinginevyo?? Again, kazi ya propaganda ya kisiasa ni kujenga perceptions. Maandamano haya yatajenga perception kuwa mnaonewa na mmeshashinda urais miongoni mwenu wenyewe lakini pia yataongeza perception ya kuwa CHADEMA ni chama cha watu wa dini fulani wa kutokea pande fulani za nchi. In the end hamtakua na tofauti na CUF. CCM wanapeta.......CHADEMA is supposed kuwa CHAMA kinachokuwa na with such identity u will stack with what you have now which is never enough for any substantial even radical changes u all dream of.......

Na yule anayedai kuwa kuna watu wanadhani wana hati miliki ya jiji la Dar es Salaam, unfortunately ni kweli kama ambavyo wapo ambao wanadhani kuwa wana hati miliki ya Utanzania na Urais.....ama wengine kama kina Mwafrika wanaodhani mradi Mwalimu Nyerere ni "wa kwao" kiimani basi yeye na wenziwe ndio wenye hati miliki ya ufuasi wake na wengine ni wanafiki..........

Lastly, I dare the mighty UKOMBOZI STRATEGIST Mwanakijiji aliyechokonoa hii idea kuja kuungana na wapambanaji wenziwe katika maandamano haya na kile kitachofuatia baada ya kushindwa uchaguzi kama ambavyo dalili zinaonyesha. Na asiache familia yake huko ambavyo wengine wa pande zote tayari wanashindana kuwahamisha familia zao kabla ya hiyo muitayo D-Day. No wonder I doubt Dual Citizenship..........
 
Maandamano haya yatajenga perception kuwa mnaonewa na mmeshashinda urais miongoni mwenu wenyewe lakini pia yataongeza perception ya kuwa CHADEMA ni chama cha watu wa dini fulani wa kutokea pande fulani za nchi.
Hivi wewe unalijua lengo hasa la maandamano au unajenga malengo yako kichwani na kuyalazimisha yawe ya walioandaa maandamano (Chadema). Unaweza ukawa na maoni yako kutokana na utashi (perception) na upenzi wako kwa chama husika lakini inawezekana vile vile wenyewe wakawa na malengo tofauti na yako na yakatimia siku ya maandamano. Inavyoonekana unataka (unapenda) yatokee kama unavyofikiri wewe.
 
Duu, nilikuwa nasikia tu kuwa wee ni Mzee wa Spinning, kumbe ni kweli? Hongera.

Kumbe yooote unayoongea humu ndani ni kuwa unatumia UJUZI wako uliofaulu na kuwa na uzoefu?

Hope they pay you well.........

Jamaa ndiye zake hizo, na kwa vile sasa hivi ana hasira sana kuona rafiki yake kipenzi (J Kikwete) akichemsha kwenye uongozi na kwenye kampeni, atamwaga upupu usio na kipimo hapa.... just watch this space
 
What I see here ni maadalizi ya kitachofuatia baada ya kushindwa uchaguzi. Maandamano haya yanalenga kulazimisha hisia kuwa Slaa ameshashinda uchaguzi na isipokuwa hivyo itakuwa kwa sababu amedhulumiwa. Hii ni strategy ambayo imetumiwa sana na makundi mengine kisiasa ambayo yanajua wazi kuwa bado hawana nguvu ya kutosha kufanya mabadiliko kidemokrasia.

Omar, umejuaje kuwa chadema itashindwa? unajua umeanza kunitisha sasa na maneno yako haya. Inamaana ccm mmeazimia kushinda kwa gharama yoyote ile?

Kama nilivyosema mwanzo, kama mko tayari kujiexpose zaidi na propaganda za udini na uwakuja bila ya kusahau ya wapenda vurugu/umwagaji damu, then go on.

Hamjiulizi kwanini CUF wana constant political base ambayo always ina-swing kutegemea Mgombea wa CCM tu na si vinginevyo?? Again, kazi ya propaganda ya kisiasa ni kujenga perceptions. Maandamano haya yatajenga perception kuwa mnaonewa na mmeshashinda urais miongoni mwenu wenyewe lakini pia yataongeza perception ya kuwa CHADEMA ni chama cha watu wa dini fulani wa kutokea pande fulani za nchi. In the end hamtakua na tofauti na CUF. CCM wanapeta.......CHADEMA is supposed kuwa CHAMA kinachokuwa na with such identity u will stack with what you have now which is never enough for any substantial even radical changes u all dream of.......

Spin hadi mnatisha, leo unataka kuilinganisha chadema na cuf?

Na yule anayedai kuwa kuna watu wanadhani wana hati miliki ya jiji la Dar es Salaam, unfortunately ni kweli kama ambavyo wapo ambao wanadhani kuwa wana hati miliki ya Utanzania na Urais.....ama wengine kama kina Mwafrika wanaodhani mradi Mwalimu Nyerere ni "wa kwao" kiimani basi yeye na wenziwe ndio wenye hati miliki ya ufuasi wake na wengine ni wanafiki..........

Wewe ndiye unaita watu wa kuja hapa JF... hayo mengine ni unafiki na uzandiki wako tu

Lastly, I dare the mighty UKOMBOZI STRATEGIST Mwanakijiji aliyechokonoa hii idea kuja kuungana na wapambanaji wenziwe katika maandamano haya na kile kitachofuatia baada ya kushindwa uchaguzi kama ambavyo dalili zinaonyesha. Na asiache familia yake huko ambavyo wengine wa pande zote tayari wanashindana kuwahamisha familia zao kabla ya hiyo muitayo D-Day. No wonder I doubt Dual Citizenship..........

Omar, wewe hujui mwanakijiji yuko wapi sasa hivi, nini kinakufanya useme kuwa mwanakijiji hatakuwepo kwenye maandamano?
 
Hili halikutokea. jana wakati wa habari, nilisubili sana. lakini hakukuwa na chochote. Nimesikitika maana nilikuwa tayari kwa hamu sana.
 
Muaandaji wa maandamano yupo ughaibuni wewe ukapigwe jua bure, good thing naona sasa wameanza kumstukia mchochezi yeye anabaki ughaibuni anapambana na kibodi
 
With due respect, Mkuu Mwkjj maadamano hatukuyaona na wala harufu yake hatukusikia. Au ka-inzi kalipewa taarifa feki?
Unatufanya tufikiri ulitumwa kutikisa kiberiti kuona kama kina njiti?
 
hakanaga muda wa kupewa huwa kana pika kenyewe, sasa wakati huu kamekosa wakulivalia njugu.
 
muna andamana ili iweje!! Watu wanajitayarisha kufanya uchaguzi nyinyi munafikiria kuandamana na ili mulete fujo halafu mukipata mkongoto muanze kuwalilia EU na USA kuwataka msaada!!!
 
wamepania kumwaga damu mwaka huu na majeshi yapo imara wajaribu waone..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom