CHADEMA kuchukua nchi ni baadae sana

Ninachozungumzia ni changamoto kwa CDM kujiimarisha kisiasa, sijakuelewa unachobisha ni nini? na content ya thread yangu inaongelea CDM na hivyo muamko ninaouongelea unahusiana na CDM ambacho hujaelewa ni nn?Sasa kama hakuna mikakati ya ku-penetrate kama ulivyosema tutegemee miujiza?

Ninachokiona hapa ni wewe kutubabaisha katika thread yako na kukosea kiswahili...tatizo lako hukutumia lugha uliyotakiwa kuitumia. Hata Tanzania hakuna mkoa usio na mwamko wa kisiasa wewe na unatakiwa uelewe kuwa mwamko wa kisiasa si kuijua na kuishabikia CHADEMA pekee.
 
yaani unaona sifa watu kutokuijua chadema!!!!!!?????? badala uwahurumie hao ambao hawaijui na ufanye jitihada waijue au wajue vyama vingine vya siasa kwa maendeleo yao wenyewe!!!!!
embu jaribu kulinganisha maeneo waliong'ang'ania ccm miaka yote na ulinganishe na hali ya maishi mfano Pwani, Tanga Dodoma, tabora, ruvuma, mtwara, n.k then anghalia maeneo ya Moshi, Karatu, Mwanza N.K. walilie ndugu zako kwa kutokuijua Chadema na sio jambo la kujivunia hata kidogo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Vyama vya siasa vinatakiwa kuuza sera zao ili watu wavikubali na siyo kuwalazimisha kama unavyotaka wewe pia unatakiwa ufanye "research" ili ujue ni kwa nini maendeleo ya kiuchumi yanatofautiana kati ya mkoa mmoja na mwingine. Si kweli kwamba ni kwa sababu wameikubali CHADEMA ila ziko "factors" nyingi ikiwemo "climatic factor" hali ya hewa ya Arusha na Moshi huwezi kulinganisha na Dodoma bana!
 
Hakuna ubishi kwamba CDM ndio chama kikuu cha upinzani nchini na chama makini na tegemeo la Watanzania na ili ndoto ya tegemeo hili itimie lazima tikiri bado kuna mapungufu ya kimkakati. Pamoja na ukweli huu hatuna budi kuwa wakweli juu ya mambo mbalimbali kama ifuatavyo:

  1. Kujiimarisha katika mikoa isiyo na mwamko wa kisiasa. Ni ukweli usiopingika kwamba kuna umuhimu mkubwa wa CDM kujiimarisha kichama katika mikoa isiyo na mwamko. Baadhi ya mikoa hii ni Dodoma,Tanga,Tabora, Lindi, Mtwara na Pwani. Tukiangalia kwa umakini idadi ya kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 utaona kabisa tofauti kubwa sana kati ya CDM na CDM. Mfano mkoa wa Tanga hakuna diwani hata mmoja achilia mbunge toka CDM, kura za Uraisi kwa CDM hazifiki 3,000 dhidi ya zaidi ya 20,000 za CCM kwa jimbo la Lushoto, jimbo la bumbuli ndilo linaongoza kwa mkoa wa Tanga kwa kutoa kura za Uraisi takriban 10,0000 dhidi ya zaidi ya 20,0000 za CCM pamoja na kutokwepo kwa mgombea wa Ubunge wa CDM 2010 na kutofanyika kwa kampeni yoyote. Lakini ieleweke vilevile mkoa wa Tanga ni moja wa mikoa 10 yenye idadi kubwa ya watu Tanzania.
  2. Kujenga mazingira ya kupata kupata viongozi bora.Mwaka 2013 kutakuwa na uchaguzi wa ndani wa chama kwa ngazi ya majimbo/wilaya, Mkoa na Taifa. Ni dhahiri kwamba uchaguzi huu ndio utatoa taswira halisi ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hivyo bila usimamizi makini kwa maana ya uratibu katika mchakato huu CDM itapoteza mwelekeo.
  3. Kujenga mkakati madhubuti wa kienezi kwenye mikoa isiyo na mwamko. Ni dhahiri kwamba CDM imeweka nguvu nyingi kwenye mikoa yenye muamko mkubwa wa kisiasa na kusahau mikoa yenye muamko mdogo na kwa kuzingatia kwamba gap ya kura dhidi ya CCM katika mikoa hii ni kubwa mno ipo haja ya kupunguza idadi hii kama kweli CDM imedhamiria kukamata dola. Ipo haja wa viongozi wa kitaifa wa CDM kutoa elimu ya uraia katika mikoa hii kwa maana ya ushawishi wao mkubwa kuliko viongozi wa Mikoa,wilaya/Majimbo.

  • Bila ya kupunguza gap la kura kati ya CDM na CCM kwenye mikoa isiyo na muamko ya kisiasa kukamata dola itakuwa ni ndoto kwa sababu hata katika maeneo ambayo CDM inaongoza tofauti ya kura ni ndogo na hivyo kuwa recovered kwa urahisi na kura za CCM.


hapo kwenye nyekundu ndio umeandika nini unaweza nisomea!? Yaani ulivyo muongo hujui hata kuandika tarakimu
 
mmh!
Mwamko mdogo wa kisiasa=CDM kukosa kura?
kweli tuna mbumbumbu katika kaifa hili! ila anyway 9% ndio wenye div 1-3.

Huyo atakuwa kati ya wale walioko kwenye asilimia 91, lakini cha ajabu alichangia sana ile thread ya Mwanaasha!
 
Yes hapo umenena bwn Mbelwa,kwa sasa CDM ikazane kufungua matawi na kuhakikisha inaweka viongoza imara kwenye mikoa na wilaya ngumu na ipunguze kwend mara kw mara kweny mikoa kama mbeya,Arusha kilimanjaro nk ili ijikite kweye mikoa hiyo na wilaya nyingne zinazonekana mwamko wao ktk elimu ya siasa na maendeleo ni duni ili wapate mwamko japo kiasi.
 
hii mada inalingana na mwenye kuileta mana ukisema ana makengeza unamwonea,ukisema hana akili pia unamwonea,tuseme tu kuwa watu wa aina hii ni wale wenye mtindio wa ubongo kiasi kwamba hata uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo
 
Kweli Chadema ijitanue katika Mikoa yote na ngazi zote.

Kama lengo ni kutafuta mikoa yenye mwamko wa kisiasa, kujitanua mikoa yote si itakuwa ngumu? maana mleta uzi ameshasema kuwa mikoa ambayo CHADEMA haijajisimika haina mwamko.... kaaaaaazi kweli kweli!
 
umaarufu wa chadema umetokana na udhaifu wa CCM,kama ccm itakuwa imara,cdm kwishneeyy
 
Kujenga mazingira ya kupata kupata viongozi bora.Mwaka 2013 kutakuwa na uchaguzi wa ndani wa chama kwa ngazi ya majimbo/wilaya, Mkoa na Taifa. Ni dhahiri kwamba uchaguzi huu ndio utatoa taswira halisi ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hivyo bila usimamizi makini kwa maana ya uratibu katika mchakato huu CDM itapoteza mwelekeo.

Akina SHIBUDA wako wengi tu mjitahida mtawapata na ukizingatia kuwa katika uchaguzi wa CCM wa mwaka huu wengi watatemwa.
 
CHAMA cha Wananchi (CUF) kijinasibu kuchukua madaraka ya nchi mwaka 2015 licha ya baadhi ya vigogo wa chama hicho kujiengua. Vigogo wa CUF walijiengua na kujiunga chama kipya cha ADC, kwa kile walichokieleza kupinga ubabe unaofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad

Majigambo hayo yalitolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa Chama hicho, Shaweji Mketo, alipokuwa akizungumzia ujio wa Mwenyekiti wa CUF, Taifa Profesa Ibrahimu Lipumba.
Mketo alisema CUF inajiandaa kuchukua nchi mwaka 2015 na kinaamini kuwa kuondoka kwa viongozi hao kutakinusuru chama hicho.

Alisema viongozi waliojiondoa ndani ya chama hicho walishindwa kufanya kazi yao ipasavyo hali iliyosababisha kura za mgombea urais kwa mwaka 2010 kushuka kwa kiasi kikubwa. “Maamuzi yetu yako sahihi na wanaodhani kuwa kuenguliwa au kuondoka kwa viongozi hao ni kuua chama wamepotea, kwani chama bado kina nguvu na uwezo wa kushika dola katika taifa,” alisema. Aliongeza kuwa CUF imechukua jukumu la kusafisha virusi ndani ya chama hicho na sasa kinajipanga kwa ajili ya kushika madaraka ya nchi mwaka 2015.

Alisema kama virusi visingetolewa ndani ya chama hicho ni dhahiri kingepoteza umakini wake na imani kwa wanachama. Alimtolea mfano Saidi Miraji ambaye alikuwa meneja wa kampeni wa chama, alishindwa kuonyesha umahiri wake wa kuwashawishi wananchi kukichagua CUF mwaka 2010. Alisema Miraji hivi sasa ndiye amepewa uenyekiti wa muda wa chama kipya cha ADC ambacho ana imani hakitafua dafu.

CUF pia imeilaumu serikali kwa kutowathamini wataalamu wake ambao wanatambuliwa katika ngazi za kimataifa.
Katika hatua nyingine kaimu mkurugenzi huyo aliwahamasisha wana CUF na Watanzania kwa jumla kujitokeza kwa wingi Machi 11 kumpokea Lipumba ambaye alikuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miezi mitatu kwa ajili ya kushughulikia mtikisiko wa uchumi wa nchi ya Ugiriki na nyinginezo akishirikiana na magwiji wenzake wa uchumi wa dunia.
 
Kujibu swali lako lililobeba thread:
KAFU kuongoza dola ya Tanzania 2015 iwapo Watanzania wote tutaamua KUSILIMU
 
Baada ya Hamad Rashid kukinyonyoa manyoya sasa CUF imeibuka na kutangaza kunyakuwa dola 2015.Eti kuondoka kwa baadhi ya wanachama na viongozi ni kuvua gamba ili kivutie zaidi.Nadhani kuingia ikulu ya zanzibar kumewalewesha na kudhani madaraka huchukuliwa kama unavyopakuwa tende!


Source: Tanzania Daima
 
Baada ya Hamad Rashid kukinyonyoa manyoya sasa CUF imeibuka na kutangaza kunyakuwa dola 2015.Eti kuondoka kwa baadhi ya wanachama na viongozi ni kuvua gamba ili kivutie zaidi.Nadhani kuingia ikulu ya zanzibar kumewalewesha na kudhani madaraka huchukuliwa kama unavyopakuwa tende!


Source: Tanzania Daima
hata mgonjwa anapokaribia kufa hujipa matumaini hivyo huvyo
 
Baada ya Hamad Rashid kukinyonyoa manyoya sasa CUF imeibuka na kutangaza kunyakuwa dola 2015.Eti kuondoka kwa baadhi ya wanachama na viongozi ni kuvua gamba ili kivutie zaidi.Nadhani kuingia ikulu ya zanzibar kumewalewesha na kudhani madaraka huchukuliwa kama unavyopa

kweli kwa hii staili ya kujipunyua manyoya mtachukua nchi 2015..maana watanzania ni mazezeta sasa
 
wataichukua nchi waipeleke wapi hao masheikh,ingekuwa chama makini chdm ningekubali,lakini waliojifia khaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom