CHADEMA Kawe watikisa....

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jimbo la Kawe, Mkoa wa Dar es Salaam, kimeanzisha ‘Data Benki’, ambayo hutoa ujumbe kwa wananchi ili kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao, Chama cha Mapinduzi (CCM), hakishindi.
Katibu wa jimbo hilo, Powell Mfinanga, alisema hayo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano ulioandaliwa na viongozi wa CHADEMA, mkoa wa Dar es Salaam, wenye lengo la kukiondoa chama tawala madarakani.
Mfinanga alisema walifikiria kuanzisha mfumo huo, ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa mbalimbali, kwa kuwa hivi sasa viongozi wa CCM, ‘wanachukua chao mapema’, wakielewa kuwa uchaguzi ujao hawatashinda.
“Data Benki ya CHADEMA, inatoa ujumbe kila siku, na kila wiki, kutoa meseji mbalimbali, kutoka CHADEMA, lengo likiwa ni kuwang’oa wabunge wanaolala bungeni,” alisema.
Naye Katibu wa Vijana CHADEMA, Mkoa wa Dar es Salaam, Renatus Mlashani, aliwataka vijana kubadilika na kuchagua CHADEMA, baada ya Rais Jakaya Kikwete, kukiri kuwa hali ni mbaya nchini.
Alisema hivi sasa CCM imeshakufa, kilichobaki ni kuungana na kuing’oa madarakani, kwa kuwa, hivi sasa vijana wanamaliza vyuo lakini hawajui waende wapi kwa sababu hakuna ajira.

Source:Tanzania Daima
 
Sijakuelewa vizuri mkuu namna hii data bank inavyo operate, na je walio nje ya dar watapata elimu hiyo?
 
Lilianza kama fikra likatolewa kama wazo na sasa linatekelezwa.
Huo ni mkakati utakao sambaa nchi nzima.
Peoplessssssssssssssssssssssssssssssss:peace:
 
Lilianza kama fikra likatolewa kama wazo na sasa linatekelezwa.
Huo ni mkakati utakao sambaa nchi nzima.
Peoplessssssssssssssssssssssssssssssss:peace:

Hakika CDM hakuna wa kuizuia 2015
 
Naunga mkono huo mkakati,Dar lazima majobo yote yaangukie CDM 2015,Ingawaje hayo magamba mmmhh..
 
mkuu ni data base sio data banki. data base ndo itakuwa inatumika kuwatumia ujumbe kwa njia ya sms wanachama ili kuwawezesha kupata taarifa mbali mbali. na hiyo mipango ni kwa taifa zima.
 
mkuu ni data base sio data banki. data base ndo itakuwa inatumika kuwatumia ujumbe kwa njia ya sms wanachama ili kuwawezesha kupata taarifa mbali mbali. na hiyo mipango ni kwa taifa zima.

Hongereni sana.Naona ni typing error ya gazeti
 
Wabunge na Viongozi wa CDM waelewe kuwa kuingoa CCM ni rahisi kama watafanya kwa vitendo. Waonyeshe mifano katika majimbo yaliyoshikwa na CDM ikiwemo KAWE na UBUNGO kwa kuondoa kero mbalimbali za wananchi.

Ndipo Wananchi watakuwa na Imani thabiti, Lakini kwa blabla tu kuna hatari ya kuja kudanganyika tena 2015.

WE NEED ACTION NOW!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Is a data base, hii ni mipango kwa nchi nzima (dr slaa nilishawai kumsikia akiridhumzia hili), faida yake ni kuwa chama kinakua na uwezo wa kuwapa taharifa wanachama wake kote nchini kwa kutuma ujumbe wa sms, nafikiri uongozi wa Arusha chadema wanatumia hii program ya kuwasiliana na wanachama wake kwa kutumia data base ndio maana wanafanikiwa katika maandamano kwa sababu wanachama wote wanapata ujumbe wa sms.
 
Back
Top Bottom