Hili la ofisi si Mpanda tu hata hapa Dar, maeneo mengi hayana ofisi za CHADEMA, ningeshauri hivi, pamoja na mambo mengine ya wabunge, lakini wahamasishe watu kwenye maeneo yao wafungue matawi, ukweli kinachotakiwa na hamasa kidogo tu watu wako tayari kulipia ofisi kwa gharama zao na kukiendesha chama.
Uendeshaji wa ofisi za matawi ni mgumu. Ofisi za majimbo, wilaya na mikoa inaweza kuendeshwa kwa ruzuku na michango ya wanachama. Ni vigumu mno kumwajiri mtu wa kushinda ofisini asubuhi hadi jioni. Maeneo mengine ofisi hufunguliwa baada ya muda wa kazi na muda wenye matukio muhimu!.