Chadema kata ya bangata wawafunika ccm.

Movement

Member
Mar 24, 2012
58
15
Wakuu kwasasa ndiyo tupo uwanjani kwenye shule ya msingi midawe kuanza rasmi mkutano wa hadhara kwaajili ya kumnadi mgombea wa udiwani wa chadema bwana Erick Samson mollel, kiukweli hali ya CCM kwasasa imekuwa mbaya sana baada ya juzi kutishia kuua kwa kutumia bastola, wakazi wa bangata kwasasa wanasema yaani bado hatujawapa madaraka wanataka kuua?

Tukiwapa sindiyo tutamalizwa kabisa na hawa CCM? Bangata hatujazoe vurugu kitendo cha CCM kupitia kwa kampeni meneja wao bosco kutoa bastola mbele za watu kimeonyesha kuwa CCM ndiyo wanaohatarisha amani ya nchi yetu.

Makamanda watakao hutubia mkutano waleo ni diwani wa sekei arusha mjini bwana chrispini tarimo, diwani wa oltitroto arumeru magharibi bwana Gibson Meseyeke, diwani wa sokoni two bwana fabiani kendo, kamanda milya, kamanda kilewo na kamanda wa m4c na mbunge aliyeko likizo arusha mjini jembe godbless lema.

Kiukweli kwa timu hii ya cdm sioni uhai wa ccm katika uchaguzi huu mdogo wa udiwani kwa hali hii ilivyo sasa.
 
Diwani wa sekei anasema wao wanapesa sisi tunamungu, ndiyo maana tuliwashinda arusha mjini na sekei kwenye kata yangu hakuna balozi yeyote yule wa ccm maana mimi na jua mabalozi ni wawakilishi wa nchi kwenye mataifa mbalimbali, wanao jiita mabalozi wa nyumba kumi mimi ninawaita viherehere.

Tupeni eric aingie halimashauri kwenda kuwakomboa, na tunawaambia ccm yakuwa bastola walizonazo ni chache sana waongeze nyingine lakini tutawashinda kwakuwa sisi tunamungu wao wanamuabudu shetani ndiyo maana wanatumia vitisho kuomba kura.
 
Kwasasa anapanda diwani kendo,bakumbuka kwenye kampeni za uchaguzi 2010 kikwete aliniletea mke wake eti kuja kumnadi mgombea wa ccm kuniondoa kamanda kendo wakaona hiyo haitoshi wakamuongeza makamu wao wa rais ila niliwapiga vibaya sana...
 
Kendo. Umasikini wa wananchi wa bangata haujaletwa na mungu bali umeletwa na hawa magamba ambao ni wachumia tumbo badala ya wananchi.
 
Kendo. Ctumejipanga kuliko ccm wanavyodhani na usalama wao wa taifa, tupo vizuri ndiyo maana kila mbinu inayopangwa tunaigundua ila makanda hatufi moyo ndiyo tunapata ujasiri wa kusonga mbele,
 
Kilewo. Uchaguzi huu ni uchaguzi wa dhidi ya haki na dhulumu, ukweli dhidi ya uongo, ninawahakikishia wakazi wa bangata kura zenu tutazilinda kwa gharama yeyote ile wao wanatumia silaha za moto sisi tukatumie silaha ya kura kuwaangamiza, hatutakubali tena ccm kuongoza taifa hili kama ni noma acha iwe noma.
 
Lema. Rais mwanaume anayeongoza kuombaomba duniani ni kikwete, kikwete hanatofauti na yule matonya aliyefariki hivi karibuni kwa kuombaomba, tofauti ya ombaomba wa mitaani na rais kikwete ni kuwa hawaombaomba wa mitaani ni wachafu huyu anaomba kwakutumia tai na suti.
 
Tupo pamoja makamanda..mi nipo hapa Ngulelo kuwalinda ama kutafuta tetesi dhidi ya hujuma za magamba.
 
Back
Top Bottom