GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,278
- 6,673
Nimekuwa na masikitiko makubwa kutokana na nguvu ndogo ambayo chama cha maendeleo na demokrasia chadema wamewekeza katika mkoa Mtwara. Napenda ifahamike kuwa Mtwara ni miongoni mwa mikoa ambayo CCM Haitakiwi kwa asilimia zote. Hii ni kutokana na dhuluma mbalimbali za wazi zinazofanywa na chama tawala. Pia napenda kuufahamisha uongozi wa Chadema utakapofika mtwara kwenye ziara maalum ujitahidi kuondoa sumu za udini zilizo pandikizwa na CCM. Sumu hii ni ile inayoonyesha kuwa CHADEMA wapo kwa maslahi ya kanisa. Ni wazi kuwa sumu hii imepandikizwa na CCM. Hivyo ni ombi langu kwa UONGOZI WA CHADEMA uandae ziara maalum ya kwenda kuwazindua wananchi wa maeneo hayo ili kuweza kuondokana na sumu hiyo mbaya ambayo inapandikizwa na CCM.
Nina Imani na CHADEMA kwani ni chama pekee ambacho kimeonyesha nia ya kweli ya kupambana na matatizo ya wananchi. Ziara hiyo itawasaidia CHADEMA kuelewa dhulma kubwa wanayofanyiwa wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara. Mwisho napenda kurudia tena, CHADEMA karibuni sana MTWARA!