CHADEMA Kanda ya Ziwa Magharibi yatangaza kikosi

Jangakuu

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
513
221
na Josephat Isango

amka2.gif
MKAKATI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kugatua madaraka kwa kutafsiri sera yake ya majimbo, umeanza kazi rasmi katika kanda zake 10, na sasa Kanda ya Ziwa Magharibi imetangaza kikosi kazi kilichosheni wataalamu wa fani mbalimbali.
Kanda hiyo inayohusisha mikoa ya Geita, Kagera na Mwanza, ilizinduliwa wiki iliyopita mkoani Mwanza, mbele ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.
Mkutano wa uzinduzi wa kanda hiyo uliohudhuriwa na wajumbe wa mabaraza ya uongozi, wabunge na madiwani kutoka mikoa hiyo, uliwachagua watu sita kuunda timu ya muda ya uratibu wa kanda kwa miezi mitatu.
Waliochaguliwa kuongoza kanda hiyo ni Peter Mekere (Mwenyekiti), Dk. Rodrick Kabangila (Makamu Mwenyekiti), Renatus Bujiku (Katibu), Cecilia Odemba (Mhazini) na Tungaraza Njugu.
Mekere ni mtaalamu mshauri wa biashara na utawala na mafunzo ya biashara. Ana shahada ya biashara na uongozi na stashahada ya ualimu. Ni mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango ya Shirika la nyumba la Taifa (NHC), Kanda ya Ziwa.
Kabangila ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Afya, Bugando, daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu na Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).
Ana shahada ya uzamili ya magonjwa ya wanadamu, shahada ya udaktari, shahada ya uzamili, epidemilojia na utafiti wa huduma za afya.
Bujiku ni mwalimu, mtaalamu mshauri, ofisa wa kanda ya ziwa wa shirika la ACORD kwa muda sasa. Ana shahada ya uzamili, uongozi na mipango, shahada ya Elimu, Stashahada ya Maendeleo na misaada ya kiutu.
Njugu amekuwa Meneja wa shirika la kijamii (CACT-Mwanza 2008-2010), meneja wa Chama cha Akiba na Mikopo (MWAUWASA SACCOS 2007 hadi sasa) ana cheti cha uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) na cheti cha sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Odemba ni Meneja masoko katika usafiri wa anga, mkurugenzi wa kampuni ya uwakala ya usafiri wa anga, na amewahi kuwa katibu wa kamati ya uhamasishaji ya vuguvugu la mabadiliko (M4C) kanda ya Ziwa.
Akizungumza na gazeti hili, Mekere alisema: “Timu yetu imetokana na watu wenye taaluma mbalimbali ambao wamekuwa wakitafuta nafasi kukisaidia chama kupitia taaluma zao. Tunaipongeza CHADEMA kwa kuanzisha sera ya majimbo kuandaa Watanzania kupata maendeleo kwa haraka kwani utaratibu huu wa majimbo ya chama unarudisha mamlaka kwa wananchi, na ni maandalizi ya kuongoza nchi.
“Kwa utaratibu huu wananchi wamerudishiwa madaraka yao, wana nafasi ya kuamua kuhusu rasilimali zao na kupanga namna ya kuzitumia. Utaratibu huu unaharakisha maendeleo tofauti na mfumo wa kimikoa uliowekwa na CCM.”

source: Tanzania daima
 
ziwe kanda.santur.cd.dvd.tape bila kumtoa babu pale kwenye ukatibu mkuu chama kitakufa kabla ya 2013
 
ina maana mwaka 2013 bado. Waha wanasema URUSENGERA MUKASO RUKARYA NYOKO. Maana yake ni kwamba unaweza muombea mamako wa kambo kifo, mama yako akawa ndiye akafa na akamuacha mamako wa kambo anadunda. Siku zenu zi kiduchu
 
ziwe kanda.santur.cd.dvd.tape bila kumtoa babu pale kwenye ukatibu mkuu chama kitakufa kabla ya 2013

Magamba na madalali wao mwaka huu hamtausahau, cdm inapasua nyie limumba mmekalia majungu na mizengwe, kamwambie mangula na kinana nchi inaondoka mikononi mwenu nyie DHAIFU
 
Haya majimbo yatakuwa kwa mujibu wa katiba mpya ya CHADEMA au ya Nchi?. katiba ya CHADEMA wala haijayataja achilia mbali kuyatambua.
kwa kuangalia katiba ya sasa inautambua mkoa kwa kuainisha na kusema;
Wakuu wa Mikoa Sheria ya 1984 Na.15 ib.9

61.-(1) Kutakuwa na Mkuu wa Mkoa kwa kila mkoa katika Jamhuri ya Muungano ambaye, bila ya kuathiri ibara ndogo ya (3), atakuwa ni kiongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Bara watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.
(3) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Zanzibar watateuliwa na Rais wa Zanzibar baada ya kushauriana na Rais.
(4) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (5), kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.

Cha kushangaza CHADEMA kwa sasa wanafanya shughuli ambazo haziko katika katiba ya chama na kwa maana hiyo, wanavunja katiba ya chama kwa sababu kifungu ambacho kinatambua majimbo ambayo muundo wake siyo huu wanaoufanya kwa sasa ni ;

7.6 NGAZI ZA JIMBO ZA CHAMA
Patakuwa na Majimbo ya chama kwa taratibu zitakazowekwa na Baraza Kuu kutokana
na mahitaji ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii
7.6.1 Wajumbe wa Baraza la Uongozi la Jimbo
Wajumbe wote wa mabaraza ya uongozi ya mikoa inayounda Jimbo husika.
7.6.2 Kazi za Baraza la Uongozi la Jimbo
(a) Kushauri chama juu ya mambo mbalimbali ya kisera kuhusu Jimbo husika.
(b) Kuchagua mjumbe kuwakilisha jimbo kwenye Baraza Kuu
7.6.3 Vikao vya Baraza la Uongozi la Jimbo vitakutana kila baada ya miaka miwili na nusu.
Mkutano maalum/dharura yaweza kuitishwa
 
Mkutano maalum/dharura yawez.a kuitishwa
mkuu unafikiri hao chadema wanafahamu wanachokihubiri. nikuvizia upepo tu na kwenda nao huko unakovumia. thats all.
 
mkuu haya ni majimbo kwa ajili ya kurahishisha Shughuli za Chama. ni sawa na mikoa ya kipolisi Tanzania mkoa wa kinondoni, mkoa wa Temeke au mkoa wa Ilala .kikatiba hiyo siyo mikoa ni wilaya, lakini kipolisi inaitwa mikoa kwa ajili ya kurahishisha Utekelezaji wa kazi za kipolisi. So the same kwa Chadema kuwa na majimbo ambayo kwa sasa wanayatumia kwa ajili ya kurahishisha Shughuli za chama in which ,Chadema ikishinda uchaguzi 2015. itakuwa tayari kubadilisha katiba na utaratibu wa majimbo ukaanza kutumika kikatiba. Umeelewa SOMO Mkuu?
 
,Chadema ikishinda uchaguzi 2015. itakuwa tayari kubadilisha katiba na utaratibu wa majimbo ukaanza kutumika kikatiba. Umeelewa SOMO Mkuu?
Mkuu ninaomba uniweke sawa, katiba ipi ambayo unadai itabadilishwa baada ya uchaguzi. Katiba ya CHADEMA au katiba ya nchi?.
 
Sawa na ule moto mkubwa tuliouona kule Mbeya hivi karibuni, watu tuna matarajio makubwa sana na hiki kikosi cha kanda ya ziwa CHADEMA chini ya Makamanda Makere pamoja na Kamanda Cecilia Odemba.
 
ziwe kanda.santur.cd.dvd.tape bila kumtoa babu pale kwenye ukatibu mkuu chama kitakufa kabla ya 2013

Ww kuwa na chuki na babu hakumaanishi wt wote tumchukie ww ni mwanasiasa mganga tumbo uliyetimuliwa bavicha,huna lolote sawa na sisimizi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom