CHADEMA kama mnataka kushinda Arumeru Mashariki kuweni makini na huyu jamaa!

Jamani kama ni Mbinu nzuri kwanini msiige? Kama kweli anagawa rushwa muandalieni mtego akamatwe na takukuru kuliko kupiga makerere bure, siku hizi hata watu wanatembea na vitabu vya Dini wakiwakuta watu wanawahubiria habari njema kisha nyumba za ibada zinajaa.
Mkuu, nafikiri swala la msingi hapa ni kujipanga kwa ajili ya kumkabili huyu bwana. Kumbuka CCM ina jambo moja, nalo ni kwamba, lazima ishinde no matter what, hata kwa cost kubwa kiasi gani katika chagyzi ndogo.

One of the dirty games ni kununua shahada za kura, kwa hiyo akiwakamata vijana, anaweza akanunua shahada zao, na hizo shahada zikatumika kupigia kura kwenye vituo fake. Igunga ilikuwa rahisi kwasababu ya eneo lilivyo.

i am not sure kama Arumeru wanaweza kufanya the same thing.

Kuhusu kuweka mtengo akamatwe na TAKUKURU...........Mkuu, you must be kidding me....CCM hawakamatwi na TAKUKURU, Never.
Labda jamaa waweke mtego wakimkamata wampigie ile kitu wanaita Yowe........yani mwiziii, mwiziii kimjini mjini....then wamalizane nae.
 
Ninacho jua tu ni kwamba akijifanya mjanja hawa jamaa watamuingiza choo cha kike, aulize historia yao ni watu wa ajabu mno wakiamua jambo hata uwafanyeje hawabadiliki sana sana wakiona unawazingua wanakufanyizia tu..
 
Naona Chadema wameanza kulalamika hata kampeni bado hizo ni dalili za kushindwa.
 
ukiambiwa hofu na joto linazidi kupanda ndio hivyo,kulaumiana,kejeli na kila aina ya kituko siku ya mwisho sote ni watanzania
 
Anachotoa kwa watu arumeru ni kodi zao wapokee sana lakini watu hao wajiulize maswali kwanini kodi hizo zitolewe wakati wanataka uongozi tu hawa magamba je wakishapata watagawa tena au ndiyo watawasahau.Wanaarumeru kubalini mabadiliko sasa kura kwa chadema mabadiliko ya kweli
 
Huyu jamaa hata igunga alikuwa anachanja mbuga tukasema anacheza tu mwisho wa siku tukabaki kusingizia kuibiwa. Taarifa nilizonazo jana pia alikutana walimu kribu mia na hamsin. Tayari alishakutana na wazee Wa mila, viongozi wa dini na wanachuo. Jamaa ni super strategist
 
Back
Top Bottom