Chadema kama mna dhamira ya kweli pelekeni hoja binafsi bungeni kupinga kiinua mgongo

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,889
32,289
Chadema kama kweli mna uchungu na Taifa letu pelekeni hoja binafsi bungeni kupinga viinua mgongo, achaneni na habari ya shangingi moja la Mkuu wa kambi ya Upinzani Mbowe,
Kila mbunge ataondoka na zaidi ya Sh46 milioni kama kiinua mgongo baada ya Rais Jakaya Kikwete kulivunja bunge. Jumla ya wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni 350, na kila Mbunge anapata jumla Sh1.921,000 kwa mwezi ni kipato kikubwa sana. Kwenye pesa za kiinua mgongo taifa linapoteza zaidi Bilioni 12 zitalipwa kwa wabunge wote pamoja na wa Chadema, cha kushangaza kwenye ili mbowe na wenzake wamekaa kimya wanaleta usanii kwenye Shangingi moja tu na posho za 60,000,

Hii issue ya posho imekaa kiwivuwivu, tatizo si watz huwa hatupendi kuona mtu anapata kitu huwa tunajenga wivu wa kwanini yule kapata badala ya kufanya kazi,ukijiuliza deeply hiyo posho ni shilingi ngapi utagundua upuuzi wa kuijadili hoja hii, what I think watu wangekuja na constructive ideas za kuongeza income from individual level up to nation level na wala si kumsakama mbunge masikini kama ninavyowafahamu baadhi yao na hata kama watanyimwa posho hizo bado sioni unafuu wowote kwa mtanzania, the issue here tuongeze uzalishaji tuache wivu wa kimaskini.

Tatizo ni CCM itapinga just kwasababu CHADEMA ndio wamepeleka hiyo hoja binafsi na wataishoot down

Bunge la CCM sio sawa na la Kenya ambalo kama hoja binafsi itafaidisha Taifa Wabunge wa Kenya wataunga Mkono sababu ni for the motivation of the nation as general, kwetu kila kitu sawa ni from CCM na waka more than 280

Nimemuona Mhe Mkumbo online nikamuuliza swali

Mheshimiwa Dokta Kitila Mkumbo hisima yako,

Nikiwa Mtanzania mwenye uchungu na nchi hii sijafurahiwa na hatua iliyochukuliwa na wabunge wa chama chako mpaka sasa kuhusu kupunguza matumizi ya Serikali. Kama kawaida yetu kwa ajili ya ujuha tulionao mmefanikiwa "kututeka" na hoja ya posho. Lakini ukiangalia hizo posho wanazozizungumzia kina Zitto Bungeni ni pesa ndogo sana.

Je ni lini mtarudia ile dhamira ya Mhe Dr Slaa ya kupunguza mishahara ya wabunge? maana hapo ndio Serikali itafanya savings ya uhakika si tunafahamu kwa mujibu wa kiinua mgongo kwa wabunge kinatolewa kwa mujibu wa sheria ya mafao ya viongozi wa kisiasa namba 3 ya mwaka 1999 ambayo ilianza kutumika 2000 na kisha kufanyiwa marekebisho mwaka 2005 katika kipengere cha sheria namba 12.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, iliyotokana na marekebisho ya sheria ya awali ya mafao ya viongozi maalum wa kitaifa ya mwaka 1986, sio wabunge wote watakaovuna kiasi hicho cha fedha, kwa kuwa muda wao wa kuwa bungeni unatofautiana.

Mfano tukichukulia idadi tuseme Bunge la Jamhuri ya Muuungano lina wabunge 327, kati yao 49 ni mawaziri na manaibu waziri. Ukiondoa mawaziri na manaibu wao ambao kinua mgongo chao hulipwa na serikali, hivyo watakaolipwa na Bunge ni 278. Kwa mantiki hiyo, jumla ya Sh12,724,704,000 zitalipwa kama kiinua mgongo kwa wabunge hao ukiondoa mawaziri.

Fedha hizo ni sawa na asilimia 40 ya mishahara ya miaka yote mitano ya utumishi bungeni ambapo kwa mujibu wa marekebisho ya mishahara ya viongozi wakuu wa nchi na viongozi wa kisiasa yaliyofanywa Julai mwaka 2009.

Ukilinganisha na kazi wanayoifanya wabunge hawastahiki kupokea kiwango kikubwa kama hiki huu ni unyonyaji na wizi wa mchana kweupe kuliko wizi wa posho ambazo mnazipigia kelel ili kuwin popularity. Tujaribu kuwa wazalendo kidogo tufanye ya ukweli.

Asante sana mheshimiwa na ni matumaini yangu kina Zitto wataibua hoja ya mishahara ya wabunge ili kupunguza viinua mgongo vyao.

Songela sana/

Lakini akaingia mitini.

Mkuu CDM kawa wana dhamira ya kweli wao pekee wakiandika barua wapokee nusu mshahara na nusu uingizwe kwenye mendeleo na mwiho viinua mgongo vyao wapewe nusu na nusu vizungushe maswala ya maendeleo watakuwa wamefanya jambo la mbolea maana wabunge 50 mara nusu ya mil 46 ni sawa na Bil 1.150 yaani ni pesa zaidi ya mara nne ya posho za miaka mitano kwa wabunge wote!!!

Yaani cdm wanatufanya watanzania majuha sana bora slaa aliweza kulipigia kelel hili la mishahara wakaamua kumuuzia mbuzi kwenye gunia kwa kujua hata kuwa rais na hoja ya mishahara itakuwa imekufa kwani hatakuwa tena mbunge.

Hii issue ya posho imekaa kiwivuwivu, tatizo si watz huwa hatupendi kuona mtu anapata kitu huwa tunajenga wivu wa kwanini yule kapata badala ya kufanya kazi,ukijiuliza deeply hiyo posho ni shilingi ngapi utagundua upuuzi wa kuijadili hoja hii, what I think watu wangekuja na constructive ideas za kuongeza income from individual level up to nation level na wala si kumsakama mbunge masikini kama ninavyowafahamu baadhi yao na hata kama watanyimwa posho hizo bado sioni unafuu wowote kwa mtanzania, the issue here tuongeze uzalishaji tuache wivu wa kimaskini.

Mkuu hebu tupe strategy yako ikoje?

Chadema kama kweli mna uchungu na Taifa letu pelekeni hoja binafsi bungeni kupinga viinua mgongo, achaneni na habari ya shangingi moja la Mkuu wa kambi ya Upinzani Mbowe,
Kila mbunge ataondoka na zaidi ya Sh46 milioni kama kiinua mgongo baada ya Rais Jakaya Kikwete kulivunja bunge. Jumla ya wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni 350, na kila Mbunge anapata jumla Sh1.921,000 kwa mwezi ni kipato kikubwa sana. Kwenye pesa za kiinua mgongo taifa linapoteza zaidi Bilioni 12 zitalipwa kwa wabunge wote pamoja na wa Chadema, cha kushangaza kwenye ili mbowe na wenzake wamekaa kimya wanaleta usanii kwenye Shangingi moja tu na posho za 60,000,

Mkuu kwa hili mimi nakuunga mkono na wala sijifichi. Hapa tunachezewa kamchezo tu ka kitoto. Kuna miposho mingi sana ambayo inalipwa kwa wabunge. Tumeambiwa kuwa KUB anapokea million 2 kila mwezi kwa ajili ya viburudisho kwa wageni wake. KUB amekataa shangingi, sawa. Zitto amekataa posho ya vikao lakini kuna posho ya mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mashitrika ya umma mbona hajaikataa. Wanachukua mikopo ya million 90 mbona hawajasema kuwa million 90 kwa kununua gari ni nyingi tupewe mkopo wa million 40 ili wanunue gari ndogo? Kiuunua mgongo (sijui kama migongo yao imejipinda) ni kama million 45 kwa kutumikia mika mitano tu wakati mwalimu aliyetumikia nchi hii kwa miaka 30 hapati zaidi ya million 15! Ndugu zetu wabunge wa CHADEMA tuonyeshe dhamira ya kweli ya kuwatetea wananchi wa nchi hii na siyo hii ya kila mtu anakuja na single yake.

Nakuunga mkono mkuu lakini kwanini chadema peke yao au hao wengine wanajulikana kuwa hawana nia njema ?

Binafsi niliwahi leta thread hapa ya kuuliza base ya kiasi hicho wanacholipwa lakini sikujibiwa.

Najua umeanzisha hii, ili kuwafanya cdm waonekane wapo kwa ajili ya masilahi yao binafsi jambo ambalo sina uhakika sana.lakini ninavyofuatilia michango yako naona ndiyo mlengo wako.

Hata hivyo naunga mkono hoja kama utaondoa neno KAMA KWELI MNA UCHUNGU.

KUMBUKA HII VITA NI YETU SISI WANYONGE CDM WANATUSEMEA TU, NAO WAKIBADILIKA TUNATAFUTA MWINGINE.

CHADEMA pamoja na uchache wao na mizengwe toka ccm wameweka record kwa kuibua na kupinga mambo mengi ya msingi. Wewe ritz pamoja na wa-ccm wenzako hamna moral authority ku-challenge chadema on anything regarding governance. Mmeshindwa hata ku-challenge misahama ya kodi kwenye maeneo mnayowakilisha kupitia the so called 'ECONOMIC FREE ZONE'.

Hii issue ya posho imekaa kiwivuwivu, tatizo si watz huwa hatupendi kuona mtu anapata kitu huwa tunajenga wivu wa kwanini yule kapata badala ya kufanya kazi,ukijiuliza deeply hiyo posho ni shilingi ngapi utagundua upuuzi wa kuijadili hoja hii, what I think watu wangekuja na constructive ideas za kuongeza income from individual level up to nation level na wala si kumsakama mbunge masikini kama ninavyowafahamu baadhi yao na hata kama watanyimwa posho hizo bado sioni unafuu wowote kwa mtanzania, the issue here tuongeze uzalishaji tuache wivu wa kimaskini.

Unatakiwa kupimwa akili. Haki ya Mungu. Ni vyema ujue kuwa sote ni mali ya udongo na tutakufa. Ni bora ujue kuwa Mungu yupo. Ujue kuwa watanzania wengi zaidi ya asilimia 50 hawajui wale nini leo, kesho na daima. Ujue kuwa Wizi wa posho na takrima ni dhambi. Alafu ujue kuwa watu wanahitaji ata tu sh. 2000/ ili wasife hospitalini....... Nina hasira na wewe mimi. Watanzania sasa. tutaanza kuuana... kama ujinga ndo huu... Mi niko Lindi, jana nilimsikiliza Nape akipiga porojo anawadanganya masikini, iliniuma sana.

Nilikuwa tayari nimetembelea wilaya ya Lindi vijijini hasa jimbo la Mchinga (Nchinga) na Mtama. Hali ni mbaya. Nadhani kwa ugumu huu wa maisha basi kama Mungu yupo nakubaliana na bora ngamia kupita kwenye tundu la sindano.......

Kwani miaka 50 ya ccm walishapinga lipi ambalo ni la kuwanyonya wananch wa Tz? kwa uzalendo waliouonyesha chadema wanastahl kupongezwa sana, big up chadema

kama kwa hili dogo serikali yaccm inakataa na kuwatishia kuwafukuza wabunge watakao acha kusaini posho, unadhani watalielewa na kiinua mgongo.
safari hatua wameanza na posho likifanikiwa hilo wanakwenda another step

CDM mkiamua kupiga mambo ya pesa bungeni msichague aina za posho, hata hivyo viwango vya mishahara havijumuishi posho za vikao, mafuta ya gari na fedha za kujikimu ampapo sasa mbunge mmoja anapata Sh 135,000 kama posho kikao kimoja, hizi pesa nazo wabunge wa CDM wanachukuwa hakuna anaepinga sio Zitto wala Mbowe, Kwao ushindi ni kurudisha Shangingi la Mkuu wa kambi ya Upinzani bungeni, lakini kuna gari lingine kapewa Mbowe tofauti na ilo Shangingi afananyie kazi zake ilo nalo kakaa kimya hawa jamaa wasanii sana

Hii inadhihirisha jinsi gani watz wengi walivyo vilaza. We unajifikilia chadema iwe na dhamira, je we kama wewe una dhamira gani? Au ndo mawazo gando? Kama mawazo yenyewe ndo haya, walahi basi watz tunasafari ndefu isiyo na kikomo kufika mahala tunapohitaji kufika.

Mkuu vilaza ni posho gani hiyo tena? Yaani posho zipo nyingi kiasi hicho?

Naweza kusema wabunge wa Tanzania wanapata pesa sana, sina tena imani na wabunge wetu! Hawa nao kutoka upinzani tulikuwa tunawategemea kumbe nao lao ni moja kutafuna pesa tu vitu kama hivi wamekaa kimya, hakuna biashara nzuri kama ubunge auna hasara, CDM tunawapongeza kukataa posho ndogo ndogo na kurudisha gari, lakini kuna mambo mengi kumbe bungeni

binafsi sikatai swala la wabunge kupewa posho bt qanachopewa its too much!!siku zote mbunge kwa matakwa yake mwenyewe huomba ridhaa kwa wananchi ili wawatumikie kwa njia ya kuleta maendeleo jimbon na taifa kwa ujumla.sasa badala ya kuwasaidia kuwapa maendeleo wanawasaidia kutumia kodi zao tena asilimia kubwa kwa maendeleo binafsi,hakuna hela ndogo jaman kwa wananchi wa hali ya chini kuna watu wanaithamin mia km elf Kumi,na posho ndo zinasababisha walimu na watu wa fani mbalimbali kuacha kazi zao na kukimbilia ubunge hatimaye sehem nyingine kupwaya,kwel kupunguzwa kwa posho ni jambo la msingi sana

Back
Top Bottom