Chadema jaribuni sasa kuwaonyesha wananchi nini cha kufanya kabla ya kuingia madarakani

sikio la kufa siku zote halisikii dawa,tunacho subiri ni maziko ya CCM

Ndio mnavyojidanganya? CCM itakufa kama vilivyokufa vyama vingine duniani, kafa 'mungu" itakuwa CCM? lakini chadema hakitotawala Tanzania, kwa kura zipi? Hilo kumbuka.
 
Tumeona kasi na ukuaji wa chama cha CHADEMA,kiukweli kasi yake ni kubwa na haishikiki.Hujuma nyingi wanafanyiwa ikiwa lengo la kukichafua chama na kukivunja nguvu ambayo imekuwa tishio kwa chama tawala.Kasi hii haiwezi kupuuzwa na kuachwa ipite hivi hivi tu bila kuwa na changamoto ambazo CDM lazima iweze kukabiliana nayo.

Watanzania humu nchini asilimia kubwa wamegubikwa na umasikini uliokithiri,wamekata tamaa ndiyo maana wanaona kimbilio la wakati huu ni CDM.Lakini cha msingi hapa ni kuto kubweteka kwa CDM na kudhani wame concur the world bila kufanyia kazi chanagamoto hizi zinazo wakabili Watanzania maskini.

Tumeona waziri wa serikali ya awamu ya nne ana kiri bila kutafuna maneno kuwa ule mkakati wa kuondoa umasikini hakufikia malengo yake,lakini hajatuambia nini kilichosababisha MKUKUTA 1 kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa,zaidi ya umaskini kuongezeka japokuwa takwimu za makaratasi zinaonyesha umepungua kwa asilimia 2.6%.

Nchi ina lalamika,watu wake wanalalamika,serikali ina lalamika,wasomi wameshindwa kuonyesha na kutumia taaluma yao ili kuweza kuinusuru nchi na janga hili la kitaifa.

Kwakuwa hata watawala hawajui tatizo la umasikini wetu ni nini kiasi cha Watanzania kupoteza imani na chama tawala na kuamua kuhamishia nguvu za zote na matumaini yao kwa CDM,basi tunaishauri CDM ionyeshe njia kwa vitendo kuliko maneno ya majukwaani kwa kuwakomboa Watanzania kivitendo zaidi kuliko maneno.

Programme ya kwanza ya MKUKUTA haijafikia lengo,je nini plan B ya CDM ili kuweza kufikia malengo ya MKUKUTA.Pili kwa kuwa CDM wamejenga imani kwa wananchi na wananchi kuunga mkono harakati za M4C harakati hizo kwanini zisitumike sasa kwa kutengeneza mazinigra rafiki kwa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kujenga hospitali zenye tija na kuboresha elimu kwa watoto wetu.

Changamoto ni nyingi ila support hii ya wananchi isiwafanye mbweteke kiasi cha kusahau matatizo ya Watanzania,kwa ushauri huu wa bure utatuweka Watanzania katika nafasi ambayo tutaamini CDM ndiyo kimbilio letu.Tunajua kweli hamna vyanzo vya mapato lakini mtaji mkubwa wa rasilimali watu mliojivunia katika operation Sangara kwa kuwavua gamba na kuwavalisha gwanda.

Mkakati huu ikiwezekana uitwe okoa uchumi wetu tunza rasilimali zetu.Wananchi wapo tayari kutumia nguvu na rasilimali walizonazo ikiwa tu watashirikishwa katika ujenzi was taifa letu na rasilimali zao.Wakati wa malumbano uimeisha tunataka plan B kuthibitisha mkipewa nchi mnaweza.Anzaeni sasa,tafakarini na chukueni hatua.Nawasilisha

556469_362627057145142_1046740414_n.jpg



Watu wa CCM Wamelewa na Madaraka angalia Mh. Bernad Membe ana madharau sana... cheki ALIVYOMSHIKA huyu MAMA wa

watu MKONO WAKE kama Vile ni Mdudu... Hii inatosha kabisa CCM wanatakiwa kuondolewa Madarakani

Kidogo ILI WAIONE DUNIA; Hawajui DUNIA IKOJE...




 
Kila mja hukikimbilia kifo chake muda na saa ikifika ndo maana sikio la kufa halisiki dawa,kila baya wanalo fanya hawa CCM hawaoni kwa kuwa tu upofu umeshawaingia,hata kaumu Ruttu,walipojenga safina kuna wengio wao waliona kama kiroja mvua ilipoaanza ndipo wakakurupuka wakiwa too late.
 
Kifo chake ni mithili ya kifo cha mende,mende hufa miguu ikiwa juu.Mtasema sana lakini mwisho wake mate ya mlevi hayafiki chini huishia kifuani.



Ndio mnavyojidanganya? CCM itakufa kama vilivyokufa vyama vingine duniani, kafa 'mungu" itakuwa CCM? lakini chadema hakitotawala Tanzania, kwa kura zipi? Hilo kumbuka.
 
Mabadilikom nchini mwetu lazima,tunataka human resources ziweze kuwasaidia wananchi,sawa kabisa tuana kubali CDM mmetufumbua macho na kujua ukweli upo wapi kiasi cha kasi yenu kuwachanganya watawala,impact kubwa tunayo itegemea ni mmewaandaje wananchi kuweza kuzisimamia rasiliamli zao na kuzitumia katika kuleta uchumi endelevu na wenye tija kwa taifa na watu wake,kama kuwakosoa CCM mmesha wakosoa kiasi cha kutosha sasa tunatka plan B nini tufanye kupitia hii M4C Kuleta mabadiliko na uchumi wa kweli kwa kila Mtanzania
 
Mtaumia sana mnaoishi kwa kufuja mali za nchi hii tunawakikishia tutawakatamata na kuwa shitaki. Mnajijua na wewe Zomba ukimbie nchi kesi ya Ulimboka tutaifufua, Said Mwema mauaji yoote dhidi ya chadema utajibu, JK jiandae kusimama kizimbani. Nape na propaganda zako chafu hautapona.
 
Back
Top Bottom