Chadema jaribuni sasa kuwaonyesha wananchi nini cha kufanya kabla ya kuingia madarakani

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Tumeona kasi na ukuaji wa chama cha CHADEMA,kiukweli kasi yake ni kubwa na haishikiki.Hujuma nyingi wanafanyiwa ikiwa lengo la kukichafua chama na kukivunja nguvu ambayo imekuwa tishio kwa chama tawala.Kasi hii haiwezi kupuuzwa na kuachwa ipite hivi hivi tu bila kuwa na changamoto ambazo CDM lazima iweze kukabiliana nayo.

Watanzania humu nchini asilimia kubwa wamegubikwa na umasikini uliokithiri,wamekata tamaa ndiyo maana wanaona kimbilio la wakati huu ni CDM.Lakini cha msingi hapa ni kuto kubweteka kwa CDM na kudhani wame concur the world bila kufanyia kazi chanagamoto hizi zinazo wakabili Watanzania maskini.

Tumeona waziri wa serikali ya awamu ya nne ana kiri bila kutafuna maneno kuwa ule mkakati wa kuondoa umasikini hakufikia malengo yake,lakini hajatuambia nini kilichosababisha MKUKUTA 1 kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa,zaidi ya umaskini kuongezeka japokuwa takwimu za makaratasi zinaonyesha umepungua kwa asilimia 2.6%.

Nchi ina lalamika,watu wake wanalalamika,serikali ina lalamika,wasomi wameshindwa kuonyesha na kutumia taaluma yao ili kuweza kuinusuru nchi na janga hili la kitaifa.

Kwakuwa hata watawala hawajui tatizo la umasikini wetu ni nini kiasi cha Watanzania kupoteza imani na chama tawala na kuamua kuhamishia nguvu za zote na matumaini yao kwa CDM,basi tunaishauri CDM ionyeshe njia kwa vitendo kuliko maneno ya majukwaani kwa kuwakomboa Watanzania kivitendo zaidi kuliko maneno.

Programme ya kwanza ya MKUKUTA haijafikia lengo,je nini plan B ya CDM ili kuweza kufikia malengo ya MKUKUTA.Pili kwa kuwa CDM wamejenga imani kwa wananchi na wananchi kuunga mkono harakati za M4C harakati hizo kwanini zisitumike sasa kwa kutengeneza mazinigra rafiki kwa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kujenga hospitali zenye tija na kuboresha elimu kwa watoto wetu.

Changamoto ni nyingi ila support hii ya wananchi isiwafanye mbweteke kiasi cha kusahau matatizo ya Watanzania,kwa ushauri huu wa bure utatuweka Watanzania katika nafasi ambayo tutaamini CDM ndiyo kimbilio letu.Tunajua kweli hamna vyanzo vya mapato lakini mtaji mkubwa wa rasilimali watu mliojivunia katika operation Sangara kwa kuwavua gamba na kuwavalisha gwanda.

Mkakati huu ikiwezekana uitwe okoa uchumi wetu tunza rasilimali zetu.Wananchi wapo tayari kutumia nguvu na rasilimali walizonazo ikiwa tu watashirikishwa katika ujenzi was taifa letu na rasilimali zao.Wakati wa malumbano uimeisha tunataka plan B kuthibitisha mkipewa nchi mnaweza.Anzaeni sasa,tafakarini na chukueni hatua.Nawasilisha
 
Chama huwa kinaandaa ilani wakati wa uchaguzi ambazo inakuwa kama mkataba wanaotakiwa kuutekeleza pindi watakapopewa ridhaa. Nadhan muda bado.
 
Mbona kila mikutano ya CDM wanawaambia wananchi Chakufanya mojawapo kubwa ni kuwanyima CCM kura wawape wao. Na baada ya hapo CDM itachukua Uongozi waanze kutekeleza Ilani yao ya Uchaguzi majibu yapo wazi Mkuu kama ni muudhuriaji mzuri wa mikutano yao lakini kama unategemea JF tuu itakuwa ngumu kidogo
 
Nani alikudanganya Chadema watapata madaraka ya kuongoza hii nchi? Hizo ni ndoto za alinacha.
 
Nakuombea maisha marefu ili ushuhudie mageuzi ya nchi hii 2015. Hakika tutakula kunywa na kusherehekea pamoja!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nakuombea maisha marefu ili ushuhudie mageuzi ya nchi hii 2015. Hakika tutakula kunywa na kusherehekea pamoja!

Namimi nakuombea maisha marefu uwe disappointed. Utanikumbuka. Chadema ni chama kwa ajili ya watu aina fulani tu si cha kila mtu, hilo halina siri.
 
Tumeona kasi na ukuaji wa chama cha CHADEMA,kiukweli kasi yake ni kubwa na haishikiki.Hujuma nyingi wanafanyiwa ikiwa lengo la kukichafua chama na kukivunja nguvu ambayo imekuwa tishio kwa chama tawala.Kasi hii haiwezi kupuuzwa na kuachwa ipite hivi hivi tu bila kuwa na changamoto ambazo CDM lazima iweze kukabiliana nayo.

Watanzania humu nchini asilimia kubwa wamegubikwa na umasikini uliokithiri,wamekata tamaa ndiyo maana wanaona kimbilio la wakati huu ni CDM.Lakini cha msingi hapa ni kuto kubweteka kwa CDM na kudhani wame concur the world bila kufanyia kazi chanagamoto hizi zinazo wakabili Watanzania maskini.

Tumeona waziri wa serikali ya awamu ya nne ana kiri bila kutafuna maneno kuwa ule mkakati wa kuondoa umasikini hakufikia malengo yake,lakini hajatuambia nini kilichosababisha MKUKUTA 1 kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa,zaidi ya umaskini kuongezeka japokuwa takwimu za makaratasi zinaonyesha umepungua kwa asilimia 2.6%.

Nchi ina lalamika,watu wake wanalalamika,serikali ina lalamika,wasomi wameshindwa kuonyesha na kutumia taaluma yao ili kuweza kuinusuru nchi na janga hili la kitaifa.

Kwakuwa hata watawala hawajui tatizo la umasikini wetu ni nini kiasi cha Watanzania kupoteza imani na chama tawala na kuamua kuhamishia nguvu za zote na matumaini yao kwa CDM,basi tunaishauri CDM ionyeshe njia kwa vitendo kuliko maneno ya majukwaani kwa kuwakomboa Watanzania kivitendo zaidi kuliko maneno.

Programme ya kwanza ya MKUKUTA haijafikia lengo,je nini plan B ya CDM ili kuweza kufikia malengo ya MKUKUTA.Pili kwa kuwa CDM wamejenga imani kwa wananchi na wananchi kuunga mkono harakati za M4C harakati hizo kwanini zisitumike sasa kwa kutengeneza mazinigra rafiki kwa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kujenga hospitali zenye tija na kuboresha elimu kwa watoto wetu.

Changamoto ni nyingi ila support hii ya wananchi isiwafanye mbweteke kiasi cha kusahau matatizo ya Watanzania,kwa ushauri huu wa bure utatuweka Watanzania katika nafasi ambayo tutaamini CDM ndiyo kimbilio letu.Tunajua kweli hamna vyanzo vya mapato lakini mtaji mkubwa wa rasilimali watu mliojivunia katika operation Sangara kwa kuwavua gamba na kuwavalisha gwanda.

Mkakati huu ikiwezekana uitwe okoa uchumi wetu tunza rasilimali zetu.Wananchi wapo tayari kutumia nguvu na rasilimali walizonazo ikiwa tu watashirikishwa katika ujenzi was taifa letu na rasilimali zao.Wakati wa malumbano uimeisha tunataka plan B kuthibitisha mkipewa nchi mnaweza.Anzaeni sasa,tafakarini na chukueni hatua.Nawasilisha

Ina maana CDM hawana mpango wowote kiasi hicho hadi waanze tena kuendeleza ya CCM? Nilijua tu, hawa jamaa vurugu, maandamano na matusi haviwezi kuwafikisha mahali popote. Sasa kama hawana hata cha kuanza nacho hiyo ridhaa nani atawapa?
 
Tumeona kasi na ukuaji wa chama cha CHADEMA,kiukweli kasi yake ni kubwa na haishikiki.Hujuma nyingi wanafanyiwa ikiwa lengo la kukichafua chama na kukivunja nguvu ambayo imekuwa tishio kwa chama tawala.Kasi hii haiwezi kupuuzwa na kuachwa ipite hivi hivi tu bila kuwa na changamoto ambazo CDM lazima iweze kukabiliana nayo.

Nchi ina lalamika,watu wake wanalalamika,serikali ina lalamika,wasomi wameshindwa kuonyesha na kutumia taaluma yao ili kuweza kuinusuru nchi na janga hili la kitaifa.

Japo mm simsemaji wa chama lakini kuwa na uhakika tu CDM inalijua hili fika na baadhi ya wataalamu wake wanamipango mingi tu na ya uhakika kuondoa hii hali kwa mipangilio ya muda mfupi wa kati na wa muda mrefu..Tatizo ni moja tu kwakua tumeona CCm wakiwa waigaji wazuri na kudandia mipango isiyoifahamu vizuri kwa lengo tu la kuwa entice wapiga kura si busara kui-expose kwa sasa mpaka tutakapo ikamata dola...Usijali everything unde control na CDM is among the best party katika ku-tap human resource iliyopo TZ kitu ambacho chama kilichopo kinapeleka kila kitu kisiasa hata pale siasa haihitajiki..

Angalia jinsi CCM inavyokosolewa na wasomi wengi wa nchi hii ni kwa sababu tu kuna gap kubwa kati yao hao na serikali inayoendeshwa kisiasa zaidi kuliko kitaalamu.
 
Namimi nakuombea maisha marefu uwe disappointed. Utanikumbuka. Chadema ni chama kwa ajili ya watu aina fulani tu si cha kila mtu, hilo halina siri.

Mbona midomo inatetemeka hujiamini???? tulia lete points acha ulojo
 
Namimi nakuombea maisha marefu uwe disappointed. Utanikumbuka. Chadema ni chama kwa ajili ya watu aina fulani tu si cha kila mtu, hilo halina siri.

Mchango wa chadema katika kupambana na upuuzi wa ccm unajulikana.
Akili za tiss nu sawa na akili za mwigulu. Propaganda haisaidii lilote kwenye society ya watu wanaojitambua.

Get a life dude.
 
Ni kweli mkuu Zomba, CDM ni chama kwa ajili ya watu wenye akili timamu tu, siyo cha mazuzu kama ninyi.
 
Mchango wa chadema katika kupambana na upuuzi wa ccm unajulikana.
Akili za tiss nu sawa na akili za mwigulu. Propaganda haisaidii lilote kwenye society ya watu wanaojitambua.

Get a life dude.

Mngekuwa mnajitambuwa msingejiita wapiganaji.
 
Hao bado wana safari ndefu sana. Maneno ya sitta yaliwachoma sana kutokana na ukweli wake. Mi najiuliza, 2015 kina sugu,mnyika,mdee,slaa sijui watakula wapi. Ni vizuri wajaribu kuweka kafungu fulani pembeni lasivyo watakufa njaa siku za mbeleni. 2015 ndio mwisho wao.
 
Namimi nakuombea maisha marefu uwe disappointed. Utanikumbuka. Chadema ni chama kwa ajili ya watu aina fulani tu si cha kila mtu, hilo halina siri.

Yaani wewe Nape atakuwa anakulipa elfu 5 kwa siku.......kwa ukilaza umewazidi wenzio wote!

System At Work daaah!
 
Hao bado wana safari ndefu sana. Maneno ya sitta yaliwachoma sana kutokana na ukweli wake. Mi najiuliza, 2015 kina sugu,mnyika,mdee,slaa sijui watakula wapi. Ni vizuri wajaribu kuweka kafungu fulani pembeni lasivyo watakufa njaa siku za mbeleni. 2015 ndio mwisho wao.

Hilo likilaza jengine na pumba zake!
 
Back
Top Bottom