CHADEMA iwe makini na Mbatia pamoja na Zitto

Wana JF napenda kutoa angalizo kwa CDM kuwa makini na hawa jamaa wawili kwa hawa wanakazi muhimu kwao ya kuibomoa CDM kwani ni maagenti wa usalama wa taifa.

Huyu Mbatia kwa wale tuliokuwa naye pale chuo kukuu mwaka wa 1990 mtakumbuka mambo aliyotufanyia tulipoanzisha ule mgomo. Mwenzetu tulikuwa tunapanga na yeye kwenye mkutano wetu kumbe usiku wake anapelekeka taarifa ya kile tunachopanga tunawahiwa na tulimgundua na kutenga.

Mtakumbumbuka pia alisababisha Rais wa Campas ya muhimbili ndugu Kimaro kufukuzwa chuo na hakurudi tena baada ya kugundua kuwa msaliti alikuwa katikati yetu. Huyu jammaa anajifanya mpinzani hamna lolote ni sawa na Zitto nionavyomienendo yake.

Kama hamuamini subiri siku zinakuja mtagundua hayo nisemayo.

Hawa jamaa hupandikizwa kwa staili ya hali ya juu sana kiasi cha nyie kutotambua cha msingi ni kuwa makini na hawa jamaa wasije wakachelewesha ukombozi wa Watanzania.
Red, say again.
 
TISS wamemtuma J.K amteue MBATIA awe infomer wao
kuhusu mipango ya CHADEMA wakiwa BUNGENI!!!!!
pia kuwachokonoa wabunge wa CDM baada ya kuhusiana nao!!!!

AFRICA tutatoka
 
Wadau nadhani angalizo la Joblube lina ujumbe wa muhimu kuwa na tahadhari na hasa jina moja la James Mbatia unaona tayari JK amemteua kuwa moja ya wabunge ili ateuliwe kuwa mmoja wa mawaziri.Kumbe huyu hakuwa kiongozi wa upinzani bali alikuwa na kazi maalumu kwa serikali ya magamba! Zitto mimi sina shida naye ni mpiganaji makini nadhani pia hata akiteuliwa kuwa mmoja wa serikali ya magamba ataikataa hiyo offer.
 
Zitto ni kijana mzuri sana kwa hoja but tatizo kuna vitu anakuwa anavifanya ambavyo sio comfirmed sana ambavyo vinamuondolea imani kwa wanachama wenzak na kuhusu mbati huyo ni kibaraka haswaaa.
 
zitto ni jembe ila huwa anateleza kama wanadamu wengine,na huu ni muda wa Zitto kurudisha imani kwetu sie Walalahoi.

Mbona Slaa, Mbowe, Lema, Lissu na wengine hawatelezi kuteleza kwake... ni bora zito akawa anasoma comments kama hizi na kuzitumia kuji-evaluate, vinginevyo hawezi kuaminika hata akifanya jambo gani zuri, cha msingi awe consistent
 
Nitasema kuhusu Mbatia. Ya Zitto nitakuachia mwenyewe - mi simjui kivile.

Stori yako ya 1990 si sahihi.... I know all what happened (who did what when where).
Na kusema Mbatia ni usalama wa taifa nalo si sahihi..... Namfahamu sana Mbatia fyi.

Lakini nakiri kuwa siasa zimem-transform sana Mbatia. Sifa ya upiganaji aliyokuwa nayo pale UDSM na wakati anajiunga NCCR sasa imemtoka kabisa...amekuwa opportunist na mtu wa kupenda misifa.

Haambiliki hata akishauriwa ....so, si mtu wa kumwamini tena na amekosa sifa kama mpambanaji kuelekea ukombozi tunaoutamani kwenye taifa hili.

Na mimi nafahamu alikuwa mpambanaji chuo kikuu; na alikuwa mmoja wa waliofukuzwa....sijui hata ile degree yake ya engineering alikuja kumalizia wapi....
 
Ukweli ni kuwa zito tumempoteza, na sio tena tegemeo letu kama kamanda wa kuleta mabadiliko. TIME WILL TELL. Unafahamu walivomkata maini huyo zito? mafisadi wamempa 400Milioni na kumfunglia kampuni ya ujenzi mheshimiwa Zito. Unafahamu walichofanya baada ya hapo? tenda zote za ujenzi wa madaraja mkoani Kigoma kapewa yeye zito na kampuni yake. This is true, not longolongo za mitaani. Asanteni

mi namkubali kamanda zito kwa mambo ambayo kalifanyia taifa. binadamu hakosi mapungufu ni kawaida lkn kufikia kuframe tuhuma km hizi! 7babu kamanda zito yupo jf am sure atakuja kutoa ufafanuzi juu ya hizo kampuni km yeye ni ceo or whatever. pia kama sikosei cdm watakuwa na full data ya every move ya issue hiyo kama ipo since wana vitengo vya kufuatilia(kama vipo).
 
Umenena Mzee wa TFDA!

Wana JF hebu tuwe positive thinker! kweli kwa mtu mwenye akili timamu unahitaji mfano gani ili ujue kama zito ni BOMU ambalo CDM tunalo kitandani na kuna siku litaripuka? Labda kwa wale msiomjua zito kwa uchache kumbukeni kipindi cha uchaguzi 2010 alivyokuwa anawasiliana na USALAMA WA TAIFA ili kuihujumu CDM, alipewa mpaka ushahidi wamaneno yaliyonaswa wakati wa mazungumzo yao na HAJAKANA mpaka leo. Tatizo watanzania wengi tupo kama mtu na hawala yake. Leo anakufumania kesho akikupeleka shoping (akikupa maneno mazuri-mwanasiasa) Unasahau kabisa.....Kweli zito Kawashika kama si kuwaloga wengi humu JF. Au kuna watu atakuwa anawalipa kwa kazi ya kumsafisha.
 
Wana JF napenda kutoa angalizo kwa CDM kuwa makini na hawa jamaa wawili kwa hawa wanakazi muhimu kwao ya kuibomoa CDM kwani ni maagenti wa usalama wa taifa.

Huyu Mbatia kwa wale tuliokuwa naye pale chuo kukuu mwaka wa 1990 mtakumbuka mambo aliyotufanyia tulipoanzisha ule mgomo. Mwenzetu tulikuwa tunapanga na yeye kwenye mkutano wetu kumbe usiku wake anapelekeka taarifa ya kile tunachopanga tunawahiwa na tulimgundua na kutenga.

Mtakumbumbuka pia alisababisha Rais wa Campas ya muhimbili ndugu Kimaro kufukuzwa chuo na hakurudi tena baada ya kugundua kuwa msaliti alikuwa katikati yetu. Huyu jammaa anajifanya mpinzani hamna lolote ni sawa na Zitto nionavyomienendo yake.

Kama hamuamini subiri sikuzinakuja mtagundua hayo nisemayo.

Hawa jamaa hupandikizwa kwa staili ya hali ya juu sana kiasi cha nyie kutotambua cha msingi ni kuwa makini na hawa jamaa wasije wakachelewesha ukombozi wa Watanzania.

ZITO NI BOMU, SIKU LIKILIPUKA WATU NDIO MTAAMINI! Huyu mtu ni mjanja sana, ana maneno mazuri na anaelewa watanzania wanapenda nini ili wadanganywe kirahisi. Zito CCM imekupatia nini? Unajua adhma yako ya kuivuruga CDM ikishindikana mpaka 2015 ndio utakuwa mwisho wako kisiasa.
 
Your are not serious! ZITO ni tatizo, Huu ndio mtihani mgumu kuliko yote tulionao CDM. Watanzania wengi wanamkubali bila kumuelewa dhamira yake kisiasa ni ipi? Hivyo kuwaaminisha kwamba ZITO ni tatizo hapo ndio inakuwa shida, but i believe one day a true ZITO tutamjua wote na huo ndio utakuwa mwisho wake kisiasa!
 
ni hoja yako; lakini jihadhali sana kuzua migawanyiko ndani ya CDM-mkombozi wetu kama utakuwa umetumwa!!. Km mbatia ongelea, lakini zitto ni jemedari wetu wa CDM-muache kumugusa na usimuhusishe na mbatia!!

Mbatia hawezi kulinganishwa na Zito.

Zito
Tatizo lake kubwa anapenda sana madaraka. Kutokana na kutokuwa na uhakika atayafikia kwa namna gani madaraka, mara nyingi amejikuta akichanganya mambo, mara kuwa kinyume na viongozi wenzake (alimradi tu aonekane kuwa bora kuliko wenzake), mara kuwa karibu na CCM na viongozi wake (akidhani kwa namna fulani wanaweza kumsaidia kufikia malengo yake ya kuyapata madaraka), mara kutumiwa na usalama wa Taifa akidhania kuwa nao wanaweza kumsaidia, mara kujisogeza kwa mafisadi, n.k. Ni mtu ambaye ajenda yake kubwa ni namna ya kuyapata madaraka makubwa bila ya kujali anayafikia kwa namna gani. LAKINI pamoja na matatizo yote haya, kuna mambo kadhaa ambayo Zito anaweza kusimama mbele ya Watanzania na kusema kuwa nimefanya mambo kadhaa kwaajili ya Taifa langu. Mbatia hana hata moja la kujivunia, kama kuna kumbukumbu ya matendo ya Mbatia, yote ni ya kuliangamiza Taifa.

Mbatia
Huyu haeleweki kabisa, na uwezo na upeo wake ni mdogo sana ukilinganisha na Zito. Ni mtu mnafiki, toka akiwa Chuo Kikuu, ni mtu aliyekuwa akiyapenda sana madaraka lakini asiye kuwa na uwezo. Miaka ya hivi karibuni, maisha yake yote amekuwa akitegemea ufadhili wa CCM. Kwa sasa ni mtu aliyekata tamaa, ambaye yupo tayari kupokea chochote kuokoa maisha.
 
Welll well, well, time will tell all in open. Mwanzoni Mrema zilikuwa ni story za hapa na pale lakini wakati muafaka ulifika kila mtu akajua uhalisia wake.
 
Zitto ni jembe la ukweli na ni yeye aliyesababisha CHADEMA kipate mvuto wa kipekee kutoka kwa vijana,ni Zitto ndiye aliyefungua milango kwa vijana kutaka uongozi kupitia CHADEMA. Pia zitto anapunguza nguvu hoja ya kwamba CHADEMA ni chama cha watu wa kaskazini hasa wachaga,ingawa kuna ukweli ndani yake.Kama wewe hutambui mchango wa zitto utakuwa na matatizo makubwa ama vp mfukuzen basi muone,mabwege nyie. Kwanza nani kakwambia ulete jamvin thread hii we paka shume? Mijitu mingine b'ana.
 
Zitto Zuberi Kabwe huwezi kumfananisha na Mbatia hata kwa bahati mbaya!!Sifa kubwa aliyonayo Zitto ambayo inamgharimu mbele za watu wasiofikiri sana ni uwezo wa kusema na kusimamia ukweli bila kujali ni nani anachukia au kufurahi as long as maslahi ya taifa hayaathiriki.Uchaguzi wa 2010 Zitto aliongoza harakati za kupigania ushindi wa Ally Mlehe(mgombea wa CDM Kigoma mjini),alishikiliwa na police for >6hrs lkn leo mnasema mawasiliano yake na TISS yalilenga kuihujumu CDM!??CDM ipi???Tuhuma za Zitto kuitwa bomu hazikuwepo mpaka alipotangaza nia ya kugombea uenyekiti wa chama jambo ambalo lilikuwa haki yake kikatiba,mafisadi walioko kwenye upinzani wamekuwa wakitumia Mwanahalisi na Tanzania Daima kumchafua kwa nguvu zote.Zitto alionekana msaliti eti kwa kusema JK pamoja na udhaifu mkubwa wa serikali yake amejitahidi kuleta maendeleo Kigoma akilinganishwa na marais watatu waliomtangulia,mlitaka aseme nini wakati ndio ukweli???
 
Wana JF napenda kutoa angalizo kwa CDM kuwa makini na hawa jamaa wawili kwa hawa wanakazi muhimu kwao ya kuibomoa CDM kwani ni maagenti wa usalama wa taifa.

Huyu Mbatia kwa wale tuliokuwa naye pale chuo kukuu mwaka wa 1990 mtakumbuka mambo aliyotufanyia tulipoanzisha ule mgomo. Mwenzetu tulikuwa tunapanga na yeye kwenye mkutano wetu kumbe usiku wake anapelekeka taarifa ya kile tunachopanga tunawahiwa na tulimgundua na kutenga.

Mtakumbumbuka pia alisababisha Rais wa Campas ya muhimbili ndugu Kimaro kufukuzwa chuo na hakurudi tena baada ya kugundua kuwa msaliti alikuwa katikati yetu. Huyu jammaa anajifanya mpinzani hamna lolote ni sawa na Zitto nionavyomienendo yake.

Kama hamuamini subiri sikuzinakuja mtagundua hayo nisemayo.

Hawa jamaa hupandikizwa kwa staili ya hali ya juu sana kiasi cha nyie kutotambua cha msingi ni kuwa makini na hawa jamaa wasije wakachelewesha ukombozi wa Watanzania.

Haya uliyoyaandika yanaanza kuonekana kamanda.
 
humu watu wengi huwa wanaandika kishabiki cjui kwa faida ya nani..na wengine lengo ni kuibomoa cdm thats y utackia kaskazini..kiukweli mimi aliyenivutia cdm ni silaa hapa aliposimamia ile list of shame pamoja na vitisho vyote..na hata alipowapiga wanajeshi beat kuhusu meremeta,which is quat unusual..nilivutiwa na zito alipokuwa msimamizi na mchambuzi mahiri wa migodi yetu..ana hazina ya takwimu na elimu nzito ya migodi yetu,kiwango cha uvunaji, na hata muda wa kuisha madini ktk migodi husika..kaamua kuificha hiyo elimu..nilibahatika kumckia kidogo miaka hiyo..hasemi tena.. Nimejua buzwagi,n-mara,tulawaka,bulyanhulu na pamoja na viwango vya mrabaha from zitto..je ukimya huu ni kwa faida ya nani..? nimekosa imani na huyu kaka yangu..
 
Wana JF napenda kutoa angalizo kwa CDM kuwa makini na hawa jamaa wawili kwa hawa wanakazi muhimu kwao ya kuibomoa CDM kwani ni maagenti wa usalama wa taifa.

Huyu Mbatia kwa wale tuliokuwa naye pale chuo kukuu mwaka wa 1990 mtakumbuka mambo aliyotufanyia tulipoanzisha ule mgomo. Mwenzetu tulikuwa tunapanga na yeye kwenye mkutano wetu kumbe usiku wake anapelekeka taarifa ya kile tunachopanga tunawahiwa na tulimgundua na kutenga.

Mtakumbumbuka pia alisababisha Rais wa Campas ya muhimbili ndugu Kimaro kufukuzwa chuo na hakurudi tena baada ya kugundua kuwa msaliti alikuwa katikati yetu. Huyu jammaa anajifanya mpinzani hamna lolote ni sawa na Zitto nionavyomienendo yake.

Kama hamuamini subiri sikuzinakuja mtagundua hayo nisemayo.

Hawa jamaa hupandikizwa kwa staili ya hali ya juu sana kiasi cha nyie kutotambua cha msingi ni kuwa makini na hawa jamaa wasije wakachelewesha ukombozi wa Watanzania.

Mbona James naye alifukuzwa na hajawahi kurudi Chuo Kikuu cha Dar es salaam? Let us be objective.
 
zitto ni jembe ila huwa anateleza kama wanadamu wengine,na huu ni muda wa Zitto kurudisha imani kwetu sie Walalahoi.

''Mawaziri msimsingizie Raisi na kumchafua kwa uzembe wenu na ubaridhifu wenu wa kushindwa kusimamia mali na pesa za walipa kodi kwa manufaa yenu binafsi i lazima muwajibike na mchukuliwe hatua stahiki''-ZITTO KABWE ZUBERI
 
Back
Top Bottom