Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,482
- 40,001
Mojawapo ya vitu ambavyo sipendi kwenye CCM ni huu utaratibu wa kikomunisti ambapo watu fulani katika majoho yao wanatengua maamuzi ya kura kwa ajili ya maslahi ya "chama". Badala ya kuwachuja watu kabla ya kupiga kura CCM ikabuni mtindo mbovu kabisa wa kuwachuja watu baada ya kura.
Matokeo yake, mtu ambaye amefanya vizuri kwenye kura za maoni na kwa uhalali wote anaweza kujikuta anaenguliwa baadaye kwa sababu na kisingizio chochote kile. Hivyo, mfumo wa rushwa, kubebana na kuburuzana umeendelea kudumishwa.
Sasa, chama ambacho kinataka kuleta mabadiliko cha CHADEMA kinasikitisha kuwa nacho kimerithi na kukumbatia mfumo huo huo mbovu. Habari kwamba baadhi ya wagombea wake walioshinda katika kura za maoni baada ya kufanyia jasho kuenguliwa na vikao vya juu vya "chama" ni habari za kusikitisha na zinaonesha kuwa mfumo ule ule mbovu wa demokrasia ya 'chama' umerithishwa ndani ya Chadema na utaleta matatizo yale yale (kama bado haujaleta).
Kwamba wagombea kama Regia Mtema (kilombero) na Rachel Mashishanga (Segerea) wameombwa kuachia nafasi zao kuwapisha watu wengine (wote wanaume) ni jambo la kufanya watu kutikisa vichwa vyao. Chadema haiwezi kuendelea kusubiria viti vya vijana au wanawake ili kuwapa nafasi za kugombea.
Moyo wa ujasiri uliooneshwa na kina dada hao hata wakaamua kugombea kwenye majimbo na kuonekana kuwa wako tayari kuhukumiwa na wapiga kura wote ni jambo ambalo Chadema inapaswa na ilipaswa kulitetea na kuwapigania hadi dakika ya mwisho. Kina dada hawa wameonesha ujasiri na utayari ambao haupaswi kubomolewa kwa sababu Makao Makuu wanataka watu fulani.
Mpendazoe na huyo wakili wa Kilombero wote walikuwa na nafasi ya kugombea toka mwanzo kama wangetaka. Lakini haya ya kuonekana kubebwa na chama kwa sababu yoyote hayaoneshe "demokrasia" bali ukiritimba wa mfumo dume ambao utawasumbua Chadema baadaye. Ni kweli kuwa katika nafasi karibu zote za juu za Chadema zinashikiliwa na wanaume lakini sitaki kuamini kuwa hilo pekee linaweza kuwafanya wasione umuhimu wa kuwalinda wagombea wake waliojitokeza.
Ninachosema ni kuwa Chadema inataka demokrasia basi iwe tayari kulipa gharama yake. Isiwe kama CCM ambayo kwake demokrasia ni anasa. Ukiondoa tuhuma za vitendo vya rushwa au ukiukwaji wa maadili Chadema iwaachilie wagombea wake walioshinda kura za maoni wasimame kama wagombea wa chama. Hao wengine kama kweli wanataka nafasi hizo wasubiri 2015.
Watanzania wanataka kitu "tofauti" na CCM; wanata kuona mfumo tofauti wa kisiasa na chama tofauti na wa CCM. Wanajua kuwa baadhi ya matatizo yaliyopo leo hii ni matokeo ya mfumo mbovu wa utawala wa kisiasa wa CCM. Lakini kama Chadema hawako tayari kubadilisha mfumo wao ili uwe wa kidemokrasia zaidi (la kushangaza ni kuwa ni chama cha "demokrasia" angalau CCM ni cha "mapinduzi.. kupinduana"). Tuwape Watanzania sababu ya kutumaini kilicho bora. Lakini kwenye madogo haya inakuwa kazi kwa makubwa itakuwaje? Natumaini cool heads will prevail.
Go Regia
Go Rachel
Kina R n R wasikate tamaa kwani hata kama wataenguliwa ukweli unabakia umeandikwa kuwa walishinda kura za maoni na walienguliwa na chama si kwa sababu ya rushwa au tuhuma za kukiuka maadili bali kwa sababu walikuwa ni aidha ni wanawake au hawakuwa tayari kupiganiwa na chama hadi ushindi.