Elections 2010 CHADEMA iwaachilie walioshinda kura za maoni wagombee

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Mojawapo ya vitu ambavyo sipendi kwenye CCM ni huu utaratibu wa kikomunisti ambapo watu fulani katika majoho yao wanatengua maamuzi ya kura kwa ajili ya maslahi ya "chama". Badala ya kuwachuja watu kabla ya kupiga kura CCM ikabuni mtindo mbovu kabisa wa kuwachuja watu baada ya kura.

Matokeo yake, mtu ambaye amefanya vizuri kwenye kura za maoni na kwa uhalali wote anaweza kujikuta anaenguliwa baadaye kwa sababu na kisingizio chochote kile. Hivyo, mfumo wa rushwa, kubebana na kuburuzana umeendelea kudumishwa.

Sasa, chama ambacho kinataka kuleta mabadiliko cha CHADEMA kinasikitisha kuwa nacho kimerithi na kukumbatia mfumo huo huo mbovu. Habari kwamba baadhi ya wagombea wake walioshinda katika kura za maoni baada ya kufanyia jasho kuenguliwa na vikao vya juu vya "chama" ni habari za kusikitisha na zinaonesha kuwa mfumo ule ule mbovu wa demokrasia ya 'chama' umerithishwa ndani ya Chadema na utaleta matatizo yale yale (kama bado haujaleta).

Kwamba wagombea kama Regia Mtema (kilombero) na Rachel Mashishanga (Segerea) wameombwa kuachia nafasi zao kuwapisha watu wengine (wote wanaume) ni jambo la kufanya watu kutikisa vichwa vyao. Chadema haiwezi kuendelea kusubiria viti vya vijana au wanawake ili kuwapa nafasi za kugombea.

Moyo wa ujasiri uliooneshwa na kina dada hao hata wakaamua kugombea kwenye majimbo na kuonekana kuwa wako tayari kuhukumiwa na wapiga kura wote ni jambo ambalo Chadema inapaswa na ilipaswa kulitetea na kuwapigania hadi dakika ya mwisho. Kina dada hawa wameonesha ujasiri na utayari ambao haupaswi kubomolewa kwa sababu Makao Makuu wanataka watu fulani.

Mpendazoe na huyo wakili wa Kilombero wote walikuwa na nafasi ya kugombea toka mwanzo kama wangetaka. Lakini haya ya kuonekana kubebwa na chama kwa sababu yoyote hayaoneshe "demokrasia" bali ukiritimba wa mfumo dume ambao utawasumbua Chadema baadaye. Ni kweli kuwa katika nafasi karibu zote za juu za Chadema zinashikiliwa na wanaume lakini sitaki kuamini kuwa hilo pekee linaweza kuwafanya wasione umuhimu wa kuwalinda wagombea wake waliojitokeza.

Ninachosema ni kuwa Chadema inataka demokrasia basi iwe tayari kulipa gharama yake. Isiwe kama CCM ambayo kwake demokrasia ni anasa. Ukiondoa tuhuma za vitendo vya rushwa au ukiukwaji wa maadili Chadema iwaachilie wagombea wake walioshinda kura za maoni wasimame kama wagombea wa chama. Hao wengine kama kweli wanataka nafasi hizo wasubiri 2015.

Watanzania wanataka kitu "tofauti" na CCM; wanata kuona mfumo tofauti wa kisiasa na chama tofauti na wa CCM. Wanajua kuwa baadhi ya matatizo yaliyopo leo hii ni matokeo ya mfumo mbovu wa utawala wa kisiasa wa CCM. Lakini kama Chadema hawako tayari kubadilisha mfumo wao ili uwe wa kidemokrasia zaidi (la kushangaza ni kuwa ni chama cha "demokrasia" angalau CCM ni cha "mapinduzi.. kupinduana"). Tuwape Watanzania sababu ya kutumaini kilicho bora. Lakini kwenye madogo haya inakuwa kazi kwa makubwa itakuwaje? Natumaini cool heads will prevail.
Go Regia
Go Rachel

Kina R n R wasikate tamaa kwani hata kama wataenguliwa ukweli unabakia umeandikwa kuwa walishinda kura za maoni na walienguliwa na chama si kwa sababu ya rushwa au tuhuma za kukiuka maadili bali kwa sababu walikuwa ni aidha ni wanawake au hawakuwa tayari kupiganiwa na chama hadi ushindi.
 
Mwanakijiji,

You hit the point, tupo wote hapa. Nampenda Regia kwa jinsi ninavyomsoma hapa ila kama wamemshika sharti bila shaka tusubiri kwa nini? naamini wote watazungumzia hili yaani uongozi na wao binafsi.
 
Kama kweli chadema wanafanya utoto huu basi ccm itaendelea kushika hatamu kwa miaka mingi sana ijayo......

Juzi kulikuwa na mtu hapa anahoji jinsi slaa alivyopitishwa na chama kugombea urais, nikadhani wamemaliza ukiukwaji wa katiba, kumbe bado wanendelea???
 
Chadema lazima iliangalie kwa dhati hili suala. Tunafurahia tumepata mtetezi wa wanyonge kumbe sera za ukiritimba bado zimeendelea kupewa kipaumbele. Regia na Rachel tunawahitaji muwe sauti yetu kina mama wa Tanzania. Msikubali kunyamazishwa kwa visingizio vya aina hii. Mpendazoe alishindwa kura za maoni, angoje kama kuna ubunge wa kuteuliwa labda apate huku. Kwani lazima awe mbunge? Akikosa this time asubiri miaka mitano. Au ndiyo yale mazoea yetu tunadhani ubunge ni profession? Kila mshindani ajue kuna kushinda na kukosa, kama kakosa aachie wengine. Wasitunyime nafasi yetu ya kwenda mbele kwa visingizio vya kubebana.
 
mwanakijiji makala yako kama imeegemea upande wa haki za wanawake hivi?!

unataka kusema chadema kuna mfumo dume?!
 
Dah! hii inasikitisha sana.

I may sit out this election if this is the kind of nonsense that is going on for I won't have anything to vote for...
 
Nyangi Ngabu............wewe kapige tu kura lakini ukae ukumbuke kuwa upinzani na ccm hakuna tofauti ya hivyo na tusitarajie makubwa.

utumbo unaofanywa ccm na upinzani pia upo...........
 
What is wrong with these CHADEMA grand poobahs to even think of going against the will of the people? If this is true then they must be retarded and therefore can't be trusted to govern.

Really? How can you go against the will of the people and call yourself the progressively democratic party? What kind of democracy is that? Where they do that at?

Sham democracy on display!!!!!!!!!!
 
Nyangi Ngabu............wewe kapige tu kura lakini ukae ukumbuke kuwa upinzani na ccm hakuna tofauti ya hivyo na tusitarajie makubwa.

utumbo unaofanywa ccm na upinzani pia upo...........

No ma'am...I vote my convictions and my conscience. I can't support CHADEMA if what is being said is true. They should forget about my vote. I'm really ticked off by it (if true).
 
Wasipo angalia wata poteza vipaji vyao vya baadae kwa kuangalia maslahi ya leo. Leo hii wagombea hao wakiamua kuhama chama au kuachana na siasa nani ata walaumu? Na madhara yake ni chama kuto kuonekana mbadala bali mfumo ule ule unaopigwa ukiongzwa na sura zingine.
 
Nakumbuke mwkjj ulipotoa tathmini ya Chadema hapa mpaka kule kwenye comment kwenye moja ya comment zako baada ya watu kukushambulia kwamba hauitakii mema chadema ulisema kuwa huu ni udhaifu wa kisera hujagusa wa kiuongozi maana ungekusa huko ungewajeruhi vibaya I AGREE WITH YOU NOW YOU THOUGH LATELY BUT YOU WERE RIGHT.
 
No ma'am...I vote my convictions and my conscience. I can't support CHADEMA if what is being said is true. They should forget about my vote. I'm really ticked off by it (if true).

Ngabu, sikutegemea kabisa kama unaweza kuwa na mtu wa kuchukua maamuzi mazito kama hayo bila hata kusikiliza na kufahamu kwa undani nini kimesababisha hadi hao akina dada wakaondolewa katika nafasi zao. Inabidi usubiri upate ufafanuzi kwanza wa pande zote mbili kutoka katika chama na kwa dada Regia mwenyewe maana ni mwanachama wa JF hivyo naamini atatueleza nini kimesababisha.
Hiyo kura yako ni muhimu sana kwa ajili ya mabadiliko na kama unaweza badilisha msimamo ndani ya dakika moja basi inawezekana kabisa hata siku ukienda kupiga kura unaweza badili mawazo kutokana na maneno utakayosikia watu wanaongea siku hiyo.
 
kwenye baadhi ya jimbo mojawapo husika habari ni kuwa watu wako tayari kuyafanya yanayofanywa na wana CCM wasioridhika. Chadema watupe tumaini kuwa wako tofauti.
 
Mojawapo ya vitu ambavyo sipendi kwenye CCM ni huu utaratibu wa kikomunisti ambapo watu fulani katika majoho yao wanatengua maamuzi ya kura kwa ajili ya maslahi ya "chama". Badala ya kuwachuja watu kabla ya kupiga kura CCM ikabuni mtindo mbovu kabisa wa kuwachuja watu baada ya kura.

Matokeo yake, mtu ambaye amefanya vizuri kwenye kura za maoni na kwa uhalali wote anaweza kujikuta anaenguliwa baadaye kwa sababu na kisingizio chochote kile. Hivyo, mfumo wa rushwa, kubebana na kuburuzana umeendelea kudumishwa.

Sasa, chama ambacho kinataka kuleta mabadiliko cha CHADEMA kinasikitisha kuwa nacho kimerithi na kukumbatia mfumo huo huo mbovu. Habari kwamba baadhi ya wagombea wake walioshinda katika kura za maoni baada ya kufanyia jasho kuenguliwa na vikao vya juu vya "chama" ni habari za kusikitisha na zinaonesha kuwa mfumo ule ule mbovu wa demokrasia ya 'chama' umerithishwa ndani ya Chadema na utaleta matatizo yale yale (kama bado haujaleta).

Kwamba wagombea kama Regia Mtema (kilombero) na Rachel Mashishanga (Segerea) wameombwa kuachia nafasi zao kuwapisha watu wengine (wote wanaume) ni jambo la kufanya watu kutikisa vichwa vyao. Chadema haiwezi kuendelea kusubiria viti vya vijana au wanawake ili kuwapa nafasi za kugombea.

Moyo wa ujasiri uliooneshwa na kina dada hao hata wakaamua kugombea kwenye majimbo na kuonekana kuwa wako tayari kuhukumiwa na wapiga kura wote ni jambo ambalo Chadema inapaswa na ilipaswa kulitetea na kuwapigania hadi dakika ya mwisho. Kina dada hawa wameonesha ujasiri na utayari ambao haupaswi kubomolewa kwa sababu Makao Makuu wanataka watu fulani.

Mpendazoe na huyo wakili wa Kilombero wote walikuwa na nafasi ya kugombea toka mwanzo kama wangetaka. Lakini haya ya kuonekana kubebwa na chama kwa sababu yoyote hayaoneshe "demokrasia" bali ukiritimba wa mfumo dume ambao utawasumbua Chadema baadaye. Ni kweli kuwa katika nafasi karibu zote za juu za Chadema zinashikiliwa na wanaume lakini sitaki kuamini kuwa hilo pekee linaweza kuwafanya wasione umuhimu wa kuwalinda wagombea wake waliojitokeza.

Ninachosema ni kuwa Chadema inataka demokrasia basi iwe tayari kulipa gharama yake. Isiwe kama CCM ambayo kwake demokrasia ni anasa. Ukiondoa tuhuma za vitendo vya rushwa au ukiukwaji wa maadili Chadema iwaachilie wagombea wake walioshinda kura za maoni wasimame kama wagombea wa chama. Hao wengine kama kweli wanataka nafasi hizo wasubiri 2015.

Go Regia
Go Rachel

Kina R n R wasikate tamaa kwani hata kama wataenguliwa ukweli unabakia umeandikwa kuwa walishinda kura za maoni na walienguliwa na chama si kwa sababu ya rushwa au tuhuma za kukiuka maadili bali kwa sababu walikuwa ni aidha ni wanawake au hawakuwa tayari kupiganiwa na chama hadi ushindi.

Mwenyekiti inaonekana wewe nawe ni mwepesi sana wa kusahau maana ndani ya week hii ulishawahi kusema kwenye post yako kuwa "angalau CCM wangewarudisha wapiganaji kama vile Selelii, Kimaro" ili wakapambane vizuri, wakati huo hukuona umuhimu wa kura ya maoni na leo hii unaona umuhimu wa kura ya maoni.
Jaribu kutafakari kuhusu kauli zako mkuu maana zinakingana.
 
Ngabu, sikutegemea kabisa kama unaweza kuwa na mtu wa kuchukua maamuzi mazito kama hayo bila hata kusikiliza na kufahamu kwa undani nini kimesababisha hadi hao akina dada wakaondolewa katika nafasi zao. Inabidi usubiri upate ufafanuzi kwanza wa pande zote mbili kutoka katika chama na kwa dada Regia mwenyewe maana ni mwanachama wa JF hivyo naamini atatueleza nini kimesababisha.
Hiyo kura yako ni muhimu sana kwa ajili ya mabadiliko na kama unaweza badilisha msimamo ndani ya dakika moja basi inawezekana kabisa hata siku ukienda kupiga kura unaweza badili mawazo kutokana na maneno utakayosikia watu wanaongea siku hiyo.

My opnions are dynamic and not static. They change when the facts change.

So what possible plausible explanation is CHADEMA going to give other than political expediency?
 
Ngabu, sikutegemea kabisa kama unaweza kuwa na mtu wa kuchukua maamuzi mazito kama hayo bila hata kusikiliza na kufahamu kwa undani nini kimesababisha hadi hao akina dada wakaondolewa katika nafasi zao. Inabidi usubiri upate ufafanuzi kwanza wa pande zote mbili kutoka katika chama na kwa dada Regia mwenyewe maana ni mwanachama wa JF hivyo naamini atatueleza nini kimesababisha.
Hiyo kura yako ni muhimu sana kwa ajili ya mabadiliko na kama unaweza badilisha msimamo ndani ya dakika moja basi inawezekana kabisa hata siku ukienda kupiga kura unaweza badili mawazo kutokana na maneno utakayosikia watu wanaongea siku hiyo.
mndebile

Huyo Nyani Ngabu tayari ana negatives na Chadema whatever move itakayofanyika ndiyo maana hata kabla ya kujua nini kinaendelea ameshatoa conclusion, nimeanza ku query kama kweli huyu ni lecturer wa chuo maana mara nyingi decision zake siyo decisive.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom