Fredrick Sanga
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 3,153
- 697
Chadema Itatwaa Dola Kama Itaendelea Kama Ilvofanya Arusha na Mwanza (Uwajibikaji, uwajibishaji)
Na: Fredrick Sanga
Baada ya kuangalia mfululizo wa matukio mbali mbali katika nchi hii, kisiasa na kiusalama. Naona ni vyema kutoa neno la hekima kidogo. CCM kwa kweli wamepoteza dira, katika itikadi (Ujamaa na Kujitegemea), hawpo sasa wanafuata itikadi ya ubepari uchwara (Rwaitama; 2012) aina ya wanachama (Wakulima na Wafanya kazi), kwa sasa CCM ni rushwa, ubabe, ubepari, ubwanyenye, ukabaila na ufisadi kwenda kwa mbele. Sawa CCM wanaweza wakashinda umeya Mwanza au ule ubunge Igunga, lakini swali linakuja kwamba, walizingatia kanuni zao, katika katiba yao; mfano rushwa ni adui wa haki au nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Jibu analijua Nape na Mchemba. Chama cha namna hii hakiishii katika rushwa tu, kinaweza hata kutumia vyombo vya dola kudhoofisha upinzani, hii huwa inawaletea watumishi wa vyombo vya dola mgongano wa kimaslahi na kuharibika kimaadili. Matokeo yake ni hatari sana kwa Taifa, kwani yale ya Rwanda, Burundi na sasa Somalia yanaweza kutukuta.
Hivi karibuni tumeona jinsi Chadema ilivyosimamia kanuani zake na hata ikawagharimu kupoteza Meya na naibu wake huko Mwanza. Kwa kuangalia kwa juu juu, mmoja anaweza kusema kwamba CDM wamepoteza, Nionavyo mimi CDM wameanza kutekeleza kile ambacho watanzania tunakiitaji, yaani kuwajibishana badala ya kulindana. Matatizo mengi tuliyonayo yanatokana na kuweka vyama kwanza halafu umma unafuata baadaye, hili ni janga la Taifa, heri hata chama kikose dola kwa gharama ya maendeleo na maslahi ya Umma wa Tanzania. Na maendeleo hayaji hivi hivi tu bila kuwajibika na inapobidi kuwajibishana. What the use of having a useless Mayor anyway, ni kobomoa chama na kuugharimu umma.
Kwa falsafa ya nguvu ya umma, hatutegemei kabisa katika kipindi hiki cha miaka miwili CDM iendelee kumlinda kiongozi hata mmoja ndani ya CDM, hata kama ni nani, kama si muadilifu na mwenye maslahi kwa umma ang'olewe. Tukianza hivi sasa, hata tunapoenda kuchukua dola 2015, uwajibikaji utakuwepo. Tuanze sasa kwa umakini zaidi kuchunguza au kutathmini utendaji wa viongozi wote wa CDM, wale wa kichama, na wale walioingia katika uongozi wa umma. Kama ikigundulika kwamba wana walakini, basi waondolewe haraka hata ikibidi kupoteza hicho kiti. Kwani bila kufanya hivyo tutaleta dhana ya kubadilishana utawala na kuendelea na udhaifu uleule uliokuwepo kabla ya kubadili chama kinachotawala. Inabainika katika haya mambo ya kuunda serikali za mseto zisizo na dira. Zoezi la uwajibikaji liwe endelevu.
Kuendeleza mfumo wa CCM wa kulindana ndio hasa kutakakoondoa imani ya Umma wa Tanzania kwa CDM. Nashukuru sana kwamba siku tisini (90) za Nape ziliishaisha kitambo nao wanafikiri sisi tumesahau, tunakumbuka kila kitu alichozungumza na tutawahukumu vikali kwa hilo. Sasa hatutaki, nasema hatutaki CDM ilinde viongozi wabovu, dhaifu, wasiowajibika, wala rushwa, mafisadi nakadhalika, wanaojifanya miungu watu. Walichofanya Mwanza na Arusha iwe ni chachu tu, na mwanzo wa kujenga uongozi bora na kuvunja dhana ya bora uongozi = utawala bora.
Kwa sasa kazi ya M4C indelee kwa nguvu zaidi ili kutengeneza muundo mkakati wa kuwabana viongozi dhaifu hata ndani ya CDM. Nimeona katibu mkuu wa CDM amekuwa akilisimamia hili kwa nguvu na umakini mkubwa, akitumia muda wake mwingi, hadi kutia huruma. Unakuta mtu ni mwenyekiti wa wilaya wa CDM lakini hana faili hata moja, hana Taarifa hana mihutasari ya vikao, hata ule wa uchaguzi. Sasa huyu akitolewa katika uongozi, tuwazonge CDM, la hasha, tunataka uwajibikaji. Kuna madiwani wa CDM, ambao hawajui hata wajibu wao, mfano nenda Sinza ukajionee. Sasa tusije tukawa tunafuata nyayo za CCM. Viongozi wengine wa CDM tujiunge na katibu mkuu kukamulisha hili jukumu kabla ya 2014. Mafunzo ya kutosha kwa viongozi yanahitajika, na vichwa ngumu baibai. Hakika mafisadi watakapoinama na kuinuka watakuta CDM imo dolani.
Mwana wa Wasira ameongeza:
(i) Chadema ni Chama cha kizalendo na mkombozi wa dhati wa Mtanzania.
(ii) Chadema kinaleta matumaini mapya kwa Watanzania hasa vijana wasio na kazi na matumaini, Watanzania wenye maisha magumu hata kushindwa kumudu milo miwili kwa siku, akina mama wanaohangaika vijijini bila matibabu ya uhakika, maji, umeme, nyumba bora nk
(iii) CCM imedumaza nchi, nchi imekuwa kama mtu aliyedumaa kwa kukosa protein, haikui tena, Chadema ni damu mpya yenye kuweza kuingiza protein kwenye mishipa ya nchi iweze kufufuka na kukua tena.
(iv) Chadema kina viongozi imara na kwa maneno na matendo yake wanawadhihirishia watanzania kuwa ni waadilifu na wana nia njema ya kuipeleka Tanzania mbele. Alimalizia kwa kuwaasa vijana, akina mama na wazee wajiunge na M4C ili kuijenga Tanzania mpya. Alimalizia kwa kusema, "Kwa msaada wa Mungu, Tanzania Mpya inakuja.
Hakuna kulala mpaka kieleweke
By Fredrick Sanga (Mwanaharakati)Chadema Itatwaa Dola Kama Itaendelea Kama Ilvofanya Arusha na Mwanza (Uwajibikaji, uwajibishaji)