Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amewahakikishia wapenzi na wanachama wa CHADEMA kwamba chama hicho kitashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki utakaofanyika hivi karibuni.Dr Slaa amesema chama chake kina nguvu kubwa jimboni humo na katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 chama chake kilifungua matawi 69 yaliyo hai mpaka leo katika kila kona ya jimbo hilo.
Dr Slaa amesema CHADEMA ilijifunza mengi katika jimbo la Igunga na kutahadharisha vitendo vya ugawaji rushwa kurubuni wapiga kura kamwe havitavumiliwa Arumeru.Pia alisema chama chake kimejipanga kutoa elimu kubwa ya uraia kwa wananchi wa Arumeru mashariki kupitia kampeni mara zitakapozinduliwa.Dr Slaa ameahidi kampeni safi na za kistaarabu.
SOURCE:MTANZANIA