CHADEMA itakufa karibuni kama NCCR mageuzi - Tambwe Hiza

Binafsi namuonea imani - kujivunia nafasi ya kazi kwa kupewa cheo katika idara ya "PROPAGANDA" ni afadhali nilale njaa....maana moja kwa moja hata hao waliokupa hiyo nafasi wanatambua namna gani HAMNAZO. On a serious note, ukimsikiliza TAMBWE HIZA akiwa katika majadiliano unapata hasira sana maana HANA HATA punje ya points zenye maana....:disapointed:

Hili nalo neno
 
Mimi naaminiatakufa yeye na chama chake.Maana kila anapoongea hovyo anazidi kuwachukiza watu.CDM iko makini.

Huyu Tambwe ananikumbusha enzi zile za vita vya iraq yule aliyekuwa nafikiri ni waziri wa ulinzi
 
Nilimsikiliza Tambwe kwenye kipindi cha kipima joto ITV ambapo suala la katiba mpya lilikuwa likijadiliwa na nilimsikiliza pia Star TV hiyo jana. Anachofanya huyu bwana ni kuvuruga hii madahalo hasa ule wa ITV. Ninachojiuliza mpaka sasa ni kwamba je anafanya makusudi au ndo uelewa wake uko hivyo? Kwenye kipindi cha ITV, kuna wakati walianza kubishana na Dr. Mvungi juu ya wapi kongamano la katiba yetu ya kwanza lilifanyika. Yeye alikuwa anasema ni Lancaster wakati Dr. Mvungi akisisitiza kuwa ilikuwa ni Anatoglo DSM. Na ilibidi Dr. aonye kwamba ni vizuri mambo yaliyokuwa yanaongelewa yakawa ya kweli kwani kuna wanafunzi wanafuatilia mijadala kama hiyo na si vizuri kuwapa taarifa za uongo.

Kama waandaaji wa vipindi ndo wanaompa mwaliko huyu bwana nawashauri waache kwani anaharibu vipindi husika. Na kama ni chama chake kinamteua kuwakilisha nacho pia kiache kwani kitaendelea kuaibika. Kwa vyovyote vile,anachokifanya ni upotoshaji na jinsi anavyofanya, itafikia wakati nitaacha kusikiliza midahalo ambayo yeye anashiriki kwa vile inakuwa inakosa tija!

Ndicho hicho anachofanya kuvuruga mdahalo pia kitu kingine unaweza usimuelewe kabisa kitu huyu jamaa anachoongea
 
Niliwahi kumkuta kipindi fulani maeneo ya Kurasini wakati anagombea ubunge kwa tiketi ya CUF akisema "CCM HAIFAI KUTOKANA NA KWASABABISHIA WANANCHI UMASIKINI MPAKA WANATEMBEA NA KANDAMBILI AMBAZO ZIKO KAMA OPENA" akaonyesha kandambili iliyokuwa imetoboka kisigino.

Hivi haya maneno aliwahi kuyameza??
 
Mimi napenda kusisitiza: kama waandaaji wa midahalo hiyo wanapenda sisi tuendelee kusikiliza na kuchangia hatuko tayari kumwon kilaza kama Tambwe akiwa mshiriki. Tunataka watu wenye upeo wa kuelewa mambo, siyo Propaganda. Anachoelewa hiza Wa TZ wanaelewa mara 10 yake. Tafadhali asishirikishwe tena. Anatia kichefuchefu, na anaamsha HASIRA za wa TZ, asidhani watu hawana akili kama yeye.

OMBI: Ijumaa ya wiki hii hatutaki kumwona kwenye Kipima Joto ITV, wala hatutaki kumwona Jumapili kwenye Star TV, vinginevyo tutaona waandaaji ndo mnafurahia upuuzi wake.
 
Nimeangalia Star tv namuona Tambwe hizza akikitabiria kifo CHADEMA kama NCCR Mageuzi.

Alisema NCCR waliingia kama moto wa nyasi lkn sasa mahututi. Na CHADEMA sasa imekuja hivyo hivyo
lkn ameshindwa kuonyesha uchungu wa nchi kuhusu DOWANS. Pia ameambiwa aache upropaganda katika kujenga hoja

Kweli kabisa vyama vyenye mwelekeo wa kidini kama CHADEMA huwa havidumu
 
Wakati yeye akitabiri hayo wengine wanaklitabiria anguko kama la KANU nchini Kenya kwa kuwa mpaka sasa chama chake kimethibitisha hakipiganii Maslahi ya wananchi wwanyonge na wengi wa taifa hili. Mbona hawataki kutaja wamiliki wa Richmond kama walivyoombwa na UVCCM? Kwanini wanataka kuilipa DOWANS kabla ya bunge?kwanini hawapti suluhisho la migomo ya wanafunzi vyuoni kwa miaka 50 sasa?kwanini kila siku wananua watu mahiri toka upinzani kama yeye alivyobubuliwa yeye na uwezo wake wa kufikiri na kujenga hoja ukaisha?

Wakati yeye akitabiria CHADEMA kifo wakati alama za nyakati zinaonyesha dhahiri CCM haina miaka 5 mbele hii pia inathibitishwa na hata kushindwa kulipana posho walizo zoea
 
Nimeangalia Star tv namuona Tambwe hizza akikitabiria kifo CHADEMA kama NCCR Mageuzi.

Alisema NCCR waliingia kama moto wa nyasi lkn sasa mahututi. Na CHADEMA sasa imekuja hivyo hivyo
lkn ameshindwa kuonyesha uchungu wa nchi kuhusu DOWANS. Pia ameambiwa aache upropaganda katika kujenga hoja


Hivi nani mwenye cv za Tambwe hiza? maana unaweza kujikuta unabishana na mtu kumbe yeye keshafika mwisho wa kufikiri!
 
Hivi nani mwenye cv za Tambwe hiza? maana unaweza kujikuta unabishana na mtu kumbe yeye keshafika mwisho wa kufikiri!

Elimu:Darasa la saba
Siasa: Mgombea ubunge(1995-NCCR;2000-TLP;2005-CUF;2010-CCM) Mara zote kashindwa
Kazi:Kupiga debe(kabla ya 1995-Madaladala;1995-2000:NCCR;2000-2005:TLP;2005-2006:CUF;2006-sasa:CCM)
Hobbies:Ushabiki wa Yanga
 
Nimeangalia Star tv namuona Tambwe hizza akikitabiria kifo CHADEMA kama NCCR Mageuzi.

Alisema NCCR waliingia kama moto wa nyasi lkn sasa mahututi. Na CHADEMA sasa imekuja hivyo hivyo
lkn ameshindwa kuonyesha uchungu wa nchi kuhusu DOWANS. Pia ameambiwa aache upropaganda katika kujenga hoja


yaani nakuonea huruma umemsikiliza hana la maana analoongea juzi aliharibu kipindi ITV kwa kuropoka
 
Cv ya Tambwe hiza, kwanza yeye ni mtoto wa Makamba ..., kumbukeni ile mimba ya kigoma ya mwanafunzi wake, alisoma akaishia form three kule kwao Lushoto, akawa ana cheza mdumange kama alivyo baba yake , lakini kwa sababu damu ni nzito kuliko maji, makamba akamuiba kutoka lushoto akamleta Dar akawa anaishi kwa mzee mmoja wa kisambaa pale temeke mwembeyanga, baadaye akawa ni KISHOKA WA TANESCO , baadaye akaanza kujihusisha na mambo ya mpira na vuguvugu la vyama vingi likawa limeingia nchini, akajiunga na NCCR- mageuzi,aligombea ubunge wa Temeke mwaka 1995 kwa ticket ya NCCR mageuzi, baadaye akajitoa na kujiunga na CUF, Ditopile mzuzuri ndiyo aliyewastua CCm kwa kuwaeleza kuwa yule ni kijana wao, maana by that time MAKAMBA alikuwa hana influence kwenye chama
Baadaye baada ya Dr aliyepewa Phd na chuo ambacho hakitoi hata masters kuwa mwenyekiti wa chama, na mzee kupewa rungu fasta alimuita mwanae na kumpa kitengo ambacho hata kwenye katiba ya CCM hakipo.
HUYO NDIYE TAMBWE HIZZA MAKAMBA , RICHARD HAPENDI KULITUMIA MAANA BABA YAKE NI MUISLAM, LABDA WAMEAANZA KUMBADILISHA DINI
 
Back
Top Bottom