CHADEMA: Israel ituombe radhi

Hivi sasa tuna madini ya Urenium ni muhimu sana katika mambo ya ulinzi na utengenezaji wa silaha na nishati. Nasikia Israel walionyesha nia tukakataa. Huyu waziri kuna jambo linamuuma
 
Si kweli kwamba kila kinachosemwa na wazungu ni cha kweli. Mnyika kwa taarifa yako tu Marekani ni taifa tajiri sana duniani lakini ndio pia mkopaji namba moja duniani kwa maana ya thamani ya deni la ndani na nje.
 
Mnyika ur wrong, huwezi kuwa muhimu kwa kila mtu. Israel pia sio muhimu kwetu na hakuna sababu yeyote ya kuomba radhi.
Tazameni tena sera zenu za nje sio kila jambo na nyinyi mtoe kauli zingine mnachuna.
Hata marekani haikubariki na nchi zote, wakikukubari kenya, uganda, burundi, congo, zambia, malawi na zimbabwe inatosha sana bora hata china.
Watu weupe hawanaga urafiki wa kudumu, msijikombe kwao kabisa na michezo yao sio mizuri
 
Mnyika unatudanganya unataka kusema chadema hamkopi wala kupokea msaada? Na hapo hamjashika dola kumbuka mkishika dola matumizi yataongezeka. Kukopa si kosa... kosa ni namna ya matumizi ya mkopo..... ndivyo hata mikopo ya benki ilivyo.
 
Kama Mnyika hana agenda ya siri na tamko hilo kwa nini kaongeza maneno mengi ya kumrisha Ehud Barak..... chadema mnashangaza sana suala la ushoga hamkulipa coverage kama hii kwa sababu tu mshirika wenu conservative alianzisha dhidi ya serikali yetu. mbona hamkusema Uingereza ituombe radhi kwa sera yao hiyo mbovu dhidi ya nchi changa?
 
Naungana na Israel Kuwa Tanzania kama nchi haina maana kabisa, ni mavi matupu hivyo inanuka sana. Na hii ni faida ya kuwa na viongozi wasio na dira,Rasilimali zote tulizo nazo hazitusaidii kila siku kuombaomba tu.
 
Israel si moja ya nchi zinazotukopesha wala kuwekeza sana kwenye uchumi wetu.... Ni nini kinawakereketa?
 
Source: Mimi mwenyewe mwana CHADEMA

Source nyingine ni Home

Inasomeka hivi:
Mnyika ataka Israel ibanwe

Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Chadema, John Mnyika
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka serikali kutoa tamko dhidi ya kauli ya Waziri wa Ulinzi wa Israeli, Ehud Barak, kwamba Tanzania si ya muhimu wala ya maana kwa nchi hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Barak alipofanya mahojiano na Radio Israel na kunukuliwa na vyombo vingine vya habari vya nchi hiyo wiki iliyopita.
Alitaja nchi muhimu na zenye maslahi kwa Israel kuwa ni Ujerumani, Uingereza na Ufaransa na siyo baadhi ya nchi maskini, ikiwamo Tanzania.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Chadema, John Mnyika, alisema kupitia kauli ya kiongozi huyo wa serikali ya Israel, inaiona Tanzania sio nchi ya muhimu wala ya maana hata kufikia hatua ya kuilinganisha na eneo tu ndani ya Libya linaloitwa Tripolitania.
“Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa, Benard Membe kuitaka serikali ya Israel kuomba radhi kufuatia kauli hiyo au kueleza wazi iwapo mazungumzo hayo ya Waziri Barak ni msimamo wa nchi hiyo kuhusu uhusiano wa kidiplomasia wa mataifa yetu,” alisema Mnyika.
Mnyika alisema barua pekee ya balozi wa heshima wa Tanzania nchini Israel, Kasbian Nuriel Chirich kwenda kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Avigdor Lieberman ya kulaani matamshi hayo ya Waziri Barak na kumkaribisha mwakilishi wa Israel kutembelea Tanzania haitoshi kuifanya serikali ya nchi hiyo kutambua athari za kidiplomasia za kauli iliyotolewa.
GAZETI: NIPASHE
 
Kilichokuponza unafikiri maneno yote kwenye ukurasa wa Mnyika ni ya Ehud barak si hivyo na mbaya zaidi Mnyika kaunganisha andishi lake kama kauli ni moja bila kutenganisha nukuu na maneno yake mnyika.... shit.

Naungana na Israel Kuwa Tanzania kama nchi haina maana kabisa, ni mavi matupu hivyo inanuka sana. Na hii ni faida ya kuwa na viongozi wasio na dira,Rasilimali zote tulizo nazo hazitusaidii kila siku kuombaomba tu.
 
Huyu Ehud Barak vipi tene? hajui chama chetu kitukufu kina kauli mbiu hii "TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!" iweje aseme TZ ni nchi ya ovyoovyo eti kwa vile sisi ni ombaomba? atuache kabisa. Tena kwa taarifa yake tutaendelea kuwa ombaomba sana labda hawa Watanzania waamue kukitoa madarakani chama chetu kitukufu 2015 na kuwaweka wengine wanaochukia kipaji hiki cha kuomba omba.
Atuache bwana, asituchezee sisi tuko imara au hajaona siku ya miaka 50 ya uhuru jinsi askari wetu walivyoonyesha manjonjo?
 
Sidhani kama wamekosea waizrael ingekuwa enzi za Mwalimu wasingethubutu kuongea hayo!Ni matokea ya uongozi legelege wa JK
.

ushoga nao ni uongozi legelege? kasumba yako ni siasa za maji taka kuzileta kwenye mambo ya msingi
 
Israel wako sahihi. Si wao waliotudhalilisha bali ni kukosa kwetu akili ndiko kunakotufanya tudhalilike duniani.

udhalili ni upi mbona hawajasema sera ya mambo ya nje ya somalia? wana interest gani na Tanzania mpaka wanapata uchungu wa kuzaa mwana kwetu?
 
Kwa hiyo mnataka kusema MNYIKA Amekurupuka kutoa hili TAMKO..???!
 
hao waliochukua mafuta ya Libya na baadaye kumuua Gadaff mbona hawajasema sera za Libya zilivyowasaidia?
 
vibaraka wa Israel umeona maneno yake hapa chini


Israeli walichosema ni ukweli mtupui, Rais wetu kila siku anazunguka akiomba omba misaada (hadi chandarua JK anaomba), kwa misingi hii kwa nini tusitukanwe?
Assume wewe mwana JF kila siku jamaa wako anakuomba msaada (mara pesa ya kula, pesa ya mtoto shule, watoto wangu wanaumwa), mtu wa namna hii utahacha kumzarau?
Naungana na wachangiaji wengine inabidi C.C.M watuombe radha watanzania kwa sera zao mbovu, mikakati yao mibovu ndani ya miaka hamsini ya uhuru.
Alafu wananiuzi na msemo wao eti "TUMEDHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE" Mmeweza nini C.C.M ninyi? Hicho mlichoweza mbona hatukioni?
Huu ni muda watanzania wenzangu tuidai Tanganyika yetu.
 
Unanikumbusha usemi mmoja wa kiingereza kuwa ''beggers always have no choices". Hata mfanyaje ukweli utabakia kuwa ukweli tu na hatuna jinsi.
 
Kama kila kukicha kiongozi wa nchi yako yuko kiguu na njia nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kuhemea wewe unategemea nchi yako itaheshimiwa kweli ??????!!!!. Hata ukiwa na jirani yako tu ambaye muda wote yeye ni wa kuomba omba lazima utamdharau tu . Tanzania inasitahili kudharauliwa kwa tabia ya viongozi(KIONGOZI wake) wake kuwa wataalamu wa kuomba omba pamoja na nchi yetu kuajaaliwa raslimali nyingi
 
Back
Top Bottom