CHADEMA: Israel ituombe radhi

Tatizo watz tumelemazwa na siasa za ccm ambazo msingi mkuu ni uongo, unafiki, fitna, wizi na ufinyu wa mawazo. Sasa tusichanganye siasa zetu na zile za israel. kule ni ukweli tupu na wakikwambia ukweli hata siku moja hawawezi kuomba msamaha maana ndivyo wanavyoamini. Sie tujiulize kuwa kwani hatuko irrelevant?
 
hali zenu wakuu!!
nimejitahidi kusoma mawazo ya karibu wote waliotangulia kuchangia kabla yangu na honestly speaking inafurahisha kuona the keenness you propagate either we agree on not in your analysis.

returning to the contended declaration of Mr. Ehud Barak, well - inawezekana nitawasikitisha wengi lakini alichosema Mr.Barak is nothing but a crude truth!!! Mr Nyerere aliwahi kusema(sijui kama ni msemo wa Kizanaki au wa Kiswahili) roughly kama hujawahi kula zaidi ya kile apikacho mama yako utaamini kuwa yeye ndiye mpishi bora kuliko wengine....jaribu kula nje na utagundua kuwa hajui kupika!!!! Ninamaanisha nini, Watazania wanaoishi nje ya Mipaka ya Tanzania especially Europe na North America watakubaliana na mimi kuwa Tanzania as a country doesn't count a dried fig!!!
we have in the world only 8 countries that can determine our fate and recently that club has been politically enlarged to 20 countries that control almost 95% of world economy - najua kuna watu watauliza uchumi unaingiaje ktk hili? my friends, in this world if you dont have "monies" you're simply nothing even at the social level leave alone the so called geopolitics!!
Kama walionitangulia walivyosisitizia kuhusu UMATONYA wa Tanzania,just second to Afghanistan - sasa jiulize wewe unaesema umedhalilishwa - WAKUHESHIMU KWA LIPI????? Alichosema Barak,like it or not, ni kwamba the existance od Tanzania as a country doesn't make any difference to them - COUNTS NOTHING. Mimi sioni kama ni tusi.
Israel inasikiliza(kwa maslahi yake!) zaidi US pamoja na nchi kubwa za Ulaya kama Germany,France,GBR na Italy - pia inasikiliza malalamiko au mapendekezo ya Russia na China,kibiashara inasikiza zaidi ya nchi nilizotaja hata wanachama wa NATO.

Swali langu kwa wale wanaosema kuwa Tanzania imedhalilishwa so iombwe raddhi maana ni Taifa muhimu -NINI UMUHIMU WA TANZANIA KTK SIASA ZA ULIMWENGU???? swali hili wanaweza kunijibu vizuri wale waishio nje ya Tanzania maana wanaufahamu ukweli.
samahani kama nitakuwa nimewakwaza - najua ukweli unauma!
 
Neno kwa Dr. jakaya kikwete na serikali yake.

Jirani akikuambia nyoka yupo ndani mwako ,usimuulize yuko wapi,wewe chukua hatua kumtafuta na kumuua huyo nyoka


kwa maoni yangu nafikiri Barak hakuwa anawasema Watu wa tanzania bali Serikali ya Tanzania)
 
Ndugu zangu,

CCM Ilipoifikisha nchi yetu, yaani, I am even ashamed to call myself a Tanzanian napo pita pita huko kwenye nchi za wenzetu, unapotembea kwa wenzetu ndo utajua how our country is very irrelevant and insifiginicant in the global platform, Tanzania haijulikani kabisa wala haina umuhimu duniani hata ukijitambulisha mimi natoka Tanzania, inabidi uwaoneshe map ya africa au utaje Kenya or Zanzibar. bora zanzibar inajulikana kidogo

Kwa kweli mimi ni mzalendo but kwa mwendo huu am not even proud to call myself Tanzania kutokana na aibu kubwa na picha ambayo serikari omba omba ya ccm ina project duniani wakati tuna resources chungu mzima

Ukitaka kuamini kuwa nchi yetu ni insiginificant and irrelevant look at these data hapa chini.

gonga link hii
Country file: Tanzania
 
Ndugu zangu,

CCM Ilipoifikisha nchi yetu, yaani, I am even ashamed to call myself a Tanzanian napo pita pita huko kwenye nchi za wenzetu, unapotembea kwa wenzetu ndo utajua how our country is very irrelevant and insifiginicant in the global platform, Tanzania haijulikani kabisa wala haina umuhimu duniani hata ukijitambulisha mimi natoka Tanzania, inabidi uwaoneshe map ya africa au utaje Kenya or Zanzibar. bora zanzibar inajulikana kidogo

Kwa kweli mimi ni mzalendo but kwa mwendo huu am not even proud to call myself Tanzania kutokana na aibu kubwa na picha ambayo serikari omba omba ya ccm ina project duniani wakati tuna resources chungu mzima

Ukitaka kuamini kuwa nchi yetu ni insiginificant and irrelevant look at these data hapa chini.

gonga link hii
Country file: Tanzania


Unataka nani aisaidie Tanzania kujulikana zaidi yako wewe??

Unafikiri kila siku kwmaba hayo ni majukumu ya mtu mwingine, na mwingine anafikiri hivyo hatimaye hakuna anayefanya kitu..

Sikubaliana kwamba Tanzania ni insignificant big NO; ila sikubaliani kwamba tunahaja ya kuwalazimisha waombe msamaha NO..

Tuwapuuze tu kwa kukaa kimya..
 
Well spoken and presented. Lack of visionary leaders, rampant corruption and impunity have eroded our reputation as a nation.
a

Mkuu umsema vyema kabisa. Huwezi kupewa heshima ambayo hustahili hata kidogo. Kwa vitendo vinavyofanywa na rais wetu yafaa tulinganishwe na jimbo moja la libya. Kwa wanaolaani kauli ya waziri barak watoe mfano mmoja tu ambao Tanzania inaweza kupigiwa mfano. Kiuchumi sisi ni zero kabisa let alone kupata uwekezaji toka nje ambao kitakwimu unasimama kwa US$770m wa pili toka Uganda. Lakini hatuwezi kujisifu kuwa tumeweka mazingira mazuri ya Foreign Direct Investment(FDI) ila ni kwamba tunao bado vivutio kwa wawekezaji wa nje vilivyolindwa kama mboni ya jicho na Mwalimu Nyerere ambaye wakubwa wameamua kutumia vilaza kumkejeli lakini tumeamua kuwapa watu wa nje bila urari wa aina yoyote. Mfano ni madini ambayo tunayo mengi lakini yameishia kutajirisha wageni na watanzania wachahche wanaopkea mlungura kutokana na mikataba mibovu. Mikataba imebaki siri kwa sababu wahusika wanaogopa wasipigwe mawe. Wananchi tunaambulia ucahfuzi wa hali hewa, vyanzo vy a maji na udongo na mwisho maadaki wakishamaliza kuchimba madini. Kwa msingi huu kwa nini watu makini kama Waisrael wasikudarau. Kama hatujiheshimu basi tusitegemee mtu atuheshimu maana na ukubwa wa nchi yetu mtu ambaye hajawahi kufika atashangaa kama kweli wapo watu wanatumia ubongo au wapo katika zama za Robinson Crusoe.

Halafu kama wachangiaji wengine walivyosema tukiwa katikati ya utajiri wote huu rais anatembeza bakuli la ombaomba kama kiwete na anajigamba kwamba Tanzania imkumbuke kwa kutembea nje kuombaomba. So disgusting. Watu wanalalamikia issue ya msingi wewe unawapa jibu jepesi eti nisipotembea mtakula mchicha. Sasa umetuletea vyungu vya nyama? Viko wapi? Mbona watu wanasema bora enzi za Mwalimu walitibiwa bure, shule bure na kujengewa nyumba. Operation ondoa makuti ya Magomeni ni mfano tosha. Mliofata mmejenga nini? Na Mungu anajua kuuonyesha ukwleli. Mbali na kumkejeli Mwalimu aliyekuwa na maono mafuriko ya juzi yamewaumbua maana hata emergency na rescue facilities hamna. Hata wale mliowapa mbuga zetu wakatangaza milki yao, mkawapa madini yetu na mabenki yetu mmeshindwa kuwaomba wawape hizo facilities ili mtambie kuwa mmeziweka nyie. Shame on you and you deserve Barak's description no language to sweeten it. My friend Mnyika next time try to view things on the wide spectrum. Maoni mengine mwachie Nape
 
Tanzania tumeshadharaulika sana!! Ikifikia hatua tunaomba kupita kiasi!!
 
Na kwakweli heshima huwa hailazimishwi bali hutolewa kwa yule anaye heshimika.

Mnyika kaweka vizuri kuwa sera zetu mbovu ndiyo msingi wa haya na iwapo Membe kama waziri mwenye dhamana anataka Tanzania iombwe radhi basi angalau ashauriane na wenzake kuhusu jinsi ya kubadili sera mbovu zinazotoa upendeleo kwa watu wa mataifa ya kigeni na kuwaacha wazawa katika aibu ya umasikini usiotazamika wala kutamanika.

Vinginevyo itabakia kama taarab tu na kujirusha huku ukifahamu kuwa ndani mwako huna thamani wala heshima katikati ya watu na jamii ila kwasababu unamdomo unaoweza kuimba basi inabidi ujifariji kwa jinsi hiyo.

Mkuu Ame,

Jinsi mlivyochangia huu mjadala mnatia moyo sana.Kuna mahali nimechangia kwenye thread nyingine nikaongezea kwenye mchango wa kiranga.

Membe namuona smart kama waziri wa mambo ya nje (Make no mistake: nikimlinganisha na aliyepita) lakini response yake kuhusu hili suala la Ehud Barak amenishangaza.Ehud Barak amekosea kidiplomasia tena kwa kukiuka kanuni za msingi kabisa za diplomasia na kanuni za ustaarabu.Sasa waziri wetu wa mambo ya nje pamoja na Balaozi wetu ndiyo wanazidi kuthibitisha kwamba kauli ya Ehud Barak ni ya kweli na ilitakiwa iwe hivyo.Hatujaonyesha any seriousness katika response yetu kuhusu hili suala linalotuvunjia heshima

Kitu kingine nimejifunza ni kwamba as a nation tunaelekea kubaya.Tumeamua kukubaliana au kukataa tamaa na nchi yetu.Tabia ya baadhi ya watu kuunga mkono hii kauli kwamba Tanzania ni Irrelevant kwa sababu ya makosa ambayo yamefanywa na viongozi wetu inashangaza na kusikitisha,haina tofauti na mashabiki wa mpira ambao ni watanzania kuzomea timu yao ya Taifa wakati ikicheza na timu pinzani kisa timu yao ya Taifa imecheza vibaya.Huku ni kujivua nguo na kutokujiamini tu

Ukiona chenga anazopiga Membe ni kwa sababu anatafuta majibu binafsi bila kufuata policy ambayo ingempa roadmap ya ku-deal na masuala kama haya na ndiyo maana nikasema Sera yetu ya mambo ya nje inastahili overhaul.

Our foreign policy must be defined in terms of the goals our nation need to officially seek to attain abroad, the culture and values that bring about those objectives and the instruments necessary to pursue the goals while taking into account other nation’s prevailing foreign policies that may be established against our national interest. The essential tripods of our foreign policy strategy must be linked together such that they add value to our nation. Unfortunately for Tanzania, our foreign policy is static, unprogressive and is not benevolent to most Tanzanians.

Ukiangalia hata balozi zetu nje zinavyoshughulikia maswala yenye maslahi kwa taifa na wananchi wake,utagundua wanafanya kiujanja ujanja na mara nyingi Interest za taifa na wananchi hazitiliwi maanani ukilinganisha na balozi za nchi nyingine.Perhaps, it is not surprising why a citizen of one nation is patriotic while a citizen of another work against the interest of his nation; why a citizen of one nation exhibits political fervor while citizen of another nation shows political apathy; and why a citizen of one nation is very passionate about his country while the citizen of the other looks for every available moment to make caustic statement about his country.

Tanzania’s foreign policies have historically exhibited stagnancy, political favoritism, sometimes involve political cronyism, clueless diplomats who have no idea of their functional responsibilities which is to represent Tanzania well in times of joyous ceremonies, defending the nation in hostile environment from a hosting nation, protesting citizens’ human right abuses in the countries where such human right abuses take place, chastising nations that flout citizen’s human rights and feverishly defending Tanzania’s national interests.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

IMANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
1.
Binadamu wote ni Sawa

2.
Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa
na kuthaminiwa utu wake
shim.gif
shim.gif
3.
Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya
kujenga jamii ya watu walio sawa na huru


Hivi hawa Israel hawatudai Deni lolote tu Isije kuwa Wameona hatuwezi hata kulipa?
 
Ukioa mke asiyejua kumeza matatizo yake ya ndani na kuanika kwa watu njee siku zote lazima heshima ya nyumba njee ishuke,,,kasema ukweli kutoka rohoni kwake na sababu ni imani na ukweli wanaouamini hatuwezi kuwabadilisha wala kurekebisha kauli hiyo ambayo ina ukweli wa %100 Tanzania haiingii hata nusu kwa tripol...tripol hakuna hawana bakuli na hawafagiliii mabakuli ya dhihaka na ndio sababu leo gadafi hayuko....****** atatubatiza majina mengi kabla hajashika hatamu...juzi ushoga leo sikitu chochote what is next?
 
Tanzania tumeshadharaulika sana!! Ikifikia hatua tunaomba kupita kiasi!!

Tanzania is a rotten egg under ccm. Nyerere angekuwa hai lazima angekuwa chadema. Wezi wanalindana kuliko mfano. Mimi siku hizi najiita mnyarwanda maana angalau ina uelekekeo
 
usimlaumu huyo kaka...I own a PhD and I somehow contribute internationally in my area of specialisation...

Despite my good international reputation, i RARELY INTRODUCE MYSELF AS A TANZANIAN!!!!! i am not happy of this....

i rarely do so since just after my introduction the debate turns around to me that ...so you are there...are you happy with what is going on up back home??? e.t.c.....

it gets to the point you fail to be proud of our mother land.....SHAME UPON US!

The old good reputation we had been associated with had gone. We need total u turn to regain it under new ways of envisioning our future under new breed of leadership. Visit any neighbouring country and introduce yourself as a Tanzanian you will be shocked how neighbours view us as a land of corruption and poor good governance. This is a fact.
 
Lakini DAVID CAMEROON alipotoa masharti ya misaada sikuwasikia nyie watu! Ama ndo SILENCE MEANS YES!
 


Ukiataka kufahamu kwamba Tanzania hatuna viongozi!!! Kwa mfano; Jaribu kufikiri Israeli tuwakabidhi Nchi yetu ya Tanzania alafu wao watukabidhi Nchi yao ya Israeli, baada ya miaka hamsini tuangalie nani kapiga hatua zipi katika maendeleo kwa ujumla?

Isaka na Abimeleki

1 Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari. 2 BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia. 3 Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako. 4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia. 5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu. 6 Isaka akakaa katika Gerari.
Abimeleki akawaamuru watu wote, akisema, Amgusaye mtu huyu au mkewe lazima atauawa. 12 Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, BWANA akambariki. 13 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana. 14 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng’ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu. 15 Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu babaye
HUYO NDO BABA YAKE NA ISRAEL; UKIPENDA MWITE YAKOBO........ nani amuombe msamaha mwenziye!!!!

Hii inamaana kama mataifa yatabarikiwa kupitia wao vile vile wale watakao laaniwa ndivyo itakavyo kuwa kwao....Tanzania imelaaniwa na Mungu mwenyewe jamani hii siyo issue yakuchekelea tutubu tumrudie Mungu ndiyo maana sifa yetu kubwa ni kuongozwa na majini pamoja na kuua albino ili eti tutajirike what a mock?
 
Ukioa mke asiyejua kumeza matatizo yake ya ndani na kuanika kwa watu njee siku zote lazima heshima ya nyumba njee ishuke,,,kasema ukweli kutoka rohoni kwake na sababu ni imani na ukweli wanaouamini hatuwezi kuwabadilisha wala kurekebisha kauli hiyo ambayo ina ukweli wa %100 Tanzania haiingii hata nusu kwa tripol...tripol hakuna hawana bakuli na hawafagiliii mabakuli ya dhihaka na ndio sababu leo gadafi hayuko....****** atatubatiza majina mengi kabla hajashika hatamu...juzi ushoga leo sikitu chochote what is next?

Next statement will be foolish nation, if we shall not take serious measures to build our broken economy. Tanzanian leaders are very funny.
 
Lakini DAVID CAMEROON alipotoa masharti ya misaada sikuwasikia nyie watu! Ama ndo SILENCE MEANS YES!

For the case of fool David Cameroon silence means No, Cause he has spoken something abnormal according to human being nature. David is a crazy and shem be upon his statement plus his family.
 
Mkuu Ame,

Jinsi mlivyochangia huu mjadala mnatia moyo sana.Kuna mahali nimechangia kwenye thread nyingine nikaongezea kwenye mchango wa kiranga.

Membe namuona smart kama waziri wa mambo ya nje (Make no mistake: nikimlinganisha na aliyepita) lakini response yake kuhusu hili suala la Ehud Barak amenishangaza.Ehud Barak amekosea kidiplomasia tena kwa kukiuka kanuni za msingi kabisa za diplomasia na kanuni za ustaarabu.Sasa waziri wetu wa mambo ya nje pamoja na Balaozi wetu ndiyo wanazidi kuthibitisha kwamba kauli ya Ehud Barak ni ya kweli na ilitakiwa iwe hivyo.Hatujaonyesha any seriousness katika response yetu kuhusu hili suala linalotuvunjia heshima

Kitu kingine nimejifunza ni kwamba as a nation tunaelekea kubaya.Tumeamua kukubaliana au kukataa tamaa na nchi yetu.Tabia ya baadhi ya watu kuunga mkono hii kauli kwamba Tanzania ni Irrelevant kwa sababu ya makosa ambayo yamefanywa na viongozi wetu inashangaza na kusikitisha,haina tofauti na mashabiki wa mpira ambao ni watanzania kuzomea timu yao ya Taifa wakati ikicheza na timu pinzani kisa timu yao ya Taifa imecheza vibaya.Huku ni kujivua nguo na kutokujiamini tu

Ukiona chenga anazopiga Membe ni kwa sababu anatafuta majibu binafsi bila kufuata policy ambayo ingempa roadmap ya ku-deal na masuala kama haya na ndiyo maana nikasema Sera yetu ya mambo ya nje inastahili overhaul.

Our foreign policy must be defined in terms of the goals our nation need to officially seek to attain abroad, the culture and values that bring about those objectives and the instruments necessary to pursue the goals while taking into account other nation's prevailing foreign policies that may be established against our national interest. The essential tripods of our foreign policy strategy must be linked together such that they add value to our nation. Unfortunately for Tanzania, our foreign policy is static, unprogressive and is not benevolent to most Tanzanians.

Ukiangalia hata balozi zetu nje zinavyoshughulikia maswala yenye maslahi kwa taifa na wananchi wake,utagundua wanafanya kiujanja ujanja na mara nyingi Interest za taifa na wananchi hazitiliwi maanani ukilinganisha na balozi za nchi nyingine.Perhaps, it is not surprising why a citizen of one nation is patriotic while a citizen of another work against the interest of his nation; why a citizen of one nation exhibits political fervor while citizen of another nation shows political apathy; and why a citizen of one nation is very passionate about his country while the citizen of the other looks for every available moment to make caustic statement about his country.

Tanzania's foreign policies have historically exhibited stagnancy, political favoritism, sometimes involve political cronyism, clueless diplomats who have no idea of their functional responsibilities which is to represent Tanzania well in times of joyous ceremonies, defending the nation in hostile environment from a hosting nation, protesting citizens' human right abuses in the countries where such human right abuses take place, chastising nations that flout citizen's human rights and feverishly defending Tanzania's national interests.

Ben hilo jukumu tunalibeba sisi wenyewe vijana-watu wzima hao kina Membe wako kwenye jioni yao maana hawana zaidi ya 10 years yakuwa active so hata tukiwarushia mawe haisaidii. Inabidi tusimame kama wanaume tuwaonyeshe mataifa ni kwa jinsi gani sisi ni relevant kama wenzetu wachina walivyofanya baada ya kukumbana na dharau za jinsi hiyo miaka ya nyuma. Haihitajiki confrotations ila akili, determination, dedication na discipline ya hali ya juu ya kila anayejihesabu kama mtanzania siyo wale wanaong'ang'ana kuitwa halfcaste wakitanzania wakitamani mataifa ya wengine (Wanao dai dual citizen ship) katika kuishi na uongozi kwenye taifa letu. Let us show them how short sighted they were kwakukimbia matatizo badala ya kuyatatua.

I am in a special mission I have waited for long lakini sasa niko kwenye mission ya enough is enough and so fortunate am heavy loaded kwenye every sphere na hakuna wakunitisha wala kunikatiza my time has come which is now and not tomorrow to show the Glory of my papa God who is a creator of heaven and earth....Wale waliotayari can join my race kama you still want to put your hands in the gloves continue and wait for the mesiah to come!
 
Kauli hii jibu lake laenda mbali kidogo na wala mtu akifupisha upana wa fikra ni makosa sana.

Kitendo cha kuruhusu taifa mojawapo la Ghuba kuhamia kwenye mbuga zetu likiwa na viashirio vyote vya tawala zake za kujitegemea kabisa ndani ya nchi yetu, na vile vile jibu la jinsi gani tumekua na mchango kwa taifa la Irani ni tabu tupu hadi hapa.

Wakati tukionyesha kuchanganyikiwa na hiyo kauli tata to kwa taifa teule la Israel, mwenzetu Rostam Aziz kule Kigoma anaelewa fika kitu gani kinachomaanishwa hadi hapo.
Hapo kwenye rangi nyekundu upuuzi mtupu. Ni hekaya za Abunuasi na kigezo cha ubaguzi wa rangi na kitaifa walio nao wayahudi kwa ujumla wao.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuitaka Serikali ya Israel kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kauli ya Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Ehud Barak, kudai kuwa Tanzania si nchi ya muhimu wala ya maana.

Aidha, chama hicho kupitia Kurugenzi yake ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa kimemtaka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, kueleza iwapo hatua hiyo ndiyo msingi wa mahusiano yaliyopo kati ya nchi hizo, hasa ikizingatiwa kuwa serikali imekuwa ikieleza kwamba Tanzania ina mahusiano mazuri ya kiulinzi na Israel.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa CHADEMA kupitia mtandao wake wa kijamii.

Waziri Barak alifanya mahojiano na Radio Israel na kutoa kauli ambayo imenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari vya nchi hiyo kuwa Tanzania si nchi ya muhimu wala ya maana hata kufikia hatua ya kuilinganisha na eneo ndani ya Libya linaloitwa Tripolitania.

Mnyika alisema kupuuzwa huku kwa nchi yetu katika medani ya kimataifa kunatokana na sera mbovu ya mambo ya nje chini ya utawala wa sasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Tanzania imepoteza heshima katika siasa za dunia kutokana na diplomasia yetu kujikita katika kuomba omba kimataifa; pamoja na kuwa kimaneno na maandishi serikali inazungumza kuhusu diplomasia ya kiuchumi, kivitendo mahusiano yetu yamejengeka katika misingi ya utegemezi, kupungua kwa urari wa kibiashara na kuachia mianya ya uporwaji wa rasilimali,” alisema.

Alieleza kuwa kauli ya Waziri Barak ni muendelezo wa mataifa mbalimbali kuifanya Tanzania na baadhi ya nchi nyingine za Afrika kukosa heshima wala sauti katika siasa za kimataifa kama ambavyo serikali za Uingereza na Marekani zilivyoweka masharti yenye mwelekeo wa ukoloni mamboleo kuhusu masuala ya ushoga na usagaji.

“Barua pekee ya Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Israel, Kasbian Nuriel Chirich, kwenda kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Avigdor Lieberman ya kulaani matamshi hayo na kumkaribisha mwakilishi wa Israel kutembelea Tanzania haitoshi kuifanya serikali ya nchi hiyo kutambua athari za kidiplomasia za kauli iliyotolewa,” alisema Mnyika.

Mbunge huyo alieleza kuwa wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, Tanzania ilikuwa na heshima na sauti kimataifa si tu katika jitihada za ukombozi kusini mwa Afrika bali pia katika mahusiano ya kisiasa, kiuchumi na kijamii baina ya nchi za Kusini na mataifa mengine duniani.

Kutokana na hali hiyo, alisema iwapo hatua hazitachukuliwa kurejesha heshima na sauti ya Tanzania kimataifa, maamuzi mengi yatafanyika yenye athari kwa wananchi wengi bila ushiriki wao thabiti kama yanayoendelea hivi sasa kuhusu Mikataba ya Kiuchumi na Nchi za Jumuia ya Ulaya (EPA) yenye madhara kwa wakulima na wenye viwanda nchini.

“Ni wakati sasa kwa Watanzania kuendelea kuunganisha nguvu ya umma kusimamia uwajibikaji na kufanya mabadiliko ya kimsingi ya kiuongozi, kisera na kimfumo ya kitaifa, ili kurejesha nafasi na heshima ya Tanzania kimataifa katika mazingira ya sasa ya ushindani wa kiuchumi, kiulinzi, kijamii na kisiasa,” alisema.

Source: Mimi mwenyewe mwana CHADEMA
Naungana na Israel katika hili, sababu tunaongozwa na viwete hata tunakosa maana mbele ya mataifa mengine, wala tusijiangaishe kutaka kushindana na Israel wale wamebarikiwa na Mungu, ni taifa teule tuichukulie kauli yao kama changamoto tuweze kuwa na maana duniani vinginevyo laana zitazidi sababu Mungu aliiambia Israel atakayekubariki nitambariki na atakayekulaani nitamlaani.
 
Back
Top Bottom