Chadema isife moyo

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Kwa upande wangu huwa napata faraja Chama cha upinzani kinapopata misukosuko ,kumbukumbu za CUF ni kubwa na kwa kweli viongozi wake walifika kuswekwa jela kwa muda mrefu wakibambikizwa makesi mbalimbali hata ya uhaini.Na leo hii CUF imetinga ikulu na ipo katika kipindi cha mpito kuiteka Ikulu.wenyewe ndani ya CUF wanasema wapo transit.

Sasa nikirudi kwa CDM naona imeanza kupambana na vizingiti ambavyo vinahitaji uvumilivu na mbinu na mikakati endelezi,kuanzia kwenye vita vya umeya vilivyopelekea maandamano na pia kupoteza maisha kwa baadhi ya wananchi ,yote hayo ni katika njia ya kuelekea katika kutafuta njia za kuing'oa CCM na kukamata hatamu za nchi hii.Na hili la kupoteza nafasi ya kuwa kambi rasmi ya upinzani bungeni ,yote haya ni vipimo na mitihani inayotaka kukabiliwa kiume.Ukiangalia hapa JF nilileta mada inayosema au yenye kichwa cha habari..."Viongozi wa Chadema wanastahili wafungwe..." mada ile ikafutwa haraka sana ,najua waliofuta walikuwa na udhaifu wa kufahamu kwa kina na hawana agenda za kiintelijensia inayopelekea kuiwinda serikali na chama kinachoongoza serikali hiyo mbele ya wananchi.

Uchaguzi bado mika miine ,sasa ikitokea viongozi hawa kufungwa ,bila ya shaka yeyote ile siku ya kutoka jela watatoka kama mashujaa na wenye mvuto zaidi ,aliefuta mada yangu hakulijua hilo.

Jengine linalowaelekea CDM ni udini kuliko ukabila ndani ya chama ,hili nalo si jambo la kupuuzwa ,CUF iliandamwa na hili hadi leo bado kuna watu wameganda kasumba ilizovishwa CUF kuwa ni wadini na nawashangaa baadhi yetu humu JF nao wamekumbwa na habari hizo na wanazishangilia zionekane zina ukweli fulani..ni hatari sana.CUF wamekanusha na wamefanikiwa ,dongo sasa linaelekea kwa CDM ni lazima wajipange kukabiliana nalo.

Natoa samamahni kwa wale wanaochangiamatusi na kudharau wengine ,tunapojaribu kutoa maoni.
 
Mwiba, japo ni mapema sana lakini naona baada ya uchaguzi umeanza kubadilika na kuonekena kama mtu unayepambana na ufisadi. Kama ndivyo, basi alhamdulilah...

Kuhusu mada yako, naomba nikutoe wasiwasi kuwa kwa sasa vizingiti wanavyopambana navyo CDM, kwao ni mtaji na ni vyema vikawepo. Hivi nikuulize tu kuwa tangia limeanza bunge, kwa anayefuatilia vyombo vya habari, nini kinaandikwa zaidi? bila shaka ni CHADEMA. Sasa iwe wanaandikwa kwa ubaya au wema, sio ishu kwani hakuna namna yeyote unaweza kuwaziba midomo wabaya wako.

Kuhusu changamoto wa udini, ni kweli, CDM wanapambana nayo kwa sasa na kwa kiasi kikubwa inaelekea kuisha nguvu, kwani makakati wa CDM, ni kuteka na kusimamia haki za Watanzania wote bila kujali dini au eneo, na hiyo ndiyo sera yao. Baada ya muda, wananchi watasahau huu wimbo wa udini kama walivyosahau wa ukabila...
 
Back
Top Bottom