Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio

Mkuu, hivi mbunge wa tarime anaitwa nani?

Nyambari.jpg

Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwene (CCM)
 
Watoto bana wasione magari :biggrin1:

ha h aha ha

jirizishe mkuu kwa kauli tamu - pia kumbuka kuongoza nchi bila kuwa na support ya wananchi wako ni kazi kweli kweli - miaka mitano unaweza kuiona ni kama karne. :biggrin1:
 

KWA wiki kadhaa sasa, viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ambako wanazungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa nchi na kama ilivyotarajiwa, wakiikosoa Serikali pamoja na chama tawala katika masuala mbalimbali, ikiwamo uendeshaji na usimamiaji wa uchumi wa nchi.

Mambo mengi yamezungumzwa na viongozi na makada wa chama hicho katika mikutano hiyo, lakini jambo lililovutia wengi na kuchukuliwa kwa uzito wa hali ya juu na vyombo vya habari ni kauli zilizotolewa na mmoja wa makada wake, Fred Mpendazoe, aliyejiunga na chama hicho mapema mwaka jana.

Mpendazoe, ambaye alikuwa Mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliamua kubwaga manyanga na kuondoka CCM Machi mwaka jana, akijiuzulu ubunge huku akitangaza kujiunga na chama kipya kilichokuwa kikijulikana kama Chama Cha Jamii, kwa kifupi CCJ, ambacho kuanzishwa kwake kuliandikwa sana na vyombo vya habari kwamba kimeanzishwa na baadhi ya vigogo kutoka CCM.

Hata wakati akitangaza kujiondoa CCM, Mpendazoe alisema wazi kwamba yeye amekuwa mtu wa kwanza kujitokeza hadharani kujiunga na chama hicho na kwamba baadaye, wenzake wengi wazito kutoka ndani ya CCM, wangemfuata na kujiunga naye kama ilivyokuwa imeandikwa katika vyombo vya habari.

Lakini kwa bahati mbaya, chama hicho kilishindwa kupata usajili wa kudumu ili kishiriki katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kubaini kasoro nyingi, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa wanachama waliokuwa wameorodheshwa na chama hicho katika maeneo mbalimbali nchini. Chama hicho kikafa.

Kuona hivyo, Mpendazoe akaamua kujiunga na Chadema ili ashiriki katika uchaguzi na akagombea ubunge katika Jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, ambako kwa bahati mbaya aliangushwa na mgombea wa CCM, Makongoro Mahanga. Kesi ya kupinga matokeo hayo bado ipo mahakamani.
Mpendazoe ameibuka katika mikutano ya Chadema, kwanza ule uliofanyika wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, alikomtaja Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, kama mmoja wa watu walioshiriki kikamilifu kuanzisha CCJ, huku akiahidi kuwataja viongozi wengine wa CCM aliowaita wasaliti na wapenda vyeo.

Mjini Njombe, kada huyo wa Chadema aliwataja Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe kama miongoni mwa viongozi wengine kutoka CCM walioshiriki moja kwa moja katika kuianzisha CCJ. Anadai kuwa mwanzilishi halisi, aliyejitolea muda na mali kuanzisha chama hicho ni Sitta.

Kwa vyovyote vile, kwa chama makini kama CCM, tuhuma za aina hiyo ni nzito sana kwa sababu kama ni za kweli, basi zinaashiria kuwapo kwa wasaliti ndani ya chama ambao wapo tayari kuanzisha chama kingine kwa lengo la kutimiza ndoto zao za kisiasa.

Chama Cha Mapinduzi sasa kipo katika harakati za kujivua gamba kwa kuondoa kenge waliovamia kwenye msafara wa mamba na tunadhani usaliti katika chama ni moja ya dhambi kubwa zinazotakiwa kupatiwa adhabu ya hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wahusika wote ndani ya chama.

Si kazi yetu kuwafundisha kazi viongozi wa CCM, lakini kama kweli kina nia ya dhati ya kujivua gamba, kinatakiwa kizifanyie kazi kwa kuzichunguza kwa makini tuhuma hizi nzito zinazotolewa na Mpendazoe na kama ikibainika kuwa kuna ukweli ndani yake, basi hatua zinazofaa zichukuliwe ili kufanikisha falsafa yake ya kujivua gamba.

magazeti ya kuchambia ninayo mengi tu...moja wapo ni RAI.

kwa hiyo sasa wanataka kugeuza gia: kwamba magamba ni hao wanaowaita 'wasaliti' na si 'wanaotuhumiwa kwa ufisadi' kama alivyowahi kutamka chiligati walipokuwa dodoma.

nji hii bana.
 
Nimewapenda CDM kumbe ni wasikivu, haya mambo ya picha tuliyataka sana, tumelalamika sana na mmetusikia.Aiseeeee mnatisha CDM kama njaa vile
 
Mod weka hizi picha ukarasa wa kwanza zitaleta msisimko. Tupo pamoja wapiganaji tunafarijika sana wengine tuliopo huku Uingereza tunapoona nguvu ya umma inafanya kazi. Picha hizo zimenikumbusha Tosamaganga enzi nipo A-level. Kweli Iringa ipo juu.
 
CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (chadema) wilaya ya Iringa mjini kimesema kuwa kimepanga kuzunguka mji mzima wa Iringa leo katika maandamano yataayoanzia Kihesa hadi kata ya Mlandege kwa mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa umbali wa zaidi ya kilometa 5 hadi mkutano mkubwa wa kuhitimisha mikutano ya CHADEMA mikoa ya nyanda za juu kusini utafanyika chini ya mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, na katibu wake, Dk. Willbrod Slaa,


Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao walisema kuwa chama cha mapinduzi (CCM) kimekuwa kikidanganya wananchi kuwa kimejivua gamba wakati watanzania wakiendelea kulia na ugumu wa maisha na kuwa katika kutano wa leo wakazi wa wilaya ya Iringa watafunuliwa siri nzito ya ufisadi wa serikali ya CCM.


Wabunge hao walitaka wananchi wa mji wa Iringa kujitokeza kwa wingi katika maandamano hayo makubwa ambayo wamedai hayajapata kutokea katika jimbo la Iringa mjini .


Mbunge Msigwa alisema kuwa CCM inapaswa kujua kuwa jimbo la Iringa mjini ni ngome ya Chadema kwa mkoa wa Iringa na hivyo kutoacha kufika kuungana na wana Chadema katika mapokezi ya viongozi hao wa kitaifa .


Hata hivyo alisema katika mkutano huo ambao umepangwa kufanyika katika kata ya Mlandege ambako ni nyumbani kwa mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi ,Chadema itatumia mkutano huo pia kuwaonyesha wakazi wa jimbo la Iringa mjini ambavyo CCM isivyowajali wananchi wake kwa kuendelea kuacha miundo mbinu katika hali mbaya .



Alisema kuwa maandamano ya Chadema leo na mkutano huo pia utafuta kabisa nyayo za viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa waliofanya ziara wilayani humo kisha kutangaza msimamo wa CCM wa kujivua gamba chini ya msanii wao katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye ambaye amegeuka kuwa mfaki wa CCM.


Kwa upande wake Chiku Abwao alisema kuwa wanawake jimbo la Iringa mjini kwa miaka yote walikuwa hawana mbunge wa viti maalum mzuri na kuwa kupitia uwakilishi wake kama mbunge wa viti maalum mkoa huo wanawake wategemee makubwa katika uongozi wake na kuwa nafasi hiyo bado anaitamani kamwe CCM wasigegemee miujiza katika kulitwaa jimbo hilo la Iringa zaidi ya kusubiri kupokonywa majimbo mengine ya mkoa wa Iringa

Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com utarusha Live mkutano huo na maandamano ya Chadema jimbo la Iringa mjini .

 
Mod weka hizi picha ukarasa wa kwanza zitaleta msisimko. Tupo pamoja wapiganaji tunafarijika sana wengine tuliopo huku Uingereza tunapoona nguvu ya umma inafanya kazi. Picha hizo zimenikumbusha Tosamaganga enzi nipo A-level. Kweli Iringa ipo juu.

ulikuwa unalala bweni gani mkuu mandela au azimio........half mile unapapata?
 
Si wachunguze wao wafanye investigative journalism kama wana interest ya kujua zaidi

Wanataka nani achunguze?
 
Nenda ukawaambia wananchi haya maneno yako ya kejeli uone kitakachokupata, watu wameshajichokea - maisha magumu hawana matumaini tena wewe unaongea usharobaro...

Wewe ulishawahi kushika jembe, ulishalala njaa hata siku moja? ulishawahi kukosa ada ukakaa nyumbani term nzima? ulishawahi kuugua ukakosa buku mbili za kujiandikisha kwa daktari?

alishawahi kukosa kompasi la kufanyia mtihani wa hisabati?
Ashawahi kuuza karanga darasani?
Alishawahi kuunguzwa na viatu vya GOGO au Sadolin?

Vitoto vya siku hizi ni masharobaro tu!
 
Nenda ukawaambia wananchi haya maneno yako ya kejeli uone kitakachokupata, watu wameshajichokea - maisha magumu hawana matumaini tena wewe unaongea usharobaro...

Wewe ulishawahi kushika jembe, ulishalala njaa hata siku moja? ulishawahi kukosa ada ukakaa nyumbani term nzima? ulishawahi kuugua ukakosa buku mbili za kujiandikisha kwa daktari?

alishawahi kukosa kompasi la kufanyia mtihani wa hisabati?
Ashawahi kuuza karanga darasani?
Alishawahi kuunguzwa na viatu vya GOGO au Sadolin/mwisho saa sita?

Vitoto vya siku hizi ni masharobaro tu!
 
mkuu umenikumbusha mbali sana nilikuwa nalala azimio, mambo ya quarter mile maandazi kwa masista
 
huyo mhariri naye hajui kufikiria, samwel sita na wenzake sio wasaliti, they wanted to get away from mafisadi papa. hakuna atakayeweza wachukulia hatua sababu wao hawakuwa tatizo, na kama wangefanikiwa ingekuwa fundisho kwa ccm. wanachama waliowengi wameichoka ccm, si kwamba wanafurahishwa na mwenendo mzima wa chama, ila uvumilivu uliopita kiasi ndio unazidi waweka ndani ya chama, siku wakichoka kama walivyochoka kina sita tutasikiliza mengine. ikumbukwe kuwa walitaka kumtosa sita na wenzake kisa kesi ya richmond, sita na hao wenzake hawakuwa na jinsi zaidi ya kuanzisha chama kingine, sidhani kama sita na hao wenzake wana usafi kiasi hicho, ila kwa hilo walikuwa sahihi.
 
Back
Top Bottom