Chadema Iringa mambo si shwari

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MGOGORO ndani ya Chadema mjini hapa unaomhusisha Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na baadhi ya wanachama wanaotaka ajiuzulu, umechukua sura mpya.

Hali hiyo imekuja baada ya Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Iringa, kutangaza kumsimamisha uanachama Abou Changawa anayeongoza kundi la wanachama waliompa Mchungaji Msigwa siku saba ajiuzulu uenyekiti wa chama hicho, Iringa Mjini.

Mbali na kukataa kutambua uamuzi wa kikao hicho, Changawa aliiambia HABARILEO jana kwamba mgogoro baina yao na Mchungaji huyo unaelekea pazuri, kwa sababu utatoa fursa kwa viongozi wa juu wa chama hicho kufahamu jinsi alivyokihujumu chama wakati wa uchaguzi.

“Tutaanika yote yanayomhusu Mchungaji Msigwa kwa viongozi wa juu wa chama, ili waelewe kilichofanywa naye wakati wa kampeni na uchaguzi wenyewe, na hatari inayoanza kujitokeza ya kulipoteza jimbo hilo katika uchaguzi ujao,” alisema na kuongeza, kwamba hatambui kusimamishwa uanachama kwa sababu barua aliyopewa haijaeleza makosa yake.

Akizungumza na wanahabari mapema wiki iliyopita, Changawa na kundi lake hilo, walimtaka
Mchungaji Msigwa kujiuzulu baada ya siku saba kwa madai kwamba alikihujumu chama wakati wa uchaguzi na hivyo kukifanya kiambulie kiti kimoja cha udiwani kati ya viti 16 vya Iringa Mjini.

Taarifa ya chama hicho iliyosambazwa jana kwenye vyombo vya habari ikiwa imesainiwa na Katibu wa Iringa Mjini, Suzana Mgonakulima, inaonesha kwamba Changawa amesimamishwa uanachama kuanzia juzi, kwa kukiuka Katiba ya chama Ibara ya 10(3) na 10(4) ambayo hata hivyo haikufafanuliwa inasema nini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vikao vilivyofikia uamuzi huo ni vya Kamati Tendaji na Baraza la Wazee vilivyokaa Januari 16, baada ya kujiridhisha na mtiririko wa makosa ya utovu wa nidhamu yanayofanywa na Changawa kwa chama na kwa Mchungaji Msigwa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Taarifa hiyo iliyotakiwa kusainiwa pia na Kaimu Mwenyekiti wa Iringa Mjini, Leonard Mdeka ambaye hata hivyo hakuisaini, imempa Changawa wiki mbili kujitetea kwa maandishi na asipofanya hivyo atakuwa amejiondoa kwenye orodha ya wanachama wa chama hicho.

Pamoja na kukanusha tuhuma zinazomhusisha Mbunge huyo kukihujumu chama wakati wa uchaguzi, taarifa hiyo imesema Changawa ni mtov
 
Back
Top Bottom