CHADEMA ingekuwa na TV hotuba ya Mhe. Lema ingerudiwa wiki nzima na kuhamasisha watu

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Wandugu,

Nimeguswa na kusikitishwa sana na jinsi habari zinazohusu wabunge wa upinzani hususan wa chadema zinavyochakachuliwa wakati wa taarifa za habari kwenye vituo vya TV mojawapo ikiwa ni ITV. Jana wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili usiku walionesha kwenye headlines habari ya wabunge wa chadema waliotolewa nje ya ukumbi wa bunge eti kwa kumi-miss behave. Lakini kwenye taarifa kamili tukio hilo halikuoneshwa kabisa. Ukweli ni kwamba lazima kulikuwa na amri kutoka juu iliyolazimisha taarifa hiyo hiyo isitolewe kwani ni jambo lisiloingia kichwani kwa mtu timamu kuona jambo linaonyeshwa kwenye headlines lakini kwenye habari yenyewe kamili linaondolewa.

Nachojiuliza ni kwamba kama kweli wabunge walilikosea heshima bunge kiasi cha kufukuzwa nje ya ukumbi, kulikuwa na haja gani ya kuwaficha wananchi tukio hilo!? Kwa nini tukio hilo halikuonyeshwa kwa uwazi ili wananchi waone jinsi wabunge wa upinzani wasivyo na heshima!? Inavyoonekana ni kwamba ccm inatambua kuwa hoja iliyowafanya wabunge watolewe nje ilikuwa na mantiki na ya kizalendo na ingeungwa mkono na watanzania wengi. Kwa wenye akili hatuhitaji maelezo au uchambuzi wa kina kubaini hilo.

Lakini hiyo ni tisa, kumi ni ile hotuba ya Kambi rasmi ya Upinzani iliyosomwa na Mhe. Lema. Hotuba hiyo ni nzito, inasisimua na kuamsha ari ya ukombozi. Ni hotuba iliyosheheni maneno mazito yanayopenya ndani na kuamsha hisia kali kwa wananchi wazalendo wanaoipenda nchi yao. Ni bahati mbaya sana hotuba hiyo itaishia kusomwa kwenye magazeti tu (kama yapo yatakayochapishwa). Hapa ndipo ninapoona umuhimu wa chadema au mwanamapinduzi yeyote kuanzisha kituo cha TV. Ingekuwa hivyo, hotuba hiyo ingerushwa kwa wiki nzima mfululizo. Kuna haja ya viongozi wa chadema kutunza kumbukumbu hizi ili wakati muafaka ukifika matukio kama haya yarejewe na wananchi wapate fursa ya kuona na kusikia. Wadau mnasemaje?

Hivi kumissbehave ndio nini vile kwa kiswahili???? Maana hii taarifa ni nzuri lakini kutojua maana ya neno hilo imenifanya nisiielewe vizuri.

Kwa hakika hakuna aliyebahatika kumwona vizuri hakika hakuna m2 angeacha kwa namna moja ama nyingine msimamo mmoja. Alikuwa ni Bett angenirudia 2ngejua full scendo.

aim sure have been recorded wanaweza tupatia maana technolojia ya siku hizi iko juu sana hata mimi natumaini tutaiona hiyo hotuba live.

Hivi kumissbehave ndio nini vile kwa kiswahili???? Maana hii taarifa ni nzuri lakini kutojua maana ya neno hilo imenifanya nisiielewe vizuri.

Kanunue dictionary utafute maana yake

Usijali mkuu yana Mwisho. Soon Aljazeera inatia Timu Nairobi matangazo kwa lugha ya kiswahili wale hawafichi kitu. Vitelevision kama TBC1 tutakua tunawaachia watoto waangalie vipindi vya Cartoon

jamani mwenye nayo hebu atuwekee hapa tuisikilize - wengine imetupita nasikia ilisheheni uhondo mtupu.

Jamani tujifunze hili swala tena litufanye tuwe na uelewa wa nini CCM inafanya na wabunge wake? Mimi ni CCM kabisa ila wanavyo fanya sipendi kabisa wanaendesha nchi kibabe , wabunge wa CCM tumewatuma huko kututetea na kuwakilisha matatizo yetu si kushindana kwa kupiga kelele.
CCM shindaneni na Upinzani kwa hoja si kwa kuwakemea na kuona kile wanacho kieleza hakifai , wajibuni kwa hoja ili na wao wajione mnacho kisema ni sawa.

Wabunge wa upinzani hasa Chadema na NCCR-Mageuzi wanaonewa sana mjengoni..Hapa tusilete siasa, Magamba wamekuwa waonevu sana, ITV jana wametuboa sana, ni kweli kwenye Headlines ilikuwa iwe habari ya kwanza lakini cha ajabu hiyo taarifa haikusomwa..ITV wanashindwa na channel 10, ITV ni ajenti wazuri wa magamba...ITV+TBC=Kudidimiza Upinzani..

Jamani tujifunze hili swala tena litufanye tuwe na uelewa wa nini CCM inafanya na wabunge wake? Mimi ni CCM kabisa ila wanavyo fanya sipendi kabisa wanaendesha nchi kibabe , wabunge wa CCM tumewatuma huko kututetea na kuwakilisha matatizo yetu si kushindana kwa kupiga kelele.
CCM shindaneni na Upinzani kwa hoja si kwa kuwakemea na kuona kile wanacho kieleza hakifai , wajibuni kwa hoja ili na wao wajione mnacho kisema ni sawa.

Kuna Bwana Mdogo mmoja anaitwa Lusindde jana kaomba mwongozo eti aletwe daktari bingwa aje kupima kama wabunge wana akili timamu..Huyu jamaa yeye ni kagamba sasa sijui kama alikuwa anamanisha wabunge wa upinzani au vipi? kama huyo daktari atakuja basi ni bora akaanza na Lukuvi, Makinda, Ndugai, na wengine wenye viherehere wasiotaka kuambiwa ukweli..

Wabunge wa ccm na serikali yao hatukuwachagua walijichagua wenyewe kwaku chakachua matokeo hivyo ni wazi hawawezi kututetea huko bungeni hapa pona yetu ni kuwaondoa tu nduli hawa walioshindwa kuongoza nchi.

aim sure have been recorded wanaweza tupatia maana technolojia ya siku hizi iko juu sana hata mimi natumaini tutaiona hiyo hotuba live.

Mwanaweja, Mh. Lema alisoma hotuba yote mwanzo hadi mwisho, isipokuwa kuna paragraph moja Naibu spika alimwomba asiisome kwa sababu alizo kuja kuzitoa baadae. kilichowatoa nje ni wote watatu (actual ni wa nne including Mh. macharia), waliwasha Mic wakawa wanaongea ikawa vurugu tupu ndipo ndugai akatoa maamuzi aliyotoa. I was watching it live, Mh. Lissu was unlucky kwani aliwasha na kuzima ila makatibu walimuona waka record, ila Mh. Msigwa ndiye actually alisababisha watolewe, kwani hata Mh. Lema pamoja na kuwasha Mic alitoa sauti mara moja tu, lakini Msigwa ali mis-behave saana and it was a shame kwa mchungaji kuwa kama mtoto wa primary. Ila kwa mh. Lema it was very unfortunate kwani alikuwa na wageni wake waliotambulishwa kabla ya tukio hilo.

Actually, songombingo lilianza baada ya Mh. Lukuvi kuomba mungozo kuhusu content ya hotuba ya kambi ya upinzani ambayo ilisomwa na Mh. Lema. kama vipi iwekwe jamvini watu wasome, ila yaliyo jiri ni hayo. I am out.

Usijali mkuu yana Mwisho. Soon Aljazeera inatia Timu Nairobi matangazo kwa lugha ya kiswahili wale hawafichi kitu. Vitelevision kama TBC1 tutakua tunawaachia watoto waangalie vipindi vya Cartoon

Ukiona aljazeera inkuja hapa jirani, take from kuna maafa yanakuja!! hawajamaa huwa wanaripoti vita, mabomu nk, kama imekuja hapa karibu tusubiri tu vurugu na vifo vingi katika kanda ya africa mashariki and who knows, even Bongo land!!

Back
Top Bottom