Chadema inachukua hatua gani dhidi ya diwani aliyekutwa na silaha ya kivita ak 47?

Jamani acheni ushabiki na uzandiki....huyo diwani kama binadamu wa kawaida amefanya makosa..kama kweli hakuwa akimiliki kihalali silaha hiyo....TATIZO hapa mi naona SIASA....Watu wanahukumu chama CDM kuwa kinamiliki silaha!!! Je Silaha hiyo ilikutwa ofisi za chadema? Au ni Gilba tu za kisiasa za huyu mdau? kwa mtizamo wangu ,umiliki wake wa silaha hauna mahusiano kabisa na udiwani wake!!! MIMI NINACHOONA HAPA WATU WAMEKOZA NAMNA YA KUIDHOOFISHA CDM WANAAMUA KUPITIA NJIA ZA PANYA!!!!!!!!!!!!!!!! NDIO MAANA TUKIO HILI LIMEKUJA WAKATI WAKIJIVUA MAGAMBA!!!
 
Chadema siyo mahakama ya kuhukumu watu Kama waliomkamata yaani polisi walimsamehe kwa kujua au kutojua sheria ni kosa Lao wala si la Chadema.
Kama WATANABE umeshindwa kujivua Gamba basi nenda mahakamani
 
hakuna sheri ayyt nchini inayoruhusu raia kumiliki silaha za kivita,hakuna kibali chochote kinachotolewa kumiliki silaha za kivita,hata makampuni ya ulinzi hayaruhusiwi kumiliki silaha hizo isipokuwa majeshi ya ulinzi na usalama tu (silaha za kivita zinajumuisha SMG,UZI mashinegun,AK 47,RPG,light mashine gun,heavy mashine gun,semi automatic rifle,nk) excluding pistol of any type
 
Basi hap polisi kwa nini wamemsamehe???
Maana naamini hata polisi wanajua hayo jiulize kwa nini polisi wamsamehe????maana yeye si wa Chama Cha Magamba.
 
Basi hap polisi kwa nini wamemsamehe???
Maana naamini hata polisi wanajua hayo jiulize kwa nini polisi wamsamehe????maana yeye si wa Chama Cha Magamba.
 
Chadema si jeshi la polisi bali chama cha siasa nchini. Kila mtanzania ana haki ya kumiliki silaha ili mradi ametimiza masharti fulani na ameahidi kutii na kuheshimu sheria za nchi, haina maana kuwa umiliki wa silaha hiyo uendana na matendo ya giza na kuvunja sheria zilizopo. Nionavyo mimi, hapa chadema haina la kufanya isipokuwa tuache kwanza polisi wafanye uchunguzi wao na wakamilishe. Litakalofuata baada ya hapo nadhani litahusisha pia chadema. Si kweli kwamba pamoja na chadema kupata uungwaji mkono na watanzania wengi kwa sasa eti sasa wako juu ya sheria. Akibainika tu kumiliki isivyo basi sheria itachukua mkondo wake na chadema kitamwajibisha diwani wake. Isikupe hofu kwa sasa, it is just a matter of waiting time.
 
Ni ukweli kuwa vyama vya siasa vimeundwa na binadamu, hivyo kuwepo au kutokuwepo kwake kunategemea akili za binadamu. Tofauti na ardhi na vyote vilivyomo ambavyo kwa pamoja hujulikana kama nchi, vilivyoumbwa na mwenyezi mungu.

Hivyo Tanzania itaendelea kuwepo hata kama vyama vyama vya siasa vitaendelea kuwepo au kufutika kabisa. Hivyo mantiki na busara inanielekeza kuwa nchi ni bora kuliko chama.

Kutokana na ubovu wa sheria zetu, watawala wetu wa CCM wanatulazimisha watanzania wote tunaotaka kushiriki kwa namna moja au nyingine katika uongozi wa nchi yetu kupitia katika vyama vya siasa. Awali chama kilikuwa kimoja tu yaani TANU na baadaye CCM hivyo wengi wetu tulilazimka kuwa katika chama hicho. Ujio wa vyama vingi kidogo kidogo ukaanza kutoa uhuru wa mawazo, maoni na kupingana bila kupigana na leo ndio tulipo katika mhjadala wa katiba mpya.

Kwa kuwa vyama vya siasa navyo hubuniwa na kuongozwa na binadamu mara nyingi udhaifu wa binadamu ndani ya vyama vya siasa hususan viongozi mara nyingi hukiganda chama husika kama ambavyo CCM ilivyogandwa na ufisadi baada ya kuchelewa kuwashughulikia watu wenye tuhuma za ufisadi ndani ya CCM.

Tukio la hivi karibuni la Diwani wa chama chetu wa CHADEMA kukutwa na silaha ya kivita AK 47 haliwezi kupita hivi hivi kwa watu wazima wenye mapenzi mema na nchi yetu ambao kila kukicha tunapoteza raslimali na muda kupambana na vitendo viovu ndani ya jamii yetu.

Naomba kuuliza uongozi wa CHADEMA unachukua hatua gani dhidi ya Diwani wetu alikutwa na silaha ya kivita? Kutokana na ufisadi uliotalamaki ndani ya CCM tumepata taabu sana kuikuza CHADEMA ili angalau sauti za watanzania wanyonge ziweze kusikika. Hivyo hatuwezi kuvumilia mambo ya kuoneana haya na kukaa nyumba moja aina ya watu kama diwani huyu. Kwa kuwa hizi ni tuhuma nzito, hata kama Serikali imeamua kumsamehe naomba sisi wanachama wa CHADEMA tusimsamehe. Hakuna kutafuta ushaidi wala nini, ni yeye mwenyewe aliyjiweka katika mazingira ya kuchafuaka hivyo ang'oke kwa kuwa ametuchafua wote.

Nashauri hakuna kuhurumia kata itapotea wala nini atakiwe ajihudhuru mara moja au afukuzwe na uchaguzi mdogo ufanyike hata tukipoteza kata hiyo potelea mabili ilikuwa ni katika jitihada za kulinda maadili mema.

Naomba kuwasilisha!!!!

Watamwandikia barua ili ajijue na ajiondoe mwenyewe kwenye udiwani ndani ya 90!
 
Kuna jimbo moja hukohuko Mara Mbunge kwa tiketi ya CCM ni jambazi wa siku wa silaha na funguo bandia. Madiwani wa jimbo hilo wa CCM wengi ni wezi na wafadhili wakubwa wa wezi wa mifugo.

Ndipo CHADEMA inapotakiwa kuact differently
 
Jamani acheni ushabiki na uzandiki....huyo diwani kama binadamu wa kawaida amefanya makosa..kama kweli hakuwa akimiliki kihalali silaha hiyo....TATIZO hapa mi naona SIASA....Watu wanahukumu chama CDM kuwa kinamiliki silaha!!! Je Silaha hiyo ilikutwa ofisi za chadema? Au ni Gilba tu za kisiasa za huyu mdau? kwa mtizamo wangu ,umiliki wake wa silaha hauna mahusiano kabisa na udiwani wake!!! MIMI NINACHOONA HAPA WATU WAMEKOZA NAMNA YA KUIDHOOFISHA CDM WANAAMUA KUPITIA NJIA ZA PANYA!!!!!!!!!!!!!!!! NDIO MAANA TUKIO HILI LIMEKUJA WAKATI WAKIJIVUA MAGAMBA!!!

huyo diwani kama binadamu wa kawaida amefanya makosa-Kwa hiyo unataka kutuambia wale walioko katika orodha ya Dr Slaa ya Mwemnbeyanga ya 2007 na Tabora ya 2011 sio binadamu, ila huyu diwani wetu aliyekutwa akimiliki silaha kinyume cha sheria ndio binadamu?. Kama huo ndio utakuwa mtizamo wetu CDM hakuna haja tena ya kukemea maovu kwa kuwa maovu ya aina yoyote kwa kuwa yote hutendwa na binadamu?

Watu wanahukumu chama CDM kuwa kinamiliki silaha!! Mkuki Mzuri kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Tulisherehekea kuwagandisha CCM na Ufisadi kutokanan awao kuchelewa kuchukua hatua muafaka ndani ya wakati muafaka kutenganisha Chama chao na watuhumiwa wa ufisadi. Vivyo hivyon kwa CHADEMA kikichelewa kuchuyka hatua za kutenganisha watuhumiwa mbali mbali na chama yatatukuta yale yale ya CCM.

Je Silaha hiyo ilikutwa ofisi za chadema?kwani zile fedha EPA, KAGODA< MEREMETA< RICHMOND n.k zilzwahi kukamatwa katika ofisi yoyote ya CCM? Ni viongozi wa CCM ndio walituhumiwa kuzikwapua kama amabvyo kiongozi wetu CHADEMA kakutwa namiliki silaha isivyo halali na ikiwa amechimbiwa sham,bani kwake
.
 
Chadema si jeshi la polisi bali chama cha siasa nchini. Kila mtanzania ana haki ya kumiliki silaha ili mradi ametimiza masharti fulani na ameahidi kutii na kuheshimu sheria za nchi, haina maana kuwa umiliki wa silaha hiyo uendana na matendo ya giza na kuvunja sheria zilizopo. Nionavyo mimi, hapa chadema haina la kufanya isipokuwa tuache kwanza polisi wafanye uchunguzi wao na wakamilishe. Litakalofuata baada ya hapo nadhani litahusisha pia chadema. Si kweli kwamba pamoja na chadema kupata uungwaji mkono na watanzania wengi kwa sasa eti sasa wako juu ya sheria. Akibainika tu kumiliki isivyo basi sheria itachukua mkondo wake na chadema kitamwajibisha diwani wake. Isikupe hofu kwa sasa, it is just a matter of waiting time.

Nafikiri ili CHADEMA ijtofautishe na CCM inatakiwa kutuma ujembe maalum huko ili kupta ukweli na kuchukua hatua mara moja
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom