CHADEMA inaangalia uwezo na uadilifu; maoni binafsi yasichukuliwe kuwa ni msimamo wa CHADEMA

Wewe unaye jiita tume ya katiba naona magamba yako yana washa. Viongozi wengi wa ccm hata Hawajui kutumia keyboard wanafikiria posho tuu Hebu ichekini response ya mnyika mtazimia na roho zenu. Iko chezea CDM nyinyi
 
Mzee Mtei ni mwanzilishi na muasisi wa chama.
Kwa sasa hana nafasi ya maamuzi ndani ya chama. Chama kinaongozwa kwa kanuni, taratibu na sheria za chama.
Mzee Mtei kuwa mwanzilishi haimaanishi kuwa atakuwa na some decisions, lakini anaweza kutoa maoni yake yenye tija kwa chama na taifa.
MNYIKA unanishangaza sana,mzee mtei ni kiongozi mwenye nguvu sana CHADEMA.mimi naamini hakuteleza hii ni ajenda yake na CDM wanaifanya makusudi.halafu ajabu mpaka ZITTO kamponda ww unajifanya kumtetea.kiufupi chadema ni wadini hata kampeni zao wanaegemea upande mmoja tu.
 
Kuna haja gani ya kuwa na Mzee kama Mtei{makapi} kulopoka hovyo hovyo mbele ya mass??Kiongozi/mwanasiasa makini ni yule ambae siku zote kauli zake hazileti mtafaruku kwenye jamii.
Mzee katuonesha his true color!!!Nafikiri huyu mzee yupo kwenye CC,watu tumepuuza kauli za udini kutoka kwa viongozi wetu wa dini,hili linaturudisha kulekule.!
 
Pomoja umekuja kuweka wazi msimamo wa Chadema lakini maneno ya Mzee Mtei yameishatoka na Mzee Mtei ndio nembo ya Chadema..

Ulichofanya John Mnyika ni sawa sawa kuziba shimo la panya kwa mkate.

Endeleeni kujitetea lakini watanzania wameishawasoma na wanajua kinachoendelea bahati nzuri kuna wana Chadema humu JF wanayakubali maneno ya Mzee Mtei kuwa ndio msimamo halisi wa Chadema.
 
Mkuu nimeyaforward kwenye email maneno ya mzeemtei ili yakajadiliwe na wanajamii. inshort message imeshafika.
 
Mnyika,
Wakati nayasoma maoni ya Edwin Mtei sikupata shaka yoyote kwamba sio maoni ya CHADEMA bali ni maoni yake binafsi! Isitoshe, mara ya kwanza sikuamini kwamba ni kweli Edwin Mtei Mwasisi wa CHADEMA kwavile hayupo verified!

Lakini pamoja na yote hayo, bado ukweli unabaki pale pale kwamba Mtei bado ni very influencial person ndani ya CHADEMA hivyo maoni yake ni hatari sana yanapoonesha kasoro za wazi wazi!! Post zake nyingi, Edwin Mtei anapenda kuanza kwa kusema "nikiwa kama muasisi wa CHADEMA....!" Hii inaonesha ni jinsi gani bado anajivuna na power yake ya uanzilishi wa chama!! Najua, from political point of view, CHADEMA hawawezi kutoa msimamo kama uliotolewa na Mtei lakini hii bado haiondoi hofu kwamba kumbe one of the most influencial person in the team ana mtazamo hasi katika suala zima la dini! Itakuwa ni kujidanganya mkipuuza kauli kama hizi kwa kisingizio cha kwamba si maoni ya chama! Wewe mwenyewe unafahamu wazi kwamba, ni ngumu kumtenganisha Mtei na CHADEMA....!! Hakuna asiyefahamu nguvu ya Mtei ndani ya CHADEMA, kwahiyo, ni rahisi sana watu wakashindwa kutofautisha kati ya maoni ya CHADEMA na yake binafsi! Si vibaya hata kidogo akiambiwa wazi kwamba, kutokana na nafasi yake katika chama basi ni vyema akawa anachunga kauli zake ingawaje nimempenda kwa kutokuwa mnafiki!
 
Nafurahishwa na utendaji wako Mnyika unapojibu hoja zinazoishambulia CDM kwa wakati. Hongera kamanda
 
Pomoja umekuja kuweka wazi msimamo wa Chadema lakini maneno ya Mzee Mtei yameishatoka na Mzee Mtei ndio nembo ya Chadema..

Ulichofanya John Mnyika ni sawa sawa kuziba shimo la panya kwa mkate.

Endeleeni kujitetea lakini watanzania wameishawasoma na wanajua kinachoendelea bahati nzuri kuna wana Chadema humu JF wanayakubali maneno ya Mzee Mtei kuwa ndio msimamo halisi wa Chadema.

Lakini mkuu hata Nyerere japo alikuwa ni muanzilishi wa CCM na mwanachama mwenye kadi No. 1 ya CCM, alipotoka madarakani alikuwa anaongea mawazo yake hadharani kama kupingana na uuaji wa azimio wa Arusha na Ubinafsishaji wa NBC etc. Lakini pamoja na mawazo yake waliokuwa na mamlaka waliyachukua yale waliyokuwa wanayaona ni muelekeo wao na kuyaacha mengine kama hayo niliyotaja hapo juu.

Kung'ang'ania kuwa Mtei ni CDM ni upuuzi uliopitwa na wakati na hautaisaidia CCM kuwafanya waislam waiogope CDM na kuipenda CCM sana sana utaisaidia CUF zaidi maana ndicho chama ambacho waislam wengi wanaamini kinaweza kuwatatulia matatizo yao. I think the whole notion of Mtei's views are CDM views are nonsense and will not serve well CCM apart from personal confort for the few in CCM who think CDM is destined to take their jobs.

Kauli ya Mnyika ni kauli ya CDM, ubishi kama huu ndiyo unatukimbiza sisi wengine CCM na kuona tuna watu wenye kuendekeza blah blah blah badala ya kutua matizo ya nchi. Unawe ukawa upo kazini (propagandist) ila fikiria chama chako zaidi. Think about lifting CCM up rather than bringing CDM down.
 
Mh.Mnyika,
Shukran sana kwa taarifa hii maana jana nzima sikuingia hapa JF lakini nadhani kama ningeingia na kuyakuta maelezo ya Mzee Mtei ningekwisha nguvu kabisaa..Mzee Mtei kateleza ama pengine ndivyo anavyo amini yeye na hii ingetumaliza CHADEMA na naomba sana chama kiendelee kuwajuza watanzania maana tayari mzee Mtei kisha kiweka doa kubwa sana chama kwa jinsi navyowafahamu Watanzania.

Binafsi yangu naamini ni mawazo na mtazamo wake kama walivyoweza simama kina Warioba na Salim kutoa mawazo na mtazamo wao dhidi ya Mkapa au JK ktk baadhi ya maamuzi. Vile vile yeye anaweza kutokubaliana na uteuzi wa JK kwa misingi hiyo japokuwa katuacha na harufu ya kujamba kwake...
 
Aboud Jumbe na Nyerere ndio waasisi wa CCM 1977. Jee Jumbe akitoka huko aliko na kusema lolote hiyo ni kauli ya CCM? Mbona na Nyerere alipolipinga azimio la Zanzibar na kuuzwa kwa NBC hamkusema hiyo ni kauli ya CCM bali mkasonga mbele na kumpuuza?
Na mpaka Nyerere anauwawa na hawa jamaa msimamo wake ulikuwa ni kwamba mgombea binafsi aruhusiwe lakini wakampuuza.
Na yule Jusa aliyesema lile jimbo wakristo na wabara ni wengi tuseme ndiyo msimamo wa CUF?
 
Mzee mtei ni muasisi na ni muasisisi wa chadema maoni yake yana nguvu katika chama mnyika! hilo halipingiki hata kidogo.

CHADEMA wasitoa maelezo mngesema, sasa wametoa maelezo bado mnasema! Mzee Mtei katoa maoni yake CHADEMA wametoa msimamo wa chama mnataka nini tena?

Labda nikuulize, matusi ya Lucinde ni sera ya ccm? Msimamo wa ccm kwenye matusi ya Lucinde ni upi?
 
Mkuu umeenda mbali sana.
Viongozi wengi wa CCM hawajui hata kusoma sms kwenye simu. They are far away from keyboard
Wewe unaye jiita tume ya katiba naona magamba yako yana washa. Viongozi wengi wa ccm hata Hawajui kutumia keyboard wanafikiria posho tuu Hebu ichekini response ya mnyika mtazimia na roho zenu. Iko chezea CDM nyinyi
 
Mh.Mnyika,
Shukran sana kwa taarifa hii maana jana nzima sikuingia hapa JF lakini nadhani kama ningeingia na kuyakuta maelezo ya Mzee Mtei ningekwisha nguvu kabisaa..Mzee Mtei kateleza ama pengine ndivyo anavyo amini yeye na hii ingetumaliza CHADEMA na naomba sana chama kiendelee kuwajuza watanzania maana tayari mzee Mtei kisha kiweka doa kubwa sana chama kwa jinsi navyowafahamu Watanzania.

Binafsi yangu naamini ni mawazo na mtazamo wake kama walivyoweza simama kina Warioba na Salim kutoa mawazo na mtazamo wao dhidi ya Mkapa au JK ktk baadhi ya maamuzi. Vile vile yeye anaweza kutokubaliana na uteuzi wa JK kwa misingi hiyo japokuwa katuacha na harufu ya kujamba kwake...

Maoni ya Mzee Mtei ni sawa na maoni ya Jusa kwamba lile jimbo kule Unguja lina Wakristo wengi na Wabara wengi, tunachulia ule ni msimamo wa Jusa na siyo CUF kama chama.
 
Hivi mtu kusema kwenye tume kuna waislam wengi ni imani, mtizamo ama factual?

Siasa za unafiki ndo zinawatafuna.
 
Maoni ya Mzee Mtei ni sawa na maoni ya Jusa kwamba lile jimbo kule Unguja lina Wakristo wengi na Wabara wengi, tunachulia ule ni msimamo wa Jusa na siyo CUF kama chama.
Pamoja na hivyo two wrong can't make it right. Mtu kama Jussa anatakiwa hata kunyang'anywa Uraia sasa nashindwa kuelewa hata Mtei naye kafikia huko kwa kina Jussa?..
 
MNYIKA unanishangaza sana,mzee mtei ni kiongozi mwenye nguvu sana CHADEMA.mimi naamini hakuteleza hii ni ajenda yake na CDM wanaifanya makusudi.halafu ajabu mpaka ZITTO kamponda ww unajifanya kumtetea.kiufupi chadema ni wadini hata kampeni zao wanaegemea upande mmoja tu.

Soma vizuri, Mnyika hajamtetea Mtei, labda kama unataka kulazimisha mawazo yako.
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa taarifa kwamba maoni binafsi ya viongozi na wanachama wasiokuwa na mamlaka kwa mujibu wa katiba, kanuni na itifaki ya chama kuwa wasemaji wakuu wa masuala ya chama katika ngazi husika yasichukuliwe kuwa ni msimamo wa CHADEMA.

CHADEMA kinatoa taarifa hii kufuatia maoni binafsi ya muasisi na mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA juu ya wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba yanayoelezwa kutolewa katika mtandao wa jamii wa Jamii Forums kutafsiriwa kuwa ni msimamo wa CHADEMA.

CHADEMA kinatoa mwito kwa wachangiaji katika mitandao ya kijamii na wananchi kwa ujumla kuzingatia kuwa CHADEMA bado haijatoa kauli juu ya wajumbe wa tume husika kwa kuwa bado CHADEMA inaendelea kufanya uchambuzi juu ya wasifu wa wajumbe wa tume husika na mchakato wa uteuzi wao kama tulivyoeleza kwenye taarifa kwa umma tuliyotoa tarehe 7 Aprili 2012.

Hata hivyo, izingatiwe kwamba uchambuzi wa wasifu wa wajumbe walioteuliwa kwenye tume husika unaoendelea kufanywa na CHADEMA hauhusu dini za wajumbe wa tume kwa kuwa CHADEMA hakiamini katika udini bali unahusu uwezo na uadilifu wa wajumbe husika na iwapo umezingatia matakwa ya umma na dhamira ya kujenga muafaka wa kitaifa wa kuwa na katiba mpya na bora.

Izingatiwe pia kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ibara ya 3B kifungu cha 3.1.9 ikiwa ni sehemu ya misingi iliyopo kwenye itikadi ya CHADEMA ya mrengo wa kati, CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola na na misingi mingine ya CHADEMA ya kujenga chama na taifa lenye kutoa fursa kwa kuzingatia uwezo na uadilifu bila kujali tofauti zingine.

Pamoja na kujulisha umma kwamba CHADEMA kinaendelea kufanya uchambuzi wa wajumbe walioteuliwa kwenye tume husika, tulieleza kuwa CHADEMA kilitarajia kwamba Rais Jakaya Kikwete angeeleza pia ratiba ya kufanyika kwa marekebisho mengine muhimu ya awamu nyingine kuhusu bunge maalum la katiba na hatua ya kutunga katiba mpya na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki kabla ya mchakato kufikia katika hatua husika.

Tunasisitiza umuhimu wa Serikali kutoa kauli kwa umma kuhusu ratiba ya marekebisho ya awamu nyingine ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 kwa kuzingatia kuwa Ofisi ya Bunge imetangaza kuwa Mkutano wa Bunge utaanza tarehe 10 Aprili 2012 bila marekebisho ya sheria ya katiba kuwa sehemu ya orodha ya miswada ya sheria inayotarajiwa kujadiliwa katika mkutano wa saba wa Bunge.

Tunarejea kuutarifu umma kuwa Kamati Maalum ya Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoundwa tarehe 20 Novemba 2011 kwa ajili ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete kuhusu sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 itafanya kikao chake karibuni mara baada ya uchambuzi kukamilika kupitia taarifa ya uchambuzi unaofanywa juu ya uteuzi uliofanyika wa wajumbe wa tume na tamko litatolewa kwa umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa maslahi ya taifa.

Imetolewa tarehe 09 Aprili 2012 na:

John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
Hewaaaaa huo ni mshimamo wa CHADEMA vinginevyo ni maoni ya watu binafsi, ahsante kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kama chama kinacho jiandaa kushika dola!!!!!!!!!!!VIVA CDM VIVA MAKAMANDA!!!!!

Back
Top Bottom