CHADEMA ina washabiki wengi, Haina wapiga kura wengi

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,835
Hii ni kweli na sio uongo. CHADEMA kusema kweli imeteka watu wengi na kujiibulia washabiki wengi sana. Bali inawapiga kura wachache.

Unajua kura ni siri: Mtu anaweza akamshabikia mgombea fulani lakini ikifika wakati wa kupiga kura palepale ana badili na kumchagua mwingine, halafu akitoka anaendela kukushabikia.

Hii ndio inayo wacost CHADEMA itabidi wabadili mfumo si kufurahia ushabiki wa watu. Wawatake watu wawe na vitabulisho vay kupiga kura. pili wawaombe watu waende kupiga kura.

Au mnaonaje?
 
Nadhani huelewi hiyo nadharia inapandikizwa ili kubariki uizi wao, na kutoka hapo mashabiki wengi wa CHADEMA watajiandikisha katika daftari la wapiga kura na kuhitimisha mazishi ya CCM.
 
Kaulize mby town Iringa town arusha na kwingineko utajua kama inawashabiki au wapiga kura CDM hawana wezi wa kura tu hilo nalikubali
 
Ningekuelewa kuwa CHADEMA inapendwa na watu wengi, ina mashabiki wengi lakini haina wanachama wengi ukilinganisha na magamba!
Lakini kama ulivyosema kura ni siri, tuambie hizo kura za siri ni za nani?
Arumeru mashariki kwa mfano, CHADEMA hawakuwa na hata mwenyekiti wa mtaa, hizo kura za siri za wanachama wa ccm ndiyo iliyokipa ushinda CHADEMA.
Igunga CHADEMA hawakuwa hata wanachama, lakini kwenye uchaguzi ule walipata kura zaidi ya 23,000, pungufu ya kura 2000 au 3000 ya kura walizopata CCM.

Hivyo unatakiwa ueleweke mkuu siyo unakurupuka kupost!
 
Hii ni kweli na sio uongo. CHADEMA kusema kweli imeteka watu wengi na kujiibulia washabiki wengi sana. Bali inawapiga kura wachache.

Unajua kura ni siri: Mtu anaweza akamshabikia mgombea fulani lakini ikifika wakati wa kupiga kura palepale ana badili na kumchagua mwingine, halafu akitoka anaendela kukushabikia.

Hii ndio inayo wacost CHADEMA itabidi wabadili mfumo si kufurahia ushabiki wa watu. Wawatake watu wawe na vitabulisho vay kupiga kura. pili wawaombe watu waende kupiga kura.

Au mnaonaje?

Malizia kwa kusema huo ni mtizamo wake kulingana na upeo wako
 
Hizo ni kauli na mbinu za kuwaandaa watu kisaikolojia ili wakichakachua iwe ni kauli iliyozoeleka, hatudanganyiki sasa hivi atakayefikiria acha kuiba kufikiria tu kuiba kura utapambana na M4C! Kaa chonjo!
 
Una jaribu kueleza uma jinsi mnavyo tumia maneno ili kuwa adaa wananchi ili muibe kura zetu!

Sasa kama unajua hatuna wapiga kura mbona hujiulizi kwa nini magamba huangaika kuiba kura zetu?

Kabla hujaleta mada unatakiwa kujihoji kwanza,pengine umeleta mada baada ya kuchanganywa na "MOVEMENT FOR CHANGE"

kwanini nyie magamba mpange kuiba kura wakati mna wapiga kura wengi? Unatakiwa uwe unaona haibu hata kidogo.
 
Hii ni kweli na sio uongo. CHADEMA kusema kweli imeteka watu wengi na kujiibulia washabiki wengi sana. Bali inawapiga kura wachache.

Unajua kura ni siri: Mtu anaweza akamshabikia mgombea fulani lakini ikifika wakati wa kupiga kura palepale ana badili na kumchagua mwingine, halafu akitoka anaendela kukushabikia.

Hii ndio inayo wacost CHADEMA itabidi wabadili mfumo si kufurahia ushabiki wa watu. Wawatake watu wawe na vitabulisho vay kupiga kura. pili wawaombe watu waende kupiga kura.

Au mnaonaje?

Ndugu yangu uchaguzi wa Arumeru mlikuwa mnasema hivyo, ni kitu gani kilitokea? Jibu unalo mwenyewe
 
mara chadema chama cha kaskazini,mara chadema chama cha wambulu,mara chadema chama cha kidini,mara chadema chama cha wahuni.
Mara chadema chama cha wachochezi.
Ukijumuisha hizi kauli utaona chadema ni chama cha makundi yote ya kijamii.
 
Hii ni kweli na sio uongo. CHADEMA kusema kweli imeteka watu wengi na kujiibulia washabiki wengi sana. Bali inawapiga kura wachache.

Unajua kura ni siri: Mtu anaweza akamshabikia mgombea fulani lakini ikifika wakati wa kupiga kura palepale ana badili na kumchagua mwingine, halafu akitoka anaendela kukushabikia.

Hii ndio inayo wacost CHADEMA itabidi wabadili mfumo si kufurahia ushabiki wa watu. Wawatake watu wawe na vitabulisho vay kupiga kura. pili wawaombe watu waende kupiga kura.

Au mnaonaje?

Hebu pitia taarifa ya chaguzi zinazofanyika hivi sasa na utapata jawabu la hoja yako.
 
ndio kazi waliyonayo viongozi wa chadema kuhakikisha wafuasi wao wanajiandikisha kwenye kitabu cha kupigia kura..lakini hata ccm ambao wafuasi wao wengi wamejiandikisha kwenye hilo daftari watawapigia kura cdm.
 
Hii ni kweli na sio uongo. CHADEMA kusema kweli imeteka watu wengi na kujiibulia washabiki wengi sana. Bali inawapiga kura wachache.

Unajua kura ni siri: Mtu anaweza akamshabikia mgombea fulani lakini ikifika wakati wa kupiga kura palepale ana badili na kumchagua mwingine, halafu akitoka anaendela kukushabikia.

Hii ndio inayo wacost CHADEMA itabidi wabadili mfumo si kufurahia ushabiki wa watu. Wawatake watu wawe na vitabulisho vay kupiga kura. pili wawaombe watu waende kupiga kura.

Au mnaonaje?

Kwa hiyo ukiwa kama JF senior Expert unachosema ni kuwa inawezekana kuwa na mashibiki wachache lakini wapiga kura wakawa wengi? Kwamba CCM hawana haja ya kuhofia vyama vya upinzani sababu swala si ushabiki bali ni kura Kwamba tafiti yako ni kuwa ukiwa na washabiki wengi unakuwa na kura chache?
 
Inawezekana ni kweli kwa sasa ili before next election mashabiki zaidi ya 80% watakuwa wapiga kura
 
Ningekuelewa kuwa CHADEMA inapendwa na watu wengi, ina mashabiki wengi lakini haina wanachama wengi ukilinganisha na magamba!
Lakini kama ulivyosema kura ni siri, tuambie hizo kura za siri ni za nani?
Arumeru mashariki kwa mfano, CHADEMA hawakuwa na hata mwenyekiti wa mtaa, hizo kura za siri za wanachama wa ccm ndiyo iliyokipa ushinda CHADEMA.
Igunga CHADEMA hawakuwa hata wanachama, lakini kwenye uchaguzi ule walipata kura zaidi ya 23,000, pungufu ya kura 2000 au 3000 ya kura walizopata CCM.

Hivyo unatakiwa ueleweke mkuu siyo unakurupuka kupost!

Tena hizo kura 2000 ccm wamenunua kwa bil6!!
 
Mnaweza kumshambulia mleta mada ila ukikaa na kuchambua nadhani utapata logic. Nadhani kama kupendwa na kukubalika kwa CDM hilo sio mjadala tena kwa Tanzania yetu. Cha muhimu ni kuwahamasisha watu wakatumie haki yao na wakamalize chuki zao siku ya uchaguzi hicho ndicho alichokuwa anataka kumaanisha mleta mada.

Kuwa Arumeru, Mbeya, Iringa na Arusha na kwingineko hilo halipingiki, cha muhimu ni kuwapa watu mwamko wa kuenda kupiga kura ili kuweza kuzuia wizi wa kura na mengineyo. Unajua unapokuwa na kura nyingi hata wakijaribu kuchakachua huwa haiwezekani kama ilivyokuwa ubungo, mbeya, kawe hata Arusha mjini.

Mtu kuwa shabiki na mpenzi wa chama pia ni kuweza kukipigia kura chama chake, kura moja ni ya muhimu sana! Hakuna haja ya kujiridhisha kuwa CDM wana watu wengi bila ya hao watu kuhamasishwa kupiga kura baada ya kufahamisha haki zao na mambo yanayoendelea katika taifa letu. Otherwise itakuwa ni yaleyale.
 
Ni kweli naweza kukubaliana na wewe kwenye ili...wengi wao ni Chadema-Kata.
 
Ni kawaida ya wanaharakati, wanachotaka ni sifa na kuuza sura. Mfano rejea picha za Msigwa na Nasary Marekani.
 
Back
Top Bottom