CHADEMA imekosa Dira?

Kufuatia kushindwa mfululuizo katika chaguzi ndogo za Busanda na Bihalamuro, chama cha "demokrasia" na maendeleo chadema kimepoteza dira sasa badala ya kukaa chini na kufanya tathmini ya kisanyansi mpaka kupelekea kushindwa katika chaguzi hizo, viongozi wa chama hicho hivi sasa wanamtafuta mchawi kwa kusingizia kuibiwa kura.

Madai kama haya yamekuwa yakitolewa na chama cha wananchi cuf katika chaguzi mbalimbali lakini chadema wamekuwa wakidai kuwa cuf ni walalamishi na sasa wimbo huo unaanza kuimbwa na chadema.

Ukweli ni Chadema kimekosa mikakati thabiti kuweza kuongoza na kubaki na kulala kila uchao, kilichobaki sasa kwa Chadema ni kurudi kwenye drawing board na kuanza upya huku wakijua siasa za Mwembe ya yanga za kulipua mabomu na kuvurumisha helikopta hazilipi na watanzania washawatukia kuwa ni chama cha kikabila na familia

Hapana unaongopa Chadema ilishinndwa Kiteto tuu,Mbeya walidhurumiwa walimuenguwa mgombeya wao,Busanda walichukua Dunia yote inajua kulikuwa na uwakilisha wa wana dunia kupitia balozi zao,
Biharamulo hiyo ndio komesha CCM waone aibu puu dhuluma kila mahala

lakini kutokana na mafundisho hayo Chadema wasibaki kusema kesi zinachukua muda na nini na ni

Wapeleke kesi mahakamani nakala kwenye balozi zote ,umoja wa Africa na umoja wa mataifa wajue nchi ambayo imekuwa ikiheshimiwa duniani kwa amani iko hatarini kutumbukizwa kwenye dimbwi la matatizo makubwa ya uzandiki na uporaji wa haki za wananchi
Kulipua mabomu ni sera nzuri sana pesa za EPA kama kweli zimerudishwa manake zisingerudi ili mradi watumii vurugu kutekeleza hayo
Kutumia helicopta ni lazima ili wote wafikwe na umeona matokeo yake na mafanikio ya helkopta chadema inawafuasi wa kutosha tuu,kwa kiasi kikubwa vijijini
 
Ooh really? kwa hiyo maneno ya marehemu yashakuwa msahafu... hang on a minute... tunae marehemu mwingine anaitwa Chacha Wangwe yeye alisema Chadema ni chama cha kikabila na familia nae mka mkolimba! how about that?

Marehemu Kolimba alisema CCM imekosa dira,......
Marehemu Chacha Wangwe alisema CHADEMA chama cha kikabila lakini hakusema kuwa chadema imekosa dira.
Katika hizo kauli mbili za watu wawili waliokuwa vigogo ndani ya vyama vyao, huyo wa CCM ndiye alikiri kuwa wamekosa dira.Sasa unachoshindwa kuelewa ni kitu gani hapo?au umepofushwa na mahaba uliyonayo kwa ccm.
kaaazi kweli kweli poti.
 
viongozi wa chama hicho hivi sasa wanamtafuta mchawi kwa kusingizia kuibiwa kuraQUOTE said:
Mtoa mada naona umechanganya mambo, mimi naona siyo kwamba wanasingizia, bali NI KWELI WANAIBIWA!. we have to be clear on the fact!
 
Nafikiri Chadema isichukulie maneno haya ya jumla jumla kama ndio ukweli on the ground. Nionanvyo wanaenda vizuri kwasababu mwanzoni walijikita zaidi mijini kuliko vijijini ambako CCM ilikuwa inapeta zaidi. Challenge walioipa CCM Busanda na Biharamuro,inathibisha ukweli kwamba dynamics za siasa ya Tanzania zimenza kubadilika.Waendeleze elimu ya chama chao zaidi ili watu mpaka vijijini wakijue vizuri na wajue nini Chadema kama chama kinasimamia kama wakipewa madaraka. CCM imeifanya hiyo kazi ya elimu vijijini kwa miongo kadhaa na siyo rahisi kufuta katika mawazo ya watu bila kuwa na mikakati ya kweli ya kueneza sera zao za chama. Kuvunjika kwa kolea siyo mwisho wa uhunzi...bado wanaweza kuongeza idadi ya wabunge kwenye uchaguzi ujao.
 
Yes CCM wanatumia mbinu zote pamoja na kuiba kura au kutangaza matokeo yasiyo halali. Siku zote angalia hii; matokeo huanza kutangazwa sehemu ambako CCM wanatarajia upinzania zaidi! Kwa nini? Ili wajue difference ya kuweza ku cover-up kwenye maeneo wanakojua wapinzani hawapo au wapo shaky.

Kwa kuwa wao ndo wenye serikali na serikali inawafanyia kazi, CCM wakishatangaza kura za maeneo ambayo wako sure hawawezi kudanganya hujua tofauti wanayotakiwa kujazilizia kutoka kwenye sehemu ambazo wanakuwa wameshaziandaa mapema. Upinzani hushinda tu pale ambapo tofauti ya matokeo maeneo ambayo CCM wanatarajia kushinda inapokuwa kubwa sana.

Kwa mfano huko Biharamulo ikiwa chadema wangepata nyingi zaidi mjini bado CCM wangetengeneza kura nyingi zaidi huko vijijini. Mpaka pale watakapoona idadi ya wapiga kura ya vijijini haiwezi kuwa consistent ndo wanaamua kutangaza wameshindwa. Hicho kilitokea Tarime.

Hata siku moja CCM hawawezi kutoa matangazo ya matokeo kwenye ngome zao kwanza!! Hapa ndo siri kubwa ilipolala.
 
Ya nini kupoteza muda kuangalia kitu kisicho make sense? kwa nini "usibane" matumizi kwa kusoma thread za CUF na CCM huko?

Jamani nilishasema...hapa JF tunataka watu wenye akili timamu.....Masato ana matatizo ya kukosa ustaarabu...kwa kusoma tuu threads zake anazoleta hapa nimegundua ni mtu wa kuropoka na labda mwenzao mafisadi wa tanzania. Inakuwaje kila kitu serious kinachohusu CHAMA CHA MAFISADI yeye watu wakitoa mawazo against CCM anakasirika sanaaa.....ila anataka akikashifu wengine TUMBEBE JUICE...hii haiwezekani. Naungana na wasemaji wengine kumwomba Masato alete hoja za kufaa kudiscuss......sio ushabiki wa kutokuwa na hoja. Masato...unawezaje kucompare MAFISADI wa 45yrs na CHADEMA 15 yrs? Hebu tuambie kisomi, hii comparison yako ni ya wapi?
 
Siasa za kiafrika hasa hapa kwetu ni kwamba kupata kura nyingi siyo kushinda na ili kushinda siyo lazima upate kura nyingi. TATIZO kubwa la vyama vya upinzani hapa kwetu nadhani NI KUSHINDWA KULINDA USHINDI ambao tayari wanakuwa wameshaupata. VINGINEVYO WANAKUBALIKA KASORO TU MBINU
 
Weekend hii nilihudhuria mojawapo ya sherehe (za kiangazi) za watanzania waishio nje ya nchi. Kama kawaida ya vijana wengi wa kitanzania (ninao wafahamu mimi), mazungumzo ya siasa za bongo huchukua sehemu kubwa sana ya maongezi baina ya watu (vikundi, nk).

Baada ya kumaliza ubishi wa nani mbabe kwenye:

1. Tenesi - venus au serena
2. Soka - Ronaldo au Ronaldinho
3. Soka ya bongo - simba au yanga
4. Basiketibol - Kobe au Lebron
5. NK

Mambo yalihamia kwenye siasa za bongo, mengi yalisemwa ila moja tu ndilo lilikosa jibu mwafaka toka kwa wachangiaji (baada ya kutokea ubishi mkali - hasa baada ya heinikeni kuwakolea baadhi ya wachangiaji).

Swali kubwa lilikuwa, je ni kweli CHADEMA iliwaunga mkono CUF (kwenye ngazi ya uraisi) katika chaguzi za 1995 na 2000?

Natumaini kuwa great thinkers wa JF watauweka huu ubishi chini once and for all.
 
Ni Kweli waliunga mkono vyama vyote vilivyojitokeza kugombea urais wakati ule kabisa chini ya Bob Makani waliunga mkono hata mwaka
 
Sina kumbukumbu kamili za mwaka 1995 japo ni kweli. Kuhusu mwaka 200 ni ukweli wa asilimia 100 maana katika maeneo yote alipopita Mgombea Urais wa CUF, Prof Lipumba na mgombea Mwenza, Mh. Nasor, Chadema walishiriki kwa hali na mali na kuna maeneo Chadema walitumia magari yao, hoteli zao, mfano Kilimanjaro, Hotel Aishi ya Machame na Keys ya Moshi mjini na magari yote ya Chadema yalitumika. Kwa Moshi hata gari la Lipumba Land Cruiser short chases aliyosafiri nayo nchi nzima ikiwa imechoka alilazimika kuiacha na kukabidhiwa gari ingine yenye hadhi. Ilikuwa ni kwa nia njema na pengine kwa Chadema pia kutaka Lipumba asaidie kampeni za wagombea wao wa Ubunge, Philemon Ndesamburo kwa Moshi mjini na Freeman Mbowe kwa Hai.

Lakini hali ya sasa haishirii neema kwa mageuzi hata kidogo. CUF na Chadema sasa wanaangaliana kama mahasimu wakuu, tena kuliko hata ilivyo kwa CCM.
 
Sina kumbukumbu kamili za mwaka 1995 japo ni kweli. Kuhusu mwaka 200 ni ukweli wa asilimia 100 maana katika maeneo yote alipopita Mgombea Urais wa CUF, Prof Lipumba na mgombea Mwenza, Mh. Nasor, Chadema walishiriki kwa hali na mali na kuna maeneo Chadema walitumia magari yao, hoteli zao, mfano Kilimanjaro, Hotel Aishi ya Machame na Keys ya Moshi mjini na magari yote ya Chadema yalitumika. Kwa Moshi hata gari la Lipumba Land Cruiser short chases aliyosafiri nayo nchi nzima ikiwa imechoka alilazimika kuiacha na kukabidhiwa gari ingine yenye hadhi. Ilikuwa ni kwa nia njema na pengine kwa Chadema pia kutaka Lipumba asaidie kampeni za wagombea wao wa Ubunge, Philemon Ndesamburo kwa Moshi mjini na Freeman Mbowe kwa Hai.

Lakini hali ya sasa haishirii neema kwa mageuzi hata kidogo. CUF na Chadema sasa wanaangaliana kama mahasimu wakuu, tena kuliko hata ilivyo kwa CCM.

Hapo kwenye nyekundu umegonga kabisa kwenye kichwa mkuu Halisi. Hata mimi nashangazwa sana na kinachoendelea sasa hivi.

Anyway ... ni vizuri muda mwingine kuangalia nyuma ili kujenga mwelekeo mwema (kama upo).
 
Bwana Masatu yeye ataki siasa za Mwembe yanga bali za bungeni za JOKA LA MDIMU, ukweli upo na unajulikana kilichotokea Mbeya, Busanda na hata sasa Bihalamuro, lakini hii ni picha nzuri sana kwa wanaupinzani wote kwani wanachokifanya CCM ni sawa na mtu ambaye anajijua kabisa ni mgonjwa lakini anaficha ugonjwa wake hata kwa madaktari sasa sijuhi anamkomoa nani, Time will Tell na itakuwa soon 2010, kwani wakati huo kila mtu atapigana kivyakevyake ile nguvu yote ya CCm kwenda kwenye jimbo moja haitakuwepo maana wakati huo hata Mkwere nae atakuwa bize kupambana na kina RA, sasa sijuhi kama yule mama pale Busanda ataweza kupambana pekeyake bila Kirango au Makamba kwani na wao watakuwa bize kwenye kutetea unga wao kwenye Majimbo yao
 
Bw. mapesa si alifanyiwa hivyo hivyo, lakini akawambia nakusubiri uchaguzi mkuu, waliporejea akawabwaga, chadema ndugu zetu msijali, jipange kwa mashambulizi 2010, CCM wapo hanimuni saivi nyinyi jitayarisheni na uzazi. c'mon
 
Ni Kweli waliunga mkono vyama vyote vilivyojitokeza kugombea urais wakati ule kabisa chini ya Bob Makani waliunga mkono hata mwaka

Asante Josh,

Hata nyingi ya PM ninazopokea zinaonyesha kuwa ni kweli CHADEMA iliwaunga mkono CUF kwenye uchaguzi wa 2000 ila kuhusu 1995 bado haiko wazi.

Sasa hivi vilio hapa (na kwenye vijiwe vya kahawa) kuwa CHADEMA ni wabinafsi na hawataki ushirikiano na wengine hutoka wapi? Kama CUF waliungwa mkono chaguzi zilizopita, kwa nini muungano huo usifanyike pale inapoonekana kuwa CHADEMA ina nguvu?

Naona kuna haja ya kuwafungia Lipumba na Mbowe au Zitto na Seif kwenye chumba kimoja mpaka waweke mbali tofauti zao.

BTW ... Sioni kama kulikuwa na haja yoyote ya kuunganisha thread yangu na hii.
 
Last edited:
Masatu ingekuwa vyema ujibu hoja.
Ulitaka miaka 48 ya uhuru nimekupa ila hujajibu hoja zangu. jibu hoja za msingi wacha kuficha kichwa na kuaacha kiwili wili juani.
Nini unachoshabikia CCM?
 
Mugo"The Great";514293 said:
From CCM perspective kuongeza jimbo ni mafanikio(hii ni kweli) lakini from another angle CCM inapoteza umaarufu ndio maana ushindi wa 80-90% sasa hivi haupo. Unajua mti unaweza kuwa mmoja lakini ukiambiwa uelezee ulivyo itategemea na angle uliyopo. Kwako wewe kuongeza jimbo ni mafanikio (you are entitled to it) na kwangu mimi kupungua kwa %age ni sign ya decline. That's why katika kupima performance kuna A+, A, A-, B+, B n.k.

Lakini amini usiamini "ENZI ZA CHAMA KUSHIKA HATAMU aka UTAMU ZINATOWEKA"

Siasa ni kama askari wa miguu mafanikio ni wanapo advance na kuchukua territory kuongea majimbo yap ndio mafanikio. Chadema wao acha waendelee kujaza watu kwenye mikutano yao wengine wanakuja kuburudika na mziki, wengine wanafuata helikopta nk

Sasa kama umeamua kuangalia kwenye angle ya kujaza watu kwenye mikutano then kumuulize mzee wa Kiraracha ana somo zuri kwenye topic hiyo.
 
Masatu, isiwe tabu narekebisha namba. Miaka 48 ya uhuru na miaka 32 ya CCM na miaka ya 16 ya TANU baba ya CCM tangia uhuru. Naomba ujibu hoja .

To be more precisely its not even 48 years its 47 years na miezi 7 rekebisha tena!
 
Back
Top Bottom